Get the latest updates from us for free

Home » » Hamisa Mobetto kuwania tuzo za Starqt za Sauzi

Hamisa Mobetto kuwania tuzo za Starqt za Sauzi

Written By Vuvuzela on Saturday, August 27, 2016 | 10:45:00 AM

Hamissa Mobetto ni staa pekee wa Tanzania aliyetajwa kuwania tuzo za Starqt zinazofanyika nchini Afrika Kusini. 
Mrembo huyo ametajwa kuwania vipengele viwili; Best Dressed Lady na People’s Choice Awards.
Hii ni mara ya tatu tuzo hizo zinatolewa na huwatunuku mastaa wa Afrika kwa kazi wanazozifanya katika sekta za muziki, filamu, mitindo, michezo na zingine.“Ni kitu kikubwa, somehow kinakuwa kama kinakutikisa kidogo hivi kiakili kwasababu ukiwa mtu pekee kutoka kwenye nchi yako na mwanamke na unakutana na watu wengine, lakini kila kitu kitakuwa kheri na tuzo itarudi nyumbani,”Alisema Hamisa
“Mimi ni Mtanzania pekee niliyepo kwenye hizo tuzo na nilichaguliwa na wao wenyewe wakaamua kuniweka kwa kuona ninafaa, kwasababu mnakutana na watu wa Kenya, South Africa, Uganda, na nchi nyingine mbalimbali. Kwahiyo kuwekwa tu pale inaonesha wanakuappreciate,” ameongeza.
Mrembo huyo amewaomba mashabiki wake kumpigia kura kwa kwenda kubonyeza link iliyopo kwenye bio yake ya Instagram.
Tuzo hizo zitatolewa September 10 nchini Afrika Kusini.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts