Home » » Gigy Money Ammezea Mate Idris wa Wema...Ajitangaza kuzaa na Idris

Gigy Money Ammezea Mate Idris wa Wema...Ajitangaza kuzaa na Idris

Written By Vuvuzela on Friday, August 5, 2016 | 8:40:00 AM


Msanii wa muziki ambaye pia anafanya ‘modeling’ na utangazaji kwenye Kituo cha Redio cha Choice FM cha jijini Dar, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amejitangazia ushindi wa kumnasa aliyekuwa mpenzi wa Wema Sepetu, Idris Sultan huku akitamba kuwa, sasa atamzalia mtoto.

Awali kulikuwa na vita nzito kati ya Wema na Gigy ambapo wakati Wema akiendelea kupalilia penzi lake, Gigy aliibuka na kudai kuwa, atahakikisha anampata Idris akiamini kuwa ndiye mwanaume wa ndoto zake.

Kufuatia vita hiyo ambayo iliibuka baada ya Gigy kunaswa na Idris usiku wakiwa kimahaba kwenye ukumbi mmoja wa burudani uliopo Mikocheni jijini Dar, Wema hakuonesha kujali badala yale aliendeleza msimamo wake kuwa yeye ndiye ‘Mrs’ Idris na wengine waliokuwa wakijipendekeza hawakuwa na chao.

Kufuatia Wema kukomalia penzi lake, Gigy alijishtukia na kuamua kukaa pembeni licha ya kwamba mara kadhaa alikuwa akisema kuwa ipo siku atatimiza ndoto yake ya kutoka na Idris.

“Mimi kwa kweli nampenda sana Idris, najua yuko na Wema lakini ipo siku kile ninachokiwaza kitatimia,” alisema Gigy miezi kadhaa iliyopita akionesha kuwa hatakata tamaa kupigania penzi la mshikaji huyo.

Katika kile ambacho kilionekana ni furaha kwa Gigy, hivi karibuni Idris aliibuka na kusema kuwa, yeye na Wema wameachana na vile walivyoonekana pamoja kwenye ile shoo ya Black Tie iliyofanyika kwenye Ukumbi wa King Solomoni, Upanga jijini Dar mwezi uliopita ilikuwa ‘kupritendi’ tu.

Katika kuonesha kuwa kweli amefunga ukurasa wa mapenzi na Wema, Idris alisema kuwa, siku si nyingi atamtangaza mpenzi wake mpya, jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu na wengi.

Baada ya Idris kutoa tamko hilo, siku chache baadaye alionekana akijiachia ‘kimalovee’ na Gigy ambapo alipoulizwa kama mwanadada huyo aliyefungashia kinoma ndiye aliyechukua nafasi ya Wema, hakuwa tayari kuongea lolote ila Gigy alipotafutwa alisema kuwa, sasa ni mwendo wa mahaba niue.

Akizungumza na chanzo hicho hivi karibuni, Gigy alisema kuwa, Wema amechemka katika suala la kumzalia Idris aliyekuwa na hamu ya kuitwa baba, sasa yeye atahakikisha ndani ya siku chache zijazo anabeba mimba.

“Nilisema kwamba ipo siku ndoto yangu itatimia, Mungu kaniona na sasa najitahidi sana nisichukue siku nyingi niwe nimembebea mimba Idris na kumzalia mtoto.

“Unajua mimi nikimpenda mtu bwana inakuwa ni shida na lazima nimfanyie kitu ambacho kitakuwa historia, naweza kusema nina jini mahaba ambaye ananisumbua hivyo mkiniona kitumbo ndii, mjue ndiyo vile…” alisema Gigy.

Kufuatia kujigamba huko kwa Gigy,chanzo kimoja kilimtafuta Idris na kumuuliza kama kweli amejiandaa kuzaa na msanii huyo ambapo kama kawaida yake alisema ni kweli wako karibu na ukaribu wao unatokana na kwamba wanafanya kazi pamoja katika Kituo cha Redio cha Choice FM ila hayo mengine hataki kuyazungumzia.

Ikumbukwe kwamba, hata wakati Idris anaingia kwenye uhusiano na Wema alikuwa mzito kukubali lakini baadaye Wema akaamua kuweka mambo hadharani kwani mwanadada huyo si mtu wa kuwa kwenye penzi la kificho.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts