Home » » Huyu ndiye Mwanaume Alijitokeza na Kudai kuwa Ameporwa Demu na Nuhu Mziwanda

Huyu ndiye Mwanaume Alijitokeza na Kudai kuwa Ameporwa Demu na Nuhu Mziwanda

Written By Vuvuzela on Wednesday, August 10, 2016 | 9:24:00 AM

Ubuyu wa mjini unanyetisha kuwa, mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Jike Shupa aliomshirikisha Ali Kiba, Natfal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, anadaiwa kupora demu wa jamaa ambaye naye ni msanii wa wa Bongo Fleva, Valentino Michael ‘Vale wel’.

Mrembo anayedaiwa kuporwa kwa Vale ni yule Nawali ambaye kwa sasa Nuh anamnadi kuwa ni mpenzi wake wa kiyama.


Ubuyu ulionaswa na chanzo chetu ulidadavua kuwa mwenye demu wake alipigwa na butwaa alipomuona Nuh akimnadi Nawali kwenye mitandao ya kijamii ndipo akang’atwa sikio kuwa kwa sasa hana chake kwani ‘mtoto’ yupo mikononi mwa Nuh.


Akimwaga chozi mbele ya chanzo cha uhakika, Vale alisema kuwa mpaka sasa hajaelewa ni kwa nini Nuh ameamua kumtangaza Nawali kuwa ni mpenzi wake wakati akijua wazi kwamba ni shemeji yake na ni mwanamke wake wa siku nyingi kwani wanafahamiana.


“Kiukweli nilikuwa sijui hili wala lile. Nilipoingia mitandaoni nilipigwa na butwaa kumuona Nuh akijitangazia ufalme kuwa mpenzi wake kwa sasa ni Nawali.
“Mwanzoni nilijua labda ni mambo ya kiki kwa sababu nijuavyo Nuh hana malengo mazuri na Nawali.

“Baadaye ndipo nikawa nahakikishiwa na watu wangu wa karibu kuwa ni wapenzi na hawafanyi kificho.
“Kinachoniumiza nilikuwa sina tatizo wala ugomvi wowote na Nawali na bado naamini ni mpenzi wangu kwa sababu hatujaachana na tukikutana huwa tuko kama kawaida,” alisema Vale.

Vale alizidi kutokwa povu kuwa kwa sasa hasemi sana kwa sababu hana mkwanja wa kumpa Nawali hivyo ule usemi wa mwenye kisu kikali unamtafuna kwani inawezekana Nuh anatumia vijisenti alivyonavyo kumnyang’anya tonge mdomoni.

“Lakini ukweli ni kwamba ‘nafaiti’ na mambo yatakaponinyookea nitahakikisha nafanya kila njia kumrudisha Nawali kwenye himaya yangu kwani ndiye mwanamke wa maisha yangu.

“Najua nilipomtoa, ni mwanamke ambaye ninampenda sana na nimetumia muda mwingi kumbadilisha kimuonekano kwani mwanzoni hakuwa alivyo sasa, alikuwa mgumu hivyo nimefanya jitihada za hali ya juu kumfanya aonekane ‘soft’,” alimalizia Vale.
Baada ya ubuyu huo ulionyooka kutua kwenye chanzo chetu, waandishi wetu walimweka ‘mtukati’ Nuh aliyedai kuwa hapendi kumuongelea mpenzi wake huyo kwa sababu kama ni maneno yameshasemwa mengi.

“Unajua kuhusu huyu demu wangu, maneno mengi sana yamesemwa hadi nimechoka. Kama huyo mwanaume yupo na anaamini ni mwanamke wake basi amchukue akakae naye,”
alisema Nuh akiomba kuachwa atulize mawazo.


Kwa upande wake Nawali, alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hamjui Vale na wala hajawahi kupiga naye picha za kimahaba.

Habari kutoka kwa Wana-Ubuyu wanaolinyaka vilivyo sakata hilo wanadai kwamba Vale ana uhakika kuwa huyo ni mpenzi wake na picha ametoa wakiwa wawili tena kimahaba hivyo inakuwaje Nawali anabisha?

Mbali na Nawali, baada ya kufungishiwa virago na Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Nuh alitua kwa mrembo mwingine shombeshombe ambaye hata hivyo hawakudumu

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts