Home » » Diamond Afunguka kuhusu Uhusiano wake na Hamisa Mabeto

Diamond Afunguka kuhusu Uhusiano wake na Hamisa Mabeto

Written By Vuvuzela on Wednesday, August 3, 2016 | 11:16:00 AM


Ukaribu wake kwenye mitandao ya kijamii siku za karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori za Diamond Platnumz kuwa amekua na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo wa bongo Hamisa Mobetto.

Stori zilianzia kwenye birthday party ya mama Diamond baada ya Hamisa kuonekana kuwa karibu na familia hiyo hasa dada wa Diamond lakini pia kuna picha iliyosambaa inaonyesha wawili hao kila mmoja amepiga picha kwa wakati wake lakini kwenye mazingira ya chumba yanayofanana

.
Diamond Platnumz ametolea ufafanuzi ishu hiyo na kusema “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana kwasababu yupo katika industry hizi za kufanya fashion, nimekua nikimjua muda mrefu kidogo na sikuwahi kuwa na matatizo nae yoyote sababu tumekuwa ni watu tu ambao tunaheshimiana …..

"Sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikua kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na nafikiri hiyo imechangia kuingiza hayo maneno, kufanya video Tanzania mara nyingi huwa inaleta manenomaneno"


Sikiliza hapa chini:

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts