Get the latest updates from us for free

Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 41 & 42 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 41 & 42 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Vuvuzela on Thursday, September 8, 2016 | 11:15:00 AM


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa 

Ilipoishia...

Kwa kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona askari lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu


Endelea...

Kutokana tayari injini za ndege zilishaanza kuata moto haikuwa rahisi kwa kuisimamisha ndege ambayo taratibu ilishaanza kuondoka kuzipisha ndege nyingine ambazo zinasubiri kutua na kila kitu katika uwanjwa huu wa ndege vinakwenda na muda wanao jipangia.Macho yangu yakashuhudia jinsi tunavyo ziacha gari za polisi na ndege inavyo ongeza mwenza na kuitafuta njia ya kurukia
“ehee mola niokoe mimi mja wako kwa maana mmmm”

Nilijizungumza kimoyo moyo na kweli ndege ikakaanza kunyanyuka taratibua na kuiacha ardhi ya afrika kusini hadi ndege inakaa sawa angani ndio nikapata amani na kajasho taratibu kakanishuka huku kwa mbali nikijasikilizia jinsi mapigo ya moyo yanavyo punguza kasi yake,safari ikaendelea kwa amani na kutokana na uchovu mwingi nikajikuta nikilala fofofo pasipo na kitu kilicho nistua ni kipaza sauti cha rubani akituomba tufunge mikanda yetu vizuri kwani ndege inajiandaa kutua katika uwanja wa jomo kenyata nchini kenya
“mmmmmmm”

Nikajikuta nikiguna kwani sijazoea kuziona ndege zinazo toka nchini afrika kusini kutua kenya ili kwenda tanzania na isitoshe kwa maelezo niliyo yasikia wakizungumza mama na balozi wa tanzania ni kwamba ndege inakwenda moja kwa moja tanzania.Moyo wangu ukaanza kupoteza amani tena ikanilazimu kumiya muhudumu wa ndege na hakusita kunifwata sehemu nilipo na kunisikiliza haja yangu niliyo muitia

“sijui nimesikia vibaya au....? Ni kweli tutatu kenya?”
“ndio kuna mzigo tunaishusha kwanza na pia kuna mmoja wa abiria nanhitajika kurudisha afrika kusini kwahiyo tunaiwahi ndege ya shirika letu inayo ondoka kenya saa sita usiku na tutamkabidhi abiria huyo kwa askari.”
Moyo ukawa kama umelipuliwa na bomo,kuzungumza nikajikuta nikishindwa na kubaki nikimtazama muhudumu kama sanamu la kushangaza

“halloo mr”
Nikastuka na kumtazama muhudumu wa ndege ambaye alikuwa akinipungia mkono mbele ya uso wangu baada ya kuniona nikiwa nimegandishwa kama sanamu
“umesema kuna mtu anashushwa?”
“ndio hiyo ni taarifa tuliyo powa tukiwa njiani”
“ni mwanume au mwanamke”
“kusema kweli hatujatajiwa ni jinsia gani?”
“nashukuru”
“na wewe pia”

Muhudumu akaondoka na kuniacha nikitawaliwa na mawazo na laiti ingekuwa nipo kwenye gari nigeweza kuruka na kufilia mali.Kitu cha ndege ni ngumu sana kujirusha,rubani akatutangazia kuwa zimesalia dakika tano kwa ndege kutua na kila mto ahakikishe kuwa amejifunga vizuri  mkanda wake hapo ndipo nikakumbuka na mimi kujifunga mkanda.

Ndani ya dakika tano ambazo rubadi alisema ndivyo jinsi iliyo kuwa na ndege nikaanza kushuka chini kwa kasi na matairi yake yakaanza kukanyaga ardhi ila gafla tukasikia mlio wa ‘kwaaa’ kama kitu kilicho katika na kuifanya ndege kuegemea upande wangu niliopo na wezangu tulio kaa upande huu.Milio ya vyuma kukatika katika tukazidi kuisikia na si mimi mwenye niliye anza kupiga kelele za kumuomba mungu ila hadi wezangu nao wakafanya hivyo huku kila mmoja akiomba kwa lugha anayo ijua yeye mwenyewe

Ndege ikazidi kulala upande wetu na kazidi kuserereka na mbaya zaidi moto mwingi ukaanza kuwaka sehemu ya nyuma mita chache kutoka ilipo siti yangu na kunilazimu kuufungua mkanda ili kuyaokoa maisha yangu kama wanavyofanya wezangu.

Nikawahi kuishika siti ya mbele yangu ili kujizuia na upepo mwingi unao nivuta nyuma kutoka katika sehemu ulipo moto ambao umepasua sehemu nzima ya nyuma.Nikajikaza kwenda mbele na watu walio shidwa kujishikilia walivutwa nyuma kwenye moto.Kelele na vilio vikazidi kutawala na kila sehemu na watu wengi wakawa wamebanwa na siti zao kiaisi kwamba baadhi yao walijigonga vibaya kwenye vyuma na vichwa vyao kupasuka vibaya na wengine kukatika viungo vya miili yao.

Ndege ikagonga sehemu na kusababisha mtikisiko mkubwa na kupinduka kichwa chini miguu juu jambo lililosababisha mikono yangu kushindwa kuhimili kuishikilia siti niliyo kuwa nimeishika na nikajikuta nikiachia na kuanza kuvutwa nyuma na upepo mkali uliochanganyika na moto ambao ni mkali sana,gafla nikastukia nikidakwa mkono na kuangalia vizuri nikamkuta ni sheila ambaye amenishika mkono huku na yeye akiwa amekaa kwenye siti yake na kuzuiwa na mkanda alio jifunga na huku mkono mmoja akiwa ameushika kwenye siti iliyopo pembeni.

Nikamtazama kwa macho ya huzuni na kumuona akishindwa kuhimili uzito wangu kwani tegemezi lote la mwili wangu ni mkono wake na sikuwa na sehemu yingine ya kushikilia
“sheila niachie nife”
“eddy unasemaje?”
“niachie.”

Nilizungumza huku nikimtazama sheila machoni ambaye anatumia nguvu nyingi kunizuia nisichomolewe nje ya ndege na mbaya zaidi pembeni yangu hakuna kitu ambacho ninaweza kusema kuwa nitakishika ili kinizuie nisichomolewe nje kwani siti zote za nyuma zimechomoka na watu wake.

Ndege ikaendelea kugonga majengo yaliyopo ya hapa uwanja wa ndege hadi ikasimama ndipo sheila akaniachia mkono na mimi nikaanguka chini na kujigonga mkono wangu wa kushoto kwenye upande wa pili wa ndege.Sheila akaaanza kupata shida ya kujifungua mkanda wa siti yake na mbaya zaidi kwa jinsi ndege ilivyo anguka imemfanya awe kichwa chini miguu juu

Nikaanza kusikia ving’ora vya gari za zimamoto zikija katika eneo la tukio na kuazna kuuzima moto  unaoendelea kuiteketeza ndege,moshi mwingi ulio tawala ndani ya ndege ukanifanya nianza kukohoa na taratibu nikaanza kujivuta nje ya ndege huku mkono wangu ukitawaliwa na maumivu makali.Niavutwa nje na waokoaji na gafla mlipuko mkubwa wa ndege ukatokea na kuturusha mbali mimi pamoja na waokoaji na nikajzidi kuuegemea mkono wangu ambao ninahisi unamaumivu
“no sheila?”

Nikajinyanyua na kuanza kutembea huku nikiyumba na kujitahidi kurudi kwenye ndege ila baadhi ya waaokoaji na askari wakanizuia,machozi mengi yakaanza kunitawala kwani moja kwa moja ninatambua kuwa sheila ni miongo mwa walio lipuka na ndege.

Wazo la kwamba ninatafutwa na polisi na ninahitajika kurudishwa afrika kusini kujibu mastaka yangu likanijia kichwani.Nikawatazama askari na waokoaji nikaona kila mmoja yupo na mihangaiko ya kuwaokoa majeruhi wengine na taratibu nikaanza kutembea kwa kujikaza  pasipo kutazama pembeni wala nyuma zaidi ya kwenda mbele huku mkono wangu wa kushoto nikiwa nimeushikilia vizuri.

Machela moja ikapitishwa kwa haraka pembeni yangu na waokoaji huku wakikimbia kwa kwasi na mtu waliye mmbeba juu ya machela nikamtambua ni sheila japo mwili wake umeharibika sana kwa moto kitu kilicho nifanya nimtambue kwa haraka ni nguo zake alizo zivaa,wakamuingiza ndani ya gari ya wagonjwa na wakaondoka

Nikabaki nikiwa na mshangao sikujua ni nini nifanye,nikiwa ninaendelea kushangaa nikwaona askari wawili wakinifwata sehemu niliyo simama.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka huku nikigeuza geuza shingo yangu nyuma na kuwatazama askari na kuwoana nao wakiongeza mwendo wa kunifwata.

Moto mkali ulio andamwa na upepe mkali ukaanza kushika majengo mengine ya uwanja wa ndege na kuwafanya watu waliopo kweye eneo hili kuaanza kukimbia kimbia ovyo kuyaokoa maisha yao.Nikajichomka katikati ya watu wanaokimbia kuokoa roho zao na nikafanikiwa kutoka nje ya uwanja wa ndege.Nikaendelea kukimbia hadi nikafanikiwa kutoka nje ya uwanja wa ndege na nilipo tizama nyuma yangu sikuweza kuwaona askari wakinifwata.

Mauivu ya mkono yakazidi kunitawala na sikuwa na jinsi zaidi ya kujikaza kiume na kuendelea kutembea nisipo pajua na kunyoosha barabara ya lami ambayo nikatembea kwa umbali mkubwa na kukuta kibao kilicho andikwa athi river na kutokana na uchovu mwingi nikatafuta sehemu nikajipuumzisha pembezoni mwa barabara,nikapata sehemu nikajipumzisha hadi kulipo pambazuka mida ya saa kumi na moja alfajiri nikasimama barabarani na kuanza kusimamisha magari yanayo pita.

Nikafanikiwa kuahatisha gari moja la watalii aina ya landrover ikasimama
“where are you going young boy?”(unakwenda wapi kijana?)
“am going tanzania”(ninakwenda tanzania)
“are you a tanzanian?”(wewe ni mtanzania?)
“yes”(ndio)

Mama wa kizungu alinihoji maswali hayo kisha akazungumza na mume wake kwa lugha ya kireno,ambaye ni dereva wa gari lao na akanikubalia kupanda ndani ya gari lao na safari ikaanza.Ndani ya gari ukimya ukatawala huku nikiyasikilizia maumivu ya mkono wangu ambao unavuta kwa kiasi kikubwa na sikuhitaji waweze kujua juu ya kuvunjikwa kwangu mkono kwani wangenihoji maswali mengi yasiyo na msingi wowote kwangu

“what’s  your name?”(jina lako ni nani?)
“my name is eddy”(jina langu ni eddy)
“you have a good name as our soon”(unajina zuri kama mtoto wetu wa kiume)
“thanks”(asante)
“my name is madam loren we are going moshi”(jina langu ni madam loren,tunakwenda moshi)

Sikutaka kujua wanakwenda moshi kufanya nini kwani mkono wangu unaniuma kupita maelezo,hadi tunafika arusha tanzani mida ya saa sita mchana hatukuweza kusimamishwa na askari njiani na tuliingilia kwa njia ya monduli hadi tunafika arusha mjini nikawaomba wanishushe na nikawashukuru kwa masaada wao kisha wakaendelea na safari yao kwani walinieleza wanaelekea moshi.Nikaanza kupandisha barabara ya old moshi na moja kwa moja nikaenda nyumbani kwa madam mery.Nikafika nyumbani kwa madam mery na kukuta mabadiliko kidogo kwani rangi ya ukuta na gati lake vilikuwa vimebadilishwa

Niikaanza kugonga kwa kutumia mkono wa kulia na nikasikia sauti ya kike ikisema inakuja kufungua,nikasimama kwa dakika kadhaa na gati likafunguliwa na akasimama msichana akiwa amemshika mtoto mdogo mkononi mwake akiwa anasura inayo endana na mimi
“nikusaidie nini kaka?”
“ehee madam mery nimemkuta?”
“hayupo amekwenda kazini”
“wapi?”
“shuleni hapo juu...Karibu ndani”

Nikatazama pande zote za nje kisha nikaingia ndani huku nikimtazama mtoto aliye bebwa na mtoto msichana ambaye ninahisi ni msichana wa kazi na kusema kweli kila kitu ambacho mimi ninacho kwenye sura yangu kipo kwa huyu mtoto mdogo.

Binti akatangulia kuingia sebleni na akanikaribisha kwenye masofa mapya niliyo yakuta ndani ya sable hii kidogo nikashusha pumzi,gafla macho yangu yakagongana na mume wa madam mery ambaye siku zote ni adui yangu na mara ya mwisho nakumuka nilimpiga kichwa na akanitolea bastola na jamaa sura yake ikabadilika gafla akanitazama kwa umakini kisha macho yake akayahamishia kwa mtoto aliye bebwa na mfanyakazi wake

                               *****sory madam*****(42)

“waooo ni muda sasa sijakuona naona umekuja kuchukua kiumbe chako si ndio?”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku nikimtazama mume wa madam mery na kajasho kembamba kakaanza kunimwagika

“nipe huyo mtoto”
Mfanyakazi wa ndani akamkabidhi mume wa madam mery mtoto ambaye tayari nimegundua kuwa ni mwanangu.
“nenda ndani?”
Mfanyakazi wa ndani akaondoka na kutuacha na mume wa madam,japo ninamaumivu ya mkono nikajaribu kunyanyuka ila niweze kujiokoa,mume wa madam mery akamshika mwanangu kichwa chini miguu juu na kumfanya mtoto kuanza kulia kwa sauti

“kaa hapo hapo la sivyo huyu paka wako ninamwangamiza mbele ya macho yako”
Nikamangalia jinsi mtoto wangu anavyolia na kujikuta roho ya huruma ikinitawala na nikakaa chini nikimtazama mume wa madam mery,akatoa simu na kuipiga
“njoo nyum bani”

Jamaa akakata simu na kurudisha mfukoni kisha akaniangalia machoni na kutabasamu.Akamshika mtoto vizuri na kuanza kumbembeleza huku akizunguka huku na huku ndani ya sable.Mlango ukafunguliwa na akaingia madam  mery akiwaavalia vizuri na ule uzuri wake umezidi kuongezeka na baada ya kunioana akaonekana akistushwa.Akapitiliza hadi kwa mume wake na kumpiga busu la shavu kama ishara ya salamu

“nenda kakae kule”
“ehee”
“nenda kakae kwa mshenzi mwenzako”
Jamaa alizungumza kwa hasira hukua akimsukuma madam mery kuja kukaa kwenye sofa ambalo nimekaa
“jamani derick mume wangu si tulisha lizungumza na limeisha mbona unataka kuanzisha ugomvi?”
“nyamaza malaya mkubwa wewe,hivi unajua uchungu nilio kuwa nao wewe,au unadhani kukaa siku zote kulea kiumbe kisicho changu hivi unajua ni maumivu gani ambayo ninayo moyoni mwangu”

Derick alizungumza huku machozi yakimwagika na mtoto wetu akiwa amemshika mikononi mwake.Madam mery machozi yaakanza kuutawala uso wake
“derick nakuomba unisamehe kwa mara nyingine sito rudia tena kukusaloti mume wangu”

“ahaaa chagua mawili kati yangu au huyu panya wako?”
Macho yakanitoka nilipomuona derick akifanya kitendo cha mara ya kwanza cha kumshika mwanangu kichwa chini miguu juu huku akiwa amemuinua kwa mkono mmoja
“derick nyote ni muhimu sana kwangu ninakuomba mume wangu unisamehe nina kupenda sana mume wangu”

“wewe manamke ni muuaji,kumbuka mimi ndio nilikufanya kupata elimu yako hadi akawa mwalimu ukaona haitoshi ukanisaliti mara ya kwanza nikakusamehe......Baba yako alifariki mikononi mwangu tukimuwahisha nchini india kwa matibabu na zote zilikuwa gharama zangu senti tano kwenu mulikuwa hamuna nimevunja vibanda vyenu na kuwajengea nyumba nzuri ili nanyi muonekane watu kati ya watu ila bado umeona hatoshi kabla ya ndoa yetu umebeba mimba ambayo si yangu ni ya uyo paka hapo.”

“ni mara mia ungetembea na mtuu aliye kuzidi umri ila wewe ukachukua serengeti boy unadhani atakusaidia nini huyo mwehu wako”

Derick aliendelea kuzungumza kwa hasira huku machozi yakiendelea kumwagika na mwanangu akiendelea kulia kwa maumivu anayo yapata.Madam mery kapiga magoti na kuanza kuburuzika taratibu akimfwata mumewe sehemu aliyo simama

“rudi huko huko la sivyo ninamuua huyu paka wenu.”
Madam mery akaanza kurudi nyuma taratibu huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi.Kelele za mwanangu kulia kwa maumivu zikanifanya nishindwe kuvumilia huku hasira ikinipanda nikanyanyuka huku nikiwa nimeushika mkono nilio vunjika na kupiga hatua mbili mbela za kuikwepa miguu ya madam mery
“wewe rudisha miguu yako huko la sivyo ninamuachia huyu mtoto”

Derick aliniambia akionekana kutokuwa na huruma kabisa na maumivu anayo yapata mwanangu,nikashindwa kuizuia miguu yangu na kujikuta nikizidi kupiga hatua kwa hasira kali iliyo nitawala mwili mzima.Derick akampiga mwanagu chini kwa nguvu na kumfanya mtoto wangu kunyamaza kimya na kelele kali ikatoka kwa madama mery pamoja na mfanyakazi wa ndani ambaye alikuwa amejificha kwenye ukuta akishuhudia kila kinacho endelea.

Sikujali kama mkono wangu mmoja umevunjika kwa hasira nikamrukia derick ambaye akanikwepa na kunisindikiza kwa teke kali la mgongoni na kujigongwa kwenye uso kwenye ukuta  na kuangukia pembeni ya miguu ya mfanyakazi wa ndani ambaya mkononi mwake ameshika kisu na kitunguu.

Nikamuomba mafanyakazi wa ndani kisu kabla hajanipa derick akauwahi mkono wa mfanyakazi wa ndani ulio shika kisu ikanilazimu na mimi kuuwahi mkono wa mfanyakazi kwa kuutumia mkono wangu mmoja usio vunjika.Derick akatuzidi nguvu na kumshika mfanyakazi wa ndani na kusukumia pembeni na kisu kikaanguka chini.Kabla derick ajakiokota nikampiga teke na kuifanya miguu yake yote miwili kunyanyuka chini na akaangukia mgongo.

Nikajisogeza kwa haraka na kabla sijakiokota kisu akanikanyaga vidole vya mkono wangu wa kulia nilio unyoosha kukiokota kisu.Derick akakipiga kisu mbali kido na eneo ambalo nililo angukia akanipiga teke la mbavu lilinifanya nijikunje huku nikigumia kwa maumivu makali.
“derick utamuua mtoto wa watu”

Madam mery alizungumza huku akimwagikwa na machozi na mikpono yake ikiwa imejaa damua na vitu vyeupe vyeupe na kugundua kuwa mwanangu amepasuka kichwa chake.Nikanyanyuka huku meno yangu nikiwa nimeyang’ata kwa nguvu.

Nikajaribu kuuyanyua mkono wangu wa kushoto ulio vunjika na kuufanya kuuma kwa maumivu makali yaliyonifanya nitoe ukelel wa kuumia kwani kuna kitu kinanichoma kwa ndani.Derick akayashusha macho yake hadi kwenye mkono wangu kisha akayarudisha machoni  mwangu na kwa haraka akanitisha kama ananipiga teke kwenye mkono na kuufanya niukinge mkono wangu kwa kugeuka na kumpa mgongo na kushtukia akininyanua miguu yangu na kuivuta na kuanguka kifudifudi huku mkono ulio vunjika nikiwa nimeulalia

Derick akanikalia mgongoni na kuishika mikono yangu yote miwili na kuivuta kwa nyuma.Maumivu ninayo yapata sikuwahi kuyapata tangu nizaliwe.Madam mery akauweka chini mwili wa mtoto wetu na kukimbilia sehemu tuliyupo na kumsukuma derick na akaanguka kwa mbele yangu.Sikuwa na uwezo wa kunyanyuka kuokana  na maumuzi makali na kubaki nikilia kwa uchungu.

“ni binadamyu gani usiye na huruma wewe,umenilia mwanangu kikatili ila bado unataka kumuu huyu kijana wa watu”
“niliapia ni lazima nimuue huyu kijana pamoja na wewe na leo ndio mwesho wenu”
Derick alizungumza huku akinyanyuka kwa haraka  na akamshika madam mery nywele zake na kumbwaga chini kwa nguvu na kumfanya madam mery kutoa ukulele wa kulia kwa maumivu
“shemeji mikono yako nyoosha juu”

Niliisikia sauti ya mfanya kazi kwa nyuma yangu na kunifanya nigeuke nyuma  na kumkuta akiwa ameshika kisu huku mwili mzima ukimtetemeka.Derick akacheka kwa dharau na kumfwata mfanyakazi kwa kasi na kupiga kabali ya gafla na kumpokonya kisu na pasipo kuwa na huruma derick akamchoma mfanya kazi wa ndani kisu cha tumbo na kumtupa chini.Derick akanisogelea huku kisu chake kikiwa kinavuja damu za mfanyakazi,akaniinamia na kunitazama kwa umakini huku akicheka

“nilikuumbia siku nikikutia mikononi mwangu nilazima nikuue”
Maneno ya derick hayakuhafikiana na moyo wangu kuyakubali kiharaka na kirahisi kama anavyo fikiria.Kwa haraka nikainyanyua miguu yangu kuikaba shingo ya derick na kwa nguvu zote.Madam mery akamuwahi kumshika derick mkono ulio shika kisu na kumpokonya,kila nilipo kumbuka jinsi mwangu alivyo anguka chini ndivyo jinsi nilivyozidi kumkaba derick shingo yake ambaye akaanza kunishindilia ngumi za mbavu na akaubana mkono wangu uliovunjika na kuzidi kunifanya niachie ukele mkali
“madam nisaidieeeeeee”

Madam akabaki akiwa ameshika kisu asijue nini afanye,nikamuomba tena anisaidie ndipo akastuka kama yupo sehemu ya tukio la hatari,akatutizama tena kwa umakini na kwaharaka kisu akakishusha na kikatua kwenye bega la derick na kumfanya aniachie na kunyanyuka kama mbogo na kumsukuma madam mery ambaye akaangukia mwili wa mtoto wetu na kutulia chini
“nitaendelea kukusaka”

Derick alizungumza huku akiingia ndani kwa haraka na kutoka akiwa na begi la kuburuza na akanitazama kwa muda kisha akanipiga teke la kichwa na kizunguzungu kikali kikanitawala kikiambatana na giza kubwa lililo tanda kwenye macho yangu na nikatulia tuli

 ***

Milio ya ndege pamoja na mwanga mkali vikanistua na kujikuta nipo kwenye chumba chene kitanda kimoja tuu.Pembeni ya kitanda kuna meza ndogo pamoja na kiti,kila ninapojaribu kuitadhimini sehemu hii ninashindwa kujua ni wapi.Mbaya zaidi sehemu hii haifanani na hospitalini kwani kitanda nilicho lala kinaukubwa zaidi ya kitanda cha hospitalini.Nikajichunguza vizuri na kuukuta mkon wangu ukiwa umefungwa bandeji gumu(p.O.P.O).

Nikashuka kitandani na kwenda dirishani na kufungua dirisha nikaona migomba mingi nikstukia kwa nyuma mlango ukifunguliwa na akaingia mama mmoja mtu mzima
“umeamka mwanangu?”
“shikamoo”
“marahaba,unajisikiaje?”
“vizuri tuu”

Akanishika mkono na kuugeuza geuza kisha akanitazama usoni huku akiwa ameachia tabasamu pana
“mimi ninaitwa mama natujwa na hapa ulipo ni moshi”
“nimefikaje?”
“umeletwa na rafiki yangu anaitwa mery na tangu uje hapa huna hukuwahi kuyafumbua macho yako na ulikuwa ni mgonjwa mahututi sana”

Ikanibidi kurudi kitandani na kukaa kwani niliaza kuhisi kizungu zungu,mama natujwa akakaa pembeni yangu huku akinishika shika kichwa changu na kunigeuza huku na huku“mimi ni daktari wa mifupa ninamiliki hospitali yangu hapa moshi,na kipindi mery alipo kuleta nilikufanyia oparesheni hospitalini kwangu na tukakulaza kule kwa kipindi cha mwezi mzima huku tukikulisha kwa mipira maalumu.Nilipo kuleta hapa nyumbani kwangu tatizo lililo kuwa kubwa ni wewe kurudi katika hali yako ya kawaida”

“ni kipindi gani kimepita?”
“unakwenda mwezi wa tatu sasa,japo mery alikata tamaa ya kudaidi kuwa huto weza kurudi katika hali yako ya kawaida”
“na yeye sasa hivi yupo wapi?”
“yupo arusha anaendelea na kazi...Tena ngoja nimpigie simu nimjulishe kuwa umezinduka?”
Nikamzia mama natujwa kumpigia simu madam mery
“kwa nini unanizuia?”
“sihitaji alijue hili sawa”
“je akija?”
“nimekuambia sihitaji aweze kugundua jambo hilo”

Akili na wazo juu ya mauaji ya mwanangu likanijia kichwani mwangu,picha niyingine ya jinsi nilivyo teseka kwenye pango nchini afrika kusini likanijia kichwani mwangu na sura ya baba yangu mkubwa mzee godwin ikanijia kichwani huku ikifwatiwa na sura ya derick.
“hii kazi nitaifanya mimi mwenyewe”
Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya mama natujwa kuniuliza ninasemaje
“hapana sijazungumza kitu”

Nikaka nyumbani kwa mama natujwa kwa wiki moja,nilipo ridhika afya yangu ipo kamili nikamuomba ruhusa ya kuondoka na akanikubalia ila kwa kipindi chote sikumuomba asizungumze chochote kwa madam mery,nikapanda basi hadi dar es salaam na sikufikizia nyumbani kwetu nikelekea nyumbani kwa sheila na kukuta geti lake likiwa wazi na gari yake ikiwa imesimamishwa nje.

Nikapata matumaini ya uwepo wake na moja kwa moja nikaufungua mlango wake na sikuamini macho yangu baada ya kumkuta akiwa ananyonyana denda na mwanaume mwengine ambaye kwa haraka nikamtambua ni derick mume wa madam mery......

Itaendelea....
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts