Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 47 & 48 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 47 & 48 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Vuvuzela on Thursday, September 15, 2016 | 7:30:00 AM

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
Alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo.Nikiwa ninavua kofia,mkuu wa shule ambaye tunawindana kama paka na panya naye akawa anaingia ndani ya ukumbi huku akiwa ameongozana na mkuu wa shule.Akabaki akinitazama kwa hasira na kuanza kupiga hatua za haraka kunifwa huku mikononi mwake akiwa amekunja ngumi

Endelea...
Nikaanza kurudi nyuma huku nikimtazama mkuu wa shule,akazidi kuja kwa kasi ikanilazimu kusimama nikimtazama kwa umakini.Wanafunzi wote wakawa na hamu ya kuangalia ni nini ambacho atakifanya mkuu wa shule.Hatua chache kabla hajanifikia nikaifunua tisheti yangu sehemu ya kiunoni na kumuonyesha bastola niliyo ichomeka kiunoni.Kidogo akapunguza kasi hadi ananifikia munkari wote ulimuishia.
 
“toka katika shule yangu”
Alizungumza huku meno yake ameyang’ata kwa hasira.Nikamtizama na macho makali na ukumbi mzima wa shule upo kimya hata kijiko kikianguka mlio wake utasikika vizuri.
“sitoki”
 
Wanafunzi wote wakashangilia,mkuu wa shule akawatizama wanafunzi na wakakaa kimya
“walinzi mupo wapi?”
Mkuu wa shule alizungumza kwa sauti kubwa,hapakuwa na mlinzi hata mmoja aliye nifwata kila mlinzi aliye niona kuwa ni mimi aliishia mlangoni na kusimama.Mmiliki wa shule akatufwata sehemu tulipo simama na mkuu wa shule
“jamani,kuweni wapole.Mkuu unaniambisha bwana”
 
Mkuu wa shule akajifanya kama hamsikii muajiri wake,kitu kinacho niumiza kichwa ni kwanini mkuu wa shule hadi leo yupo wakati amafanya mambo ya ajabu hadi muda huu hajachukuliwa hatua zozote.Akanisogea katibu yangu,nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu.Nikataka kulipiza nikaisikia sauti ya john ikiniita jina langu na nilipo mtizama nikamkuta john akitingisha kichwa akiniashiria nisifanye chochote
 
Mkuu wa shule akanitandika kibao cha pili,ila john akawa na kazi moja ya kuniomba hadi machozi yakawa yanamwagika,nisilipize chochote kwa mkuu wa shule.Machozi ya hasira yakaanza kunimwagika,huku kifua changu kikianza kutanuka kwa hasira kali,akataka kunitandika kofi la tatu nikamdaka mkono wake.
“nitakuua”
 
Nilizungumza kwa sauti ya ukakamavu,huku macho yangu yakimtazama mkuu wa shule.Akajaribu kuuchomoa mkono wake kutoka kwenye mkono wangu ila akashindwa.John kwa haraka akaja na kuingia katikati yetu na kuniachanisha mkono wangu na mkuu wa shule na kunishika mkono na kuanza kunitoa nje
“eddy achana naye huyo mzee”
Machozi yakazidi kunimwagika,pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote
 
“john niachie,tafadhali”
“eddy siwezi kukuachia,nakujua.Tuliza kwanza hasira”
“john,yule mzee ananitafuta nini mimi?”
“mpotezee bwana,hajui atendalo”
“john,mama yangu hata siku moja hajawahi kunizalilisha mbele ya watu kwa kunipiga.Sembuse yeye kikaragosi”
“ndio,naelewa hilo eddy ila punguza jazba”
 
Tukaingia kwenye moja ya darasa lililopo chini ya ukumbi kwani ukumbi upo gorofani.John akanikalisha kwenye moja ya kiti na yeye akakaa mbele yangu juu ya meza.Moyo na mwili wangu vyote vikawa vinajisikia vibaya sana kwa kitendo cha kuzalilishwa.Kwani katika maisha yangu tangu nikiwa mtoto sikupenda mtu kunizalilisha wala kunionea.

Hata awe ni mkubwa vipi nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kupambana naye hata akinipiga basi ipo siku nitamvizia hata kwa mawe nimpige,ndio maana hadi hapa nimekua bondia mzuri tuu.Nikaichomoa bastola yangu kwa haraka john akanibeta na kunipokonya
“eddy,unataka kufanya nini?”
“lete hiyo bastola”
“ahaa eddy sikupi”
 
John alikimbia nyuma ya darasa,huku bastola akiwa ameishika mkononi.Nikamtazama kwa macho makali sana yasiyo pepeseka hata kidogo.Kwa haraka nikatoka mlangoni na kumfungia john kwa nje.Nikakimbia na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea kwenye ukumbi.Kitendo cha mguu wangu wa kwanza kukanyaga sakafu ya ukumbini nikatazama wapi alipo mkuu wa shule.

Nikamuona akiwa amekaa kwenye meza ya wageni waalikwa akiwa katikati ya waalimu wengine na mmiliki wa shule.Kwa kasi ya ajabu nikakimbia hadi alipo kaa na kujirusha na sote wawili tukaanguka na kiti,mbaya zaidi yeye akangukia mgongo na kunipa mimi nafasi nzuri ya kumkalia kwenye kifua chake na kuanza kumshambulia kwa ngumi zisizi na idadi kwenye uso wake
 
Kelele za wanafunzi kushangilia zikazidi kuongezaka,waalimu walio karibu yetu wakaanza kunivuta,kuniachanisha na mkuu wa shule.Wakanisimamisha na kunipeleka pembeni.Mkuu wa shule akasimaa huku akitaka kunifwata ila waalimu wezake wakanizuia.Ukumbi mzima wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wakawa na kazi ya kunishangilia huku wakilitaja jina langu na kupiga makofi.
 
“eddy......Eddy........Eddy........Eddy”
Mkuu wa shule akawazidi nguvu,waalimu walio mshika na kuja kutuvaa na waalimu ambao wamenishika mimi.Sote tukaanguka chini,kabla mkuu wa shule hajafanya chochote nikamuwahi kumdaka  shingo na kumpiga kabali.Akaanza kunishindilia ngumi za mbavu,nikamuachia shingo yake na kumsukuma pembeni na kunyanyuka juu kidogo.Akanyanyuka kwa kasi na kunifwata,kabla hajanifikia nikaruka juu kwa kutumia mguu wangu wa kulia,nikautulisha kwenye kifua chake na kumuangusha chini.Waalimu wakaendelea kutushika,kelele za wanafunzi wezangu zikazidi kuongezeka.Hata ambao wawanijui vuzuri,nao pia wakawa katika mkombo wa kushangilia
“nitakuua wewe kijana”
 
Mkuu wa shule alizungumza huku akiwa ameshikwa na wezake kwa nguvu.Nikabaki nikitabasamu kwa dharau zaidi nikamnyooshea kidole cha kati kama tusi.Ndio nikawa nimemfungulia hasira zake zote.Akajibabadua mikononi mwa waalimu wengine na kunifwata.Nikasikia mwalimu mmoja aliye nishika akiwaambia wezeke
“hembu muachieni tuone atakacho kifanya,mzee mgomvi kama nini”
 
Wote walio nishika wakaniachia,ila wakawa wamechelewa kwani mkuu wa shule alishafika mbele yangu na kuachia ngumi nyingi zilizo nijia kwa kasi mwilini mwangu.Kikubwa cha kwanza nilicho jilinda nacho ni sura yangu,mikono yangu ikawa na kazi ya kuzizuia ngumi hizo zisiingie sana kwenye mwili wangu.Jinsi ninavyoziuia ngumi zake ndivyo jinsi ninavyo mpata wakati mzuri way eye kuzirusha ngumi zake.Nikaona ni ujinga
 
“bora ngumi kumi kuliko mia”
Ni usemi ambao mzee godwin kipindi alipo kuwa akinifundisha kupigana utotoni alipenda sana kuniambia,akimaanisha nibora kupigwa ngumi kumi kuliko ukazuia ngumi miamoja.Nikaanza kuiruhusu mikono yangu kufanya kazi ya kumshambulia mkuu wa shule.

Kila ngumi ambayo niliirusha sikukosea sehemu ya kupiga,kila ambapo ninahitaji kupapiga ndipo nilipo papiga.Nikaanza kumuona mkuu wa shule akishinda kustahimili,nikazidi kuongeza kasi ya mashambulizi,ngumi kama nne zikatu sehemu za njuu kwenye jicho lake la kulia na kuifanya sehemu hiyo kuchanika na kutoa damu nyingi.Mkuu wa shule akaanza kuyumba yumba akionekana kuchanganyikiwa
 
Nikampiga mtama ulio muangusha chini,akajaribu kunyanyuka ila akshindwa.Nikataka kumkanyaka kifuani,kwa haraka akanyanyua mikono yake juu
“eddy nisamehe,nimekukubali”
 
Kauli yake ikasikiwa karibi na wanafunzi wote,ukumbi mmzima ukanyanyuka kwa furaha,wanafunzi walio na simu ambazo haziruhusiwa shuleni ila kwa furaha wakazitoa na kuanza kupiga picha,huku wengine wakirekodi tukio zima.Walinzi wakamsimamisha mkuu wa shule na kumtoa nje ya ukumbi.

Baadhi ya waalimu ambao wakikuwa wamenishika wakaanza kupiga makofi,ila mmiliki wa shule alipo watazama wakaacha mara moja na kujifanya wakiwanyamazisha kelele wanafunzi ambao hawakuacha kuficha furaha zao.Japo nimeumia baadhi ya sehemu katika mwili wangu ili nikabaki nikiwa nimesimama mbele ya wanafunzi wezangu huku nikiwa ninahema sana.Nikawanyamazisha wanafuni wezangu na wakakaa kimya wakisubiri nizungumze
 
“rafiki zangu,ndugu zangu,nawashukuru sana kwa upendo wenu.Ninaimani kwa kitendo hichi nilicho kifanya,sizani kama sheria za shule zinaniruhusu mimi kuwa mwanafunzi halali wa hii shule”
“nawatakia masomo mema na mungu awalinde”
 
Ukumbi mzima ukawa kimya,macho yangu yakawa na kazi ya kuwatizama wanafunzi wezangu.Kuna baadhi ya wasichana wa kidato changu wakashindwa kuyazuia machozi yao na kujikuta wakiwa wanamwagikwa na machozi.Mwalimu wa nizamu akanitazama kwa macho ya masikitiko kisha akawatazama wanafunzi wengine
 
“wewe,wewe leteni simu zenu”
Mlwalimu wa nidhamu aliwanyooshea wanafunzi wawili walio zishika simu zao,wengine kwa haraka wakazificha.Wanafunzi walio itwa wakabaki wakimtazama mwalimu wa nizamu.
“hamunisikii?”
“boooooooo”
 
Wanafunzi wote wakaanza kumzomea mwaliwa na nizamu,
“tunataka haki zetuu...Tunatakaaa hakizetu”
Wanafunzi mmoja alianza kuimba na wengine wakaitikia,sauti zikaendelea kurindima kwenye ukumbi,sikujua ni haki gani ambayo wezangu wanaitaka.
“waambie wezako wanyamaze bwana”
 
Mwalimu wa nizamu alizungumza kwa sauti ya kuninong’oneza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.Kwa jinsi ninavyo wajua wanafunzi wezangu,muda wowote anaweza kuanzisha fujo.Nikajaribu kuwanyamazisha na kweli wakanyamaza na kila mmoja nikamuomba kukaa kwenye kiti chake na wakatii
 
“jamani,munataka nini?”
Niliwauliza na karibia kila mmoja akanyoosha kidole juu akiomba nafasi ya kuzungumza.Nikamchagua mwanafunzi mmoja akasimama na wengine wakakaa kimya
“kaka eddy kwanza hatumtaki mkuu wa shule”
“ndioooooo”
Wakaitikia wote kwa furaha
“pili tangu hii shule tumefungua,chakula tunacho kula ni kibovu,sio kama pale awali.Sasa hizo milioni mbili za ada kazi yake ni nini?”
 
“semaaa babaaaa”
Msichana mmoja aliropoka kwa sauti ya juu
“yangu ni hayo kaka”
Nikamchagua mwengine na akasimama
“kaka eddy kwa niaba ya wezangu,kwanza tunakuomba urudi shule.Pili tunakuteua kuwa kaka mkuu wa shule kuanzi sasa hivi”
 
Ukumbi mzima ukanyanyuka kwa furaha,sikuamini na ukorofi wangu wote kama ipo siku nitakuja kukubalika shule nzima.Mwalimu wa nizamu akabaki kimya asijue nini cha kuzungumza
“jamani asanyti kwa uchaguzi wenu.Ila swali langu ni je nitaruhusiwa kurudi shule?”
“ndiiooooo”
 
Lengo la swali langu,alijibu mwalimu wa nazamu ila nikashangaa wakijibu wanafunzi wezangu.Nikamgeukia mwalimu wa nazamu akabaki akiduwaa
“ndio....Ndio....Ndio.....Ndio”
Wanafunzi wezangu walipiga kelele za ‘ndio’.Mwalimu wa nizamu akakubali kwa kunijibu ndio
“ila siku utakayo rudi uje na mzazi wako”
“sawa”
 
Ratiba nzima ikavunjika,kama kaka mkuu mpya wa shule nikamuomba dj kufungulia mziki na wanafunzi wakaanza kuserebuka.Furaha ikarudi moyoni mwangu,baadhi ya rafiki zangu wakanifwata na kunipongeza,nikakumbuka kuwa john nimemfungia darasani.Nikaanza kushuka kwenye ngazi za kuelekea madarasani.
 
“eddy...Eddy”
Nikasikia sauti ya kike ikiniita,nikageuka nyuma na kumkuta msichana mmoja ambaye sikuwahi kumuona siku hata mmoja ila sketi aliyo ivaa nikatambua watakuwa ni miongoni mwa wanafunzi wapya walio jiunga na kidata cha tano
 
“samahani mwaya kaka eddy”
“bila samahani”
“ninaitwa hellen,najua utakuwa hunijui?”
“ahaa umesha niambia jina lako,ndio nimesha kujua”
“kweli kaka,nimeona nikikaa kimya pasipo kukupongeza nahisi leo nisinge lala vizuri”
“kwa nini?”
“ahaa sijawahi kuona mwanafunzi anaye jiamini kama wewe”
“asante”
“naweza kukupa zawadi?”
“ndio”
Hellen akanifwata taratibu na kunibusu shavuni
“I like you”
 
Alizungumza kwa sauti nyororo na taratibu akaondoka huku akinipiga busu la upepo(busu la mbali) huku akikichezesha kiganja chake cha mkono wa kulia akiashiria kuniaga.Nikaachana na hellen na kufika katika mlango wa darasa nililo mfungia john.Nikaingia ndani na sikumkuta john,kabla sijatoka nikastukia meza iliyopo nyuma ya darasa ikianguka na john akasimama huku bastola akiwa ameielekezea kwangu
 
“eddy nakuua,nalipiza kwa kile ulicho nifanyia leo asubuhi”
John alizungumza huku akiwa anamaanisha kile anacho kizunguma kwani macho yake yamekuwa mekundu na machozi membaba yanachuruzika kwenye machavu yake na sura yake ikiwa imetawaliwa na mikonjo na tangu niwe na urafiki na john sikuwahi kumuona katika hali kama hii
 

                               *****sory madam*****(48)

Nikabaki nikimtazama john kwa macho yaliyo jaa mshangao mwingi.Nikajaribu kupiga hatua moja nyuma
“ukisogea nakuchangua ubongo wako”
John alizungumza huku jasho likiwa linamwagika huku akitetemeka mwili mzima,nikameza fumba la mate ili kusawazisha koo langu kabla sijazungumza chochote
“john wewe leo hii ni wakunishikia mimi bastola?”
“I don’t care”(sijali)
“even if,remember am your friend......Real friend”(hata kama,kumbuka mimi ni rafiki yako.....Tena rafiki yako wa kweli)
 
Nilizungumza kwa hisia kali,kwa sauti ya chini sana ya unyenyekevu,kwa mbali machozi yakinilenga lenga
“eddy usiniigize mkanda wa kuigiza,wewe nikatili sana wewe ni muuaji,wewe ni hustahili kuishi kwenye hii dunia.Kumbuka ulimuacha yule dereva wa watu wa shule aliye pata ajali,alikufa mikononi mwangu,kisa ulikuwa unamuendekeza yule malaya wako salome”
 
John alizungumza kwa uchungu,huku sauti yake ikiwa imebadilika sana.Ucheshi wote ulimpotea
“john,kumbuka tumefanya mambo mengi.Kumbuka ‘o’ level wewe uligongwa na nyoka tukiwa shamba la shule,ni nani aliyekuwa wa kwanza kuyaokoa miasha yako”
Nilizidi kuzungumza kwa sauti ya upole sana kwani nikifanya ujinga wowote john anaweza akanifumua kichwa
“hiyo sio kigezo eddy,wewe sio rafiki wa kweli.Wewe ni muuaji eddy”
 
Nikakosa cha kuzungumza,ikanilazimu nianze kutafuta njia nyingine ya kuepukana na tatizo lililopo mbele yangu.Nikaikazia macho bastola aliyo ishika john,nikavitazama vidole vyake nikagundua hakuna kidole hata kimoja kilicho ingia sehemu yenye traiga ya kufyatulia risasi,nikashusha pumzi nyingi na kutabasamu.Nikaanza kupiga hataa moja baada ya nyingine mbele huku nikiwa nimejiamini kupita maelezo
 
“eddy ukinifwata nitakuua,ninakuapia haki ya mungu”
John alizungumza kwa kubabaika,nikazidi kupiga hatua mbele zaidi huku macho yangu yakiwa kwenye vidole vya vilivyo ishika bastola.Hatua mbili kabla sijamfikia akakiingiza kidole kimoja kwenye sehemu yenye traiga ikanilazimu kusimama kama namba moja
 
“eddy rudi nyuma,moja........Eddy rudi nyuma,mbili......”
Sikumpa nafasi john aendele na mchezo wake wa kunihesabia namba zake kama mtoto mdogo.Urefu wangu ukanisaidia kurusha teke lilikoupiga mkono wa john wenye bastola na ikaangukia pembeni kwenye meza na viti.John akataka kuikimbia bastola sehemu ilipo simama ila nikamuwahi kumshika shati lake na kumvuta nyuma hadi akaanguka chini.Nikaiwahi bastola na kitu cha kwanza nikaichomoa magazine na kuiweka mfukoni
 
John akanyanyuka na kunifwata kwa hasira hadi sehemu nilipo simama,akataka kunipiga ngumi,nikaikwepa na kurudi nyuma hatua haraka nne na kuacha umbali kidogo
“john usimtafute mungu maneno”
 
Nilizungumza huku nikimtaza john machoni,hakunisemesha chochote zaidi ya kuendelea kuhema kwa hasira,ili kuepusha mafarakano nikaanza kupiga hatua kuelekea mbele ya darasa kwenye mlango,hellen akaingia akachungulia kwenye mlango
 
“eddy nilikuwa ninak.......Eddy nyuma yakoo”
Nikageuka kwa haraka na kukutana na kiti alicho kirusha john,kwa juhudi zangu zote nikajitaidi kukikwepa kiti,ila nikawa nimechelewa na sehemu ya kuegemea kwenye kiti alicho kirusha john ikanipiga puani na kuniangusha chini.Kizunguzungu kikali kikanikamata huku damu zikaanza kunitoka puani.Nikajaribu kunyanyuka ila nikashtukia teke la kifua lililo nilaza chini
“wee kaka,muachie mwenzako”
 
Hellen alizungumza huku akiwa amemshika mkono john,kofi zito likatua shavuni mwa hellen na kumuangusha chini huku akito ukele mmoja tuu akatulia.John akanigeukia na kutaka kunivamia ila nikajitahidi hivyo hivyo kumpiga teke kwenye miguu yake na akaanguka chini.Nikajikaza kumtazama ila machoni mwangu ninaona vitu vya ajabu ajabu(mawenge mawenge) na kwambali ninaona vitu vilivyopo humu ndani ya darasa.John akaniwahi kunikalia kifuani na kanza kunitandika ngumi za uso nilizo zizuia kwa mikono yangu.
 
Nikauingiza mkono wangu mmoja ndani ya mfuko wenye magazine ya bastola na kuichomo,nikaishika vizuri na kumpiga nayo john ya kichwa na akaangukia pembeni.Sote tukabaki tukiwa tumelala huku mimi nikiwa ninatafuta chanel ya kichwa changu irudi vizuri kwani hadi sasa hivi inasoma no signal(hakuna mwasiliano).Nikaanza kujihisi vizuri kwa msaada wa ukuta nikaasimama huku ninayumba kama mlevi aliye pitisha kiwango cha ulevi.Nikatafuta kiti na meza,nikakaa huku kichwa changu nikiwa nimekilaza kwenye meza na damu za pua taratibu zikawa zinamalizikia kutoka.Nikashusha pumzi mara kadhaa na kusimama juu.
 
Nikamtazama john na kumuona akiwa anayafumbua fumbua macho yake,hellen bado emejikunyata chini.Nikaiokota magazine na kuanza kuitafuta ilipo bastola.Nikaiona bastola na kuikota.Nikaichomeka magazine na kurudi kwenye kiti nilichokuwa nimekikaa na kusubiria john aamke.John akakaa kitako na kunitazama huku kwenye kichwa chake akivuja damu sehemu ya upande wa kichwa nilipo mpiga na magazine ya bastola
 
“john,ni nani aliye kuroga?”
John hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuendelea kunitazama.Tukatazamana na john kama dakika mbili kisha nikacheka kichoko cha kejeli na kusimama na kumpita.Nikachuchumaa na kumtazama hellen
“hellen”
“mmmm”
“amka”
 
Hellen akainuka huku akiwa na mawenge mawenge
“unajisikiaje?”
“ehee”
“unajisikiaje?”
“mmmmm”
Nikajua bado hellen anakiwewe,nikamnyanyua na kumkalisha kwenye kiti na kumtazama john ambaye alianza kulia pasipo kuwa na sababu ya msingi
“hujaingia kwenye idadi ya watu ninao wachukia na usitake uingie kwenye idadi hiyo”
 
Nikafungua mlango wa darasa na kuondoka huku bastola nikiichomeka kiuoni na kuifunika na sweta nililo livaa,nikashusha ngazi za gorofa la shule na kueleka zangu nyumbani kwa madam merry.Kabla sijafika nikakuta gari ya polisi ikiwa nje ya nyumba ya geti la madam mery.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio,nikarudi nyuma na kutafuta sehemu yenye nyumba nikajibanza na kuangalia kitu kinacho endelea.Nikamuona manka na madam merry wakiwa wanatoka kwenye geti wakiwa wanazungumza na askari mmoja.Wakasimama kwa muda nje huku wakizungumza na mimi
 
Askari akawaaga na akaingia kwenye gari na kuiwasha na kuondoka,nikawasubiri waingie ndani ya geti.Nikakimbia kwa kasi hadi kwenye geti na kulipiga kikumbo kabla manka hajalifunga vizuri.Mstuko wa geti kufunguka ukamstua sana manka na madam mery.
“yule ni nani?”
Wote wakaa kimya wakinishangaa kwani sweta zama limejaa damu
“si ninawauliza nyinyi kenge,yule ni nani?”
“mumekwenda kunistaki sio?”
 
Wakatazama,pasipo kunijibu swali langu.Nikichomoa bastola na kuwaishika mkono wa kushoto,kwani ni mkono wangu wenye nguvu kuliko mkono wa kilia.
“eddy,sisi yule askari ni rafiki yetu tuu na naa......”
Manka alinijibu huku akipata kigugumizi cha hapa na pale
“yaani wewe manka leo hii ndio unaamua kwenda kunistaki polisi si ndio?”
 
“hapana....Yule ni naniliuuuu”
“naniliuu nani?”
“eddy mpenzi wangu ni.....”
“wewe mery koma mimi sio mpenzi wangu.Manka tambua mimi ni ndugu yako,baba yangu ni baba yako sasa wewe endelea ku........”
 
Nikasikia milio ya magari polisi kwa mbali kidogo ikionekana kuja ilipo nyumba ya madam mery.Nikaacha mazungumzo na kwaharaka nikaingia ndani ya gari na kuliwa,madam mery na manka wakakimbilia ndani.Nikakanyaga mafuta kwa nguvu huku nimekanyaga breki na kuyafanya matairi ya gari kusereleka chini,nikalitazama geti lililo jifungua kidogo,nikajifunga mkanda wa siti yangu ya dereva na kushusha pumzi nyingi zilizo changanyikana na vichembe chembe vya damu vilivyo toka puani mwangu.

Nikaachia breki za gari na kulifanya liende kwa kasi na kugonga geti na kufumba na kufumbua nikajikuta nikiwa nje huku geti ni kiwa nimelivunja.Nikakanyaga breki galfa na kuifanya gari kuzunguka mzunguko mmoja katikati ya barabara,ulio ifanya gari ya polisi iliyo tangulia kupita kwa kasi.Gari ya pili ya polisi ikanikwepa na kwenye kuuvaa ukuta wa madam mery.
 
Uzuri wa gari hili,unaweza kutumia mfumo wa ‘manuel’ au ‘automatic’ katika uendeshaji wake.Nikabadilisha mfumo kutoka automatic hadi manuel ambayo inaniruhusu kuingiza gia mimi mwenyewe tofauti na automatic gia zinajiingiza zenyewe.Kwa kioo cha pembeni nikalishuhudi gari la polisi likikunja kona kwa bahati mbaya likazima na dereva akawa na kazi la kuliwasha
 
“muombeni mkuu wenu awanununulie magari mapya”
Nilizungumza huku nikiiachia breki na kuondoka kwa kasi.Namba za mbele na nyuma ya gari langu nikazigeuza kwa kuminya kitufe kinachofanya kazi hii ya kuzibadilisha namba hizi za gari.Sikupanga kurudi dar es salaam leo ila ikanibidi kufanya hivyo kwani tayari arusha nimesha haribu hali ya hewa.Nikafika moshi na kuendelea na safari yangu,gafla nikaona gari mbili nyeusi zikinifwata kwa nyuma kwa mwendo wa kasi
“nani hawa?”
 
Zikazidi kunifwata kwa kasi kubwa,kila ninapojaribu kuongeza mwendo ndivyo nazo zinavyozidi kuongeza mwendo,hadi nanafika usangi bado zikawa katika kunifukuzia kwa nyuma.Nikaanza kuchangayikiwa pale gari moja lilipo nikaribia kwa ukaribu sana na kuanza kunigonga kwa nyuma.

Nikajitahidi kwa uwezo wangu wote katika uendesha gari na hadi hapa nilipo fikia kwenye mwendi kasi wa miambili na arobaini,pembeni kilipo kioo kidogo kikaanza kunionyeshea vipicha vya watu walio bebe jenaza na kunindikia maandishi ya kuniomba kupunguza mwendo.Katika kona zote nikawa na kazi ya kukanyaga breki kidogo na kukunja mskani wa gari langu kama ni kushoto au kulia
 
Jasho jingi la woga likazidi kunimwagika japo nimewasha ac(air condition) ambayo inanisaidia kunipepea ila haikufua jasho.Kwa mwendo ninao kwenda nao nimewaacha jamaa kwa umbali kidogo,ila nao bado wanakuja kwa kasi.Hadi ninafika mombo bado jamaa wananifwata,akili moja nikawa ninawaza niingie katika kituo cha polisi mombo kujisalimisha.Ila akili nyingine ikanikataza kabisa kufanya maamuzi ya kijinga kama haya
“nitakuwa mpumavu”
 
Nikaendelea kwenda kasi,hadi ninafika korogwe jamaa bado wananifwata.Machozi yakaanza kunilenga lenga.Sikujua ni kwanini machozi yananilenga lenga.Mtu ukiziona gari zetu unaweza kusema ni mbio za mashindano ya magari
“hizi sio gari za polisi.”
 
Nilijisema kimoyo moyo huku nikiendelea kuzitazama kwenye kioo cha pembeni.Muda umeshatimu saa nane usiku,nikafika segera na kunyoosha barabara ya kwenda tanga bila kwasha taa ya pembeni inayo niashiria ninaingia wapi,nikakunja kwenye stendi mpya iliyopo hapa segera na kuzifanya gari hizo zote kupita na ndipo nikagundua ni gari aina ya range rover ndio maana mwendo wake ni mkubwa sana.Nikatokea upande wa pili wa stendi na kunyoosha barabara ya kweda dar es salaam.Nikazidi kukanyaga mafuta,nikaziona gari zilizo kuwa zikinifukuzia kwa nyuma zikija kwa kasi nyuma yangu
“hawa ni kina nani?”
 
Nilizungumza kwa sauti ya juu.Nikazidi kuongeza mwendo ndivyo nazo zilivyo zidi kunifwata.Maeneo ya kabuki nikaliona gari kubwa aina ya scania lilika mbele yangu kwa kasi huku limetanda barabarani.Nikabana upande wa kushoto niliopo ila dereva wa scania naye akabana nilipo,nikarudi kulia naye akanifatwa huko nilipo elekea huku akiniwashia taa zake zote.
 
Nikaachia msunyo mkali na kuirudiisha gari yangu upande wa kushoto nilipo toka na jamaa akanifwata nilipo,sikuwa na budi zaidi ya kutoka nje ya barabara kuepika kugongana uso kwa uso na gari hilo.Gari ikaanza kunishinda nguvu badala ya kufunga breki kwa kuchangunyikiwa nikawa na kazi ya kuongeza kasi.Nikastukia gari ikaanza kupiaga kubingiria kwa kasi ya ajaba.Jinsi inavyobingiria ndivyo jinsi ninavyo jigonga ndani ya gari hadi giza jingi likayavaa macho yangu na kutulia kimya......

Itaendelea....

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts