Home » , » RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 29 & 30

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 29 & 30

Written By Bigie on Tuesday, October 25, 2016 | 10:04:00 AM

MUANDISHI : EDDAZARIA 

ILIPOISHIA
Mtu huyo wa ajaba akaendelelea kutazama tazama kila kona ya sable hii, akapiha hatua mbili mbele na kuzama ndani kabisa ya sable hii, na kuwapa mgongo Rahab na Raisi Praygod walio simama nyuma yake. Akaendelea kuvuta vuta pumzi, iliyo muashiria kwamba humu ndani kuna binadamu waklio hai, akalikoki bunduli lake aina ya gobore na kulishika vizuri huku kidole chake kimoja akiwa amekizamisha kwenye traiga, kwa haraka  akageuka nyuma na kuwaona Rahab na Raisi Praygod wakiwa nyuma yake wanamtazama

ENDELEA
Kwa haraka Rahab akaruka hewani na kuipiga teke bunduki ya mtu huyu mwenye muonekano wa ajabu sana, bunduki yake ikaanguka chini na kumpa nafasi nzuri Raisi Praygod kumrukia mtu huyo kwa kutumia bega lake lililo tua begani kwa mtu huyo na wote wawili wakaanguka chini.

 Rahab kwa haraka akaiokota bunduki ya mtu huto na kwakutymia kitako cha bunduki hiyo aina ya gobore akampiga nayo kichwani zaidi ya mara kumi mtu huyo, na kupelekea kichwa cha mtu huyo kupasuka kwa na kuvuja damu yenye rangi nyeusi ti.
“Mtu gani huyu….?”
Rahabu aliuliza huku akihema kwa nguvu akionekana kuchanganyikiwa kwa kumuona mtu wa aina hii ambaye tangu azaliwe hajawahi kumuona.
 
“Tuondike hakuna haja ya kuendelea kukaa hapa”
Raisi Pragod alizungumza huku akichungulia mlangoni kutazama kama wale watu wengine wa kutisha wamesha ingia ndani walipo kua wakiingiza mizoga ya watu walio waua. Wakatoka nje wakiwa katika tahadhari kubwa huku Rahab aklwa ameishika bunduki ya mtu huyo. 

Wakafanikiwa kutoka nje pasipo kuonekana na watu hao ambao wapo ndani ya kijumba chao wakiendelea kuwakata kata vipande marehemu walio wachukua na kuwafanya ndio chakula chao cha usiku. Wakaanza kutokomea porini huku wakimuomba Mungu waweze kutoka kwenye msitu huu ambao bado haujawapa matumaini ya kuweza kuziokoa nafsi zao zilizo kwenye matatizo makubwa
 
Hasili ya watu hawa wa kutisha wanajulikana kama Mazombi, walio anza kujitokeza mwaka 1819 katika bara la ulaya. Inasemekana watu hawa ni wale walio weza kupoteza maisha kwa sumu zenye kemikali kubwa na waliweza kurudi katika ulimwengu huu wakiwa katika hali hiyo ya kutisha na kuweza kuwafanya wanadamu halisi kama ndio vitoweo vyao vya kila siku.
 
Rahab na Raisi Praygod wakaendelea kukata mbuga pasipo kuchoka, japo wanatamani kuweza kupata japo dakika waweze kupumzika, ila kila walipo kumbuka maiti za watu walio waona wakishushwa na mazombi hayo hawakutamani kamwe kuweza kusimama.
 
Hali ya majonzi ikawatawala mazombi walio mshuhudia mwenzoa aliye pasuliwa kichwa na kusababisha ubongo wote kumwagika nje. Hawakua na hamu hata ya kuendelea kupata vitoweo walivyo kuja navyo na ziadi kila mmoja akachukua silaha yake na kuingia msituni kufwatilia watu hao walio sababisha mauaji ya mmoja wao. Kutokana na kuufahamu vizuri msitu wao, wakajigawa kwenye makundi ya mazombi wawili wawili na kupelekea kuwa na vikundi vinne. Kila mmoaja akajiapiza kuweza kufanya mauaji ya kikatili kwa watu walio sababisha mauji ya mpendwa wao
                                                                                                    ***
Samson na wezake wakafanikiwa kufika katika kiswa cha Kunashir nchini Russia, kwa bahati nzuri wakafanikiwa kupokelewa na mkuu wa kikiso kilicho asi nchi ya Russia bwana Rusev, Wakapelekwa moja moja kwa moja kwenye jengo lenye ofisi za kikundi hichi kinacho endelea kufanya mapinduzi kwenye nchi yake ikiitaka serikali kuweza kuunda serikali mbili, ili wao  wajipatie mamlaka ya kuweza kutengeneza silaha hatari za nyuklia.
 
Kila mmoja akakabidhiwa kinywaji alicho kihitaji yeye, ili kuweza kujipozwa kwa uchovu mwingi wa safari yao ndani ya maji, tangu pale walipo kamtwa na jeshi la polisi nchini Tanzania. Fetty na wezake hawakuwa na uwezo wa kuielewa lugha ya kirusi, ambayo Samson yeye aliweza kuizungumza vizuri pasipo matatizo ya aina yoyote. Alicho kua akikifanya Samson ni kuwatafsiria kila kitu ambacho alicho kua akikizungumza na bwana Rusev.
 
“Jamaa anauliza eti, tunaweza kujiunga na kundi lake?”
“Mmmm……!!” Anna aliguna
“Hatuwezi sisi tupo hapa kwa ajili ya biashara”
Samson akamjibu bwana Rusev kitu alicho kizungumza Fetty anaye onekana kuto kubaliana na swala zima la wao kujiunga na kundi la bwana Rusev
“Je anauliza tunahitaji kiasi gani cha pesa ili tuweze kumkabidhi hii manohari?”
“Sasa hapo ndio umenena la maana” Halima alizungumza huku akitabasamu
“Anatulipa kwa dola au shilingi?” Agnes aliulza
“Hembu na wewe acha ushamba wako, huku shilingi aitolee wapi?” Fetty alimkosoa mwenzake
“Haya yaishe kiongozi Fetty”
“Muambia sisi tunataka dola milioni mia zinatutosha”
Samson akamgeukia bwana Rusev na kumueleza kiasi walicho kitaja wezake na bwana Rusev hakuwa na hiyana zaidi ya kukubali kuwalipa kiasi hicho.
 
“Anauliza tunataka cashe au hadi benki?”
Anna akashusha pumzi na kubugia fumba moja la juisi anayo kunywa
“Hapa cha msingi kila mmoja apewe kiasi chake mkononi, tusepe” Halima alizungumza huku akiwatazama wezake machoni
“Ujue hizo pesa ni nyingi sana, na kama kuzibeba itakua ngumu?” Fetty alishauri
“Sawa Fetty, haya tukisema tupewe kwenye, akaunti namba tutazitolea wapi, hiyo moja, mbili sisi site hapa tunatafutwa karibia dunia nzima, ni benki ipi tutazipeleka sura zetu na kwenda kuitoa hiyo pesa?”
 
“Kumbe siku moja moja na wewe. Anna unazungumzaga poiti. Kikubwa hapo Samso muambie huyo mtui wako tunahitaji cashe hapa hapa, kam ni kwenye mabegi tutabeba, cha msingi ni kupewa pesa na kwenda kuanza maisha mapya mbele ya safari”
Agnes alizungumza na wote wakakubaliana waweze kukabidhiwa pesa zao mkononi, Samson akamueleza bwana Rusev maamuzi waliyo yafanya wezake. Bwana Rusev akanyanyua mkonga wa simu yake ya mezani, akaminya namba kadhaa na kumpa maelekezo mlinzi wake, pamoja na muhasibu wake.
 
“Jamaa anasema pesa inakuja”
Kila mmoja akajiweka mkao wa kupokea kitita chake, ili aweze kuendelea na maisha yake mbele ya safairi. Baada ya dakika kumi na tano kukatika kundi kubwa la watu wapatao kumi, wenye bunduki wakaingia ndani ya ofisi ya bwana Rusev, jambo lililo anza kuwapa wasiwasi Fetty na wezake ambao hawakueelewa ni kitu gani kinacho endelea kwani, watu hao wameingi gafla na moja kwa moja wakamzingira bwana Rusev.
                                                                                                ***
    Kitendo cha Rahab kujikwaa na kuanguka chini, ikawa ni bahati nzuri kwake, kwani mshale ulio kuwa umelengwa na zombi mmoja ulipita juu yake na kugonga kwenye mti uliopo mbele yake.
 
“Haaa……!!!”
Rahab alijikuta akiduwaa na kutazama nyuma, kwa mbali akamuona mtu huyo aliye fura hasira akija kwa kasi ya ajabu, kwa haraka Rahab akaikota bunduki yake, kwa bahati nzuri akakuta kuna risasi moja, akaikoki kwa haraka na kumlenga zombi huyo anaye mfwata kwa kasi. Kama kawaida yake Rahab, hakukusoea kuifyatua risasi hiyo iliyo tua kichwani mwa zombie huyo na kumpua kchwa na kugawanyika vipande vipande. Raisi Praygod akaendelea kushangazwa na uwezo mkubwa wa upambanaji alio kua nao Rahab ambaye  hakumdhania kwamba anweza kuja kuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha ya kuiokoa roho yake. Rais Praygod akampa mkono Rahab na kumnyanyua kutoka chini alipo kua ameanguka. Wakaendelea na kukimbia.
 
Mlio wa bunduki, ukawastua mazombi wote walio kua kwenye msitu huu, wakafahamu ni wapi mlio huo wa bunduki ulitokea, walicho kifanya ni kubadili mielekeao yao na kwenda sehemu ya tukio huku akijifariji kwamba watu wanao wawinda watakua wamekamatwa na mmoja wao. Wote wakajikuta wakishikwa na butwaa baada ya kumkuta kiongozi wao akiwa amechanguliwa kichwa chake kama ilivyo kua kwa mwenzao waliye mkuta ndani ya kijumba akiwa amekufa, Baadhi yao hawakuweza kuyazuia machozi yao kuweza kumwagika kwani kiongozi wao huyo ndio kila kitu katika maisha yao.
 
Rahab na Raisi Praygod wakaendelea kutokomea msituni, huku mwanga wa mbalamwezi ukizidi kuwapia uwezo wa kuweza kuona ni wapi wanapo kwenda na niwapi wanapo tokea. Wakafanikiwa kufika barabarani ambapo wakalikuta gari la watu hao wa ajabu, likiwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara. Wakaanza kulinyatia taratibu, huku kila mmoja akiwa amepita upande wake. Wakafanikiwa kufika mbele, kwenye kichwa cha dereva, wakachungulia ila hapakuwa na mtu wa aina yoyote zaidi funguo inayo ning’inia pembeni ya mskani
 
“Panda”
Raisi Praygod alimsisitiza Rahab ambaye alikua akiendelea kulichunguza gari hilo linalo toa harufu kali ya mizoga iliyo kufa. Rahab akafungua mlango na kuingia, Raisi Praygod akawash gari, taratibu wakaanza kuondoka katika eneo hilo huku, raisi akijitahjidi kuongeza mwendo wa gari hilo linalo toa mgurumo mbaya, kama mabati yanayo gonganga kwa nguvu
 
Mlio wa gari, ukawastuaa mazombi hao walio kua wakiendelea kusononeka na kuomboleza kifo cha kiongozi wao. Wanne kati yao, wakakimbilia sehemu mlio wa gari unapo tokea huku wengine wakiubeba mwili wa mkuu wao kuurudisha kwenye makazi yao.
 
Gafla raisi Praygod akajikuta akifunga breki kali, baada ya kuwaona mazombi wanne wakiwa wamesimama katikati ya barabara huku kila mmoja akiwa ameshika bunduki aina ya gobore, wakiwa wamezielekezea kwao, wakiwa tayari kwa kuwalenga Raisi Praygod na Rahab.
 
                                    ***
Wanajeshi wa bwana Rusev walio mzingira, wakamnyanyua kiongozi wao, huku wakimuhitaji aweze kukumbia kwani kuna mashambulizi ya ndege za kijeshi la Russia yanaweza kufanyika ndani ya dakika kadhaa zinazo kuja. Wakatoka kw mwendo wa kukimbia huku wakiwa wamemzingira kiongozi wao huyo wanaye mtukuza kama muumba wao.
“Jamani inakuwaje, mbona tumeachwa peke yetu?”
Anna aliuliza huku akiwa amesimama wima akichungulia mlangoni na kumuona kiongozi huyo akiingia kwenye lifti yeye na wanajeshi wake na kushuka chini.
 
“Tuondokeni”
Samson alizungumza huku akiongoza msafara wa kuelekea walio elekea bwana Rusev na wanajeshi wake, kwa mwendo wa haraka wakafanikiwa kufika kwenye lifti, ikawalazimu kuweza kusubiri baada kwa muda kidogo kwani bwana Rusev na watu wake walikua wanaelekea chini wakitokea gorofa ya tano. Baada ya muda lifti ikafunguka na wote watano wakaingia ndani na Samson akaminya kitufe cha kuelekea chini. Wakiwa katika gorofa ya tatu, mtikisiko mkubwa, wa bomu ukatokea na kuisababisha gorofa hilo kuyumba na umeme ukakatika na kuipekea lifti hiyo kusimama na kumfanya Agnes kupiga ukelele mkali, kwani gorofa lilianza kuteguka vipande vidogo vidogo likielekea kuanguka chini.
 
 SHE IS MY WIFE(30)
  
   Mtikisiko ukaendelea kulitetemesha jengo lihi ambalo lilipigwa kombora na ndege ya jeshi la Russia, ikiwa ni shambulizi la kustukiza kwenye kikosi hichi kinacho itesa serikali kwa kipindi kirefu. Kwa bahati nzuri mlango wa lifti ukaweza kuachia upenyo mdogo, kwa kutumia nguvu Samson akaanza kuufungua hadi ukafunguka, kwa bahati nzuri sehemu lifti ilipo kwamba ni gorofa ya pili, wakatoka wote kwa pamoja na kutafuta eneo lenye ngazi za kushukia. Kwa bahati nzuri eneo la ngazi halikua mbali sana na eneo zilipo lifti.
 
Milio ya risasi, ikaanza kusikika vizuri masikioni mwao, ikitokea nje, hhuku kindi la Mr Rusev likipambana na wanajeshi walio kuja kuvamia katika kisiwa hicho, wakafanikiwa kutoka nje huku gorofa hilo wakiliacha likendelea kumeguka vipande vidogo vidogo.
 
“Twendeni huku”
Samson alikua kiongozi wa wengine, na hapakuwa na wakumuuliza kwamba ni wapi wanapo elekea kwani kila mmoja alihitaji kuyaokoa maisha yake au kuuokoa usalama wake kutoka mikononi mwa jeshi la serikali hiyo inayo linalo sifika kwa maamuzi magumu pale wanapo mkamata mtu anaiye jihusisha na ugaidi, na mara nyingi wa wa namna hiyo wameweza kuambulia kifo kwa kupigwa risasi nyini zisizo na idadi mwilini mwaoa kama alivyo fanyiwa kiongozi Saddam Hussein.
 
Wakafanikiwa kufika kwenye moja ya jengo, ambalo milango yake yote imefungwa kwa makufuli makubwa
“Samson tunafanyaje sasa?”
Halima aliuliza huku macho yakimlenga lenga. Samson hakumjibu chohote Halima zaidi ya kuziangalia ndege za jeshi, aina ya Jet zikipita kwa kasi katika eneo mbali kidogo na sehemu walipo, huku zikimwaga risasi nyingi kwa wanajeshi wa Bwana Rusev. Hapa ujambazi wao wakauona haufui dafu mbele ya shambulizi hili lililo wapagawisha akili zao huku kila mmoja asijue ni wapi kwa kwenda.
 
Kwa bahati nzuri bwana Rusev akafanikiwa kuingia kwenye manohari walio kuja nayo Samson na rafiki zake, akiwa na kundi la wanajeshi wake walio kuja kumchukua ofsini kwake. Hapakupoteza muda zaidi ya kuondoka katika eneo la kisiwa ambacho kwa sasa hali yake imekua mbaya zaidi ya kuzimu. Ila nafsini mwake bwana Rusev akatokea kuwaonea huruma sana Samson na mabainti wadogo alio kuja nao, ambao Samson aliwaeleza walikuwa ni magaidi wanao anza kuchipukia katika swala zima la kigaidi.
 
Kazi ikawa ni ngumu kwa Samson na wezake ambao hadi sasa hivi hali inazidi kuwa tete kwao, hawakujua ni wapi waende kukweukwepa mkono wa serikali, mfano mzuri wanaouona kwa askari wa bwana Rusev wanavyo angushwa chini kama kuku wenye videri kwani, risasi kutoka kwenye ndege hizo za jeshi hazikukosea wapi kwa kupiga.
“Jamani hapa hatuna la kufanya, kila mmoja atawanyike kivyake akaokoe maisha yake mbele ya safari”
Samson alizungumza huku akihema kwa nguvu
“Nyoo atawanyiki mtu hapa, wewe ndio umetuleta na wewe ndio utatuokoa”
 
Agnes alizungumza kwa hasira akionekana kumpiga Samson vikali, kwa wazo lake alilo liropoka
“Sikia SAMSOM. Nahisi hutujui vizuri wewe eheee?”
Fetty alizungumza huku sura yake ikiwa imebadilika kabisa, akionekana anaweza kufamfanya Samson kitu chochote muda wowote kuanzia sasa. Samson ikambidi awe mpole kana ni uwezo wa kupigana na Fetty na wezaka anao, ila hajui ni watu wa aina gani hadi wanajiamini kiasi hichi na kuwa magaidi wanao sakwa na jeshi la polisi Tanzania.
 
“Twendeni huku”
Ikamlazimu Samson kuwa kuanza kukimbia kuelekea asipo pajua, ila alihitaji kuepukana na varangati la Fetty na wezake, kwani anafahamu varangati la Rahab, alilo anzishiwa siku alipo kua naye chumbani, na hawa ni rafiki wa Rahab, ina maana wote varangati lao si lakitoto. Wakazidi kukimbia huku wakimfata Samson kwa nyuma. Kila walio ona mwili wa askari aliye fariki hawakusita kuiokota bunduki ya askari huyo, Wakaingia kwenye msitu uliopo kwenye kisiwa hicho, Kila mmoja akajitahidi kufyatua risasi pale walipo weza kupata nafasi ya kufanya hivyo kwa wanejeshi wa serilali walio anza kuingia kisiwani wakitokea kwenye boti zao walizo kuja nazo kupitia baharini.
 
Hapakuwa na muda wa masihara tena zaidi ya wao kufanya kazi moja tu ya kuua kila mwanajeshi aliye jitokeza kwenye macho yao. Mashambulizi ya ndege za kivita yalisitishwa kutokana na wanajeshi kuingia ndani ya kisiwa, kwahiyo ingewawia ngumu marubani wa ndege hizo aina ya Jeti kuendelea kufanya mashambulizi ambayo yangeweza kuwadhuru hadi wezao. Hiyo ikawa ni nafuu kubwa sana kwa Samson na wezake. 
 
Wakafanikiwa kufika ufukweni ambapo, wakaweza kukuta nguo maalumu za kuogelea, zilizo vuliwa na wajeshi baadhi walio tumia njia ya kuogelea kuingia ndani ya kisiwa hicho na kuanza kufanya mashambulizi ya kimya kimya. Wakayavua mavazi yao waliyo yavaa, wakavaa mavazi hayo ya kuogelea ambayo yana mitungi midgo ya gesi inayo valiwa mgongoni, huku ikiwa na shivikizo vidogo. Kisha wakakimbilia ndani ya maji na kuanza kuogelea kwa kasi kila mmoja anayo imudu yeye.
                                                                                                   ***
“Usipunguze mwendo muheshimiwaaaaa”
Rahab alizungumza kwa sauti kali, iliyo mbadilisha mawazo Raisi Praygod, na kumfanya ausogeze mguu wake kwenye brake na kuongeza mwendo huku wakiinama chini. Mazombi hawa kwa hasira wakaanza kufyatua risasi kwenye kioo cha gari pasipo kulipisha, Raisi Praygod akazidi kuongeza mwendo, hadi misuli ya mwili wake ikakaza kabisa, huku akiwa amayang’ata meno yake kwa nguvu akihakikisha anawafikia mazombi hao walio endelea kupiga risasi. 

Kwa bahati nzuri gari hilo likawaponda ponda vibaya mazombi hao walioweka mgomo wa kulipisha gari hilo na kupelekea kuwaponda ponda vibaya na kufafa. Kwa haraka Raisi Praygod akajiweka sawa kuendelea kuliendesha gari hili linalo kwenda kwa kasi, wakaendelea kuifwatisha barabara hiyo ya lami ambayo ni ndefu sana na haina kona nyingi sana, na ipo katikati ya msitu huu mnene na wakutisha. 
 
Wakafanikiwa kukuta kibao kilicho andikwa kwa herufi kubwa za kushongesha ‘GOOD BYE BLACK FOREST’ Ikiamaanisha kwamba msitu huo ndio jina lake, kabdi walivyo zidi kwenda ndivyo walivyo zidi kuoata matumaini ya kuingia kuokoka kwani, waliweza kukutana na barabara nyingine, ambazo zina magari ya watu wa kawaida.
“Asante Mungu”
Rahab alizungumza huku akionekana kuto kuoamini kwamba wapo salama wakitokea kwenye mikono ya watu ambao walihitaji kuzitoa roho zao. Taratibu gari hilo likaanza kupunguza mwendo kasi wake, likiashiria kuishiwa na mafuta
“Vipi….?”
Rahab aliuliza huku akimtazama Raisi Pragod usoni
“Yatakua ni mafuta yamekwisha”
 
“Ohooo itakuaje sasa”
“Kwa hapa hakuna tatizo kutokana kuna magari yanayo pita tunaweza tukaomba msaada na kuchukuliwa”
“Mmmmm”
Raisi Praygod akalisogeza gari hadi kando kando ya barabara na kuliegesha, kisha wao wakashuka huku wakiwa wamevalia magauni, waliyo weza kuyapata usiku ulio pita. Magari yakazidi kukatiza kwenye barabara waliyo kuwepo, hii ni kutokana na kupambazuka, na mwanga wa juu kuchukua nafasi yake katika dunia. Mwanga wa juu la asubuhi, likaendelea kupiga kwenye miili yao, na kuwafanya wajihisi vizuri kwenye miili yao, ila njaa kwa mbali zikaanza kuyasumbua matumbo yao yaliyo kosa chakula kwa masaa mengi.
“Muheshimiwa hapa tunaelekea wapi kwa maana sielewi elewi”
 
“Tusimamishe simamishe magari tutajua pa kwenda, kikubwa tumetoka kwenye hatari”
Wakaanza kazi ya kuyasimamisha magari yanayo katiza kwenye barabara waliyopo, kila mmoja aljitahidi kupunga mkono kwa kila gari lililo kua likikatiza ila madereva wa magari hayo hawakuweza kusimamisha magari yao kuhofia jinsi watu hao walivyo vyaa, wakihisi ni wendawazimu.
“Tutembee tembee mbele”
Raisi Praygod alishauri na wote wakaanza kutembea, huku wakiendelea kuyasimamisha magari hayo pasipo kufanikiwa.
“Muheshimiwa nikuulize kitu?”
“Uliza tu”
“Unavyo hisi kwa sasa, Tanzania, itakua inaongozwa na nani?”
“Aisee, hata mimi sijui ila kisheria makamu wangu, ndio anaweza kukaimu kiti changu cha uraisi hadi zipite siku tisini ndio wanaweza kufanya uchaguzi wa kumchagua raisi mwengine, kama mimi sinto jitokeza”
“Ila inabidi uwahi kurudi nchini, ninaimani kwamba watu watakua wanahisi umefariki”
 
“Ni kweli, ila kwa sasa inanilazimu kuweza kupumzisha akili yangu, kabla ya siku tisini ninaweza kurudi nchini Tanzania”
“Sawa, je familia yako nayo si itakua na majonzi makubwa?”
“Yaaa, ila mke wangu alishafariki mwaka sasa umepita”
“Alaa, sijawahi kuisikia hiyo?”
“Ulikuwa wapi?”
“Aisee kipindi hicho mimi wala sikuwa ninajihusisha na maswala ya serikali, nilikua nikitafuta pesa kwa shida kubwa sana”
“Kwani ulikua unafanya kazi gani?”
Rahab akakaa kimya kuweza kutafakari ni nini amjibu Raisi Praygod, ambaye bado ni kijana mdogo wa miaka thelathini na tano. Rahab aliwaza endapo atamuambia kwamba alikua akifanya kazi ya kuuza mwili wake, atajishusha thamani. Pia akahisi akimueleza kwamba alikua ni jambazi inaweza kuleta picha tofauti
 
“Vipi mbona kimya, haujibu swali langu?”
“Ahaaa, kusema kweli muheshimiwa mimi, nilikua ni miongoni mwa wale wasichana watano majambazi walio isumbua serikali kwa matukio ya uvamizi wa benki”
Raisi Praygod akastuka kidogo, ila akajitahidi kuuficha mstuko wake, akaachia tabasamu pana kiasi usoni mwake na kumfanya Rahab, asihisi kitu chochote kinacho endelea kwa Raisi huyo
 
“Sasa kwa nini muliamua kufanya ujambazi?”
“Kusema kweli sisi tulichukuliwa na mzungu mmoja, aliye kua akifanya kazi kwenye hospitali ya jeshi kama daktari mwalimu wa kuwafundisha madaktari wa jeshi kutengeneza sura bandia. Ambao yeye alikua akitufundisha kisha na kutupa kazi ya kuweza kuua baadhi ya watu maarufu”
Hadi kufika hapa Raisi Praygod akawa amemuelewa Rahab, nini anacho kizungumza kwani kazi hiyo yeye ndio alipanga ianyike, akishirikiana na rafiki yake Dokta William, kutokea Israel, kwa lengo la kuweza kuwaangamiza watu wote wanao enda kinyume na serikali kwa kipindi hicho. Ila hadi wasichana hao kuigeuka serikali hakufahamu kuna kitu gani kilicho kua kikiendelea katikati.
 
“Ahaaa, ila kwa sasa si umeuacha?”
“Sina haja tena inabidi, nifanye kazi halali, kwani hata yule daktari hatujui ni wapi alipo. Wezangu nao ndio hivyo wamekamatwa, nahisi watakua wemesha nyingwa. Kwani kwa makoso tuliyo yafanya sidhani kama wataacha hai”
Raisi Praygod hakuzungumza chochote zaidi ya kuangaza angaza tena macho yake barabarani, akaona gari kubwa aina ya scania, likija kwa mwendo wa kawaida, akalipungia mkono, ila likawapita pasipo kusimama. Kufika mbele kidogo dereva huyo akalisimamisha gari hilo, na kuwapigia honi Rahab na Raisi Praygod, waende wakapande.
 
Raisi na Rahab wakalikimbilia gari hilo hadi sehemu lilipo simama, ambapo dereva wa gari hilo wakakuta ni mtu mwenye asili ya Afrika. Mtu huyu akaonekana kumtazama Raisi Praygod kwa muda kisha, huku akiwa haamini macho yake
“Wewe si raisi wa Tanzania, bwana Praygod Makuya……!!?”
Mtu huyo alizungumza kiswahili, sahihi akiashiria kwamba yeye ni mtanzania, Rahab akamtazama Raisi aliye pata kigugumizi cha gafla, ila akajikaza hivyo hiyo kumjibu mtu huyo
“Ndio, ndio mimi”
“Ingieni ndani”
Mtu huyo alizungumza kwa furaha, na kuwafanya Rahab na Raisi Praygod kuingia ndani ya gari na kukaa kwenye siti mbili zilizo kua wazi.
 
“Mimi ninaitwa Azaria, ni mtazania”
“Tunashukuru kukufahamu, hivi hapa ni wapi?”
“Huku ni Mexco, kidogo nimekuja  kutafuta tafuta maisha, nimepata kazi kwenye kampuni hii ya kusafirisha mafuta. Vipi tena mbona huku?”
“Tulipata ajali ya ndege, mimi na huyu binti ndio tumefanikiwa kupona”
“Aisee poleni sana wapendwa, unajua mara yangu ya mwisho kuondoka Tanzania ndio kilikua kipindi cha kupiga kura. Nilikupa kura yangu muheshimiwa”
“Asante sana, pia asante kwa kuweza kutusaidia”
“Aisee poleni sana, pia muna bahati hapa ninaelekea mjini, ninapo ishi. Ninatoka mikoa ya chini huko kupeleka mafuta”
“Ahaaa asante sana, huyu ni msaidizi wangu anaitwa Rahab”
 
“Nashukuru kukufahamu dada Rahab”
“Asante na wewe pia kaka Azaria”
Wakafika kwenye mmoja wa mgahawa ambapo Azaria akashuka na kwenda kuwanunulia chakula pamoja na vichwaji, kisha akarudi navyo kwenya gari na kuwakabidhi Raisi Praygod na Rahab ambao wanaonekana kuchoka sana, kwani tangu walipande gari hilo yamekatika masaa sita wakiwa barabarani. Wakaanza kukila chakula hicho taratibu huku wakionekana kuwa na hamu kubwa ya kula chakula kizuri kama hicho. 
 
“Hii safari itachukua muda gani kufika jijini Mexco City?”
Raisi Praygod alizungumza huku akiwa amefundia kipande cha paja la kuku, lililo nona sana
“Hapa bado sana itatuchukua masaa mengine kama saba, hivi. Tuombe Mungu tusisimamishwe na askari kwa maana huku wanajali sana kukagua passport”
“Aisee kumbe ni kurefu sana?”
“Sana tu, kwa dereva ambaye si mzoefu anaweza kulitupa gari, nje ya barabara. Ila kwa sisi wazoefu tunaona ni jambo la kawaida.”
 
Kutokana na kushiba, uchovu mwingi ukamtawala Rahab na kujikuta akilala fofofo huku, akiwaacha Raisi Praygod na Azaria wakiendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale.
“Muheshimiwa inatubidi kuweza kulala kwenye Motel moja hapo, mbele, kwani hapo mbele kuna kizuizi cha ukaguzi, na jinsi ninyi mulivyo watatupa shida na giza limesha ingia muda huu”
“Sawa hakuna shida, tena umefanya la maana, kwani kuna rafiki yangu yupo hapa Mexco ninaweza wasiliana naye akanipa hifadhi kwa muda”
“Kwa nini usiupigie ubalozi wa Tanzania ukakuletea msaada?”
“Kwa sasa sihitaji msaada wa kiserikali kuna mambo inanilazimu niyakamilishe kabla sijarudi nchini kwangu”
“Sawa muheshimiwa Raisi”

Wakafika kwenye moja ya Motel iliyopo mbembezoni mwa barabara, na kuna magari mengi makubwa, ikiashiria hapo ni sehemu ya madereva wengi kuweka vituo vyao, ili kuendelea na safari zao muda walio upanga wao wenyewe. Azaria akamuomba Raisi abaki ndani ya gari, kisha yeye akashuka kwenda kukata vyumba vitatu, kisha akarudi akiwa na funguo mkononi
“Tunaweza kwenda”
Raisi Praygod akamuamsha Rahab ambaye muda wote alikuwa amelala fofofo, hii ni kutokana na kukesha siku nyingi pasipo kulala. 
 
“Ehehee….”
Rahab aliweweseka kwa wenge la usingizi, huku akijitahidi kuyafumbua macho yake kuweza kutazama ni wapi walipo.
“Tumefika, shuka twende”
Raisi Praygod akamsaidia Rahab kushuka ndani ya gari na wote wakaongozana na Azaria hadi kwenye vyumba vyoa, huku kila walipo pita baadhi ya watu waliwatazama RaisI Praygod na Rahab kwani wemechafuka sana, huku miili yao wakiwa wameisitiri kwa magauni yaliyo chafuka.
Wote wakaingia kwenye chumba kimoja cha Raisi, ambapo kuna simu maalumu, yenye uwezo wa kupiga sehemu mbalimbali.
 
“Muheshimiwa niwaletee vyakula tena?”
“Hapana kwa mimi nipo sawa, labda kwa huyo bibie”
“Mimi ninausingizi mwaya, asanteee”
Rahab alizungumza huku akipiga miyayo na kujirusha kitandani, hakujua kwamba hichi chumba si chake. Azaria akataka kumuamsha ila Raisi Pragod akamzuia.
“Wee muache tuu hakuna shida, akilala hapa”
“Sawa muheshimiwa ngoja mimi niende chumbani kwangu”
“Sawa na uwe na usiku mwema”
“Sawa muheshimiwa”
Azaria akatoka na kumuacha Raisi Praygod akiendelea kuminya minya baadhi ya batani za simu akijaribu kukumbuka namba za rafiki yake huyo aliye soma naye kipindi cha nyuma nchini Canada. Kwa bahati nzuri akakuta namba ya rafikia yake huyo ipo hewani, ikaita kwa muda, kisha ikapokelewa.
 
“Who?”(Nani?)
Sauti nzito ya kiume ilisikika upande wa pili wa simu
“Praygod Makuya hapa vipi wewe”
“Ahaaaa kaka, upo Mexco nini?”
“Ndio mskaji wangu, nipo kwenye motel moja hivi nimechili”
“Raisi unakaa kwenye Motel, vipi bwana mbona kuna mijihoteli mingi mikubwa kwa hadhi yako”
“Kaka yaliyo nikuta wewe acha tu?”
“Vipi kuna tatizo?”
“Yaaa tena si dogo, ila kukipambazuka tu nitakupigia ujue ni wapi nilipo uje kunifwata”
“Ahaaa kaka kwanini usiniambie sasa hivi nije kukuchukua. Kwa maana usakama wako wewe unahitajika na mimi ninavijana wengi  tu wa kukulinda”
“Hapana Frednando, tusubiri kupambazuke nitakupigia au wewe unaweza kupiga kwa namba hii, nitakuambia ni wapi nilipo”
“Sawa kaka, haina shida, ngoja niweke mazingira vizuri”
“Sawa”
 
Raisi Praygod akakata simu na kuanza kushangilia kwani matumaini ya usalama wake kwa ujumla yamesha rudi, kwani rafiki yake ni miongoni mwa matajairi wakubwa ndani na nchi ya Mexco. Macho ya Raisi Praygod yakatua kwenye mapaja ya Rahab, aliye lala kifudi fudi, na kuacha makalio yake makubwa kiasi kuonekana vizuri. Taratibu Rais Praygod akamsogelea Rahab, akachuhuka shuka kubwa na kumfunika. Rahab taratibu akajigeucha na kumtazama Raisi Praygod.
“Wewe hulali?”
Rahab aliuliza kwa sauti ya unyonge, huku akimtazama Raisi Praygod kwa macho yaliyo jaa usingizi, hadi akajikuta akirembua.
 
“Nataka nikaoge”
Rais Praygod akapiga hatua moja, ila Rahab akamshika mkono na kumvuta kwa nguvu na kuangukia kitandani. Rahab kwa haraka akausogeza karibu mdomo wake kwa Raisi Praygod na wakaanza kunyonyana, huku wakionekana kuwa katika hisia kali. Raisi Praygod akalivua gauni lake na kulitupa pembeni. Akalishika la Rahab na akamvua, wote wakabakiwa kama walivyo zaliwa.

ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts