Home » » Mtoto atekwa, gari laibwa

Mtoto atekwa, gari laibwa

Written By Bigie on Monday, October 24, 2016 | 10:52:00 AM

Mtoto wa miaka mitatu wa askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Kapteni Innocent Dallu ametekwa na watu wasiojulikana baada ya mzazi huyo kumuacha ndani ya gari pamoja na mwenzake ili aingie buchani kununua kitoweo.

Watekaji hao walimshusha mtoto mmoja na kuondoka na mwingine anayejulikana kwa jina la Light.

Kapteni Dallu ni ofisa afya wa JWTZ ambaye alikuwa akifanya kazi Hospitali ya Lugalo, lakini kwa sasa amehamishiwa Darfur nchini Sudan. Kwa sasa yuko jijini Dar es Salaam kwa mapumziko.

Kapteni Dallu amesema tukio hilo lilitokea jana saa 6:00 mchana eneo la Mbezi Juu wilayani Kinondoni baada ya  kuhudhuria ibada katika Kanisa la Roma Mbezi Juu.

Kapteni Dallu amesema mtoto huyo ana  rangi ya maji ya kunde, mwembamba na alikuwa amevaa gauni la rangi ya bluu.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts