Home » » Mtangazaji wa Channel 10, Cassius Mdami afariki dunia

Mtangazaji wa Channel 10, Cassius Mdami afariki dunia

Written By Vuvuzela on Thursday, September 22, 2016 | 3:18:00 PM

Mtangazaji wa kituo cha runinga cha Channel 10, Cassius Mdami amefariki dunia Jumatano hii mchana katika hospitali ya Mazimbu mkoani Morogoro.

Cassius aliugua ghafla kabla ya kufariki mkoani humo ambapo alikuwa kwenye mapumziko yake mafupi mjini humo ambapo ndipo yalipokuwa makazi yake ya muda mrefu.

Mwandishi huyo enzi za uhai wake amefanikiwa kuipata heshima kubwa kituo chake cha runinga cha Channel 10 kupitia kipindi chake cha Utalii Tanzania ambacho kilifanikiwa kupata tuzo kadhaa kutokana na uhamasishaji wake kwenye sekta hiyo ya utalii.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi majira ya saa tisa nyumbani kwake mkoani Morogoro. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Cassius Mdami mahali pema peponi. Amina.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts