Home » » Diamond kuiuza albamu yake mpya kimataifa

Diamond kuiuza albamu yake mpya kimataifa

Written By Bigie on Thursday, August 11, 2016 | 9:38:00 AM


Mkali ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amepanga albamu yake atakayoiachia kabla ya mwaka kumalizika kuiuza hadi nje ya Tanzania.

Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yeye ni msanii wa kimataifa na kwamba anafuata nyayo za kina Usher.

“Ukisema utatoa album halafu unauza ndani tu ndio nini sasa, tunataka ukitoa album iuzwe kama zinavyouzwa album za kina Usher huko, sasa hivi na mimi nipo kimataifa,” alisema Diamond.

Ni muda mrefu Diamond amekuwa akiahidi kuachia albamu yake mapema, hata mwezi Februari mwaka huu kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika, “Albamu yangu mpya, ngoma mpya na albam ya Harmonize, na ujio mpya wa Raymondtiptop. Soon zitakuwa masikioni mwako.”

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts