Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 57 & 58 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 57 & 58 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Bigie on Wednesday, September 28, 2016 | 9:37:00 AM

Mtunzi: Eddazaria g.Msulwa

Ilioishia
Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni

Endelea
“vua cheni yako”
Askari anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi chini kwenye miguu,
“safari njema”
Dada aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
“asante na wewe pia kazi njema”
 
Nikapita kwenye kizuizi na kuwafanya sashah na rajiti kushusha pumzi nyingi kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari, tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru mungu, siti zetu tatu zipo sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini kenya
“eddy” rajiti aliniita
“naam”
“unajua kwamba unaonekana tofauti sana”
Alizungumza kwa sauti ndogo
“kweli?”
“ndio, umekuwa bonge la handsome”
“mmmmm”
“kweli vile”
“jamani acheni kelele watu wamelala” sashah alizungumza
“ahaaa shauri yao, bwana”
 
Masaa yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo, baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari ikaendelea.Tukafika nchini iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura bandia,
 
Sikuwa na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni sashah na rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja wa ndege na sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye mkuta ndani ya teksi hii, tukafika kwenye moja ya hotel kubwa iliyo andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya kiarabu
Sashah akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja, akatufwata sehemu tulipo simama na rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho sashah alikodisha
 
“eddy utakaa hapa siku mbili, ili uyazoee mazingira kisha tutaelekea makao makuu”
Sashah alizungumza
“na nyinyi munakwenda wapi?”
“sisi, tunakwenda kufwatilia mambo muhimu, kwa ajili ya kazi zetu, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hili eneo.Tumekulipia chakula kila mahitaji utakayo yahitaji tumegharamia”
“sasa jam….”
“eddy hapo hakuna cha sasa kikubwa ni wewe kuwa makini, usipende kujitokeza tokeza kwa watu kwani watu wa huku hawana huruma, wana roho za kinyama.Yaani ukitembea sana wewe mwisho wako ni kule chini kwenye sehemu ya chakula”
“sawa nimewaelewa, je nikihitaji hudumu ya kuwapigia wahudumu wa hii hoteli?”
“kuna kitabu pale juu ya meza kwenye ile simu basi utaweza kuitumia hiyo sawa, na kabla sijasahau chukua hizi cuppon ukienda kuchukua chakula unaonyesha, zipo za ana mbili, moja ya chakula na nyingine ya kinywaji.Ukizipoteza baba utashinda njaa hizi siku mbili”
“powa”
 
Sashah na rajit wakaondoka na kuniacha nikiwa nimesimama, nikawasindikiza kwa macho hadi walipo funga mlango ndipo na mimi nikapiga hatua hadi kweye mlango na kuufunga kabisha kwa funguo na kurudi kujilaza kwenye kitanda kikubwa kilichomo ndani ya hii hotel.Nikanyanyuka na kusimama mbele ya kioo kikubwa na kujitazama sura yangu, kusema kweli nimebadilika kwa kiasi kikubwa
Nikavua suti niliyo ivaa na kuingia bafuni, nikaoga huku kichwani kwangu nikiwa nimejawa na mawazo yaliyo ambatana na maswali mengi juu ya wapi alipo mama yangu,
“hii ni nafasi yangu ya mwisho kupambana na mzee godwin, nilazima nimuue kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Nilizungumza huku nikiwa nimekiinamisha kichwa chwangu kwenye ukuta, huku nikiyatazama maji yanayo tiririka na kuingia kwenye kijishimo kidogo
“ilipo fikia inatosha”
 
Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi, nikamaliza kuoga na kurudi chumbani, saa ya ukutani inanionyesha inakwenda majira ya saa kumi na moja kasoro jioni.Nikapanda kitandani, kutokana na uchovu mwingi nikajikuta taratibu nikiwanza kusinzia hadi usingizi ukapitia kabisa
Nikastuka kutoka usingizini, na macho yangu yakakumbana na giza, nikashuka kitandani na kupiga hatua za ungalifu hadi sehemu ilipo swichi, nikawasha taa cha kwanza kukitazama ndani ya chumba ni saa iliyopo ukutani na kukuta ikionyesha ni saa nne na dakika kumi na nane usiku, nikavaa nguo zangu na kutoka nje ya chumba, nikashuka chini sehemu ya watu kujipatia chakula
 
Nikaa kweny moja ya meza, muhudumu akanifwata na kuniuliza kwa lugha kingereza ninatumia chakula gani, kati ya vyakula vilivyo orodheshwa kwenye menyu yao.Kila chakula ambacho ninakisoma kwangu ni kigeni, nikaamua kuweka tiki kwenye chakula ambacho niliona jina lake linanipendeza, kinywaji nilicho kielewa kikubwa ni maji tuu ndio niliyo amua kuyawekea tiki
Muhudumu akaondoka na baada ya muda akarudi akiwa na chakula nilicho muagiza, nikajikuta nikishusha pumzi nyingi kwani chakula nilicho kiagiza, ni konokono wakiwa wamechemshwa vizuri huku wakiwa wamepambwa na nyanya zilizo katwa vizuri na kuwekwa pembezoni mwa shahani hiyo
 
“mmmm, bora nirudi bongo, kwa staili hii”
Nikawatazama watu wengine kwenye meza zao, kila mmoja yupo bize na mambo yake, jamaa mmoja aliye kaa pembeni yangu nikamuona akiwekewa chakula kama changu na muhudumu aliye muagiza, bila hata ya kusita akaanza kutafuna nyama za konokono hao huku akishushia na soda.Kwa jinsi jamaa anavyo wala nikajikuta nikianza kujihisi kichefuchefu kwa mbali, kila ninapo watazama konokono wangu ndovyo jinsi kichefuchefu kinavyo ongezeka na kujikuta nikisimama na kumsimamisha muhudumu mmoja
“where is toilet”(choo kipo wapi)
Nilizungumza huku kiganja cha mkono wangu wa kulia kikiwa mdomoni mwangu kuzuia kutapika, muudumu akanionyesha kwa kidole mlango wa kuelekea chooni, nikaanza kupiga hatua za kwenda kuufwata mlango huku ninatizama chini kwa bahati mbaya nikamgoga msichana mmoja mmrefu aliye nipa mgongo, na pochi yake ikaanguka
“so….”
 
Sikuweza hata kuimalizia samahani yangu, tayari kechefuchefu kilikolea, nikazidi kutembea kuelekea chooni, ila kwa msonyo alio uachia huyu dada ikanilazimu kugeuza kichwa kumtazama huku nikiwa ninatembea, macho yangu yakamshuhudia dorecy akimalizia kunyanyuka huku akiwa ameshika kipochi chake kilicho anguka, kutokana na hali mbaya niliyo nayo sikuwa na budi kuingia chooni.Nikasimama kwenye moja ya sinki la kunawia mikono na kuanza kutapika, dakika tato mfululizo nikajikuta ninatapika hadi chakula nilicho kula ndani ya ndege.
 
Tumbo likaanza kunisokota, sikujua hata ni kitu gani kilicho nikumba kwa dakika chache hizi, ikanilazimu kujisaidia haja kubwa, kidogo nikapata nafuu ya tumbo kuniuma.Nikajiwek sawa na kunawa mikono yangu, nilipo hakikisha ninaonekana vizuri nikafungua mlango na kumkuta yule jamaa aliyekuwa anakula konokono akiwa amesimama juu ya meza huku mkoni mwake akiwa na bomu la kurusha kwa mkono, watu wote wakanza hulala chini huku wakipiga kelele, jamaa akafungua kikoti chake alicho kivaa na nikamshuhudia akiwa amejifunga mabomu mengine makubwa kama maane na akaanza kuzungumza kwa sauti ya juu kwa lugha ya kiarabu na neno nililo lielewa ni moja tu
“walha wakhbar”
Kisha akalirusha juu bomu la mkoni, alilokuwa amelishika, huku mabomu mengine aliyo yavaa mwilini mwake yakisoma zero nyingi zinazo onekana kwa rangi nyekundu
 

*****sory madam*****(58)

Fumba na kufumbua, nikajikuta nikiwa nimerushwa na kurudishwa nyuma ndani ya choo nilipo tokea, huku sauti kubwa ya mlipuko wa bomu ikisikika, sikujua hata nini kufanya kwani akili yangu ikakakosa maamuzi ya hataka ya kuamua, hadi ninaanza kupata chakufanya, tayari nimesha chelewa kwa maana kuta za choo zilisha anza kuporomoka na kusababisha upenyo mdogo sana.Nikazidi kuchanganyikiwa kiasi kwamba sikujua ni nini niweze, gafla nikashuhuda kifusi kikubwa cha mchanga kikilifunikia sehemu zima la chooni na taratibu nikaanza kupoteza pumzi na kulegea, na giza jingi likanitawala machoni mwangu
                                                                                              ***
Nikaanza kuhisi kitu kikinistua kwenye kifua change, sikuweza kuelewa mapema ni vitu gani.Kelele za watu za watu mchanganyiko zikazidi kunipa hamasa ya kutamani kuona ni kitu gani kinacho endelea kwenye maisha yangu kwa wakati huu.Haikuwa rahisi sana kama ninavyo hitaji mimi kuwa, kwani kila kitu kinacho endelea kwenye ulimwengu huu niliopo ni chatofuti sana, na sijawahi kukiona hata siku moja mbele ya maisha yangu.Mwanga mkali ukasimama mbele yangu, na kundi kubwa sana la watu walio valia mavazi meupe yanayo ng’aa sana, wakiwa wapo kwenye marika tofauti kuanzi watoto wadogo hadi wakubwa, wote wakiwa wapo kwenye jinsia tofauti nikimaanisha jinsia ya kiume naya kike.
 
Kila niliye mtazama akaanza kutingisha kichwa, akionyesha kukaataa kitu na sikujua ni kitu gani ambacho anakikata, wakaanza kuninyooshea mikono ya kuniomba nirudi ninapotoka, sikujua ni wapi nilipo taoka kutokana sehemu nzima niliyo simama imetawaliwa na mwanga mweupe mtupu ambao sikuweza kuona ni wapi popote zaidi ya hawa watu walio simama mbele yangu
“eddy, wakati wako bado.Rudi”
 
Sauti nzito ya kutetemesha ilisikika masikioni mwangu, na gafla nikisikia mstuko mkali kwenye kifua change ulio nifanya nistuke na kukaa kitako huku ninahema sana, na jasho jingi likiwa linanimwagika mwilini mwangu.Watu waliopo pembeni yangu walio valia mavazi ya kijana huku sura zao wamezifunika kwa vitambaa vinavyo fanana na mavazi yao, wajanirdusha haraka kulala kwenye kitanda.Nikaanza kuminyanana nao huku nikiomba waniachie
 
“niachieni nyinyi, mimi mzima sijafaaaa”
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku nikijitahidi kunyanyuka, ila wakazidi kunishikilia na kunikandamiza nisirudi kukaa, nikamuona dada mmoja akichukua sindano na kuichoma kwenye kwenye kichupa kidogo na kuvuta dawa nyingi kwa haraka
“haaaaa, haaa unataka kuniua eheeee, kudadadeki nitakuua kwanza wewe”
 
Nilizungumza huku macho yangu nikiwa nimemtumbulia dada mwenye sindano, ila wezake wakajitahidi kunishika kwa nguvu zao zote, na nikamshuhudia dada akiichoma sindano kwenye mkono wangu wa kushoto, na kadri jinsi anavyoisukuma dawa ndivyo jinsi na mimi nilivyoanza kupoteza nguvu na usingizi mzito ukaanza kunitawala kila nilivyo jaribu kufumbua macho yangu nikashindwa kabisa
                                                                                               ***
Nikastuka na kukuta, mashine ndogo ikiwa pembeni yangu ikionyesha mishale mishale ambayo imepinda panda, kujichunguza vizuri nikajikuta nikiwa nimevalishwa kitu kilicho funika pua yangu na mdomo wangu, sikuwa na nguvu za kufanya kitu chochote zaidi ya kuendelea kujilaza kwenye kitanda nilicho lazwa.Taa mbili nyeupe za chumba hichi hazikunipa uwezo wa kugudua kama huu ni usiku au mchana.Nikajaribu kujiinua ila nikashindwa na kuendelea kulala kitandani
 
Baada ya muda kidogo ukaingia nesi akiwa amebeba kisinia chenye sindano, pamoja na vichupa viwili vyenye rangi tofauti tofauti
“unajisikiaje?” aliniuliza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole mwingi
“vizuri”
“vizuri, usiwe na wasi wasi upo sehemu salama na utapona sawa kaka”
Alizungumza huku akivaa gloves nyeupe kwenye mikono yake
“kwani hapa nilipo nipo wapi?”
“upo hospitali, ila kwa sasa tunajitahidi kukushuhulikie ili uweze kupona haraka”
“kwani hapa ni tanzania?”
“hapana hapa ni iraq”
“mbona unazungumza kiswahili kizuri”
 
Nilimuuliza huyu nesi mwenye asili ya kiarabu, akatabasamu na kuvuta dawa kidogo kwenye kichupa, kwa kutumia sindano kisha akachukua pamba na kuipaka dawa kidogo na kunipaka kwenye mkono wa kulia sehemu ya kikunjio, akanichoma sindano yanye dawa
“pole eheee”
Alizungumza kwa sauti yepesi sana iliyo jaa upendo na upole
“asante”
“ikifika asubuhi nitakuja kukuchoma sindano ya kutuliza maumivu”
“sawa”
 
Akakusanya kila kilicho chake na kutoka ndani ya chumba.Masaa yakazidi kwenye na kuzidi kukatika taratibu huku nikiwa nimesongwa na msongamano wa mawazo nikijaribu kuvuta kumbukumbu za hapa kufika hospitali ila sikukumbuka kitu cha aina yoyote, jina ambalo ninalo kichwani mwangu ni tanzania, pamoja na lugha yangu ya kiswahili ambayo kwangu ndio lugha ya taifa
 
Wakaingi madaktari wawili wote wakiwa waarabu, wakanisogelea hadi kwenye kitanda nilicho lala na kuanza kuzungumza huku mmoja akianza kunishika mashavuni na kuniminya minya.Wakaendelea kuzungumza huku mmoja akiandika kwenye kijikitabu kidogo alicho kuja nacho.Mmoja akanifunua shuka na kumuonyesha mwenye kijikitabu mkononi sehemu ya mguu wangu, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kuuona mguu wangu wa kulia ukiwa umefungwa kitu kikubwa cheupe.Akaingia nesi wa jana usiku na kusimama pembeni ya madaktari hawa, huku akiwa ameshika kisinia chake cha jana usiku.Nikaanza kumuona nesi akitingisha kichwa akionekana kukataa mazungumzo ya madaktari hao
 
Wakaanza kubishana, na sikujua ni kitu gani wanacho bishana.Hadi ikafikia daktari mmoja wa aliyekuwa anazungumza na mwenzake anaandika akataka kumzaba kibaa nesi huyo, ila mwenzake akakataa na kumtoa nje, kuepusha ugomvi kutokea ndani ya chumba hichi.Nesi akaanza kuzunguka ndani ya chumba huku akimwagikwa na machozi na kuzidi kunichanganya kwani sikujua ni kitu gani kinacho mwaga machozi kwa kiasi hichi.
“kuna nini?”
Nilimuuliza na kumfanya asimame na kunitazama, akautazama mlango na kwenda kuufunga kwa ndani, kisha akarudi na kukaa pembeni yangu huku akinifunika na shuka
“eti nesi, kuna nini?”
 
Nilimuuliza kwa sauti ya upole iliyo jaa huzuni, akanitazama na machozi yakazidi kumwagika kiasi cha kuzidi kunichanganya mimi
“watu wa huku, wana roho mbaya sana pale wanapo waona watu wenye ngozi yeupe”
Alizungumza huku akijifuta machozi yanayo mwagika kwa kutumia kiganja chake
“kwa nini?”
Akanitazama kwa umakini na kwamacho yaliyo jaa huzuni kiasi cha kunifanya nihisi kuna jambo baya ila sikujua ni nini
“kiufupi hawawapendi watu weusi, ndio maana wanafanya mpango wa kukukata huu mguu wako ulio vunjika”
 
Nilijihisi moyoni mwangu kama nimepigwa shoti ya umeme, kila nilivyo mtazama nesi sikujua nizungumze nini.Machozi yakaanza kunimwagika kama maji,
“usilie, nitahakikisha unapona na hakuna mtu anaye weza kukufaniyia ukatili kama huo”
“kwani umekatika?” nilimuuliza kwa sauti ya upole sana huku nikiendelea kulia
“hapana haujakatika, umefunjika mara mbili, ila nashangaa ni kwanini hapa wanapanga kuukata”
 
“ila usilie, nipo radhi nipoteze kila kitu kwangu, ila si kukubali kuuona ubaguzi wa rangi kama huu.Kwa maana wakiukata kinacho fwatia hapa ni wewe kupelekwa katika kambi ya walemavu iliyopo bangdad na kila siku hiyo kambi, walemavu wanakufa kwa njaa kali na mateso makali, na mbaya zaidi wengi wanao pelekwa kule ni wale ambao si raia wa nchi hii”
Maneno ya nesi yakazidi kuniogopesha na kuendelea kunipa wasiwasi mkubwa ulio zidi kunimwaga machozi yangu.
“jikaze usilie, ngoja nikuchome sindano ya kutuliza maumivu na kukausha kidonda.Wakikuletea chakula tafadhali usile hadi nikuletee mimi”
“sawa”
 
“wanaweza kukupa sumu, ufe bure mtoto wa watu bila ya sababu maalumu”
Nesi alizungumza na kuendelea kunichoma sindano alizo niambia,
“sasa hivi ninatoka, kazidi ninakwenda nyumbani kukuandalia chakula, hadi saa sita nitakuwa nimesha rudi kukuletea chakula na nikija nitakuja tuzungumze mengi.Ila vumilia njaa yako, usile chakula wala kunywa maji yoyote utakayo letewa na mtu wa aina yoyote sawa”
“sawa, nashukuru kwa msaada wako nesi”
“hata wewe nashukuru kwa uelewa wako, niite neshi phidaya”
“naitwa eddy”
 
“mungu mkubwa utapona na vua hiyo mashine”
Nikakivua kifaa nilicho kuwa nimevalishwa kwenye uso kisaha, nesi phidaya akaondoka na kila kitu chake, baada ya muda kidogo akaingia nesi akiwa amebeba sahani nyenye chakula pamoja na maji kwenye glasi, akaviweka pembeni ya meza yangu na kunitazama usoni.Akawa anatamani kuzungumza na mimi ila anashindwa na nikahisi lugha zetu zipo tofauti sana.Akanza kunionyesha kivitendo kwamba chakula kipo mezani ninaweza kula, na mimi nikamjibu kivitendo kwamba nitakula, akatoka na kuniachia chakula mezani. Harufu ya chakula ikazidi kunitamanisha kuweza kukila kwani inavutia sana, ila kila nilipo jaribu kukumbuka maneno ya nesi phidaya nilijikuta nikuwa ninakidharau
Baada ya muda mrefu kidogo nesi phidaya akarudi akiwa emeshika mfuko mweupe wenye vyombo,
“nani kakuletea chakula?”
 
“nesi mmoja mfupi, mwarabu”
Nesi phidaya akaachia msunyo mkali baada ya kumuambia nesi aliye niletea chakula hicho
“ndio wale wale”
Akakisogeza chakula nilicho letewa akaniwekea chakula chake mezezani, akaanza kuninywesha taratibu uji alio uweka kwenye kikombe
“watu wa huku hawana ubinadamu, ndio maana kila siku wanakazi ya kujitoa muhanga na mabomu yao”
“hivi ni kwa nini?”
“uchizi tu ndio unao wasumbua, kuna wanao amini kwamba ukijitoa muhanga, mbele za watu mbinguni utaingia moja kwa moja wakati ni uongo mtupu”
“hivi unakumbuka kitu chochote cha nyuma?”
“hapana”
 
“ona sasa, wamekuchoma sindano ya kukupotezea kumbu kumbu, ndio maana nakuambia watu wa huku hawana maana”
“wamenichoma sindano?”
“ndio, na kuna kitu kinacho endelea, na ile siku ya oparesheni kama nisinge kuwepo ninaimani wangekumalizia, nikutokana katika watu walio okolewa wakiwa hai kwenye lile jingo wewe ni mmoja wao na idadi kubwa ya waarabu walikufa pale”
“kwenye jengo, jengo gani?”
“usiwe na haraka, hapa itabidi nifanye mpango wa kukutorosha la sivyo watakupoteza”
 
Maneno ya nesi phidaya yakazidi kunipotezea imani moyoni mwangu na kunijaza moyo wa woga kwani imani ya kuwaamini madaktari wengine ikaanza kunipotea moyoni mwangu.Nesi phidaya akamaliza kunilisha chakula alicho niletea na kunihaidi atarudi usiku kisha akaondoka zake
                                                                                                    ***
Masaa yakazidi kusonga, huku moyoni mwangu nikiomba sana nesi phidaya atokee aje kunisaidia kwa maana kila daktari kwangu sikuweza kumuamini, kila nilipojaribu kuvuta subira sikuweza kumuona nesi phidaya akiingia kwenye chumba change, mlango ukafunguliwa na kujikuta nikianza kutabasamu, macho yangu yakiwa na shauku ya kuweza kumuona nesi phidaya.Nikashangaa kuwaona wale madaktari wa asubuhi wakiingia na kusimama pembeni yangu
 
Mmoja akafungua kitabu chake kilicho andikwa na maandishi ambayo akanionyesha na sikumuelewa ni maandishi ya lugha gani, akaniandikia tarehe kwenye kijikitabu chake na kuniambia kwamba hii ni tarehe ya leo, kish akaniandikia tarehe nyingine ambayo ni siku inayo fwata.Kisha akachora kijimguu na kukiwekea alama ya ‘x’ akiashiria kwamba kesho ndio siku ya mimi kukatwa mguu wangu.Alipo maliza kunionyesha kwa ishara wakatoka huku wakiwa wanacheka sana.
 
Hadi kunapambazuka sikuweza kumuona nesi phidaya, hali ya hatari ikaanza kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi phidaya anaweza kuwa amekutwa na matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke
                                                                
 ITAENDELEA...
 Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts