Home » » Nuh Mziwanda Akodi Bodigadi ili kukabiliana na Shilole

Nuh Mziwanda Akodi Bodigadi ili kukabiliana na Shilole

Written By Vuvuzela on Tuesday, August 2, 2016 | 10:23:00 AM

KUFUATIA kuwepo madai kuwa msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda kutishiwa kupewa kichapo na mijemba inayodaiwa ilitumwa na aliyekuwa mpenzi wake Shilole, hatimaye  Nuh aamua kukodi bodigadi wa kumlinda.

Nuh alionekana akiwa na bodigadi huyo kwenye Tamasha la Mwendokasi lililofanyika Viwanja vya Posta jijini Dar hivi karibuni jambo lililozua minong’ono kwa baadhi ya mashabiki wake.

Katika tamasha hilo burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Barnaba, Isha Mashauzi, Juma Nature, Rich One, Man Fongo, G. Nako, Lord Eyes, Navy Kenzo, Snura, Nay wa Mitego ziliwapagawisha mashabiki.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts