Home » , » RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 13 & 14

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 13 & 14

Written By Vuvuzela on Saturday, September 24, 2016 | 1:19:00 PM

MUANDISHI : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA....
“Meneja hizo pesa nitoe za benki au zako binafsi?”
“Toa za benki mtu akikuuliza, muambia aje kwangu”
Bwana Turma akiwa anasubiria zoezi la kufungiliwa akauti, gafla milio mingi ya risasi ikaanza kusikika ikitokea nje na kuanza kuwachanganya bwana Turma na muhasibu wake


ENDELEA......
Kitendo cha wasichana, makatili kuiingilia bank ya CNB, na kuwazalilisha wananchi walio kuwemo ndani ya benki kwa kuwatoa nje uchi kinazidi kuiumiza serrikali.Isitoshe inamuwia ugumu Bwana Turma, na akashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano maalumu kwani gari lake la thamani, limehusika katika matumizi ya uvamizi wa Benki.
                                                                                             
Dickson anatoa nje ya kibanda chake, huku akiwa na wasiwasi mwingi akiwatazama askari wawili wanaokuja kwenye kibanda chake
“Habari yako kaka?”
Askari mmoja alimsalimia Dickson
“Salama tuu mambo vipi?”

Dickson alizungumza kwa kujikaza tuu, kuuficha wasiwasi wake kwa maana msichana ambaye ni Rahab aliye muacha ndani anaonekana hana masihara kabisa katika matumizi ya silaha

“Hukuona, msichana aliye vaa akipita katika maeneo haya?”
“Ahaaa kusema kweli, sijamuona kwa maana hizi bunduki kwa jinsi zilivyokuwa zikinguruma huko nje sikudhubutu hata kuitoa miguu yangu”

Askari wakamtzama kwa umakini Dickson, ambaye anazungumza kwa kubabaika
“ Basi tunakuomba ufunge duka lako”
“Sawa”
Askari wakaanza kuondoka na kurudi katika eneo walipo wazao, Dickson akarudi ndani huku jasho jingi lkimwagika mithili ya maji.
“Waameniambia nifunge” 

Dickson alimsemesha Rahab ambaye kichwa chake amekiinamisha kwenye ukuta huku sura yake ikitazama juu.
“Dada, dada.Wamesema nifunge duka langu”
Rahab hakujibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya, huku akimtazama Dickson jinsi sura yake inavyo mwaga jasho jingi
“Powa”
Rahab alijibu kwa kifupi, na kuzidi kumchanganya Dickson
“U...takaa humu ndani?”
“Ndio wewe funga”
“Mmmm”

Dickson akabaki akiwa anashangaa  shangaa, Rahab akainyanyua bastola yake na kumuwekea Dickson ya kichwa, mwili mzima wa Dickson ukawa kama umepigwa na shoti ya umeme, taratibu suruali yake ikaanza kutengeneza mchoro sehemua ya zipu, kwani woga umemfanya hadi ameshindwa kuzuia haja ndogo
“Huwa sipendi, nizungumze mara mbili mbili.Potea”

Rahab alizungumza huku sura yake akiwa ameikunja, na anaonekana kuwa na hasira kali.Kwa hahara Dickson akatoka nje ya kibanda chake, na kuaanza kufunga geti la kaduka kake hata baiskeli anazo zitengeneza hakukumbuka kuziingiza ndani.Kwa kuchanganyikiwa akajikuta akitembea asijue ni wapi anaelekea
                                                                                                             
Wote wanne wakiwa na bunduki zao mikononi, wakawa wanaitazama njia ambayo ni yakuingilia kwenye eneo lao la handaki.
“Tutawanyike wawili wawili”

Fetty alizungumza huku akiikoki bunduki yake, Anna akamfwata Fetty huku Halima na Agnes wakiwa wamesimama sehemu moja.Wakatazamana kwa muda pasipo mtu yoyote kuzungumza neno , kisha wakaanza kukimbia mtuni, wakiwa wameganawana kila watu wawili sehemu yao.Fetty na Anna walielekea magharibi mwa msitu wao, huku Agnes na Halima wakielekea Mashariki mwa msitu wao.

Askari wakiongozwa na mbwa wao, walio fundishwa mafunzo maalumu ya kunusa kila sehemu ambayo amepita mtu ambaye askari wanamuhitaji, ndivyo walizidi kuendelea kuingia msituni wakiwa na bunduki zao.Huku kila mmoja akiwa na hasira kali juu, ya maauaji yaliyo tokea siku chache zilizo pita juu ya wezao walio uwawa kwenye kituo cha gesi kwa mlipuko mkali.Amri mmoja iliyo tolewa na mkuu wa jeshi la polisi Bwana Gudluck Nyangoi ni kwamba wahakikishe wanawatia nguvuni ili wahukumiwe kifungo kikali kitakacho ishangaza dunia

Askari wakiongozwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Ngurumo, wanaendelea kuuzingira msitu huku wakiwa na imani ya kufanikiwa na abushi yao wanayo kwenda kuifanya kwenye msitu unao sadikika ndipo walipo ingia majambazi kipindi wakitokea kufanya tukioa benki, na maelezo haya yalitolewa na msamaria mwema ambaye, gari lao lilisimamisha kipindi askari wa usalama barabarani walipokuwa wakifanya uchunguzi kwa kila gari ambalo lilikuwa likikatiza katika barabara kuu ya kuelekea mikoa ya Tanga na Arusha

Wakiwa katikati ya msitu, mbwa wao wakaanza kubweka kwa sauti ya juu, na kuzidi kuwastua askari na kuamini kuna jamba ambalo lipo kwenye eneo ambalo wamefika.
“Waachie mbwa”

ACP Ngurumo aliwaamrisha askari sita walio washika mbwa wao, Mbwa wakaanza kuelekea katika maeneo walipo Fetty na Anna, ambao bunduki zao wameziweka tayari kwa kila kitu. Kwa kutumia bunduki zao zenye lensi ya kuvuta mtu kwa ukaribu sana, Fetty akawashuhudia mbwa wakiwakaribia katika eneo walilo jificha huku kwa nyuma kukiwa na kundi la askari wapatao sita, wakiwa na bunduki mikononi mwao.Anna akaishika bunduki yake, kabla hajafyatu risasi Fetty akamzuia
“Ngoja nikuonyeshe mchezo, wasikumalizie risasi zako”
Fetty alizungumza huku akikichomo kisu chake, kikali na kirefu sana mfukoni,
“Anna nilinde”
“Powa”

Fetty akaanza kutambaa kwa haraka kuuelekea mbwa wanapo tokea na na askari wao, akajibanza kwenye mti mkubwa ambao ndio njia ambayo mbwa na askari ndio wanatokea, Macho ya Anna yakawa na kazi ya kuwatazama askari wanao kimbia kwa kasi wakiwa nyuma ya mbwa wao, Fetty akachomoa kisu kingine kinacho fanana na kisu alicho kishika mkono wake wa kulia, Akashusha pumzi kidogo kisha akachungulia kidogo sehemu wanapo tokea mbwa na kuwaona wakiwa wamebakisha hatua chache kutoa sehemu alipo jificha
“It’s My time now”(ni wakati wangu sasa)

Fetty alizungumza huku akishusha pumzi nyingi, kwa haraka akachuchumaa chini, kitendo cha mbwa wa kwanza kujitokeza sura yake usawa wa Fetty, ikawa ndio muda wa mbwa huyo mwenye kasi kupita wezake, kukumbana na kisu cha koo na kumfanya kutoa ukelele mmoja tuu, mithili ya panya aliye banwa na kitu kizito na kutulia kimya.Akaskari wakasimama baada ya kuona mbwa wa kwanza akiwa amepotea gafla, kasi ya mbwa wengine watano ikaanza kupungua na kuwa ya kusita sita baada ya kumuona mwenzao akiwa ametupwa katika njia waliyo kusudia kupita, huku akiwatokwa na damu nyingi.

Askari kwa kuchanganyikiwa wakaanza kufyatua risasi pasipo kuwa na mpangilio maalumu, kwani hawakujua ni wapi alipo jifich mtu aliye sababisha kifo cha mbwa huyo, ambaye anaaminika sana kupita mbwa wote.Fetty akaachia tabasamu pana, huku akiwa amejibanza kwenye mti aliopo wenye unene kiasi, unao msaidia kutokuweza kuonekana, wala risasi kumfikia alipo.

“Nyinyi kuna kitu gani kinacho enelea huko.OVER”
Sauti ya Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) bwana Ngorumo ilisikika kupitia simu ya upepo, hii ni baada ya kusikia milio ya risasi nyingi zikimiminika.
“Wapo, huku mkuu, Over”
Askari mmoja alizuingumza huku akiendelea kufyatua fyatua risasi ovyo
“Tunakuja, Over”

Macho ya Anna yakakutanana na macho ya Fetty ambaye, akaendelea kumkonyeza asifanye kitu chochote cha kijinga.Anna akazidi kupatwa na wasiwasi kwani akujua ni kitu gani kinachompa ujasiri Fetty kuendelea kung’ang’ania nyuma ya mti alio uegemea

Fetty akatupa visu vyake chini na kuchomoa bastola mbili kwenye viatu vyake, ambazo zimejaa risasi za kutosha, kwa ishara ya mmdomo pasipo kuzungumza kwa sautia, Anna akamtaarifu Fetty kwamba askari wameongezeka katika eneo walilopo.Askari walioongezeka kwenye eneo walipo wezao, bila hata ya kuuliza ni wapi walipo majambazi, wao wakaanza kufyatua risasi zao wakishambulia kile eneo

“Zima motoo”
ACP Ngurumo alizungumza kwa sauti ya juu, baada ya kuona risasi zao zikiendelea kumiminika pasipo kuwa na mafanikio yoyote ya kuua majambazi
“AK47 tangulia mbele”

Aliwaamrisha askari wenyebunduki aina ya AK47 kupita mbele, huku wengine wanye bunduki aina ya SMG wakiwa wamebaki nyuma ya wezao huku wamelala chini.Askari wapatao nane wenye bunduki aina za AK47, wakaanza kutembea kwa kunyata wakielekea ulipo mti ambao pembeni kuna mbwa wao aliye lala chini, tayari akiwa amekata roho.

Kwa kutumia ishara ya vidole Fetty akaanza kunyanyua kimoja, kikafwata cha pili, hadi cha tatu anakinyanyua, Anna akaanza kufyatua risasi mfululizo kwa askari wote nane wenye bunduki aina ya AK47, na hakuna hata mmoja aliye baki akiwa amesimama kwani, risasi zote alizo zifyatua kwa kutumi bunduki yake aina ya ‘M8AI’, zilitua vichwani mwa askari hao.

Askari walio lala chini wakaanza kuchanganyikiwa kwa shambulizi walilo fanyiwa wezao, wakaanza kufyatua risasi kuelekea sehemu yenye jiwe kubwa alipo lala Anna, na kusahau kuuangalia mti ambao askari nane walio uwawa walikuwa wakinyata,Fetty kwa kutumia bastola zake mbili, moja ikiwa aina ya ‘COLT 1911’ huku nyingine aina ya ‘DESERT EAGLE’ akaanza kuwashambulia askari kwa nyuma, walio kuwa wameelekea upande alipo jificha Anna.Kila mmoja akaanza kuchanganyikiwa kwani kila alipojaribu kufyatua risasi walipo majambazi ndivyo alivyo jikuta akianguka chini na kupoteza maisha yake hapo hapo.

Hadi shambulizi linazima, akabaki Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Ngurumo akiwa amelala chini akiwashuhudia maiti za askari wake wakiwa wamelala chini, wakivunjwa na damu nyingi mwili mzima.Fetty akapiga hatua za umakini hadi sehemu alipo lalaa ACP Ngurumo, na kumuwekea risasi ya kichwa
“Fetty”

Anna aliita kwa sauti ya juu, na kumfanya Fetty kutazama sehemu alipo Anna na kumuona akiwa amesimama huku akiwa anavujwa na damu za paja lake la kushoto, ikiashiria katika risasi zote zilizo fyatuliwa na askari hao kuna iliyo mpiga kwenye mguu wake

Agnes na Halima waliendelea kuzisikia kelele za risasi nyingi, ila hawakudhubutu kunyanyuka sehemu walipo kwenda kwani hawakujua ni wapi risasi hizo zinapo tokea.Kila wanapojaribu kutazama sehemu zote za msitu wanaona ukimya mwingi baada ya risasi nyingi zilizo fyatuliwa zaidi ya nusu saa

“Mbona mapigo yangu ya moyo yanakwenda kasi”
Halima alizungumza huku akinyanyua kichwa chake akitazama mbele yao, pasipo kuona kitu chochote
”Acha uoga chost” Agnes alijibu
“Sio woga, ila mapigo yanakwenda mbio, haijawahi kutokea siku hata moja”
“Hembu ngoj.......”

“WEKENI SALAHA ZETU CHINI, WANAHARAMU NYINYI”
Kabla hata Agnes hajamalizia sentesi yake sauti ya ukali ikawamrisha nyuma yao, wakageuka kwa haraka na kukutana na kundi la askari wapatao kumi wenye bunduki mikononi mwao, huku bunduki zao zote zikwa zimeelekea upande wao, na sura za askari hawa zimejaa mikunjano inayo ashiria hasira kali walizo nazo....


           SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……14

.....Taratibu Halima na Agnes wakaweka silaha zao chini, kila mmoja akanyoosha mikono juu, kutokana na amri waliyo pewa na askari hao wenye hasira kali kupita maelezo.Askari wawili wakawasogelea Agnes na Halima na kuwafunga pingu, za mikononi

Katika maisha yao Halima na Agnes hawakutarajia kama ipo siku watakuja kukamatwa kizembe kama hivi walivyo kamatwa.Askari wakamchukua Halima na Agnes na kuwapeleka kwenye magari yao walipo yaacha, huku wakijawa na furaha sana, juu ya kuwakama wasichana makatili walio itingisha nchi kiasi kwamba viongozi wa ngazi za juu kila mmoja alihisi kuchanganyikiwa kwa matukio makubwa yaliyo tokea katika wiki mmoja mfululizo.Moja likiwa ni tukio la askari wengi kuuawa katika kituo cha gesi huku benki ya biashara kuvamiwa na pesa nyingi kuuawa
                                                                                                
Hasira nyingi ikazidi kumpanda Fetty, baada ya kumuona Anna akivujwa na damu kwenye paja lake, Fetty akaishika vizuri bastola yake na kunyanyua kwa nguvu (ACP) Ngurumo na kumpiga kabali kwa nyuma

“Unaona washenzi wako walicho kifanya kwa rafiki yangu”
Fetty alizungumza huku akiendelea kuishika bastola yake akiikandamiza kichwani mwa ACP Ngurumo, ambaye mwili mzima unamtetemeka kwa woga, japo amefanya kazi kwa kipindi kirefu ila hajawahi kukutana na wanawake makatili kama Fetty na Anna.Anna taratibu akaanza kujikongoja hadi sehemu walipo simama Fetty na ACP Ngurumo
“Chukua mkanda ujifunge kwenye paja damu zisiendelee kukumwagika” 

Fetty alimuambia Anna naye akafanya kama alivyo ambiwa, akauchomo amkanda mmoja wa askari aliye fariki na kuufunga kwenye paja, akiwa anaendelea kujifunga simu ya upepo ya ACP Ngurumo ikaanza kukoroma ikiashiria kuna simu inaanza kuingia
“Ipokee, na ole wako uropoke nauchangua ubongo wako”
Fetty alizungumza huku akiichomoa simu ya upepo ya ACP Ngrurumo aliyo ichomeka kiunoni
“115 Kikosi, OVER”

Sauti kutoka upande wa pili kwenye simu ya upepo ilisikika
“Ninakusikia Over” ACP Ngurumo alijibu
“Mkuu tumewakamata majambazi wawili, Over”
ACP Ngurumo akanyamaza kimya, huku akiwatazama Anna na Fetty, ambao wanaonekana kustushwa na taarifa ya wezao kukamatwa
“Waulize wapo wapi?”
Fetty alizungumza kwa sauti ya chini sana, ambayo si rahisi kwa mtu aliyepo upande wa pili wa simu kuweza kuisikia

“Mupo wapi. Over?”
“Tupo kwenye point B, Over”
“Nimewapa” Simu ya upepe ikakatwa
“Ongoza njia hadi kwenye point B yenu”
“Fetty, mimi sinto weza kwenda mbele”
Anna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga kwani maumivu anayo yapata ni makali sana kupita maelezo
“Jikaze mpenzi”
“Siwezi Fetty, amini kwa kitu ninacho kuambia”

Fetty akamtazama ACP Ngurumo kwa macho makali, gafla Fetty akafyatua risasi moja iliyo tua kwenye paja la ACP Ngurumo na kumfanya atoe ukelele mkali ulioambata na kilio cha maumivu na kuanguka chini, Fetty akataka kufyatua risasi nyingine kwenye mwili wa ACP Ngurumo ila Anna akamkataza
“Usimuue, tafadhali” Anna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga
“Anafaida gani, jiangalie wewe sasa hivi unavyo mwagikwa na machozi ya maumivu laiti ingekuwa sio wao, sasa hivi ungekuwa unalia?”

Fetty alizungumza huku machozi ya hasira yakimwagika
“Fetty najua kwamba, unaupendo na mimi na sisi sote tunapendana ila tafadhali usimue huyo baba, tambua yeye anaweza kuwa na mke na watoto wadogo sana, wanaoweza kuhitaji maleli ya baba na mama”

“Anna acha ujinga, wewe upo tayari kwenda kufia segerea?”
“Hata kama sipo tayari kwa hilo ila kwa......”
Fetty akajikuta akifya risasi mbili zilizo tua kifuani mwa ACP Ngurumo na kumfanya apoteze maisha hapo hapo,
“Mbona sasa umemua?”
Fetty alimuuliza Anna
“Alitaka kukupiga risasi”
Anna alizungumza huku akimtazama ACP Ngurumo aliyekuwa ameishika, bastola yake kwenye mkono wa kushoto

Makao makuu ya jeshi la polisi ikazidi kuwaongezea nguvu askari walipo, msituni wanao endelea kuwasaka majambazi sugu walio fanya tukio la kulidhalilisha jeshi hilo la polisi, Askari wapatao arobaini wa kikosi maalumu, wakaingia kwenye msitu wa Maliga pasipo wezao kufahamu, uwepo wapo.Wakafanikiwa kuuzingira msitu mzima ambao katikati wapo wezao wakiendela kuwasaka wasichana watano.Wakazidi kuingia ndani ya msitu na kufanikiwa kufika katika enoa walilo simama wasicha wawili wakiwa wamesimama huku kila mmoja akiwa na bunduki yake mkononi

Kitendo cha kufumba na kufumbua Fetty na Anna wakajikuta wakiwa wamezingirwa na kundi kubwa la askari walio valia nguo za jeshi huku sura zao zikiwa zimefuchorwa chorwa na rangi nyeusi.
“Anna, tumekwisha”

Fetty alizungumza huku macho yake yakiwatazama askari wanao zidi kuwasogelea kwa umakini, machozi yakazidi kumwagika Anna kwani hakutaraijia kama naye ipo siku atakuja kukamatwa na polisi, tartibu Fetty na Anna wakapiga magoti na kujisalimisha mikononi mwa askari
                                                                                                                                                                                                                      ****

Kila Samson anavyo jaribu, kujilaza kwenye kitandani, anajikuta akikosa usingizi kutokana na kumuwaza msichana aliye mfungia ofisini mwake.Akaichukua simu yake aina ya nokia tochi, akaiminya kitufe kilicho kifanya kioo kidogo cha simu hiyo kuwaka mwanga hafifu, saa iliyopo kwenye simu yake ikamuonyesha kwamba muda wa sasa ni saa sita na dakika mbili usiku.Taratibu akajiinua kitandani mwake na kuutazama mlango wake alio jaa nguo nyingi chafu alizi zinging’iniza kwenye misumari iliyopo nyuma ya mlango wake

Akatoka kwenye neti yake na kusimama pembeni ya kitanda chake na kuanza kujivuta vuta viungo vyake, kisha akaichukua suruali mmoja aina ya jinzi na kuivaa mwilini mwake, akachukua tisheti yake na kuivaa, akainama na kutoa viatu chini ya mvungu wa kitanda chake na kuvivaa
“Potelea pote”

Samson alizungumza mwenyewe na kuichukua, baiskeli yake aina ya ‘Oscar Chopa’ na kufungua mlangoa wa chumbani kwake na kutoka nje, akashusha pumzi zake na kuangalia angani na kukuta mawingu mengi yamejikusanya kwa pamoja ikiashiria muda wowote mvua inaweza kunyesha, akapanda kwenye baiskeli yake na taratibu akaanza kuiendesha huku taa ndogo ya baiskeli hiyo ikimsaidia kuyakwepa mawe na vishimo vidogo vidogo vilivyopo barabarani.

 kila jinsi anavyozidi kuongeza mwendo wa baiskeli yake ndivyo jinsi anavyozidi kuikaribia sehemu anayo fanya kazi, mwendo wa dakika ishirini barabarani, ukamsaidia kufia kwenye kibanda chake.Cha kumshukuru Mungu baiskeli zake zote alizo ziacha nje amezikuta, akashuka kwenye baskeli yake, akatazama pande zote za eneo kilipo kiduka chake hakuona dalili yoyote ya kuwa na mtu wa ina yoyote.

Akajikoholesha kidogo na kuitoa funguo ya geti la kibanda chake na kufungua, mlango, akaingia ndani na ngumi kali ikatua kwenye uso wake na kujikuta akianguka chini
“Ni mimi”
Alizungumza huku akimtazama Rahab aliye shika bastola, akimnyooshea

“Samahani”
Rahab alizungumza huku akiirudisha bastola yake kiunoni, kwani tayari amevaa nguo zake tarari alizo kuwa amezivua kipindi akikimbilia ndani ya kibanda hicho walipo toka kuvamia benki
“Nimekuja kukuchukua” Samso alizungumza
“Kwani, huko nje hakuna watu?” Rahab alizungumza
“Ndio, ila ngoja niingize baiskeli zangu”
“Fanya fasta basi”

Samson akatoka nje huku akiishika shika pua yake iliyo jaa maumivu ya kupigwa ngumi na Rahab, Samson akaingiza baiskeli ya kwanza na kutoka nje akiwa ameishika baiskeli ya pili akitaka kuingia ndani, gafla breki za gari aina ya Defender yenye askari wa kikosi cha F.F.U wapatao sita wakashuka kwenye gari kwa haraka huku wakiwa na bunduki na kunza kumfwata Samson sehemu alipo simama....

   ITAENDELEA... 
 Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts