Get the latest updates from us for free

Home » » Godbless Lema Afikishwa Mahakamani.......Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana

Godbless Lema Afikishwa Mahakamani.......Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana

Written By Bigie on Wednesday, November 9, 2016 | 8:28:00 AM

Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema jana alifikishwa mahakamani mkoani Arusha na kusomewa shtaka la uchochezi kwa viongozi wa serikali.

Lema amefikishwa jana mahakamani akiwa tayari amekaa rumande takribani siku 7 tangu alipokamatwa.

Lema anakabiliwa na shtaka la uchochezi ambapo ni pamoja na kumtishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kauli yake aliyoitoa dhidi ya Rais Dkt Magufuli kuwa Mungu amemuonyesha asipojirekebisha atafariki.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Lema amerejeshwa rumande baada ya kukosa dhamana kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama imeeleza kuwa itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya Lema Novemba 11 mwaka huu.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts