Get the latest updates from us for free

Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 75 & 76 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 75 & 76 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Bigie on Saturday, October 22, 2016 | 6:37:00 PMMWANDISHI : EDDAZARIA 

ILIPOISHIA
Macho yangu yakakutana na macho ya Lutfia, aliye pembeni ya mwili wa baba yake, aliye fariki dunia. Nikatembea kwa haraka hadi ulipo mwili wa chifu, kabla sijaugusa, nikastukia, Lutfia akinisukuma kwa nguvu na, nikaanguka chini
"Eddy, hupaswi kuugusa mwili wa baba yangu. Haya yote wewe ndio chanzo. Umekisababishia kijiji changu matatizo...."
 
"Lutfia ila si mimi niliye waua hawa wote"
"Wewe, ni chanzo Eddy, nakuanzi sasa hivi ninakuomba uondoke kijijini kwangu, la sivyo utakwenda kuungana na kifo cha hawa wote walio tangulia mbele za haki"
Lutfia alizungumza kwa msisitizo, huku machozi yakimwagika, ñà kifua chake kikipanda na kushuka kwa kasi akionekana kujawa na jazba kubwa dhidi yangu.
 
ENDELEA SASA
"Lu....."
"Eddy nimesema ondoka"
Lutfia alizungumza kwa kupaza sauti, hadi wanakijiji wote wakatutizama sisi, natambua hawajui lugha tunayo izungumza ila, matendo yanaashiria kwamba Lutfia hataki kuniona mbele ya macho yake. Nikamtazama Chifu, huku machozi yakinilenga lenga. Midomo ya Lutfia, inatetemeka kwa kufura kwa hasira, uzuri wake alio kua nao umetoweka kabisa. 

Taratibu nikauweka chini upanga wangu, kisha nikasimama na kutazamana na Lutfia aliye nitumbulia mimacho kiasi cha kunifanya nimuogope. Kila mwana kijiji ninaye mtazama sura yake imetawaliwa na majonzi mengi, wamama wengine wakiwa wanalia kwa uchungu huku wakigara gara kwenye vumbi, wakionyesha ni jinsi gàni, walivyo umizwa na tukio zima lililo tokea muda mchache ulio pita.
 
Sikumuangali mtu yoyote usoni zaidi ya kugeuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka, ulio changanyika na hasira kali. Nikafika kwenye kijumba changu, nikachukua kibuyu changu, ninacho hifadhia maji ya kunywa, nikachukua na kisu changu cha akiba, na kutoka nje ya kibanda changu. Nikautizama mji jinsi unavyo teketea kwa moto, hasira dhidi ya John ikazi kunipanda. Nikaanzà kutokomea msituni, nikijaribu kutafuta njia ya kutokea kwenye kijiji hiki, kutokana na hasira pamoja na uchungu ulio nitawala moyoni mwangu, nikajikuta nikitembea hadi kuna pambazuka, pasipo kuchoka.
 
  Nikafika kwenye moja ya mlima mrefu, ulio zingirwa na miti mingi, kwa mbali nikaanza kusikia mngurumo wa gari, likipita eneo la karibu na mlima huu, kwa haraka nikashuka, nikiufwatisha mgurumo huo ni wapi unapo tokea. Kwabahati nzuri nikaiona barabara ya lami, iliyo chongwa kwenye mlima huu. Matunaini ya kufika ninapo pahitaji yakaanza kunijia moyoni mwangu.
 
Nikasimama, katikati ya barabara. Sikuona aibu kwa jinsi nilivyo vaa nusu uchi, huku sehemu zangu za siri, zikiwa nimezifunika na ngozi ya chui. Mlio wa gari sikuusikia tena, kwani ninahisi lilisha pita, kabla ya mimi kuifikia barabara. Nikaendemea kuzunguka zunguka maeneo ya barabara, nikijaribu kusubiria kama ninaweza kupata usafiri.
 
Gafla gari moja ndogo, likapita kwa kasi pasipo kufanikiwa kulipungia mkono, ila halikufika mbali sana, likasimama. Dereva wa gari hilo akaanza kulirudisha nyuma kwa kasi, hadi sehemu nilipo simama. Kioo cha upande wa dereva kikashuka, nikamuona mvulana mmija wa kizungu, àkiwa na mchumba wake, wakabaki wakinishangaa kwa jinsi nilivyo vaa.
Binti wa kizungu akatoa kamera yake, aina ya digital, na kuanza kunipiga picha, huku akiwa amesimama upande wa lili wa gari, nikaanza kuwafwata taratibu
 
"Casey get in the car"(Casey ingia ndani ya gari)
Mvulana huyu, alizungumza kwa haraka baada ya mimi kilikaribia gari lao, kabla hajafanya chochote, nikawahi kuingiza mkono kupitia upenyo wa kioo alicho kifungua. Nikachomoa funguo ya gari lao, nakulifanya lizime. Jamaa akashuka, huku akiwa amekasirika, akajaribu kunirukia, ila nikamuwahi kumtuliza kwa ngumi ya shingo iliyo muangusha chini na kuzimia hapo hapo.
 
Msichana akajaribu, kukimbia ila nikamuwahi na kumdaka, nikambeba begani na kumrudisha ndani ya gari. Nikachomoa kisu changu na kumuwekea kooni mwake huku kidole changu kimoja kikimpa ishara ya kukaa kimya la sivyo nitamkata kichwa. Nikaufunga mlango wake, ña kuzunguka upande wa pili, sehemu alipo anguka mpenzi wake. Kwa haraka nikamvua nguo mpenzi wake, na kuzivaa mimi japo hazinitoshi sana ila nikazilazimisha kukaa mwilini mwangu.
 
Nikachukua soksi za jamaa, na kumkandamiza nazo mdomoni, kisha nikamnyanua na kufungua, uoande wa pili wa gari. Kwa bahati nzuri nikakuta kamba, kwa haraka nikamfunga miguuni na mikononi. Kisha nikamuwena vizuri nyuma ya gari, hii yenye viandishi vidogo vilivyo andikwa Verosa, kisha nikafunga, nikarudi alipo mpenzi wake.
Nikamkuta akihangaika na simu yake, akijaribu kupiga namba anazo zijua yeye, kwa bahati mbaya, maeneo tuliyopo hakuna mawasiliano. 
 
Nikampokonya simu yake na kuiweka mfukoni mwangu
"Ukijaribu kufanya ujinga wowote, nitakuu"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali nikitumia lugha ya kingereza, jambo lililo mfanya binti huyo kushangaa, kwani nahisi alijua kwamba mimi ni mtu misiye jua lugha yoyote zaidi ya lugha ya jamii niliyo tokea
Nikawasha gari na kuondoka, huku mara kwa mara niki muamrisha binti huyu kunielekeza barabara ya kufika kwenye mji wowote. Mwendo wa karibia masaa tisa, tukafika kwenye moja ya mji wenye nyumba, nyingi sana zilizo tengenezwa kwa mbao
"Hapa ni wapi?"
"Soweto"
 
Casey alinijibu kwa kifupi huku, akiwa amenuna, kwani hajafurahishwa na uwepo wangu mimi, ndani ya gari hili. Nikasimamisha gari nje ya baa moja, iliyo tulia sana,
"Mbona umesimamisha gari?"
"Nahisi njaa, nahitaji kula, nipatie pesa"
Casey akanitazama kwa woga, taratibu akaingiza mkono wake kwenye, mfuko wa suruali aliyo ivaa, akatoa noti moja ya dola mia na kunikabidhi, nikafungua mlango, kabla sijashuka, nikamgeukia Casey.
"Shuka ndani ya gari, tuongozane"
Casey hakuwa na kipingamizi zaidi yakushuka kwenye gari, tukaingia ndani ya baa hii kwa bahati nzuri tukakuta, sehemu wanauza chakula
 
"Wewe unaitwa nani?"
Casey aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendelea kukisubiria chakula tulicho kiagiza
"Eddy"
"Una jina kama la mchumba wangu"
"Yupi, huyo niliye mfungia kwenye buti ya gari?"
"Hapana, huyo ni kaka yangu, mpenzi wangu yupo hospitali"
"Anaumwa na nini?"
"Alishambuliwa na majambazi, wiki moja iliyo pita"
"Ohoo pole saña, ila hali yake inaendeleaje?"
"Sio nzuri, kwani yupo chini ya uangalizi wa madaktari, kwani alipigwa risasi nne za kifua, alipokua anapeleka pesa benki"
 
Casey alizungumza kwa sauti yaunyonge huku kwambali nachozi yakimlenga lenga, tukachukua chakula tulicho kiagiza na vinywaji, tukarudi kwenye gari
"Eddy nakuomba kitu kimoja"
"Kitu gani?"
"Ninakuomba umfuñgulie kaka yangu, nahisi atakuwa anajihisi njaa"
Casey aliniomba kwa utaratibu, nikamtazama kwa umakini, machoni mwake
 
 Nikamkabidhi mfuko wa chakula nilicho kishika, nikazunguka nyuma ya gari, nikajifikiria kwa muda kisha nikakishika vizuri kitasa cha kufungulia buti ya gari.
Kabla sijafungua, gari ya polisi, ikasimama nyuma yangu, jambo lililo nifanya nisitishe zoezi, nikaanza kuondoka, nyuma ya gari
"Hei kijana"
Sauti ya askari mmoja ikaniita, nikageuka kwa kujiamini, na kuwatazama askari wawili walio simama mbele ya gari lao, dogo linalo endana na gari ninalo liendesha.
"Njoo"
 
Nikapiga hatua kurudi walipo, askari hawa walio zichomeka bastola zao viunoni mwao
"Fungua, buti ya gari. Tunahitaji kukagua gari yako"
Alizungumza askari mmoja huku akinifwata sehemu bilipo simama, nikaanza kuchanganyikiwa baada ya Casey kushuka ndani ya gari na kuja tulipo
"Ofisaa"
Casey alimuita askari mmoja, aliye simama akitutiza, Casey akanitazama kwa macho makali, jambo lililo wafanya askari hao kuipeleka mikono yao kwenye bastola zao walizo zichomeka viunoni.
   SORRY MADAM 76
  Nikataka kurudi nyuma, ila nikajikuta miguu ikipata uzito wakutekeleza azma yangu ya kurudi nyuma. Askari wakazichomoa bastola zao, kwa haraka wakatusukuma mimi na Casey, tukaanguka chini.
"Laleni chini"
Askari mmoja alizungumza kwa sauti ya juu huku akianza kutambaa, wakielekea ilipo baa, tuliyo toka muda mchache. Milio ya risasi ikaanza kurindima, ndani ya baa, nikatazama vizuri, nikashuhudia kundi la majambazi walio valia makofia meusi vichwani mwao, yaliyo bakisha sehemu za macho yao, wakiwamrishà watu waliomo ndani ya baa hiyo kutoa walivyo navyo.
 
Ikawa kama mkanda wa kuigiza, kwani majambazi hao walianza kuwashambulia askari hao walio kua wakitambaa, mmoja wao, akapigwa risasi ya kichwa na mmoja wa majambazi, na ukawa ndio mwisho wa askari huyo, aliyetoka kuzungumza na Casey muda mchache ulio pita.
Nikamtazama Casey, na kumuona akijaribu kunyanyua kichwa chake kuchungulia upande walipo majambazi hao, na akaanza kupiga mayowe yaliyo wafanya majambazi kutazama eneo lilipo gari, letu.
"Weka kichwa chako chini, Casey"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali, huku nikibingiria kwa haraka, na kumuwahi Casey aliyekuwa ameshikwa na butwaa, akimshuhudia askari aliye zungumza naye, jinsi ubongo wake ulio changanyikana na damu, ulivyo sambaa chini.
 
"Heiii, nisikilize wewe"
Nilizungumza huku nikimpiga piga Casey mashamvuni, ili arudi katika hali yake ya kawaida.
"Eheeee!"
Alizungumza huku akiwa amenitumbulia mimacho, asijue nini azungumze. Gari yetu ikaanza kushambuliwa kwa risasi na majambazi hao, huku sisi tukiwa upande wa pili wa gari hili. Nikatazama upande lilipo gari la polisi, nikachungulia kupitia durisha la gari, tulilopo nikao majambazi wawili wakilisogelea gari letu huku wakiendea kuzimimina risasi kwenye upande wa pili wa gari letu.
 
"Hei Casey, unaweza kutambaa?"
"Heee"
"Unaweza kutambaa?"
Casey akanijibu kwa kutingisha kichwa kwamba anaweza.
"Nakuomba, utambae uende lilipo gari lapolisi"
"Eddy una akili kweli wewe, unataka na mimi nife kama hao polisi?"
Casey alizungumza kwa sauti ya kuto kujiamini huku akinitazama usoni, huku jasho likimtiririka.
"Fanya kama nilivyo zungumza"
Nilizungumza, huku nikiwachunguli majambazi hao, wanao zidi kulisogelea gari letu lilipo.
 
Casey hakuwa na uchaguzi mwengine zaidi yakufanya nilivyo muambia kufanya. Kwa haraka akatambaa hadi lilipo gari la polisi na kujibanza huku akihema sana, macho yake yote yakawa kwangu. Ukimya ukatawala gafla, kwani majambazi waliacha kupiga risasi, nikachungulia nikawakuta wakinong'onezana, mmoja akaanza kunyata taratibu, akilisogelea gari nililopo, huku bunduki yake akiwa ameiishika vizuri mkononi mwake.
 
Nikakichomoa kisu changu, na kukishika kwa mkono wangu wa kulia. Taratibu nikanza kuhesabu moja mpaka tatu, kitendo cha jambazi huyo kuufungua mlango wa gari, upande wa dereva, ikawa ninafasi yangu kufanya shambulizi la kukirusha kisu changu kwa nguvu zangu zote, kisu changu
 
kikatua shingoni mwa jambazi aliye simama, hatua chache toka gàri lilipo, akatoa ukelele ulio mduwaza mwezake, aliye karibu yangu. Kwa haraka nikapanda juu ya gari, nikajizungusha kwa kasi, kwakuitumia miguu yangu, na kumpiga kichwani jambazi, akaanguka chini. Nikawahi kuochomoa bastola iliyo kiunoni mwake, na kumpiga risasi kadhaa za tumbo.
 
  Nikakimbia kwa haraka, hadi kwenye moja ya gari, lililopo kwenye maegesho ya hapa baa, nikajibanza kutazama ni kitu gani kinacho endelea ndani ya baa. Jambazi mmoja akajitokeza mlangoni kuwachungulia wezake, alipo waona wamelala chini, akarudi ndani kwa haraka, sekunde kadhaa wakatoka majambazi wanne, wakaanza kufyatua risasi zao ovyo, pasipo kujua muhusika mkuu wa mauaji ya wezao wawili yupo wapi.
 
Sikuhitaji kufanya makosa, ambayo yangenigharimu maisha yangu. Kwa haraka nikanza kufyatua risasi zilizo wapeleka chini, majambazi wote wanne, Nikatoa magazini ya bastola, nikskuta imebakiwa na risasi nne tu.
"Shitii"
Nilizungumza huku nikiirudisha kwa harana Magazine hiyo ndani ya bastola, nikanyanyuka kwa umakini, nikaanza kukimbilia katika mlango wa kuingilia baa.
Nikachungulia na kuwakuta watu wote wakiwa wapo chini ya ulinzi mlali wa majambazi sita waliomo ndani ya baa hii, iliyo kusanya wateja wengi.
 
Jambazi mmoja, akajisumu kutoka nje, nikamrukia kwa nyuma na kumkaba kabali, huku nikimvuta pembeni kabisa ya mlango. Taratibu jambazi huyu akaanza kuiaga dunia, kwa nguvu zangu zote nikaivunja shingo yake.
"Nisalimie huko uendapo"
Nikamlaza chini, taratibu nikachukua bunduki yake àina ya 'Short Gun', Nikamvua jaketi lakuzuia risasi alilo livaa, nikaanza kushangaa baada ya kuguñdua jambazi huyu ni mwanamke.
  Nikalivua kofia lililopo kichwani mwake, sikuamini macho yangu, kwani ni binti mdogo sasa, jinsi anavyo onekàña usoni mwake. 
 
"Umekosa nini, binti mzuri kama wewe?"
Nilizungumza huku nikilivaa jaketi la kuzuia risasi. Kazi ikawa ni moja tu, kuhakikisha ninawamaliza mambazi wote. Haikuwa ngumu kwangu, kwani ndani ya dakika kadhaa nikafanikiwa kuwaua majambazi wote ndani ya baa hii. Mtu mmoja akaanza kupiga makofi, mwenzake wa pembeni naye akafanya hivyo, watu wote waliomo ndani ya baa wakaaendelea kunipigia makofi kwa kazi nzuri niliyo ifanya.
"Asanteni"
Nilizungumza, kwa kizulu jambo lililo zidi kuwafurahisha, walio na simu zao wakawa na kazi ya kunipiga picha, huku wengine wakichukua video. Casey akanifwata na kunikumbatia, huku akitokwa na machozi
"Vipi?"
 
Nilimuuluza kwa wasiwasi, huku kitu cha kwanza kukifikiria kichwani mwake ni kaka take, niliye muacha ndani ya buti ya gari lililo shambuliwa vibaya kwa risasi.
"Umeyaokoa maisha yangu"
Casey alizungumza huku akiendelea kulia
"Casey tuondoke"
Sauti ya kaka yake ilisikika, na kutufanya sote tutizame mlangoni na kumkuta àkiwa amesima, huku akiwa na nguo ya ndani tu. Akajistukia mwenyewe baada ya watu wote, kumshangaa.
"Naweza kupiga simu?"
Casey alimuuliza mmoja wa wahudumu aliye valia sare kama wahudumu wengine
"Ndio"
 
Casey akaonyeshwa simu iliyo kwenye moja ya ukuta ndani ya hii baa, akaniachia na kwenda kupiga simu, baada ya kumaliza akarudi nilipo simama
"Nimempigia simu baba, atafika muda si mrefu"
Ving'ora vya gari za polisi vikafika katika eneo la tukio
"Kumbe hawa nao hawana tofauti na wabongo"
Nilijisemea kimoyo moyo, huku nikiwatazama askari hawa wakiingia kwa mbwembwe ndabi ya baa hii huku, wakiwa na bunduki mikoni mwao
"Weka silaha yako chini"
Askari mmoja aliniamrisha huku, wakinielekezea bunduki zao.
 
Nikashangaa wazee wawili wakisimama mbele yangu huku, mikononi mwao wakiwa wameshika chupa za bia.
"Nyinyi muda wote mulikua wapi? Huyu kijana yeye ndio aliye waua majambazi wotw hawa, bila aibu munakuja sasa hivi"
"Kwanza hamshangai, jinsu tulivyo mzingira huyu kijana, munadhani ni jambazi?"
Wazee hawa walipokezana kuwatandika maswali askari hawa, walio baki wakibabaika wasijue nini chakuwajibu wananchi hawa waliopo ndani ya hii baa. Askari wakaachana na mimi, wakaanza kushuhulika na miili ya majambazi hao. Kundi kubwa la waandishi wa habari walio kuja baada ya askari kufika, wakaanza kunihoji naswali ambayo sikuyajibu hata moja.
 
"Eddy baba yangu amekuja"
Casey alizungumza huku, akinishika mkono na kutoka ndani ya baa. Nijakuta gari nne , nyeusi zinazo fanana, aina ya GVC, zika zimejipanga pembeni, huku zikiwa na vijibendera vidogo vya marekani. Walimzi wapatao kumi, walio valia suti nyeusi, pamoja na miwani nyeusi, wakashuka kwenye magari hayo. Kaka yake Casey akaongoza zilipo gari hizo, huku mkononi mwake akiwa ameshika kamera ya Casey, akashuka mzee mmoja mwenye mvi kichwani mwake.
 
"Eddy yule ni baba yangu"
Casey alizungumza huku akiendelea kunishika mkono nielekee zilipo gari hizo.
"Ngoja kwanza, siwezi kwenda kwa baba yako nikiwa kwenye halii hii"
"Wewe twende baba yangu hana tatizo"
Casey alizungumza huku akiendelea kunivuta, tukafika zilipo gari zao, akakumbatiana na baba take.
"Baba, huyu ni shujaa aliye yaokoa maisha yangu. Anaitwa Eddy"
 
"Eddy huyu ni baba yangu, ni balozi wa Marekani, hapa Afrika kusini"
Nikampa mkono, baba Casey naye akaupokea wa kwangu huku akiachia tabasamu pana.
"Asantw kijana kwa kazi nzuri uliyo ifanya"
"Asante mzee"
Casey akamuomba baba yake niweze kujumuika nao kwenda wanapo ishi, ikawalazimu walunzi kunikagua, mwili wangu kamakuna kitu kinaweza kuwadhuru. Wakachukua bastola yangu, wakaniruhusu kuingia ndani ya gari.
 
  Sikupanda gari moja na Casey na baba yàke, gari nililo panda likari wawili walio kaa siti ya mbele mmoja akiwa ni dereva. Kwangu ikawa kama bahati kukutana na balozi huyu wa Marekani. 

Japo mama yangu ni waziri wa nchini Tanzania, ila sikuweza kubahatika kukutana ni viongozi wa nchi kubwa kama Marekani. Katika siti niliyo kaa, nyuma ya siti ya dereva kuna Tv ndogo inayo onyesha, vipindi mbalimbali. Matangazo ya kituo cha television kinacgo itwa ENEWS, kikaanza kuonyesha tukio la majambazi walio kufa, huku ikisadikika kundi hilo la majambazi lilikuwa likitafutwa na jeshi la polisi la Afrika kusini, zaidi ya miaka mitano sasa, pasipo mafanikio.
 
'NI MTU MMOJA TU, AMEWEZA KULISAMBARATISHA KUNDI HILO HARAMU'
Nimaneno ya mtangazaji wa taarifa hiyo, huku picha za video zikinionyesha, walivyo kua wakinihoji.
"Wewe ni askari?"
Mlinzi mmoja aliniuliza, pasipo kugeuka nyuma kunitazama
"Hapana"
"Umewezaje kutumia silaha?"
"Nilifundishwa na baba yangu, yeye alikua ni mwanajeshi"
"Yupo wapi?"
"Amesha kufa"
 
Nilidanganya, huku nikiangalia saa ndogo iliyopo pembezoni mwa dereva, ikionyesha ni saa sita usiku. Nikageza shingo yangu kutazama pembezoni mwa barabara, ambapo kuna bonde kubwa na endapo dereva akikosea basi tukianguka, huko bondeni tutakua tutasagika sagika bibaya,na isitoshe gari zote zipo kwenye mwendo kasi sawa kwa uzoefu wangu, spidi wanayo tembelea ni zaidi ya spidi mita mia moja. 

Matone matone ya mvua yakaanza kutotesha vioo vya gari letu tulilo panda, ambalo ni lapili kutokà mbele, kati ya msafata wa magari manne yaliyo ongozana. Kitu ninacho wasifu madereva hawa, ni utaalamu wao kukunja kona, bila kupunguza mwendo wa magari yao, zilizopo kwenye hii bararaba iliyo chogwa kitaalamu, pembezoni mwa mlima ninao weza kuufanan uliopo mkoani Iriñga ni Tanzania.
 
Nikiendelea kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la mbele yetu, nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka hewani mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu kufunga breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari lililo anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi ya mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma yakijitahidi kubaki barabarani.

  ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts