Home » » Dini imesababisha Nisifunge Ndoa na Chuzi Zaidi ya Kuzaa Naye Tu- Jini Kabula

Dini imesababisha Nisifunge Ndoa na Chuzi Zaidi ya Kuzaa Naye Tu- Jini Kabula

Written By Vuvuzela on Monday, August 8, 2016 | 9:17:00 AM

MIRIAM Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka sababu iliyomfanya ashindwe kufunga ndoa na mzazi mwenzake Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuzi’ ni wosia kutoka kwa wazazi wake ambao walimwamru kutobadili dini yake ya Kikristo.

“Nilishaapa siwezi kubadili dini kwa ajili ya Ndoa hata nilipozaa na Mr. Chuzi kikwazo ilikuwa dini siwezi kupingana na wosia wa marehemu Baba yangu,”anasema Kabula.

Kabula anasema kuwa anachofurahia ni yeye kufanya kazi na mzazi mwenzake kwa heshima kwani kwa sasa anamchukulia kama bosi wake na si mume wala mtu ambaye ana malengo nayo kwa ajili ya kuishi naye kama mke na mume zaidi ya kufanya kazi tu.

Jini Kabula alikuwa na mahusiano na mtayarishaji na muongozaji wa filamu na tamthilia Swahilihood Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuzi’ na walifanikiwa kuzaa mtoto wa kike ajulikanaye kwa jina la Salma Kihangala ambaye pia anafuata njia ya wazazi wake katika uigizaji.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts