Home » » Emmanuel Mbasha aomba Radhi Mashabiki wake

Emmanuel Mbasha aomba Radhi Mashabiki wake

Written By Vuvuzela on Saturday, August 13, 2016 | 6:58:00 AM

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Emmanuel Mbasha amesema anaomba radhi kwa mashabiki wake wote ambao walikuwa wanafuatilia habari zake kuhusiana na kutengana na mke wake Flora Mbasha na yeye kukataa kuzungumzia habari hizo kwa muda wote.

Akizungumza na EATV kipindi cha FNL, Mbasha amesema hapendi kuzungumzia mambo yake na Flora Mbasha kwa sababu tayari Mungu amemshindia kesi ya ubakaji iliyomkabili na baadaye akaweza kushinda hivyo hapendi kumzungumzia tena mambo hayo.

”Kesi nimeshinda na amenishindia Mungu hivyo sipendi kuzungumzia mambo hayo tena, na hata wanasheria wangu wamenishauri nisizungumzie tena mambo hayo, ila kikubwa ninachowaomba mashabiki wafuatilie sasa ni nyimbo yangu mpya ya ‘Haribu Mipango ya Shetani” ambayo imetengenezwa na mtayarishaji wa nyimbo Pablo.

Aidha Msanii huyo amesema hajarudiana na Flora Mbasha na yupo Single kwa sasa na anachokifanya kikubwa kwa sasa ni kumtumikia Mungu.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts