Home » » Picha Inayowaonyesha AliKiba na Diamond Wakishikana Mikono Yawatoa Povu Mashabiki

Picha Inayowaonyesha AliKiba na Diamond Wakishikana Mikono Yawatoa Povu Mashabiki

Written By Vuvuzela on Thursday, August 11, 2016 | 5:06:00 PM

Katika mitandao ya kijamii Jumatato hii kumezuka mjadala mkubwa baada ya mashabiki wa Diamond Platnumz na AliKiba kuona picha yakutengenezwa inayowaonyesha wawili hao wakipeana mkono.
Wachache kati ya mashabiki hao wanaamini picha hiyo ni yakutengenezwa huku wengi wao wanaamini wawili hao kweli wamepatana.

Pia miongoni mwa mashabiki hao waamini endapo wawili hao watapana basi na muziki wao utashuka kutokana na kupoteza ushindani.

Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao kutoka katika mitandao ya kijamii.
Francis Michael
Tukubali kuwa hakuna jambo lisilokuwa na mwisho kwa upendo wao wenyewe wameona tukiendelea hivi mpaka lini tutamaliza tofauti zetu kwa kuwa wasanii hawa wote wanapeperusha bendela yetu ya TZ, Nimefurahi sana kusikia hivi tofauti zao zimekwisha nawaomba kama kweli umekwisha wafanye kolabo yao wasanii hawa wawili watuchezeshe sasa turuke.

Glory Shayo
Haitawezekana kamwe coz Diamond ana wivu na nyimbo za King Kibaa hiyo itabaki tu story.

Joseph Salvatory
Haitatokea kumaliza tofauti zao hadi Diamond arudishe ile kolabo aliyo mshilikisha Kiba na Kiba kumfunika Diamond, kwa roho mbaya ya Diamond akaifuta.

Veronica Godluck
Elewa kwamba kuna maisha mengine baada ya muziki, na uwezi jua mungu amepanga nini juu yako, so haina haja ya mabifu chamsingi kila mtu awangalie mashabiki wake wanataka nini. Kumake money ndio kila kitu.

Albert Kariuki Tz
Binafsi nita jihisi vibaya kwa kuwa ule ushindani hautakuwepo na muziki yao ni kama vile ita chuja.

Juma Masifia
Umesema ukweli wote coz kama hawa mastari wangekuwa wana bifu lazima serikali au baraza lao lingeingilia kati na kupelekana mahakamani siyo daily tunasikia mambo tofauti mengi kwenye media na midomo ya watu kumbe hakuna chochote isipokuwa ushabiki wa watu na media

Haruna Hamisi
Kama wakiungana muziki nao utakuwa umekwisha kwa Diamond & Ally Kiba kwakuwa sasa hivi upinzani wa wasanii hao tu ni gumzo unafanya kuwapa mafanikio makubwa sana kiukweli sasa hivi muziki wa bongo fleva, kwenye soko wameliteka Diamond & Ali Kiba, yaani tunawaangalia wao tu Kiba katoa nini na Mond katoa nn? Sasa wakiungana muziki kwao hakuna tena, kwa hiyo bifu linachangia muziki kwenda mbal

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts