Home » » Bw. Hassan Abbas ateuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)

Bw. Hassan Abbas ateuliwa kuwa mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO)

Written By Vuvuzela on Wednesday, August 10, 2016 | 10:21:00 AM

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemtangaza  Bw.Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  na Msemaji Mkuu wa Serikali  kuanzia Agosti 5 Mwaka huu.

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 kifungu Namba 6(1)(b) kufuatia uhamisho wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw. Assah Mwambene uliofanyika  tarehe 7 Machi 2016 kwenda Wizara ya Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe.Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa Wanahabari na Wananchi  kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bw Abbas atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.

“Ninawaomba Wanahabari na Watanzania kwa ujumla mumtambue Bw Abbas na mtoe ushirikiano unaostahili katika utendaji wa kazi zake”.Alisema Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri Nape alimpongeza Bibi Zamaradi Kawawa aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo kwa  kujituma na kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu na uadilifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo mpya amekubali uteuzi huo na ameahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa uadilifu mkubwa na ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo na Watanzania kwa ujumla.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Hassan Abbas  alikuwa ni Meneja Habari na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais inayosimamia Utekelezaji wa Program ya Matokeo Makubwa sasa (President`s Delivery Bureau).

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts