Get the latest updates from us for free

Home » » Bifu ya Gigy Money na Amber Lulu Yachukua Sura Mpya...!!

Bifu ya Gigy Money na Amber Lulu Yachukua Sura Mpya...!!

Written By Bigie on Sunday, October 16, 2016 | 12:22:00 PM


Ma-video queen wasumbufu Bongo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ wapo kwenye vita baridi (vita ya maneno) kufuatia Gigy kumchamba mwenzake kutokana na yale madai ya kukamatwa na ‘unga’ jijini Arusha.

Chanzo makini kililonga na paparazi wetu kuwa baada ya habari kuzagaa kuwa Amber Lulu amekamatwa na polisi Arusha akiwa na unga, Gigy amekuwa akimsema mwenzake huyo vibaya, mazingira yaliyosababisha wawili hao waanze kuraruana kwa maneno.

Akizungumza hivi karibuni, Amber Lulu alisema: “Nawashangaa hao wanaonisema vibaya kufuatia hizo tetesi, hasa Gigy ila siwezi kujibishana naye kwani siyo levo yangu.”

Gigy naye akafunguka: “Ni kweli nilimsema kuwa kama kweli kakamatwa na unga atakuwa katuaibisha sana. Huo ndiyo ukweli sasa akitokwa na povu atokwe tu.”


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts