Home » » Watu 11 wafariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya magari 3 eneo la Veta Dakawa

Watu 11 wafariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya magari 3 eneo la Veta Dakawa

Written By Bigie on Friday, July 1, 2016 | 4:48:00 PMWatu 11 wafariki na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mafuta na basi la Ota, Dakawa Morogoro leo alfajiri Polisi yathibitisha.
  

Ajali hiyo iliyotokea wilaya ya KILOSA ikihusisha Bus la kampuni ya OTTA CLASSIC yenye namba DGK T.201 likitokea BUKOBA kuelekea D'SALAAM likigongana na loli la mafuta lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.
          
                   
Kuna abiria wamekufa ikiwajumuisha na madereva wote wawili na wasaidizi wao pamoja na abiria wengine. Miili ya marehemu imekimbizwa na mingine bado inapelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa utambuzi na kwa itifaki ila mahututi wengine wanapatiwa matibabu hapo hospitali ya ST JOSEPH inayomiliikiwa na Kanisa la Roman Catholic.

Rai:Kama una ndugu unahisi au unafahamu alikuwa anasafiri basi fanya mawasiliano naye mapema.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts