Home » , » RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 33 & 34

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 33 & 34

Written By Bigie on Saturday, October 29, 2016 | 11:07:00 AM

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Hembu Halima acha roho mbaya, tumekuja pamoja tutaondoka pamoja haiwezekani tumuache mwenzetu hapa”
Fetty alizungumza kwa msisitizo na kuzidi kumchefua Halima. Bwana Rusev akamuamrisha askari kuwasiliana na wezao walio ndani, naye akafanya hivyo kupitia simu ya upepo. Taaa zote nje ya jumba hili zikawashwa, na kuwafanya Fetty na wezake waonekane waliopo, Walinzi wapatao hamsini, wakiwa na bunduki, waliiekekeza mitutu yao katika eneo walilo lala Fetty na wezake na kuwafanya wanyanyuke taratibu huku mikono wakiwa wameinyanyua juu.

ENDELEA
“Hichi ndicho mulichokua mukikihitaji?”
Halima alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza akionekana kukasirishwa na kitendo hicho cha wezake kuwa wabisha hadi wametiwa nguviuni na wanajeshi hjao wa bwana Rusev ambaye kwa mara ya kwanza walimuona ni mtu mwema kutokana na ukarimu wake alio waonyesha kipindi akiwapoke na kuzngumza nao hukusiana  na biashara ya kuuza manohari waliyo fanikiwa kuiteka kutoka katika jeshi la wana maji wa Tanzania.
 
Wakaamrishwa kuelekea sehemu ambapo yupo Samson, akiendelea kulia kwa maumivu makali aliyo yapata kutokana na risasi aliyo pigwa mguuni mwake.
 
Mr Rusev akaagiza wapelekwe kwenye chumba chenye giza zito na wafungiwe humo hadi kutakapo pambazuka ndipo ajue ni nini awafanye kwani siku zote hua hapendelei mtu kugundua siri zake na isitoshe wao ndio walio sababisha kwa makao makuu ya vikosi vyake kuweza kuvamiwa na jeshi la nchi yake ya Russia na kusababisha vifo vya wanajeshi wake wengi sana.
 
Fetty na wezake wakingizwa kwenye chumba chenye giza zito, hata kam ni jasiri kiasi gini giza la chumba hicho ni lazima uogope kwani hata mtu wa pembeni yako ha ta hauwezi kumuona zaidi ya kuisikia sauti yake.
 
                        ***
      Wakafika kwenye jumba la Frednando, ambalo lipo katikakti ya jiji la Mexco, Raisi Praygod na Rahab wakapokelewa kwa heshimwa kubwa na wafanyakazi wa Frednando ambao alisha wapa taarifa juu ya ugeni huo wa rafiki yake kipenzi. Wakakaribishwa kwenye moja ya seble ambayo kuta zake zimepabwa na madini ya dhahabu, huku sofa zake zikiwa zimetengenezwa kwa mtindo ambao Raisi Praygod hakuwahi, kuuona katika maisha yake
 
“Kaka uajua jumba  lako ni zuri kuliko ikulu yangu?”
“Weee, acha utani kaka”
“Kweli vile Frednando, inanibidi nikirudi hivi Tanzania ikulu yangu niweze kuibadilisha, kidogo mfumo uwe kama huu wako”
“Ila unakumbuka kwamba ikulu si yako, ukimaliza kipindi chako anakuja mwengine?”
“Hata kama ila, kwa kipindi nitakacho kuwepo mimi itanibidi nikae kidogo sehemu ambayo ninaihitaji mimi”
 
Wakiwa kwenye maongezi ya furaha, wahudumu wakawa na kazi ya kuandaa chakula na vinywaji, kwa ajili ya wageni hawa. Kwa upende wa Rahab, kila kinacho tokea kwake anaona kama ni ndoto, kwani hakutarajia ipo siku atakuja kuishi maisha ya kuheshimiwa kama haya. Moyo wake ukajikuta ukiuchukia ujambazi ambao alikuwa anaufanya na rafiki zake ambao hadi sasa hivi ajui kama wapo hai, kwani kwa fununu alizo kua akizisikia, ni kwamba marafiki zake hao nilazima waweze kunyongwa, hii ni kutokmna na uhalifu mkubwa walio ufanya wa kuwaua askari wengi wa jeshi la polisi.
 
“Kuna klitu Frednando nahitaji kukifanya hivi karibuni?”
“Kitu gani?”
“Ninahitaji kumuoa Rahab wangu”
Rahab akastuka kusikia hivyo kwani hakutegemea kwamba inaweza kuwa jambo la haraka kama anavyo hitaji Raisi Praygod
“Waooo, kaka hilo ni jambo jema, tena unaonaje ukalifanya hapa hapa kwangu”
“Ndio maana nikakuamnbia nahitaji kulifanya siku hizi za karibu, kutokana nampenda sana Rahab, bila yeye nahisi kwa sasa ningekua marehemu”
“Kweli kaka, wewe sema ni lini unahitaji kumuoa, niweke mambo sawa si unajua tena”
“Huyu hana siku nyingi hata siku mbili hizi zijazo pia itakua ni sawa”
 
Rahab akaachia tabasamu pana lililo zidi kuipendezesha sura yake iliyo teumbwa vizuri kwa haraka haraka ukimtamza unaweza kusema ni binti wa kirwanda aliye changanyia na msukuma, kwa maana, urefu amepewa, sura ndio usiseme, hicho kiuno chake sasa, kimefungashia mzigo wa wastani wa makalio yanayo mfanya awe na sifa zaidi ya sifa wanazo pewa asichana wengine.
 
Raisi Praygod na Rahab wakapewa chumba cha kupumzikia ambacho kina kila sifa ya kuitwa chumba cha kuweza kulala Raisi Praygod pamoja na mkewe mtarajiwa. Furaha ikazidi kutawala mioyoni mwao, kwani kila walipo kua pamoja hawakusita kuipa miili yao burudani ambayo, Raisi Praygod, alijikuta akizidi kuipenda kwani, mburudishaji alimjulia jinsi ya kumburudisha.
 
                                    ***
     Siku iliyo fwata, Fetty pamoja na wezake wakatolewa kwenye chumba ambacho walifungiwa, hawakujua ni wapi alipo Samson, ambaye walimuacha nje kipindi wakipelekwa kwenye chumba hicho. Wakafunga pingu mikononi mwao pamoja na nyororo ndefu miguuni mwao. Wakapelekwa kwenye moja ya chumba chenye kuta za vioo vigumu ambavyo si rahisi kuwez kumuona mtu wa nje, ila mtu aliyopo nje unaweza kumuona.
 
Chumba hicho hakikuwa na kitu cha aina yoyote, jambo lililo wapa alama ya kuuliza kila mmoja kwamba humo ndani wameletwa kufanya nini. Mr Rusev akaamrisha baunsa mmoja kuingia ndani ya chumba hicho kuweza kuwapa mkong’oto mkali Fetty na wezake ambao wanaendele kushangaa shangaa. 
 
Halima akawa wa kwanza kuliona jitu refu si chini ya Futi nane likiingia ndani ya chumba hicho, huku likiwa limejengeka kwa misuli mikubwa, huku likiwa tumbo wazi na suruali ndefu, aaliyo ichimeka kwenye mabuti yake makubwa ya kijeshi.
 
“Hei jamani chekini kule”
Halima aliwaambia wezake ambao walikuwa wametazama pande nyingine ya chuma hicho, kila mmoja akajikuta akitawaliwa na woga mwingi kiasi kwamba wakaanza kurudi nyuma nyuma, huku wakilihofia jitu hilo linalo toa mihemu mizito kana kwamba limetoka kukimbia safari ndefu.
“Jamani tuweni pamoja”
 
Fetty alizungumza na kuwafanya wote wanne wajiweke sehemu moja huku wakiwa na wanalitazama kwa umakini jitu hilo lililo anza kupiga hatua za taratibu kuwafwata walipo.
Jitu hilo likarusha ngumi ambayo, ilimpata Anna na kumuangusha chini huku akitoa ukelele mkali, wa maumivu kwani ngumi hiyo ilimpata begani. Mr Rusev na watu wake waliopo nje ya chumba hicho wakashangilia kwa kitengo cha jitu hilo walilo lipachika jina la Great Lundark.
“Anna nyanyuka”
Halima alizungumza huku akimpa mikono yake miwili, Anna na kumnyanyua kutoka katika sehemu ambayo ameanguka.
“Jamani tuweni makini, tutawanyike”
 
Fetty alitoa agazo ambalo kila mmoja alilitekeleza na kumzunguka jitu hilo, kutokana na minyororo mirefu waliyo fungwa miguuni iliwasaidia kuweza kupiga ndefu kiasi, Fetty akajirusha juu na kwakurumia pingu yake, akaipitisha kwa haraka kwenye kichwa cha jitu hilo, na kuanza kuning’inia kwa kwa mgongoni, na kulifanya jitu hilo kuanza kutapatapa, huku likijaribu kuiweka mikono yake shingoni, ili pingu hiyo isiendelee kumuumiza kuromeo lake. Halima na Agnes wakawa na kazi la kupiga magoti ya jitu hilo na kulifanya lianza kuyumba. 

Anna kwa hasira akalisogelea na kwakutumia mikono yake akalibamiza kwenye sehemu zake za siri na kulifanya litoe ukelele mkali. Anna akarudia tena kulibamiza kwenye sehemu za siri na kuzidi kulifanya jitu hilo kuyumba yumba. Fetty akazidi kutumia nguvu zake kuendelea kuivuta kwa nyuma shingo ya jitu hilo, huku miguu yake akiwa ameikunja na kukanyaga kwenye makalio ya jitu hilo, lililo anza kuishiwa nguvu.
 
Kwa usirikiano wao wakaweza uliangusha chini jitu hilo, hapo ndipo ikawa nafasi nzuri kwa Fetty kuimalizia kuivunja shingo ya jitu hilo na kuwashangaza bwana Rusev na watu wake waote ambao hawakutegemea kwamba jitu lao linaweza kufa.
 
Bwana Rusev akaagiza wapelekewe majitu mengine mawili yanayo fanana na jitu hilo walilo liua. Majitu mengine ambayo kwa jinsi yalivyo unaweza kuyapa jina la magoliati, hii ni kutokana na urefu wao na miili mikubwa waliyo nayo. Ikaingia ndani ya chumba huku ikiwa imeshika silaha mikononi mwao, huku wakionekana kuwa na hasira kali ya mwenzao kuuawa.

SHE IS MY WIFE(34)
   
Ikwa ni kazi kubwa sana ya Fetty na wezake kujiweka sawia kuhakikisha wanapambana na mijitu hiyo ambayo kusema kweli, ikikubahatisha kukutandika konde moja litakupa maumivu makali sana ambayo kuyavumilia kwake ni lazima machozi yakulenge lenge.
 
Fetty na Anna wakajiunga kupigana na jitu moja, huku Halima na Agnes wakaungana kupambana na jitu la pili. Haikuwa kazi rahisi kwako kuweza kupambana na majitu hayo yenye yenye silaha mikononi. Kwa bahati mbaya Fetty akatandikwa ngumi moja kifua iliyo muangusha chini na kujkikuta damu zikimtoka mdomoni. 

Anna kuona hivyo akarusha teke kali lililo piga sehemu za siri za jitu hilo na kulifanya litoe mguno wa maumivu huku likijikunya na kumpa nafasi nzuri Anna kuweza kuufikia uso wake. Kwa kutumia vidole viwili vya mkono wa kulia, Anna akavisokomeza kwa nguvu kwenye jicho la kushoto la jitu, akavitoa kwa nguvu na kuchomoka na jicho lote jambo lililo wastua bwana Rusev na wanajeshi wake
“Arrhgaagaa”
 
Jitu hilo lilitoa mlio wa maumivu huku, likiitupa silaha yake chini, na kupiga goti moja chini, huku likiendelea kulia kwa maumivu makali
Anna akaokota panga kubwa la jitu hilo na kulishika kwa mikono miwili, hii ni kutokana na uzito wake, akamtazama jitu hilo linalo endelea kuvujwa na damu nyingi kwenye jicho lake alilo lichomoa dakika mbili zilizo katiza. 
 
“Mother Fu….”
Jitu hilo lilimtusi Anna na kumpa hasira kali ya kulipitisha panga hilo kwenye shingo yake na kulitenganisha jitu hilo kichwa na kiwiliwili, jambo lililo zidi kumuogopesha bwana Rusev na watu wake na kujiuliza hawa wasichana ni watu wa aina gani.
Jitu linalo pambana na Agnes na Halima, likazidi kuwaadamisha mabinti hawa, kila mmoja amemshika shongoni mwake na mkunyanyua juu na kuendelea kuwababiza ukutani mwa chumba hichi kilicho tengenezwa kwa vioo vigumu sana.
 
Kila walipo jitahidi kujitoa mikononi mwa jitu hili walishindwa, na kila wanapo bamizwa ndivyo nguvu za mwili zinavyo waishia na kujikuta wakitokwa na damu za pua.
“Ha..lima na Ag..nes wana…kufa kule”
Fetty alizungumza kwa sauti ya kukata kata huku akinyanyua mkono wake wa kulia akimuonyesha Anna kwa kutumia kidole sehemu wanapo sulubiwa wezao hao wawili ambao wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha.
 
Anna kwa haraka akaanza kutembea huku mkono wake mmoja ukiliburuza panga hilo refu kuelekea walipo wezake, kitendo cha Anna kulikaribia jitu hilo, akaushirikisha mkono wake wa pili kulikamata panga hilo, na kwakutumia nguvu zake zote akalipeleka kwenye mguu wa kushoto wa jitu hilo, akautenganisha na mwili wa jitu hilo na kumfanya awaachie Halima na Agnes, na wakaanguka chini. Kwa hasira kali Anna akaanza kulikata kata jitu hilo kwa panga hilo kali, akazidi kulilarua huku akipiga makelele ya uchungu, kiasi kwamba akazidi kulitesa jitu hilo, linalo endelea kupiga makelele ya kuomba msaada wa walipo nje
 
“Ahaaaaaagrahhh”
Anna alipiga ukelele huku akilishusha kwa nguvu zake zote panga kwenye shingo ya jitu hilo na kulitenganisha kabisa kichwa mwili wake. Anna akalitupa panga hilo chini na kujikongoja hadi walipo Halima na Agnes, ambao kila mmoja anahema juu juu, kiasi cha kuwa katika hali mbaya sana. Fetty taratibu akajinyanyua na kwenda walipo wezake na kukumbatiana kwa pamoja huku machozi yakiwamwagika kwa uchungu mwingi, kwani wanapitia katika kipindi kigumu cha maisha.
 
”Bosi tuwapige risasi wafe?”
Mlinzi wa bwana Rusev aliuliza kwa lugha ya kirusi, bwana Rusev hakutoa jibu lolote zaidi ya kuendelea kuwafikiria wasichana hawa jinsi walivyo majasiri katika kupambana.
“Mkuu tuwaue tu hawa”
Askari mwengine alizungumza kwa hasira huku akionekana akiikoki bunduki yake. Kwa haraka bwana Rusev akachomo bastola yake na kumtandika risasi ya kichwa askari huyo, aliye koki bunduki yake kwa ajili ya kutaka kwenda kuwaua Fetty na wezake. Askari wote wakashangaa, na kujikuta wakimtazama mwenzao huyo aliye lala chini huku damu zikumvuja kichwani
 
“Kuna mwengine anaye taka kwenda kuwaua hao mabinti”
Bwana Rusev alizungumza kwa sauti ya ukali kwa lugha ya kurusi na kuwafanya askari wake wote kukaa kimya, huku wakimtazama bosi wao huyo aliye badilika na kuvimba. Bwana Rusev akapiga hatua hadi kwenye kitasa cha mlango wa kuingilia ndani ya chumba hicho. Akakishika kwa nguvu na kuufungua mlango huo na kuingia ndani huku bastola yake ikiwa mkononi, akawafanya Fetty na wezake kustuka, na kujikuta wakimtazama bwana Rusev, wakisubiri kupata hukumu yao kwa kuwaua majitu hayo
 
                                                                                   ***
     Siku ya harusi ya Raisi Praygod na Rahab, ikawadia huku ikiwa imeudhuriwa na wasio zidi ishirini. Rahab katika siku alizo weza kujikubali kuwa yeye ni mzuri, ni hii siku aliyo weza kuvishwa shele lenye dhamani kubwa sana ya pesa. Aliweza kupambwa na mwanamitindo waliye mpa kazi hiyo kutokea nchini Italia. Huku Raisi Praygod, akiwa ndani ya suti nzuri iliyo tengenezwa na kiwanda maarufu nchini Italia, na suti hiyo ina sifa za kipekee, ambayo mara nyingi huwa anaivaa raisi wa Marekani.
 
Kwana suti hiyo ina mionzi ambayo inaweza kuzuia risasi, ya aina yoyote kuweza kumfikia mvaaji wa suti hiyo, pili ni suti ambayo inaweza kuhimili mazingira yote ya hali ya hewa, kukiwa na joto sana inaweza kukuba ubaridi kwenye mwili, kukiwa na baridi sana kunaweza kukupa ujoto kwenye mwili wako. 

Hawakuamua kwenda kufunga sherehe hiyo kanisani bali walicho kifanya ni kumchukua mchungaji ambaye akawafungisha harusi hapo hapo nyumbani, baada ya tukio hilo muhimu la kufungishwa ndoa, wakafanya sherehe iliyo furahiwa na kila mmoja, ni mpiga picha mmoja tu aliye kodishwa kwa kuifanya kazi hiyo, huku watu wengine wakikataza kupiga picha hizo kutokana Raisi Praygod hakuihitaji kuweka wazi uwepo wake kama yupo hai. Furaha kubwa ikaendelea kutawala kwenye moyo wa Rahab ambaye hadi sasa hivi anajiona mwanamke wa kipekee sana kwenye maisha yake kwa kumpata raisi Praygod
 
Frednando akajitole kumzawadia rafiki yake huyo ndege aina ya Jet, aliyo inunua siku chache kabla ya harusi kimya kimya, pasipo mtu yoyote kulifahamu hilo. Ndege hiyo yakifahari ambazo zinamilikiwa na matajiti wachache duniani, hua zinaingia abiria wasio zidi watano, huku kiwa inaendesha wa marubani wawili, na nindege ambazo zinakwenda kwa kasi sana, na huwa imekamilika kwenye idara kuanzia idara ya kujulinda kwa kuweza kufungwa mitambo ambayo inazuia risasi na mabomu pale inapo kuwa imevamiwa angani.
 
“Rafiki yangu, hii ndio zawadi yangu kwako na shemeji yangu”
Bwana Frednando alizungumza wakiwa wamesimama kwenye kiwanja cha ndege kilichopo kwenye kwenye eneo la jumba lake hili lakifahari. Wote watatu wakaingia ndnai ya ndege hiyo huku wakiwa na furaha. Frednando akawatambulisha raisi Praygod na Rahab kwa marubani wao ambao, wameajiriwa kwa kazi ya kuiendesha ndege hiyo popote pale ambapo Praygod na mke wake watahitaji kwenda. 
 
“Tuzungusheni kidogo angani, ili wafaidi utamu wa ndege yao”
Bwana Frednando alizungumza kwa lugha ya kimexco, marubani hao wakaifanya kazi yao iliyo wafanya wawe hapo. Taratibu mashine za ndege zikaanza kunguruma zikiashiria kwamba zinajiweka sawa kwa safari. Taratibu ikaanza kutembea kwenye kiwanja hichi ambacho nikikubwa kiasi. Jinsi ilivyo zidi kuongeza mwendo kasi ndivyo ilivyo anza kuiacha ardhi, huku kila mtu akiwa amekaa kwenye kochi lake, lililo lililo tengenezwa vizuri, huku pembeni kukiwa na kijimeza cha kuwekea juisi 
 
“Unajua hii ndege, nimeinunua Dola milioni thelathini na tano”
“Duuu mbona pesa nyingi, hiyo inalisha nchi yangu”
“Ahaa kawaida ndugu yangu kwa maana, kuna yakwangu kama hii nayo niliinunua kwa bei kama hiyo seme zimetofautiana rangi, yangu ni nyeusi, nakumbuka kuna siku uliniambia kwamba unapenda sana rangi ya silva, nikaamua kukukamilishia moja ya ndoto zako”
 
“Asante sana Fred”
Wakiwa juu angani, wakaendelea kupata vinywaji mbalimbali, huku wakitazama baadhi ya chanel, za tv ndogo iliyopo kwenye kila meza ya safa lililopo ndani ya ndege hiyo ya kifahari. Gafla Rahab akaanza kujihisi vaibaya vibaya, huku mara kadhaa, akawa anajikaza ili Praygod asijue ni kitu gani kinacho endelea, ila gafla akajikuta akianza kutapika na kulichafua gauni lake alilo livaa

ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts