Home » » Video:Diamond afunguka kuwa album yake ijayo itakuwa ya kimataifa.

Video:Diamond afunguka kuwa album yake ijayo itakuwa ya kimataifa.

Written By Vuvuzela on Sunday, August 28, 2016 | 1:42:00 PM

Hivi karibuni, Diamond Platnumz alieleza kuwa album yake ijayo itakuwa ya kimataifa. Na sasa amefafanua zaidi kwanini itakuwa na hadhi hiyo kupitia interview aliyofanya Ijumaa hii na Radio Maisha ya Kenya.

“Mwanzo nilikuwa natoa album lakini nilikuwa nafocus tu Tanzania nikaja nikafocus na East Africa so hapa katikati nilikuwa napigania soko la kidunia. So baada ya kufanya nyimbo za kidunia, nikimaanisha kwamba kushirikisha baadhi ya watu, sababu ukisema album yako yote iwe nyumbani Tanzania inakuwa imekaa kiselfish so lazima ufanye na watu wan chi tofauti tofauti, Kenya, Nigeria, South Africa unachukua Uganda kidogo, kutoka hapo unafanya na America, unafanya na Europe. Hata production pia, producers sometimes unachanganya na videographer hiyo inakuwa ni international album kwasababu kila nchi mtu ataona ni album yao,” alisisitiza.

Pia alidai kuwa imemchukua muda kuachia album yake ili kuweza kulisoma soko la dunia na kwamba cha kwanza alichokifanya ni kuhakikisha mfumo wa kuuza kidijitali wameuweka vyema.Wikiendi hii staa huyo anatumbuiza mjini Meru.


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts