Home » , » RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 3 & 4

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 3 & 4

Written By Bigie on Wednesday, September 14, 2016 | 10:27:00 AM

Mtunzi : EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Hakikisheni huyu dada nina lala naye usiku wa leo sawa”
Muntar aliwaamrisha wapambe wake na wakamtii na mmoja wao akanyanyuka kwenda kumfatwa Agnes kwenye eneo la kuuzi vinywaji ili kuzungumza ombi la bosi wake analo lihitaji

ENDELEA
“Habari yako dada?”
Kijana wa Muntar alimsalima Agnes ambaya kwa haraka akaliachia tabasamu lake mdomoni na kuufanya uso wake kuzidi kunawiri kwa uzuri
 
“Salama mamo vipi?” Agnes alizungumza kwa sauti nyororo ya kuvutia hadi muhudumu kiume wa vinywaji akaguna
“Salama.....kwa jina mimi ninaitwa Kibopa na yule pale alavalia cheni nyingi ni bosi wangu anaitwa Muntari”
“Aahaa nashukuru kuwafahamu,Samahani kaka ninaomba unipatie Red’s mbili za baridi kiasi”
“Muhudumu mpe katon nzima pesa nitalipa mimi?”
“Jamani kaka yangu mimi sio mnywaji sana”
“Ahaa usijali nyingine unaweza kunywa leo au hata kesho”
“Asante sana”
 
Muhudumu akamkabidhi Agnes katoni ya kinywaji alicho muagizia na kibopa akatoa pesa na kumlipia muhudumu.
“Sasa sister kama huto jali ninaomba namba yako ya simu”
Agnes bila wasiwasi akamtajia Kibopa namba yake ya simu,wakaagana ana Agnes akarudi sehemu alipo Rahab
“Jamaa ameshaingia mkenge sasa kazi ni moja sawa”
“Hapo ndipo ninakupendea Ag”
“Chezea mimi wewe,kumbe mtu ukiwa na kalio kubwa nalo linasaidia”
Wakacheka na kufungua vinywaji na kuanza kunywa taratibu.Muntar akakabidhiwa namba na Kibopa na akaipiga na Agenes akaipokea na kama kawaida na sauti yake nyororo aliyobarikiwa kutoka mbinguni akazungumza
“Nani mwenzangu?”
“Ukigeuka upande wako wa kushoto utaniona nimevaa shati jeupe na cheni za dhahabu”
Agnes akageuka na kumfanya Muntar kupunga mkono akimuashiria kuwa ni yeye ndiye aliye mpigia simu
“Mrembo nakuomba basi uje kujumuika name hapa?”
“Naona aibu labda nije na mwezangu”
“Hilo tuu hakuna tatizo ni wewe tuu”
“Sawa ninakuja”
 
Agnes akakata simu na kumtazama Rahab kwa pamoja wakatabasamu na wakasimama na kuanza kutembea kwa mwendo wa maringo na kupishwaviti na wapambe wa Muntar kisha wakakaa
                                                                       ***
Dokta Wiliama akawashusha kwenye gari Anna,Halima na Fety mbali kidogo na hotel ya Serena huku kila mmoja simu yake ikiwa na salio la kutosha pamoja na picha ya Karim Yussuf kijana mwenye umri mdogo ila anasifika sana kuwa na utajiri mkubwa kutokana na Sheli za mafuta anazo zimiliki kila kona ya mikoa ya Tanzania.Kila mmoja akaingia Hotelini kwa muda wake na kuelekea kuketi katika upande wake ila kwa pamoja wakawa na mawasiliano ya ujumbe mfupi wa meseji.Kutokana ni muda wa jioni hawakuwa na papara kwani watu wengi bado hawakuwa wameingia Hotelini kuendelea na starehe zao.Macho ya Fety yakatua kwa jamaa anayeingia kwenye  mlango wa kuingilia akiwa ameongozana na mwanamke mrembo
{Nimemuona}
 
Fety akausamba ujumbe kwa wezake ambao wapo maeneo ya tofauti kwenye hoteli na taratibu simu yake akaichomeka kwenye suruali yake na kuendelea kumtazama Karim ambaye moja kwa moja aka anaelekea sehemu yenye milango ya lifti zinazo kwenda juu  na kushuka chini,Kutokan-a na Lifti kutumika ikamlazimu Karimu na mpenzi wake kusimama kwa muda kuzisubiria.Kwa haraka Fety akasimama na kupiga hatua za haraka kabla hajafika sehemu alipo Karimu,lifti ambayo wanaisubiria ikafunguaka,Karim na mpenzi wake wakingia ila kabla haijajifunga Fety akawahi kuizuia na kuingia
“Habari zenu?”
“Salma”
 
Karimu kutokana na kutokuwa na aibu akaanza kumshika shika mpenzi wake na kuchezeana katika sehemu zao nyeti.Mcho ya Fety yakawangalia kwa umakini kisha akayahamishia masho yake kwenye kamera mbili za ulinzi zilizopo ndani ya lifti kabla hajafanya kitu chochote akastukia lifti ikisimama hii ni baada ya mpenzi wa Karimu kuminya kitufe cha kuisimamisha lifti.Kufuma na kufumbua Fety akastukia ngumi kutoka kwa mpenzi wa Karim ikitua kwenye shavu lake na kumsfanya kuweweseka kasha akaanza kuikwepa mikono inayoimjia mwilini mwake kutoka kwa Karimu na mpenzi wake Shamsa mwenye asili ya kiarabu.
                                                                           **
Karimu na Shamsa wanaasili ya Oman japo wanauraia wa nchi zote mbili Tanzania na Oman,japo watu wengi waliwaona machoni mwao wanadhani ni watu wema hii ni kutokana na jinsi wanavyo jitoa katika shughuli mbali mbali za kijamii na mara nyingi huwa wanawasaidia wasio jiweza kila siku ya Ijumaa na jumamosi nje ya jumba lao lililopo maeneo ya Mbezi beach.Japo wanautajri mkubwa wa magari ya kifahari,masheli,maduka na mahoteli ya kifahari ila  bado hawaridhiki na utajiri huo na wanaendelea kufanya kazi za haramu ili kuzidi kuuongeza utajiri mara dufu.Jambo la kuua kwao ni sawa na mtu kumchinja kuku siku ya sikuku.
 
Hadi wakati huu Serikali ya Tanzania inashindwa kutambua ni jinsi gani wanaweza kuwatia nguvuni Karimu na mpenzi wake wakiwa katika kidhibitisho kitakacho wawezesha kuwastaki katika mahakama kuu ya Tanzania na kuwatupilia jela.Kila mbinu ambazo serikali waliitumia wakajikuta wakishindwa hii ni baadhi ya viongozi wasio waaminifu kuwapenyezea siri Karim na Shamsa  na hujipanga upya katika kuwatoroka askari.

Amri ya kuwaua watu waote wanaoshindikana kukamatika na kirahisi ilitolewa ma raisi tena kwa siri kubwa na watu walio husishwa katika kazi hiyo ni Dokta William na Mkuu mstaafu wa jeshi bwana Clinton Tony ambao wote ni miongoni mwa watu wa karibu sana wa raisi na mara nyingi humshauri riasi katika maswala mengi ya kukabiliana na ugaidi hii ni kutokana na ujuzi wao katika maswala ya kigaidi
 
Pasipo wao kujua Agnes,Anna,Rahab,Fetty na Halima wanatumiwa na serikali kisiri na kwaimani yao wanatambua kuwa mtu anaye waagiza kazi hiyo ni dokta Williama ambaye amewafundisha mbinu nyingi za kigadi ili kupambana na magaidi wanao itesa serikali ya Tanzania pamoja na jeshi la polisi.
 
***********
Fetty anajipanga vizuri na kuanza kupambana nao kufa na kupona kutokana na ujuzi mkubwa wa kukabiliana na adui anafanikiwa kumpiga Shamsa ngumi kadhaa sehemu ya shingo na kumfanya apate wenge linalo mkalisha chini huku machoni mwake akiona nyota nyota nyingi.Karimu anashangaa kukutana na msichana jasiri anaye vumilia makonde ya mazito kutoka kwake na kwa haraka anamisha kitufe na lifti inaanza kwenda juu huku akiendelelea kuyapangua mateke ya Fetty kwa kutimia mikono yake iliyo komaa.

Lifti inafunguka gorofa ya tano na Karimu anajirusha nje kabla Fetty hajapiga hatua anastukia akishikwa mguu na kuvutwa chini na Shamsa na kuangukia uso na kumshuhudia Karimu akichanganya miguu kwa kasi kubwa na kupolelea anapo pajua mwenyewe.Shamsa akamkalia kwa haraka Fetty mongoni na kuanza kumvuta nywele huku akijaribu kukipigisha kichwa cha Fetty chini.Kwa nguvu zake zote Fetty akajikaza mwili wake kuanzia juu hadi chini na kujinyanyua kwa nguvu hadi akasimama ila Shamsa akaendelea kumng’angania mgongoni huku mkono wake ukiwa umeikaba kwa nguvu zake zote shingo ya Fetty.
                                                                                   ***
Simu za Fetty,Halima na Anna zina Software ambayo kila mmoja wao anapo kwenda ni lazima simu zao ziingize ujumbe katika simu za wezao kuwa ni sehemu gani alipo mmoja wao.Anna akampigia simu Halima na kumpa taarifa Anna wakutate katika milango ya kiingilia kwenye lifti
“Anna,Fety yupo kwenye matatizo ninavyohisi kama unaweza kuiona simu yako inavyoonyesha kuwa yupo eneo maoja  tuu kwa zaidi ya dakika kumi sasa”
“Location inaonyesha yupo gorofa namba tano”
“Sasa tujigawe,wewe pita kwenye ngazi na mimi nitumie lifti”
“Sawa”
 
Halima akaingia kwenye lifti na kuminya kitufe cha gorofa ya tano,huku alima naye akaanza kuzipandisha ngazi kwa haraka kuelekea juu gorofa ya tano japo ni ndefi ila akajikata kutembea kwa mwendo wa kukimbia
 
                                                                                     ***
Kwa haraka wazo lililo mjia Karimu ni kushuka kwa kupitia ngazi kuepukana na kukutana na Fetty ambaye tayari alisha mzidi ujanja na maarifa ya kila aina.Karimu akaanza kushusha kwenye ngazi huku akikimbia na kutazama tazama juu kama Fetty akamfwata ajue ni jinsi gani ya kuongeza juhudi za kukimbia.Macho ya Anna yakamshuhudia jinsi Karimu anavyoshuka kwa kasi huku hasho jingi  likimwagika na shati lake likiwa limejikunja kunja kama limetafunwa na ng’ombe mwenye njaa kali,Anna akapunguza mwendo na hadi Karimu anamfikia kwa ustadi mkubwa wa hali ya juu akampiga teke la miguu Karimu na kumfanya aanguke vibaya na kuanza kubingiria kwenye ngazi akielekaea chini akitoa kelele kali za vilio.
 
                                                                          ***
Fetty akaanza kuishiwa na pumzi mwilini mwake kutokana na kabali takatifu aaliyo pigwa na Shamsa msichana ambeye kwenye maeneo mazima ya kupiga anayapenda tangu akiwa mtoto mdogo wa miaka mitano.Fetty kila alipo jaribu kuitoa mikono ya Shamsa akajikuta akishindwa kwani Shamsa anahakikisha kuwa anaondoka na roho ya Fetty,taratibu Fetty akaanza kushuka chini huku jicho likiwa linaanza kumtoka akimshuhudia mtoa roo akiinyemelea roho yake.Mlango wa lift aliyo panda Halima ukafunguka na akatoka nje akatazama pande zote za kardo akaona hakuna dalili yoyote na mtu,Akasikia kishindo na kukuroma kwa mtu kwenye mlango wa pili wa lifti ambao unshindwa kujifunga kutokana na kiatu chekundu lilicho zuia katikati na kuifanya milango hiyo kujisogeza na kurudi inapotoka.Halima akamshuhudia Fatty akilazwa chini na msichana anaye miminika kwa jasho jingi japo ndani ya lifti hii kuna hewa ya kutengenezwa AC(air condion)
 
Halima hakupoteza muda,akaingia na kuzishika nywele za Shamsa na kumvuta nje kwa nguvu zake nje na kumfanya Shamsa kuburuzika kwenye sakafu iliyotengenezwa vizuri na kufanania na kioo.Akamgauza Faetty na kumkuta akikohoa kohoa akiyaruhusu mapafu yake kuingiza hewa ya kutosha.Shamsa akasimama na kuanza kukimbia kujiokoa maisha yake
“A....nak....imbi....a.”
Fetty alizungumza kwa shida huku mkono wake mmoja akimnyooshea Shmsa anayechanja mbuga
“Upo vizuri lakini?”
“Nd...io muwah....i anatoroka”
 
Halima akamtazama vizuri Fetty na kuridhishwa na afya yake na akasimama kwa haraka na kuanza kumkimbiza Shamsa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya kujirusha kwenye mlango mmoja uliopo mbele yake na kwabahati nzuri mtu aliyopo ndani ya chumba hicho ndio alikuwa ameufungua na kukishika kitasa cha mlango wake kwa ajili ya kutoka nje.

Kikumbo cha Shamsa kikamfanya mwenye chumba kuanguka chini pamoja na simu yake ambayo alikuwa anasoma meseji iliyomfanya asimame kwenye mlango huku akiwa ameshika kitasa.Shamsa hakuona sehemu nyingine ya kukimbilia zaidi ya bafuni ambapo Halima naye akaingia na kwa haraka Shamsa akachukua kibakuli chenye sabuni ya unga na kumbwagia Halima ya uso
                                                                             ***
Muntar na watu wake wakazidi kunywa pombe na kuwaomba Agnes na Rahabu wawe wageni wao kwa usiku wa leo.
“Jamani sisi hatuhitaji kulala kwenye hoteli hii.” Agnes alizungumza huku akikichezea kifua cha Muntar ambaye muda wote anakazi ya kutabasamu tabasamu
“Nyinyi mutanata wapi watoto wazuri?”
“Hoteli yoyote ila si hapa”
“Wee kibopa fanya mpango wa kutafuta vyumba vya mjini kwenye hoteli nzuri nzuri unazo zijua”
“Bosi hotel ambayo ipo powa kwa haraka haraka ninaona ni Mtendele”
“Ipo wapi hiyo?”
“Maeneo ya Chuda raha”
“Sawa twendeni”
 
Wakasimama na wote wakatoka nje,Rahabu na Agnes wakaingia kwenye gari lao na Muntar na wapambe wake wakingia kwenye gari yao aina ya HAICE na taratibu wakaanza safari ya kuelekea katika Hotel ya Mtendele
“Ag hawa watu tunawaua kwa nama gani?”
“Una maana gani?”
“Namaanisha kwa kuwanyonga au kwa kuwapiga risasi?”
“Lengo letu sisi ni huyo Muntar hao wengine tuwapotezee”
“Huoni watakuwa ni watu wa kwanza katika kutusaka sisi?”
“Sawa ila tutajua ni jinsi gani ya kuwaua endepo nao wataingia kwenye kumi na nane zetu”
“Powa hii ishu tuifanye usiku huu huu na turudi zetu kambini”
 
“Powa ni wewe tuu kikubwa ni umakini na hiyo bastola yako ikoki tayari kwa mashambulizi”
                                                                 ***
Muntar na wapambe wake wanaendelea kuburudika na mziki gafla Muntar akazima redio ya gari na kuwafanya wapambe wake kumtazama
“Sikilizeni nyinyi....mpango wetu ni kama munavyo ujua,Sisi mwanamke kwetu ni begi la safari na hawa pia iwe hiyo hivyo”
“Sawa bosi ila mimi sijaelewa kidogo hapo kwa maana hawa nao pia tunatakiwa kuwaua?”
“Ndio ni lazima wafe”
“Ahaaa bosi huoni maduu wazuri kama hawa pia tuwauee ,Acha basi tuspend nao kama siku mbili tatu nne hivi”
Kwa haraka Muntar akachomoa bastola yeka na kumelekezea Kibopa ambaye muda mwingi anapenda sana wasichana wazuri
 
“Katika wakati wa kazi huwa sipendi masihara.....na ole wenu miongoni mwenu nione mtu anajipendekeza kwa msichana yoyote nitamtoa roho,Tuna wakamata na kuwachinja na ndani ya matumbo yao tunadumbukiza shehena yote ya madawa ya kulevya tuliyo nayo.SAWA?”
“Sawa bosi’
Wote wakaitikia kwa woga huku Kibopa mwili wake wote ukiwa unamtetemeka kwani Muntar ni mwanaume asiye na huruma kwa mtu wa aina yoyote katika swala zima la biashara zake haramu.Usemi wake mkubwa ni bora punda afe ili mzigo ufike

       
SHE IS MY WIFE(NI MKE WANGU)……4

Kwa bahati mbaya katika maeneo ya barabara ya Railys,wakakuta ajali  ya daladala iliyosababisha magari mengi kusimama kwa muda,Kutokana hawakuwa na haraka ikawalazimu kupanga foleni na kuwaacha askari wa usalama barabarani kumaiza vipimbo vyao.
“Rahab nahisi kuna kitu kwenye gari la kina Muntar.” Agnes alimuambia Rahabu
“Kitu gani?”
 
“Kama wanakitu wanakijadili na ona oana jinsi Muntar anavyo zungumza huku akiichezesha chezasha mkono wake ulioshika bastola?” Agens alimuonyesha Rahab na kwakusaidiwa na mwanga wa taa za magari mengine waliweza kuliona tukio la ndani ya gari
Rahab akaitoa bastola yake na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti,akataka kushuka kwenye gari ila Agnes akamzuia
 
“Mbona unakuwa kama mjinga unataka kwenda wapi?”
“Tuwafyatue tusepe zetu”
“Huoni hao askari hapo au unataka tukimbizane kimbizane?”
Wote wakajikuta macho yao yakimsindikiza askari anaye gongwa kwenye kioo cha gari walilomo Muntar na watu wake
 
                                                      ***
Muntar akamtazama askari anaye gonga kioo cha gari lao,Akaitazama astola yake na kukishusha kioo taratibu
“Shukeni ndani ya gari.” Askari aliwaamrisha na kuwamfaya Muntar kufyatua risasi mbili kwa haraka,milio ya risasi ikawafanya watu waliopo kwenye eneo kuanza kutawanyika kuokoa maisha yao.Askari wengine watatu waliopo katika eneo la tukio wakajibanza kwenye magari mengine wakiwa na bunduki zako na kuanza kujibu mashambulizi kuelekea kwenye gari la Muntar
 
“Rudisha nyuma gai hilo.”
Muntar alimuamuru dereva wake na akatii,Wakaligonga gari walilomo Agnes na Rahab na kulifanya lirudi nyuma na kuyagonga magari yaliyopo nyuma yetu.Rahab akaanza akaanza kufyatua risasi katika matairi ya gari la Muntar na kulifanya lipoteze muoelekeo hii ni baada ya breki za gari lao kushindwa kukamata vizuri na kugonga kwenye vyuma vya reli.Watu wa Muntari,mmoja baada ya mwengine wakaanza kujirusha nje ya gari wakiwa na bunduki zao aina ya ‘Short gun’ na kuendelea kufanya mashambuliza kwa askari.
 
Agnes akafungua mlango wa gari lao na kupiga goti moja chini,Bastola yake ikawa na kazi mija tuu ambayo ni kufyatua risasi kwa kila mtu wa Muntar.Muntar akazidi kuchanganyikiwa baada ya watu wake kuwaona wakiwa wanaanguka mmoja baada ya mwengine.Hadi akabaki akiwa na Kibopa ambaye wakati wote wezake wakipambana yeye alikuwa na kazi ya kujibanza kwenye gari lao
 
Muntar akaona nafasi pekee ni kukimbia,kwa bahati nzuri pembeni kuna pikipiki iliyo acha na raia aliyekuwa akijiokoa maisha yake kwa kuiamini sana miguu yake kuliko pikipiki.Akapanda na Kibopa akadanda kwa nyuma wakaondoka kwa kasi wakikatiza katokati ya njia za reli.
 
Agnes na Rahab wakaingia ndani ya gari,Agnes akalirudisha gari lao nyuma na kupata upenyo wa kuiwezesha gari yao kupita na kupita njia ambayo Muntar amekimbilia.Askari wakashindwa kufyatua risasi kwatika gari linalo wafukuzia majambazi kwani hawakujua walio wasaidia ni kina nani.
 
Muntar akazidi kukanyaga mafuta na kuingia barabara inayokwenda mikoani akikatiza katika kiplefti cha kwaminchi,Agnes akawa na gazi ya kupiga honi akiashiria watu waliopo barabarani kuwapiasha.Akazidi kukanyaga mafuta kwa kasi huku akiikaribia pikipiki ya Muntar.Kibopa akaanza kufyatu risasi kuelekea lilipi gari walilopo Agens.
 
“Shiti....” Rahab alizungumza huku akinang’ata meno yake,alikataka kujitokeza kwenye kioo cha gari ila akarudi ndani kwa haraka baada ya kioo kidogo cha pembeni kuvunjwa kwa risasi anazo zipiga Kibopa pasipo kuwa na utaratibu wowote.Gafla kibopa akalikwepa Scania linalo toka kwenye kiwanda cha unga Pembe maeneo ya Kange na karibia robo mbili ya gari imeziba barabara na kuachanisha uwazi mdogo unao weza kuiruhusu pikipiki kupi na kuendelea mbele kwa kasi.Agnes akafunga breki za gari lake kwa kasi na kuiingiza upande wa kulia kwake kukikwepa kichwa cha gari kubwa la unga,Gari karerereka pembeni ya barabara na kwakusadiana na Rahab wakaushika mskani wa gari na kuurudisha upande wa kulia 
 
Gari ikakaa sawa barabarani,kutokana na mstuko katika injini,gari ikazima katikati ya barabara na milago yote kujifunga.Kwa kutumia vitako vya bastola zao wakapasua vioo vya madirisha ya magari na kujitoa ndani ya gari lao,linalo toa mlio wa kuashiria linaitilafu sehemu
“R...itakuwaje sasa?”
“Ndio hivyo jamaa wamesha sepa.”
“Ngoja kwanza.” Agnes akaenda eneo lenye maegesho ya boda boda(waendesha pikipiki),
“Ni kina nani wanaweza kuendesha pikipiki kwa kasi kubbwa?”
 
Kila muendesha pikipiki akaa kimya huku macho yao wakiitazama bastola ya Agnes.
“Ohoo nahisi munaiogopa hii bastola? Mimi ni raia mwema ninaomba masaada wa kuwakimbiza wale watu walio pita hapa?”
”Dada mimi piki piki yangu haina mafuta?” Jamaa mmoja alizungumza huku akilivua kofia lake,wengine wote wakakataa.Rahab akafika eneo alipo Agnes
“Ag wanasemaje?”
“Hawataki?”
 
Rahab akapiga risasi moja hewani,kila dereva aliye ipenda rogo yake akaaruka kwenye pikipiki yake na kuchanganya kwato zake kuooa maisha yake.Rahabu akapanda kwenye moja ya piki piki aina ya Boxer,ambayo dereva wake aliisahau funguo yeke.Muntar kadri anavyozidi kuendesha pikipiki ndivyo jinsi mafuta yaliyozidi kuteketea,na taratibu piki piki ikaanza kugoma na mwisho wa siku ikagoma kabisa hata kusogea hatua mbele.Rahab akazidi kuvuta mafuta ya pikipiki waliyo panda,kwa mbali wakawaoana Muntari na Kibopa wakishuka kwenye pikipiki yao na kuinga pori.
 
                                                                                     ***
Shamsa baada ya kumuona Halima anaanza kuhangaika kwa sabuni ya unga aliyo mwagia usoni,kwa haraka akafungu mlango wa chumba na kuaanza kukimbia kuelekea zilipo ngazi za kushuka.
 
Anna kwa haraka akashuka kwenye ngazi na kuanza kumshindilia mateke Karim ambaye amechoka kwa kiasi kikubwa sana.Karim akajihahidi kujiinua ila Anna akawa makini kwa kila jambo na kwa haraka akaiwahi shingo ya Karimu na kuizungusha kwa nguvu na kuivunja.Kitendo cha Karimu kuuawa kikashuhudiwa na Shamsa ambaye ndio yupo kwenye harakati za kujiokoa kutoka mikononi mwa Halima.
 
Anna hakumjali Shamsa ambaye amesimama kwa mshangao akiwa haamini kwa kitu kilicho tokea kwa mpenzi wake anaye mpenda kuliko kitu cha aina yoyote.Kwa haraka Shamsa akashuka kwenye ngazi kwa hasira na kumrukia Anna ambaye akajibamiza kwenye ukuta,Shemsa akajaribu kumrukia Anna ambaye alifanikiwa kumkwepa na kwa bahati mbaya Anna akamsukuma Shamsa ambaye akaanza kwenda chini kutoka gorofa ya nne hadi kwenye sakafu na kichwa chake kikapiga chini na kikapasuka mbele ya macho ya polisi na baadhi ya wateja wengine
 
Anna taratibu akapiga hatua na kuchungulia sehemu aliyo angukia macho yake yakakutana na askari tishio ambaye ni mpelelezi wa kutegemewa nchini bwana Jackson Luther
 
                                                                                      ***
Rahab anazidi kuvuta mafuta ya pikipiki hadi kwenye njia walio ingilia Muntar na KIbopa mbao walizidi kuongeza mwendo wa kukimbia baada ya kuiona pikipiki ikiwafwata kwa kasi nyuma yao.Kwa bahati mbaya Muntar  na  Kibopa waliishiwa risasi katika silaha zao,kila mmoja akakimbia kwa upande wake anao ujua yeye ili kutaokoa maisha yake,Rahabu akapunguza mwendo wa pikiki na Agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda Kibopa,Rahab akapita njia aliyo kwenda Muntar.

Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla Rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na Muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi


ITAENDELEA....
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts