Get the latest updates from us for free

Home » » Mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360,Hudson Stanley Kamoga, ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya

Mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360,Hudson Stanley Kamoga, ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Wilaya

Written By Vuvuzela on Sunday, September 11, 2016 | 12:40:00 PM

Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.

Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa.

Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;-

 1. Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
 2. Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
 3. Yusuf Daudi Semuguruka – Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
 4. Bakari Kasinyo Mohamed – Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
 5. Juma Ally Mnwele – Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
 6. Butamo Nuru Ndalahwa – Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
 7. Waziri Mourice – Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
 8. Fatma Omar Latu    – Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
 9. Godwin Emmanuel Kunambi – Manispaa ya Dodoma
 10. Elias R. Ntiruhungwa – Mji wa Tarime
 11. Mwantumu Dau – Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
 12. Frank Bahati – Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts