Home » » Kiba Adaiwa Kutapeli Wakenya.

Kiba Adaiwa Kutapeli Wakenya.

Written By Vuvuzela on Thursday, August 11, 2016 | 7:25:00 AM

Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ anadaiwa kuwatapeli Wakenya baada ya kupewa Sh. Milioni 33 kwa ajili ya kushirikishwa kwenye wimbo kisha kuingia mitini, hali iliyosababisha shahidi wake, Rajabu Salum ‘Mchafu’ kutaitiwa, Risasi Mchanganyiko lina full data.

Kwa mujibu wa Mchafu ambaye ni meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda na Billnas, alipigiwa simu na Wakenya hao kumuomba awaunganishe na Ali Kiba.


“Mmoja kati ya Wakenya hao ni mwanamuziki ambaye anaitwa Brown Mauzo, lengo lao kubwa lilikuwa ni Brown kufanya kolabo na Ali, hivyo nikawasiliana naye akakubali kwa sharti la kulipwa dola elfu 15 (zaidi ya milioni 30 za Kibongo).


“Walikuja Bongo, tukakutana nao Mlimani City, nikiwa shahidi wa Ali na wao walikuwa na wanasheria wawili. Wakaingia benki ili kutoa kiasi cha Sh. milioni 10 lakini wakaniomba wasitoe kwanza na kwamba nikabadilishe mkataba kwa kiasi hicho cha pesa watakachoanza nacho maana awali makubaliano ilikuwa ni kiasi hicho cha pesa (shilingi mil. 32) kwa ajili ya video, malazi na makazi.”


“Upande wa video, Ali alitaka dairekta asiwe Mbongo, hivyo tukampata Justin Campos wa Sauz. Kwa upande wa audio, Brown alimhitaji Prodyuza Manecky lakini Ali napo alikataa na kumtaka prodyuza wake ambaye ni Aby Daddy wa Chaiderz Records, hivyo akataka iongezwe tena shilingi milioni moja kumlipa prodyuza huyo, jamaa wakamaindi na kuondoka bila dili kufanyika.


 “Ali akaniambia nikaongee nao kwani hela ya prodyuza lazima ilipwe. Basi nikawafuata hotelini kuongea nao vizuri, tukaelewana wakapanga tuonane usiku, tukasaini na kumkabidhi Ali milioni 20 huku kesho yake wakiahidi kumalizia milioni 13 ili jumla iwe 33.


“Kesho yake, tukakutana studio kwa Aby, wakarekodi na kurudi nchini kwao kusubiri ikamilike. Baada ya siku chache jamaa wakawa wanahitaji wimbo wao.


“Wakatumiwa lakini hawakuridhika wakidai ulitengenezwa chini ya kiwango na haukuwa na ubora. Wakaja Bongo na kushauri ukaboreshwe kwa Man Water (Combination Sound), tukachukua mafaili ya wimbo huo kutoka kwa Aby hadi kwa Man Water.


Kufika huko, Man Walter akashauri irekodiwe upya, naye akahitaji hela nyingine. Ikabidi niwasiliane na bosi wa Brown, Kenya akatuma kiasi kingine cha shilingi milioni moja na nusu, Brown akaingiza tena sauti ikabaki kwa Ali.


“Kila akitafutwa Ali alikuwa akikwepa, akipigiwa simu ikawa hapokei. Siku alipopatikana akadai hawezi kuingiza mara ya pili.


Baadaye katika kupeleleza, tukaja kugundua kumbe Aby alipewa shilingi laki moja na nusu badala ya milioni moja. Aliposikia kwamba Ali amepewa pesa nyingi na yeye amepewa kiduchu, akapoteza morali ya kazi. Tulibishana sana lakini mwishowe, akakubali akaingiza.


“Baada ya kumaliza audio kibishi, jamaa wakawa wanahitaji namba ya pasipoti ya Ali na meneja wake ili wafanye michakato ya kusafirishwa kwenda kutengeneza hiyo video.


“Ikawa kila tukimfuatilia Ali tunaambiwa mara yupo Sauz na Barakah The Prince, mara amerudi yupo kwenye shoo za Bongo, tukimpigia simu anatupiga chenga, hapokei,” alisema Mchafu.

Imeelezwa kuwa, baadaye mabosi hao wa Kenya walipoona mambo hayaeleweki, walimkamata Mchafu kwa muda kama mmoja wa waliosaini mkataba na kwamba baada ya kuongea na Ali,aliwataka wamlipe fedha aliyofanya wimbo kwa mara ya pili na Man Water, baadaye wakamuachia.

Hata hivyo, Mchafu baada ya kusikika kwenye moja ya redio Bongo akilalamika kwa aliyotendewa, Ali alimpigia simu na kumlaumu sana, baadaye akamwambia amekubali kutengeneza video hiyo ambapo Agosti 10, mwaka huu (leo), wanatarajiwa kusafiri kwenda ‘kushoot’ Sauz.

Baada ya madai hayo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Prodyuza Aby kutaka kujua kama kuna ukweli ambapo alifunguka;

“Kwa sasa sitaki kuongelea kabisa habari hizo ila ninachoweza kusema ni kwamba Wakenya hao walikuja kuchukua mafaili ya wimbo na kupeleka kwa Man Water.”

Baada ya kumsaka Kiba bila mafanikio, tulimtafuta meneja wa msanii huyo, Seven Mosha ambaye alisema habari hizo hazina ukweli wowote.

“Ni uzushi tu huo, hakuna kitu kama hicho,” alisema Seven kwa kifupi na kuondoka hewani.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts