Home » » Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana

Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana

Written By Vuvuzela on Thursday, August 25, 2016 | 8:42:00 AM

Leo(Jana)  nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na Sisi.
 
Miezi michache iliyopita nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa kura Million 6 wakazuia mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha hadi wafanyabiashara wanaotukodishia kumbi za mikutano.

CHADEMA chama chetu ni kikubwa sana , kinawatesa , tumewachapa kweli kweli uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi wanapata Tabu , wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni wapinzani.
 
Ni jambo la kufurahia na sababu ya sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.

Pili Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na wanajua sisi ni wamoja . Na nawasihi tuendelee kuwa wamoja hivi hivi, tusiruhusu vitisho vitutenganishe.. Hakuna nguvu kubwa kama ya Umma.
 
Uongozi ni dhamana na njia pekee njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama ilivyo sasa.

KUHUSU UKUTA .
Jambo hili la UKUTA ni kubwa mno si jambo dogo hata kidogo .Jana balozi wa Marekani aliwatumia ujumbe raia wake wajiandae kuondoka tarehe 1 September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu kama tusipotekeleza hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu kila jambo na kuvunja katiba .

Wasuluhishi wanasema tuzungumze , tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini ikiwa mtu anavunja Katiba na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa. 

Mtu mmoja anajiamulia kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya ndani na wasuluhishi hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze yeye kwanza matendo yake .

POLISI niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi kabisa , police wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri tutagoambana nao mmoja mmoja, hatutahangaika na jeshi tutahangaika Na Polisi aliefanya mauaji, alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC . 

Ni bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
 
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.

Tabia za baadhi ya viongozi ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee Tanzania hata kidogo. Zipo jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue jambo tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na haki za kidemokrasia .

Tujitokeze kwa wingi sana September 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama tulivyofanya wakati Wa kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni bila hofu .

Tuna chama Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi , maendeleo na ustawi wa nchi . Tunawapenda sana, ninawapenda Na Ahsanteni.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts