Home » » Young Dee ajipanga kuachia mixtape yake

Young Dee ajipanga kuachia mixtape yake

Written By Vuvuzela on Friday, July 29, 2016 | 10:07:00 AM


Rapper Young Dee amesema anajipanga kuachia mixtape yake.Amedai kuwa yeye na uongozi wake wa MDB wamejadiliana na kuona kuna umuhimu wa kuanza kutoa nyimbo nyingi kwaajili ya mashabiki katika mfumo wa mixtape.

“Nyimbo zipo nyingi sana halafu nilikuwa kimya tulifikiria mwishoni mwa mwaka huu tutengeneze platform ambayo watu wataweza kupata ngoma zangu online, zitakuwa katika mfumo wa mixtape,” rapper huyo alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

Amesema tayari ameanza kuandaa kazi mpya kwaajili ya mixtape hiyo na baadaye ndipo watatangaza lini itatoka.Hivi karibuni rapper huyo aliachia wimbo wake ‘Hands Up.’

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts