Home » » Romy Jones ‘DJ RJ’ aibuka na kueleza kilichomfanya Diamond Asihudhurie kwenye Birthday yake

Romy Jones ‘DJ RJ’ aibuka na kueleza kilichomfanya Diamond Asihudhurie kwenye Birthday yake

Written By Vuvuzela on Friday, August 26, 2016 | 8:45:00 AM

BAADA ya hivi karibuni ndugu wa Mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuhudhuriwa na mastaa kibao isipokuwa msanii huyo na kudaiwa kuwa wana bifu, Romy Jones ‘DJ RJ’ ameibuka na kueleza kilichotokea.

Tetesi zilizagaa kwamba Diamond na Romy wana bifu ndiyo maana hakuonekana kwenye sherehe hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Next Door jijini Dar huku mastaa kama AY, Wema Sepetu na wengine wengi wakihudhuria ambapo Romy ameibuka na kueleza kuwa Diamond alikuwa na projekti muhimu studio ndiyo maana hakuonekana.

“Diamond ni ndugu yangu hatuwezi kugombana na mama zetu bado wako hai, wangekuwa hawapo labda hapo tungeweza kugombana. Sababu ya yeye kutohudhuria kwenye sherehe yangu ni kwamba alikuwa na projekti muhimu sana studio siku hiyo na ilipofika saa kumi usiku akataka aje nikamwambia asije ndiyo tunamalizia. Kifupi hatuna bifu kama watu wanavyosema, tuko vizuri kabisa,” alisema Romy.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts