Home » » Harmonize achora tattoo nyingine tatu mpya, ikiwemo ya mama yake mzazi

Harmonize achora tattoo nyingine tatu mpya, ikiwemo ya mama yake mzazi

Written By Vuvuzela on Tuesday, August 23, 2016 | 6:11:00 PM

Msanii wa label ya WCB, Harmonize amefuta tattoo ya zamani ya Diamond na amechora tattoo nyingine tatu mpya ikiwemo ya bosi wake huyo pamoja na nyingine ya mama yake mzazi.

Mapema mwezi Januari mwaka huu msanii huyo aliamua kuchora tattoo ya picha ya Diamond na chini yake aliandika jina la Simba ambalo anatumia hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ kwa kudai kuwa bosi wake huyo ametoa mchango mkubwa sana kwenye maisha yake ya muziki ndio maana akaamua kufanya hivyo.
Picha ya tattoo za Harmonize za zamani

Harmonize amepost picha kwenye mtandao wake wa Instagram inayomuonyesha akiwa na michoro mipya kwenye mkono wake wa kulia akiwa amechora picha ya Diamond, mama yake mzazi pamoja na picha nyingine ya dini la Almasi.
Picha ya tattoo mpya za Harmonize
 
“Mama Rajabu & Simba @wasafistudios,” ameandika Harmonize kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.
Lakini baadhi ya mashabiki walio comment kwenye picha hiyo wamemtaka msanii huyo achore na tattoo nyingine ya baba yake kwa kuwa kumuweka mzazi mmoja pekee ni kama amefanya upendeleo.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts