Get the latest updates from us for free

Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 45 & 46 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 45 & 46 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Vuvuzela on Monday, September 12, 2016 | 9:27:00 AM

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
“nani kachanganyikiwa”
Nilishindwa kuvumilia ikanibudi nizungumze,taratibu nikiwa ninashuka kwenye ngazi na mkononi nikiwa nimeshika bastola na kuwafanya mama na sheila kustuka

Endelea.....
Sheila kwa haraka akarudi nyuma ya mama na kujificha,mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa mshangao
“eddy mwanangu unataka kufanya nini?”
“nataka kujua huyu mwanamke kwa nini amesema kuwa mimi nimechanganyikiwa”
“hujachanganyikiwa mwanangu,tulikuwa tunazungumza kuhusiana na baba yako mzee godwin kwamba amechanganyikiwa”
 
“mama na wewe unashiriki zambi ya uongo?”
“kweli mwanangu,aliniambia kuwa amemuona sehemu fulani katikati ya jiji akiwa anaruka ruka”
Nikamtazama mama kisha nikakaa kwenye sofa na kuiweka bastola pembeni yangu.Sheila akabaki akinitazama huku akiwa hana la kuzungumza.Wote wakaka na kunitazama,ukimya ukatawala ndani ya dakika kadhaa mama akaamua kuuvunja ukimya.
 
“eddy na hiyo bastola yangu unakwenda nayo wapi?”
“kuna kazi ninataka kwenda kuifanya”
“eddy mwanangu,hembu niambie ni nini tatizo linalo pelekea kuwa na roho kama hiyo kwa maana umerudi hujazungumza na mimi vitu vingi zaidi ya kwenda kulala?”
 
“mama bado mimi nipo,tutazaungumza kila kitu”
“sawa,ila kwanini ume......”
Nikauona mguu wa rahma ukiukanyaga mguu wa mama na kumfanya asiimalizie sentesi yake.
“kwa nini umekaa huko mbali pasipo kuwa kunijulisha?”
“huyo hajakuambia?”
“yeye atajuaje mtoto wa watu?”
“ahaa mama hiyo mada tutazungumza kesho.Oya ninaomba funguo”
“za nini?”
Sheila alizungumza kwa sauti ya upole na yenye unyeyekevu mkubwa
 
“funguo za gari na nyumba yako.”
Sheila akafungua pochi yake na kunipa.
“mbona umevaa nguo hizo hizo ulizo kuja nazo?”
Nikajitazama  kuanzia chini hadi juu,nikarudi chumbani kwangu na kuvaa nguo zangu vizuri,nikaichomeka bastola kiunoni mwangu na kuifunika na tisheti nyeusi niliyo ivaa,nikurudi sebleni.
 
“wewe twende basi home”
Sheila akatazama na mama kisha akanitazama na mimi
“mmmm nitalala na mama”
“hutaki au?”
“eddy muache mwenzako alale hapa,kwani huku kwake unakwenda kufanya nini?”
“kulala”
Nikataka kutoka na mama akaniita
 
“bastola yangu ipo wapi?”
“nimeirudisha”
“wapi?”
“kwani mama ilikuwa wapi?”
“basi baba nenda salama”
Nikatoka na kuufunga mlango vizuri.Nikasimama pembeni ya dirisha na kusikilizia ni nini mama na sheila watakizungumza,kwa kupitia uwazi ulioachwa na dirisha nikawaona wakikaa kwenye sofa
 
“mbona mwanangu amebadilika namna hii?”
“mama wee acha tuu,eddy mimi ninampenda ila kwa hapa alipo fikia ninamuogopa mama”
“mmmm usimuogope”
“mama eddy kuna kipindi alipokuwa na hasira mimi nilikuwa nikimtuliza  na kumsogelea,ila sasa hivi mmmmmm ni bora nimtoroke toroke hadi atakapo kaa sawa”
 
“itabidi nitafute madaktari watakao muhudumia”
“ni kweli mama,yaani mtu anazungumza kwa sauti nzito kama simba dume”
“ila mwanangu huyu anaugonjwa wa asira,mimi wala simshangai sana kwani kuna kipindi akiwa mdogo alisha wahi kumuua mwenzake shule kwa kumpiga na chupa ya soda kichwani”
“weeeee?”
 
“ooohhh ilikuwa ni kesi kubwa kilicho muokoa ni udogo wake kwa alikuwa na miaka mitano”
“mama ina maana eddy kuua hakuanza leo?”
“eddy mwangu akiwa na hasira si mtu wa kumsogelea,nilisha mpeleka hadi kwa wachungaji wamuombee ila wapii.Nilijaribu kutafuta wana saikology labda wakae nao ila imeshindikana.Kila dawa ambayo niliambiwa inafaa kwa kipindi hicho kuwa kama kitulizo cha ugonjwa wake ila wapi?”
 
“mmmm”
“yaani na haya matatizo yaliyo tokea hichi kipindi cha hivi karibuni naona pia yanachangia sana”
Nikataka kuondoka niwahi ninapotaka kwenda ila swali la sheila likanifanya nipige hatua kadhaa kurudi dirishani
“kweli mama,hivi mzee godwin yupo wapi?”
“hadi leo sijamuona,mimi mwenyewe ninafanya uchunguzi nije kumuona ila hadi sasa hivi sijapata jibu”
 
“mama  tutasaidiana katika hilo,yule mzee ni muuaji sana”
Sikuona haja ya kuendelea kusikiliza mazungumzo yao zaidi ya mimi kuondoka,nikaingia ndani ya gari na mlinzi akanifungulia geti na kuondoka,nikafika kwenye kituo cha kuongeza mafuta.Nikajaza tanki la gari na kulipa kiasi ambacho kimegharimu kiasi hicho cha mafuta.

Njia nzima nikawa ninafikiria ni wapi alipo mzee godwin.Nikafika nyumbani kwa sheila na kushuka kwenye gari na kufungua geti,nikaliingiza gari ndani na kufunga geti.Nikafungua ndani na kuchukua kirimoti cha kufungulia sehemu ya kuifadhia gari,nikaingia na kuchukua turubai lenye mwili wa derick ambao niliubanika vizuri
 
Nikauingiza ndani ya buti la gari na kulifunga vizuri,nikafunga kila sehemu kama nilivyo iacha,kabla sijatoka nikakumbuka simu ya derick niliiacha sofa nikiwa nimeizima,nikaingia ndani na kuichukua ila sikuiwasha,nikafungua geti na kutoa gari.Nikarudi kulifunga na safari ya kuelekea arusha ikaanza,kutokana ni usiku sana hapana magari mengi zaidi ya maroli ya mizig ambayo yanakwenda kwa kasi na usipo kuwa makini utajikuta ukigongwa.

Nikazidi kuongeza mwendo na kimoyo moyo nikawa na kazi ya kumuomba mungu nisipate ajali kwani mwendo ninao tembea nao endapo nitakubwa hata na baiskeli basi kitakaocho endelea kwenye kuanguka nahisi kitakuwa ni kifo tu.Kwa hofu nikapunguza mwendo kutoka spidi 250 hadi mia moja japo gari bado ipo kwenye mwendo mkali sana.
 
Mwanga mkali wa gari linalokuja nyuma yangu ukaanza kuniumiza macho,nikapunguza mwendo na kumuwashia taa nikimuashiria apite kwani sikuweza kuendesha kwa jinsi taa zake zinavyo niumiza macho kupitia vioo vya pembeni.Nikashuhudia gari aina ya ‘hammer’ yenye rangi nyeusi na vioo vyake vyote vikiwa ni vyeusi na limefungwa likinipita,haikuwa ni moja zikapita nyingine mbili zikiwa katika kwendo kama ilivyo gari ya kwanza
“mmmmmm ni kina nani hawa?”
 
Nilijiuliza maswali,na mimi nikaanza kuongeza mwendo wa gari langu.Jinsigari hizi zinavyozidi kwenda ndivyo nami nilivyodidi kuongeza mwendo,nikaanza kuzikaribia kwa karibu.Nikawasha taa zote za gari langu ili na mimi nimtese dereva wa gari la nyuma.Nikashanga kuona gari mbili za nyuma zikitanda barabarani na kunizuia kupita.Nikaanza kupatwa na mashaka baada ya madereva hao kuanza mtindo wa kupunguza punguza mwendo gafla gafla na usipo kuwa makini unazigonga kwa nyuma.
 
Kwa mbele likawa linakuja lori ikatulazimu sote kubana upande mmoja kuliacha lipite na mchezo ukarudi na kuwa wa kuzuiana kupita.Hadi tunafika daraja la wami ndio gari hizo zikapunguza mwendo kulikwepa fuso lililo haribika pembezoni mwa barabara
 
Tukalimaliza daraja,nikaona jamaa wananichelewesha nikamuomba dereva wa nyuma kuweza kupita akaniruhusu,nikiwa ninamaliza kuliacha gari la nyuma gari la pili kutoka mbele likatanda barabarani na kuongeza mwendo.Dereva wa gari la nyuma akaongeza kasi zaid na kutanda kwa nyuma wakawa wameniweka katikati.Kwenye kioo kidogo kilichopo pembeni ya mskani kwenye gari langu nikaanza kuwaka taa nyekundu na kutoa maandishi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa.
 
{habari yako bwana eddy,gari yako ipo kwenye wakati mgumu wa usalama.Kama unataka ulinzi minya hapa au unaweza kukata}
 
Nikaminya sehemu yenye alama ya tiki(pato).Sikushangaa sana kwa maana hili gari aina ya bmw 007 limetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu na ninakumbuka sheila aliniambia kwamba amepewa na wamarekani weusi alio cheza nao filamu ya ngono.Gari ikaanza kurudi chini kidogo kisha vioo vyote kasoro cha mbele vikapitiwa na ukungu mweusi ambao sikujua ni wa nini.
 
Kwenye kioo kidogo nikaona gari la mbele na la nyuma,nikaonyeshwa jinsi zivyo ndani na idadi ya watu waliomo ndani wakiwa katika hali ya mifupa(mafuvu).Nikiwa ninashangaa shangaa nikastukia nikigongwa na gari ya nyuma na kunifanya nishindwe kulizuia gari na likamgonga gari la mbele.
 
Nikastukia kuona jamaa wawili kwenye gari la mbele wakichomoza kwenye vioo vya pembeni na kuanza kunishambulia kwa kutumia bunduki zao,kitu kilicho nistaajabisha ni jinsi risasi hizo kushindwa kuingia ndani ya gari langu.Nikaanza kujiamini kuwa gari yangu imepata kweli ulizi,nikakanyaga breki za gafla na kusababisha gari la nyuma kunigonga na kuanza kuzunguka barabarani kwa kasi na kuacha njia na kuvaamiti iliyopo pembezoni mwa barabara na kupinduka.

Nikaachia breki na kulifukuzia gari la mbele ambalo kidogo liliniacha kutokana na mwendo wao wa kasi,nikalisogelea kwa ukaribu,kila ninapo jaribu kulipita wananizuia.Nikaongeza mwendo,kutokana na gari yangu kuwa chini kidogo likaweza kupiga tairi za nyuma na kulifanya linyanyuke kidogo na dereva wake kushindwa kulimudu na kuanguka vibaya na kuanza kubingirika likiingia msituni.
 
Gari la mbele likapunguza mwendo na kutokana lipo mbali kidogo na mimi, likafunga breki za nguvu na kwa utaalamu mkubwa dereva wa gari hilo aliweza kuligeuza na likawa limegeuka nilipo mimi.Nikapunguza mwendo  hadi nikasimama mita chache kutoka lilipo gari langu.Derevaa wa gari lililopo mbele yangu akaanza kuvuta mafuta huku akiganyaga breki na kuzifanya tairi za gari lake kuzunguka kwenye lami pasipo kwenda mbele na kuzifanya zitoe mlio fulani.Nikazima taa za gari langu na dereva akazima za kwake.Nikawasha za kwangu ila nikajikuta nikinshangaa dereva wa gari hilo kwani anafanana sana na manka japo simuoni vizuri ndani ya gari hilo.

Gafla nikalishuhudia roli linalo malizia kona iliyopo karibu na lilipo simama ‘hammer’,sikujua kama dereva wa hammer ninaye mfananisha na manka kama ameliona lori hilo au la kwani anaendelea kuzifunga breki za gari lake katikati.Nikazisika honi za lori zikimuashiria dereva wa hammer kuondoka barabarani,ndani ya sekunde kadhaa nikastukia kuona lori likiligonga kwa nyuma hammer na kulisogeza pembeni ya barabara na lori likapita pasipo kusimama.
 
Ukimya ukatawala kesemu nzima,nikataka kuondoka ila nikataka kujua niliye muona ni manka kweli au sio yeye.Nikalisimamisha gari pembeni,nikaichomoa bastola yangu,nikafungua mlango na kushuka ndani ya gari.Nikatazama pande zote za barabara hapakuwa na gari lolote linalo kuja.Nikaanza kutembea kwa mwendo wa tahadhari hadi sehemu lilipo anguka gari la watu ambao ninahisi sio watu wazuri.Nikalisogelea taratibu.Nikachunguza ndani na kumuona mtu moja aliye kaa pembezoni mwa dereva akiwa amekitwa na kisiki cha mti kwenye kichwa na amefariki hapo hapo,siti za nyuma zilijaa maboksi makubwa na hapakuwa na mtu wa aina yoyote.

Dereva wa gari ambaye ni mwanamke aliendelea kujitahidi kutoka ndani ya gari pasipo kugungua kama mimi nipo eneo hilo.Akasimama huku nywele zake nyingi zikiwa zimemfunika usoni mwake,akakutana na mdomo wabastola yangu.Akajiweka nywele vizuri na nikahakikisha ni manka kwani akawa ni wakwanza kuliita jina langu
“eddy”
“naam”
 
Tukakosa cha kuzungumza,uvaaji wa manka unaashiria kuwa ni jambazi kwani kuanzia juu hadi chini amevaa nguo nyeusi tupu zinazo endana na nguo za jeshi.Mikono yake amevaa gloves nyeusi.Kifuani amejifunga jaketi la kuzuia risasi(bullet proof).Kiunoni mwake anabastola mbili zilizo chomekwa kwa kwenye kiuno
 
“umeumia?”
“hapana”
“tuondoke”
“hapana ngoja kuna kitu tusaidiane”
“nini?”
“kutatoa haya maboksi”
 
Sikutaka kuuliza yana nini zaidi ya kusaidiana kwa pamoja kuyatao maboksi mawili makubwa kiasi.Kwa uzuri yakaingia kwenye gari langu siti ya nyuma.Manka akachomoa bastola yake na akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuftatua risasi kazaa kwenye tanki la mafuta ya gari lao na likalipuka.Akaingia ndani ya gari langu na safari ikaendelea.Dakika kumi nzima ndani ya gari hakuna aliye msemesha mwenzake.
 
“eddy usiku huu unakwenda wapi?”
“arusha”
“kuna nini?”
“kuna ishu ninakwenda kufanya na wewe je?”
“nitakuambia tukitulia”
“boksi zina nini?”
“pesa”
“pesa.....!!?”
“ndio”
“za nani?”
“ndio maana ninakuambia nitakuambia tukitulia”
 
Nikazidi kuongeza mwendo na ndani ya masaa mawili tukawa tumefika arusha.Tukafika hadi kwenye mtaa wa wachaga na tukaingia kwenye moja ya nyumba iliyo tulia sana.Manka akashuka kwenye gari na kufungua geti na mimi nikaliingiza gari ndani akafunga huku akitazama pande zote kisha akalifunga geti.Akafungua mlango wa nyumba hiyo na tukayaingiza maboksi yote ndani.Tayari mwanga wa jua ulisha anza kuchomoza kwa mbali ikiashiria ni asubuhi.
 
“oya mimi ngoja nikapige mishe ninayo itaka kisha nitakustua”
Nilimuambia manka ambaye alianza kukata biksi moja kwa kutumia kisu.Nikashuhudia vibunda vya elfu kumi kumi vikiwa vimejaa ndani ya boksi 
 
“nimeshatoka kimaisha mpenzi”
“mmmm....”
Manka akanirushi kibunda kimoja cha pesa kuku vingine akivitoa na kuvirusha rusha juu kwa furaha.Manka akanifwata na kunikumbatia kwa furaha huku akinipiga mabusu mdomoni
“eddy furaha yangu imekamilika sasa”
“kwa nini?”
 
“nina pesa na nimekupata wewe,nilikutafuta kwa siku nyingi mpenzi wangu”
Wazo la manka kuwa ni dada yangu likanijia akilini mwangu.Nilipo kumbuka kuwa baba yake ni baba mkubwa nikakaa kimya pasipo kujibu chochote.
“nikupeleke sehemu ambayo unataka kwenda?”
“hapana”
“twendwe wote bwana”
“ila ubadilishe nguo zako”
“unadhani sina akili,nilazima nibadilishe”
 
Manka akaniachia na kuingia kwenye moja ya chumba.Baada ya muda akatoka akiwa amejiremba na mtu unaweza kumsahau kama yeye ndie aliyekuwa akiliendesha gari la majambazi.Nikalitoa gari nje,akafunga geti lake,akaingia ndani ya gari nasafari ikaanza.Nikalisimamisha gari nje ya geti la madam mery
 
“hapa kama napajua?”
“ni kwa mwalimu wangu mmoja”
“namjua si yule mery?”
“ndio,ila nisaidie kitu”
“kitu gani?”
“ninaomba ukagonge”
“alafu”
Nataka kuingiza gari humo ndani”
 
Manka akashuka kwenye gari na kuaza kugonga geti,dakika kama mbili gati likafunguliwa na madam mery.Wakasimuliana kwa furaha na madam mery.Kutokana na kufunga vioo vya gari langu madam mery hakuweza kuniona.Madam mery akazungumza kidogo na manka kisha akafungua geti na manka akarudi ndani ya gari.

Nikawasha gari na kuliingiza ndani.Manka akawa wa kwanza kushuka,nilipo hakikisha madam mery amefunga geti na kuanza kwenda ndani kwake ndipo na mimi nikashuka.Madam mery akastuka kuniona.Akataka kuingia ndani ila akakutana na john rafiki yangu akiwa amevaa kibukta akiwa tumbo wazi ikiashiria john na madam mery wanamahusiano ya kimapenzi.John akapigwa na bumbuazi kana kwamba anasubiria kupigwa picha ya mnato hii ni baada ya kuniona.....

                               *****sory madam*****(46)

.....Sikuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzunguka nyuma ya gari,nikafungua buti ya gari na kutaka kulitoa turubai lenye mwili wa derick,nikafikiri kwa  muda kidogo kisha nikalifunga buti pasipo kulitoa turubai
“john niaje?”
“ahaa....Ahaa powa”
John alinijibu kwa kubabaika nikabaki nikitabasamua na kumfwata manka sehemu alipo simama
“jamani,hamutukaribishi ndani?”
 
Niliuliza na kumfanya madam mery kushtuka,akatabasabu kiwoga huku midomo yake ikitetemeka akishindwa hata kuzungumza anacho taka kukizungumza
“nd...Aaaniii kar..Ibu....Ni”
 
Manka akabaki akiwa anashangaa kwani hali ya kuzungumza kati ya madam mery na john zilibadilika kwa kiasi kikubwa.Madam mery akaongoza msafara wa sisi kuingia ndani kwake,mtu wa mwisho kuingia ndani nikiwa ni mimi.Nikaufunga mlango na kwabahati nzuri nikakuta funguo ya mlango ikiwa inaning’inia mlangoni.Nilipo hakikisha nimeufunga mlango nikaidumbukiza fungoa mfukoni mwangu na kukaa kwenye moja ya sofa.
“madma kwako kumebadilika”
 
Nilizungumza kinafki kwani hapakuwa na mabadiliko yoyote tangu nilivyo paacha siku ya mwisho ninapambana na muwe ndivyo nilipo pakuta.Kikubwa kilicho badililika ni vitambaa vya makochi ni meza mpya ya kioo
 
“john,masomo yanaendeleaje?”
“masomo kidogo yapo vizuri”
John alizungumza kwa sauti ya unyonge nayaupole sana,huku sura yake ikiwa inatisama chini kwa aibu anashindwa hata kunitazama usoni
 
“sasa,ndio munaingia kidato cha sita?”
“ndio”
“hongereni”
Wakati ninazungumza na john.Madam mery na manka walikaa kimya wakitusikiliza.Macho yangu nikayahamishia usoni mwa madam mery ambaye naye hakutaka kabisa kunitazama usoni
 
“wenyeji mbona mumepooza gafla?”
Manka alizungumza na kuwafanya john na madam mery kunyanyua nyuso zao na wakazipamba kwa tabasamu ambalo kwangu ninajua ni tabasamu lililo jaa aibu na ninavyo hisi kila mmoja anaomba ardhi ipasuke na immeze
“haaa sisi,tunazungumza”
 
Madam mery alizungumza manene ambayo kama mtu mzima mwenye akili zake hawezi kuzungumza pumba kama hizi kwa maana kwa muda wote yupo kimya kama amejaza fumba la uji wa bada(uji wa unga wa miogo)
“ngoja nikawaandalie hata chai wageni wangu”
 
Madam mery alizungumza huku akinyanyuka.Nikamtazama na kutingisha kichwa nikiashiri nimekubali akafanye kazi hiyo.
“manka yule ni rafiki yangu anaitwa john,john huyu ni manka ni zaidi ya ndugu yangu”
“nashukuru kwa kumfahamu”
Manka akanyanyuka na kumpa john mkono kama wa kusalimiana kwa mara nyingine tena
“mimi ngoja niende msalani”
“sawa”
 
Nikanyanyuka na kuondoka sebleni na kuwaacha manka na john.Nikapitiliza moja kwa moja hadi jikoni na kumkuta madam mery akiwa ameuegemea ukuta,akionekana kuwa katika mawazo makali na mazito yanayo mfanya ashindwe hata kutazama maji yanayo mwagika kwenye jiko la gesi,baada ya kuchemka sana.Hadi ninazima jiko ndio madam mery anastuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo
“unawaza nini?”
“aahaa hakuna”
“siku hizi unaniongopea hata mimi?”
“eheee,”
 
“ehee,unaisoma au unaiandika?”
“tuachane kwanza na hayo,mume wako yupo?”
“nimeachana naye?”
“umeachana naye,kisa ni nini kilicho wafanya muachane?”
“wee acha tuu.Ila kila kitu wewe unakijua?”
“mimi,mbona kama sikumbuki?”
“eddy usinikumbushe ya nyuma”
“kweli? Ok labda nikutokana na kupoteza kwangu kumbukumbu”
 
Nilizungumza kwa sauti ya upole kwa kumtega madam mery.Ukimya wa dakika kama tatu ukapita huku kila mmoja akiwa atamtazama mwenzake
“mery”
“una nipenda?”
“ehee?”
“unanipenda?”
“mimi?”
“wewe,ndio?”
“ndio”
 
“kwa nini umeamua kutembea na rafiki yangu?”
“ehee.....Ahaaa uun....Ajua”
“najua nini?”
“wewe.....Wewe ulikuwa umepotelea wapi sijui?”
“hujanijibu swali langu”
“ahaa eddy tuachane na hilo bwana”
“sawa.Nataka kuliona kaburi la mwanangu”
“eheee”
“hivi hizo eheee zako ni za nini,mimi sizipendi bwana”
“eddy,sikumzika mwanao”
 
Nikakaa kimya nikimtazama ni nini anataka kuniambia
“ila ile siku nilikuwa nimechanganyikiwaa,na nilipomuwahisha mfanyakazi hospitalini.Nilipo rudi nilikuta mbwa wanamalizia kumla mwanao,huku wewe ukiwa umelaa pembeni”
Nikamtazama mery kwa macho makali yaliyo anza kuchuruzikwa na machozi ya uchungu
“wewe ni mama wa aina gani,hujui dhamani ya utu wa kiumbe ulicho kiweka tumboni miezi tisa.Unaacha kinaliwa na mbwaa?”
 
“eddy nilichanganyikiwa,niliucha mlango wa ndani wazi.Na mbwa ile siku msichana wa kazi aliwafungulia na siku zote mchana wanashinda kwenye banda lao”
“merry nidanganye kwa kingine ila sio kwa hili”
“eddy ni kweli.Hata mimi ninauchungu moyoni mwangu kuona kiumbe changu kina.....”
 
Niliunyanyua mkono wangu kwa kasi na kutaka kumpiga madam mery kofi la shavuni ila nikajizuia kabla halijatua shavuni mwake na kumfanya afumbe macho.Nikaushusha mkono wangu taratibu na kumtazama madam mery kwa macho makali nikaachia msunyo mkali,kabla sijazungumza kitu chochote manka akaingia na akabaki akiwa anatutizama.Nikajifuta machozi na kutoka jikoni na kuwaacha wao wawili
 
“naona umeamua kuniridhi kabla sijafa?”
Sauti yangu ilimstua john ambaye nimemkuta akiwa anapiga hatua za kunyata akielekea kwenye mlango wa kutokea huku nguo zake akiwa ameziweka begani
“mbona unaondoka bila kuaga?”
 
John hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kubaki akiwa amesimama kama mlingoti wa bendera.Kwa ishara nikamnyooshea mkono arudi sehemu alipo kuwa amekaa.Akabaki akiwa amesiama asijue nini afanye,nikaichomoa bastola kiunoni hapo ndipo nilipo mafanya john,kuanguka chini kama mzigo.Akajizoa zoa na kunipigia magoti
 
“eddy....Ni shetani amenipitia tu,ila sikukusudia mimi kulala na madam mery”
John alizungumza huku akimwagikwa na machozi
“john,mimi sina ugomvi na wewe.Tutabaki kuwa marafika hadi mwisho wa maisha yetu.Hawa ni wanawake hawawezi kutugombanisha”
 
Maneno yangu yakamfanya john kuunyanyua uso wake na kunitazama machoni,akayashusha macho yake hadi shehemu ilipo bastola kisha akayarudisha macho yake usoni mwangu.Nikatambua kuwa anaihofia bastola niliyo ishika,nikaichomeka bastola yangu kiunoni mwangu.Wasiwasi wa john kidogo ukapugua.Nikaunyuosha mkono wangu na kumpa john,akanipa na yeye mkono wake kisha nikamnyanyua na kumvuta juu na kukumbatiana naye.
 
“eddy sijaamini ndugu yangu kama nitakuona tena”
“hata mimi”
“asante ka.....”
Sikumpa john nafasi ya kuzungumza chochote,kigoti cha mguu wangu wa kulia kikatua tumboni mwake na kumfanya ajikunje na kutoa ukulele mkoali.Nikamsukuma pembeni kwa  nguvu,kwa haraka nikamfwata na kuanza kumpiga mateke ya mbavu.
 
“hivi unajua uchungu wa mwanamke aliye beba kiumbe changu?”
“john unanijua mimi vizuri,unajua ni kitu gani ambacho ninakifanya kwa wale wanao jaribu kuniibia kitu chochote kutoka kwangu”
 
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikiendelea kumpiga john mateke ya mbavu.Kelele za john zikawatoa kwa kasi jikoni madam mery na manka
“eddy mu......”
Manka alizungumza kabla hajaimalizia sentesi yake,niliichomoa bastola yangu na kumnyooshe na kusimama sehemu alipo.Madma  mery kwa haraka akarudi nyuma ya manka na kujificha mgongoni mwake.
 
“eddy kuwa mpole mpenzi wangu.Kwa nini unafanya hivyo?”
“manka mimi sio mpenzi wako”
Manka akakaa kimya akinitazama kwa umaki akishindwa cha kuzungumza.Nikamtazma john ambaye amejikunja chini huku akilia.Nikairudisha bastola yangu kiunoni nikampiga john teke jengine la mbavu
 
“usirudie”
Nikampa john mkono,akabaki akinitazama kwa woga.Nikainama na kuushika mkono wake kwa nguvu na kumyanyua na kumkumbatia
“wanaume huwa ahtulii”
Nikamuachia john na kumkalisha kwenye sofa.Nikawageukia manka na madam mery,tukatizamana kwa muda
“mbwa wako wapo wapi?”
“huko nyuma”
 
Nikatoa funguo na kufungua mlango na kutoka nje.Nikazunguka nyuma ya gari na kufungua biti ya gari na kutoa turubai lenye mwili wa derick.Manka akatoka na kusimama mlangoni na akabaki akiwa amenitazama.
 
“umebeba nini?”
“unataka kuona?”
“ndio.”
“muite huyo mwenzako”
“nani?’
“huyo mery”
Manka akamuita madam mery,madam mery akatoka akiwa katika hali ya kiunyonge
“shosti umeniambia umbwa wako wapo wapi?”
“huku nyuma”
“nimewaletea chakula,twende basi ukanionyeshe”
 
Madam mery akashuka kwenye kibaraza na kuongoza kwenda nyuma ya nyumba yake kwenye mabanda ya mbwa.Kwa uzuri wa yumba ya madam mery imezungushiwa ukuta ulio mrefu na si rahisi kwa mtu wa nje kuweza kuona chochote kinacho endelea ndani.Nikakuta mabanda manne nyenye mbwa wengi wakubwa kwa haraka ninaweza kuwafananisha na mbwa wa jeshi la polisi kitengo cha kutuliza ghasia(f.F.U)
 
“mbwa walio mla mwanagu ni wapi?”
“hao kwenye hilo banda kubwa”
“mbona una mbwa wengi hivi”
“huwa ninawauzia wachina,mbwa mmoja naweza akafka hata dola elfu tatu”
 
Madam mery alizungumza kwa sauti ya unyonge.Nikaliweka turubai chini kabla sijalifungua,manka akaniita
“eddy naomba funguo za gari,kuna kitu nataka nikachukue ndani ya gari”
Nikaanza kujipapasa mfukoni,wakati ninatoa funguo simu ya mume wa madam mery ikaanguka.Manka akataka kuiokota ila nikamzuia,nikamkabishi manka funguo
“hakikisha john aondoki”
“sawa”
 
Manka akaondoka na kumfanya madma mery kubaki kimya akiitazama simu ya mume wake kwa umakini hadi sura yake ikatengeneza mikunjo.Nikaiokota simu na kumpa madam mery
“naomba unishikie hii simu”
“eddy,hii simu kama ya mume wangu?”
“ahaaa...Wewe si umesema umeachana naye?
“ahaaaa eheeee”
 
Madam mery akabaki akinitazama,nikalifungua turubai,nikamtazama machoni madam mery na akastuka kuona viungo vya mwili wa mtu kwenye turubai nililo lifungua.
“mbwa yupi likuwa mmero kwa kumtafuna mwanangu?”
 
Madam mery akabaki akiwa anashangaa shangaa,nikaokota kipande cha mkono na kukirushia ndani ya banda la mbwa wakakivamia na kukigombania kwa haraka na kuanza kukila
“kwa msosi huu lazima mbwa mmoja utamuuza hata kwa dola elfu kumi”
 
Madam mery akabaki akiwa ameuziba modomo wake kwa kiganja cha mkono wake wa kulia.Nikachukua vipande viwili na kuvidumbukiza kwenye banda
“ed.....Si ni mume wangu?”
“shiiiii,mume wako yupi? Wewe si umeachana naye?”
“eddy mtu wako nimemfunga kamba,nilimkuta anataka kukimbia”
 
Manka alizungumza huku akisimama na kujishika kiuno na macho yake yakiwa kwenye turubai
“eddy si mwili wa mtu huo.....!!?”
Manka alizungumza kwa mshangao
“kwani vipi?”
“umeutoa wapi?”
“wee acha tuu”
“ni mume wangu”
 
Madam mery alizungumza huku akikaa chini,gafla akaanza kutapika baada ya kuona ninatoa kipande cha utumbo ulio kauka na kuingiza kwenye banda la mbwa.Nikavirusha vipande vyote vya mwili wa derick kwenye mamanda yote ya mbwa.
“hichi kichwa madma utachemsha kama supu ya mbwa wako”
Manka akanitazama kuanzia chini hadi juu,madam mery akazidi kutapika.
“eddy you’re a mouster”
 
Manka alizungumza huku akinitazama kwa macho makali.Akamnyanyua madam mery.Wakanza kuelekea ndani,kichwa cha derick nikakirudisha ndani ya turubai na kulibebe turubai langu na kulirudisha ndani ya buti la gari.Nikaingia sebleni na kumkuta madam mery akiwa amelazwa kwenye sofa kubwa huku mwili mzima ukimtetemeka
 
“john yupo wapi?”
Nilimuuliza manka,ila akakaa kimy akabaki akinitazama kwa hasira.
“manka si ninaungumza na wewe?”
“kamtazame huhko jikoni”
Nikaichukua simu ya derick ambayo madam mery ameiweka pembeni ya sehemu aliyo lala
“sory madam,nilifanya hivi kwa ajili ya damu yangu”
 
Nikaingia jikoni na kumkuta john akiwa amefungwa kama za mkono na miguuni huku amelazwa chini kifudifudi.Nikakaa pembeni yake
“john shule kunasemaje?”
Nilizungumza kwa dharua,huku taratibu nikimshika shika kichwa chake
“eddy mbona umekuwa katili kiasi hichi,unamtuma huyu mwanamke wako kunifunga hivi kama mwizi”
 
“wewe unajionaje,si ni mwizi.Laiti kama ungekuwa hujaniibia madam mery haya yote yasinge tokea”
“sawa eddy,najua kama nimekuumiza ila si kunifanyia hivi.Laiti kama ungejua wema nilio kufanyia wala usinge nifanyia hivi”
“wema gani?”
“eddy mimi nimekufanyia mitiahani yako ya kuingia kidato cha sita na umefaulu vizuri”
“kivipi,wakat wewe una mitihani yako?”
 
“eddy mimi nilimuhonga mwalimu wa academy.Aliniruhusu nikufanyie mitihani.Sasa jana wakati ninakuja kumuuliza madam mery kuwa anataarifa yoyote kuhusiana na wewe ndipo alipo nishawishi hadi nikalala naye.Halikuwa kusudio langu mimi kufanya hivyo.Kwa bahati mbaya leo wewe ukaja na kutukuta katika mazingira kama hayo”
John alizungumza kwa upolenhadi roho ya huruma ikaanza kunijaa moyoni mwangu
 
“eddy,wewe ni zaidi ya ndugu yangu.Kumbuka wapi tulipo toka.Kuanzia kidato cha kwanza tupo pamoja.Hadi sasa hivi,kwa nini lakini ndugu yangu”
“ila john...Wewe tangu kidato cha kwanza.Unajua jinsi nilivyo,mtu yoyote anaye jaribu kuniibia mimi kitu changu chochote nilazima akilipe kwa njia yoyote”
 
“ndio ninalijua hili,na madam aliniambia kitendo cha yeye kufanya hivi ni juzi,alimpigia mumuwe na akapokea mwanamke na akatukanwa sana ndio maana akaamu kunishawishi mimi”
 
“john.....”
“naam”
“nakuomba unisamehe kaka”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika
“usijali kwa hilo kaka,ninatambua umefanya hivi kwa ajili ya hasira tuu”
“ni kweli”
Nikaanza kumfungua john kama moja baada ya nyingine.Nikasimama na kumsaidia kumyanyua.
“mbavu zinaniuma sana”
“pole,nikupeleke hospitalini”
“ahaa wee acha tuu nipo vizuri”
 
Jinsi john anavyo zungumza nilijihisi vibaya moyoni mwangu,nikaanza kujilaumu ni kwa nini nimempiga john pasipo kumuuliza chanzo cha yeye kunisaliti.Tukarudi sebleni na kumkuta madam mery akiwa amelala na manka akiwa pembeni yake.Manka akanyanyuka na kunishika mkono na tukatoka nje
“eddy,japo mimi ni katili ila wewe umezidi”
“manka naomba hiyo mada uiache”
“eddy hata kama.Mwili wa binadamu mwenzako unaukausha kama nyama nya ng’ombe”
 
Nikaanza kumuadisia manka kuanzia mwanzo wa ugomvi kati yangu mimi na derick.Hadi ninamaliza kumuadisia manka akabaki kimya.Tukakaa nyumbani wa madam mery hadi mida ya saa moja waote wanne tukapata chakula cha usiku kilicho pikwa na manka japo madam mery anapata tabu sana ya kula.Mimi na john tukaondoka na kwenda shule nikiliacha gari la kwa madam mery.
“leo kuna welcome form five”
 
Kawaida kwenye shule yetu kila wanafunzi wa kidato cha tano wanapo jiunga na shule yetu huwa hufanyiwa sherehe wiki tatu baada ya kujiunga na shule.Wezangu ambao nilipotezana nao kwa kipindi kidogo wakaonekana kunifurahia.Mida ya saa mbili tukaingia ukumbini huku nikiwa nimevaa swete lenye kofia.Tuliongozana wanafunzi wa kidato cha sita wapatao nane ila mwalimu ambaye machoni mwangu ni mpya akanisimamisha na kuwaacha wezangu kupita
“vua kofia ya sweta”
 
Alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo.Nikiwa ninavua kofia,mkuu wa shule ambaye tunawindana kama paka na panya naye akawa anaingia ndani ya ukumbi huku akiwa ameongozana na mkuu wa shule.Akabaki akinitazama kwa hasira na kuanza kupiga hatua za haraka kunifwa huku mikononi mwake akiwa amekunja ngumi....
 
Itaendelea...

 Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts