Home » » Hamisa Mobetto Afunguka kuhusu Tetesi za Kutoka na Diamond

Hamisa Mobetto Afunguka kuhusu Tetesi za Kutoka na Diamond

Written By Vuvuzela on Tuesday, August 23, 2016 | 9:02:00 AM

Kwa muda sasa mlimbwende wa Tanzania, Hamisa Mobetto amekuwa akituhumiwa kutaka kumpindua Zari the Bosslady kwa Diamond Platnumz.

Skendo hizo zilivuma zaidi mwezi na kitu uliopita baada ya kudaiwa kuwa uwepo wa mrembo huyo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake Diamond kulitaka kusababisha timbwili kwakuwa Zari alikuwepo.


Na sasa Hamisa amefunguka kuwa yeye na Diamond hata hawajuani kihivyo!
“Hiyo sio kweli,” alisema Hamisa kwenye mahojiano na gazeti la The Citizen baada ya kuulizwa kuhusu tetesi hizo.

“Pia sijawahi kuwa karibu na Diamond na siku ya kwanza tumekutana ilikuwa ni siku anazindua video ya Number 1 pale Serena,” aliongeza. “Tena wakati hiyo habari imeanza kusambaa nilikuwa nje ya nchi.”
 
Habari hizo zilivuma zaidi wiki kama tatu zilizopita baada ya kuonekana picha ya Hamisa akiwa kwenye chumba kile kile Diamond alilala na Zari Afrika Kusini.

Diamond alilazimika kutolea ufafanuzi picha hizo kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM. Pia alielezea tetesi za kuwa na uhusiano na mrembo huyo.
 
“Hamisa nimeanza kumjua zamani sana na sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati alikuwa kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray Vanny na hiyo ndo imeleta maneno maneno yote hayo,” alisema Diamond.
 
Na kuhusu picha iliyounganishwa wote wakiwa wametumia chumba kimoja alisema, “Pale ni South Africa sehemu ile inaitwa Capital ni apartment ambazo vyumba vyake vyote vinafanana kama unavyoona hata Madam Rita pia ana share katika hizo apartment naye anayo yake na pia wabongo wengi tunapenda kufikia hapo kidogo huwa ni rahisi.”

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts