Home » » Mzee Yusuph aamua kumrudia Mungu na kuachana na Muziki

Mzee Yusuph aamua kumrudia Mungu na kuachana na Muziki

Written By Vuvuzela on Saturday, August 13, 2016 | 4:55:00 PM

Mfalme wa muziki wa taarabu mzee Yusuph maarufu kama "mfalme wa taarabu" amefunguka na kusema kuwa sasa ameamua kuachana na muziki huo na kumrudia Mungu huku akiwataka watanzania pia kumrudia Mungu.

Akiongea jana baada ya kumaliza swala ya Ijumaa kweneye msikiti wa Ilala Bungoni (Masjdi Taqwa) Mzee Yusuph alisema kwa taarifa za awali watanzania wanatakiwa kutambua kuwa yeye ameachana na muziki na sasa amemrudia Mungu na kuwataka kuwa na subira kwani atatafuta siku maalum yeye kutangaza suala hilo ambapo atafunguka kwa kirefu zaidi kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo.

"Ni kweli nimeamua kuachana na muziki na sasa nimemrudia Mungu, nawaomba watanzania wengine pia wamrudie Mungu, nitatafuta siku ambayo nitaongea kwa kirefu zaidi juu ya suala hili, hivyo watanzania watambue tu nimeachana na muziki sasa" alisema Mzee Yusuph.

Hii ni mara ya pili kwa mzee Yusuph kutangaza kuacha muziki kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka jana, alitangaza kuacha muziki na kuingia kwenye siasa lakini hakuweza kufanya vizuri kwenye siasa na kurudi tena kwenye muziki.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts