Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 87 & 88(Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 87 & 88(Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Bigie on Sunday, November 13, 2016 | 8:15:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"Hiyo ni picha ya ukurasa wa mbele katika gazeti hili la Jambo leo, ikibebwa na kichwa chà habari kisemacho, MTOTO WA WAZIRI MKUU NA MKEWE WATEKWA NA WATU WASIO JULIKANA, NA RISASI ZARINDIMA ENEO ZIMA LA KANISA"
Mtangazaji alizungumzà, huku akifunua kurasa ya ndani, akidai kwenda kuisoma taarifa hiyo kwa 
 
ENDELEA
Manka akazima tv, na kuiweka rimoti mezani, akionekana kupatwa na mawazo ya gafla.
"Mbona umezima"
Nilimuuliza kwa sauti ya upole sana
"Eddy, hichi ni nini ulicho kifanya kwa Fredy wangu?"
"Nisikili......"
 
"Eddy hapa hakuna cha kusikiliza, umemsababishia mwenzako matatizo makubwa sana"
"Ndio nalitambua hilo, ila natambua kwamba hajauliwa, lazima atakua hai"
"Una uhakika gani, hata kama Fredy hajiwezi kitandani, lakini nimempenda hivyo hivyo."
Manka alizungumza huku akiwa amekasirika sana, machozi yakaanza kulowanisha uso wake. 
 
"Oya mboma mimi siwaelewi?"
Amina alituuliza baada ya tukio lililo tokea, kushindwa kulielewa. Nilamuelezea kwa ufupi, akanielewa vizuri
"Sasa wewe, Manka huo ni unafki sasa. Tangu lini ukamlilia mwanaume?"
"Amina hujui tu maumivu, niliyo kua nayo nampenda Fredy tena sana"
"Hembu sikia, ishu hapa ipo hivi. Tunakwenda kwa hao mafala walio teka mke wa bro, tukimaliza tunakwenda kwa hao mafala wengine walio teka Fredy"
Amina alizungumza huku akiwasha sigara yake kwa kiberiti cha kutumia gesi.
"Yaani hapa nguvu zote zimeniishia"
"Zimekuishia kisa mwanaume. Mbona umekua fala sana mtu wangu?"
 
"Manka niliye kua namjua mimi ni yule wakazi, sasa Manka wewe wa kulia lia kisa mwanaume sijui umetokea dunia gani. Hembu nyanyuka tukafanye kazi"
"Siendi popote"
”Nini wewe, sasa maana ya kuja hapa ni nini?"
"Siendi"
Mgomo wa Manka ukaañza kunipa wasiwasi mkubwa, dalili mbaya ya mpango nilio upanga mbele yangu nikaanza kuuona ukianza kuharibika.
"Manka nini unafanya, nini uliniahidi kulifanya juu ya familia yangu?"
"Sawa Eddy ila elewa siendi popote"
"Sikia Eddy asikuchanganye, mziki wako nauelewa vizuri. Twende tukapige job"
 
Manka akanyanyuka na kuingia ndani, kwa Amina. Amina akamfwata kwa nyuma kwenda kuzungumza naye. Nikawasha Tv, ila nikaikuta tarifa hiyo ikiwa imekwisha, nikajaribu kuitafuta kwenye chanel tofauti, pia sikuipata.
"Oya mtu wako amekataa bwana, tujiandae twende tukapachunguze, kisha usiku twende"
"Poa"
Tukajiandaa, nikavaa miwanani pamoja na kofia, tukaingia kwenye gari la Amina na kuondoka.
"Hilo begi lina nini?"
Nilimuuliza Amina, àliye beba begi la mgongoni, alilo liweka siti ya nyuma.
"Lifungue"
Nikalichukua, nikalifungua. Nikakuta kamera moja aina ya Canoon, bastola tatu, magazine kumi na mbili, na mabomu manne yakurusha kwa mkono.
 
"Mmmmmm"
"Mbona umeguna?"
"Kazi leo ipo"
"Ahaaa ulizani nimchezo, hii ni Somalia bwana, kuingia nirahisi ila kutoka ni ngumu"
Amima alizumgumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake. Chakumshukuru Mungu, htukukutana na polisi barabarani. Mwendo wa dakika arobaini na tano, tukafika kwenye majengo ya magorofa machakavu, yaliyopo nje kidogo ya mji wa Mogadishu. Amina ajasimamisha gari pembeni na kuitoa simu yake, akaniomba namba ya simu ya jamaa aliye nipigia, akaipiga, baada ya muda ikapokelewa, akaanza kuzungumza na jamaa kisomali, ambacho sikielewi kabisa.
"Amesemaje?"
Nilimuuliza Aminà baada ya kumaliza kuzungumza na jamaa huyo.

"Anasema yupo hapa"
"Ulimuambia kwamba wewe ni nani?"
"Hapana nimemuambia nahitaji kufanya nao biashara ya mafuta"
"Kwahiyo watakuja hapa tulipo?"
"Hapana nilitaka kufahamu kwamba wapo hapa"
Tukakaa ndani ya gari zaidi ya nusu saa, sikuwa ninaelewa nini maana ya Amina.
"Tunasubiri nni hapa?"
"Usiwe na hataka utaona"
 
Tukaendelea kusubiri zaidi ya masaa mawili, magari makubwa aina ya Scania yakatoka yakiwa na matela nyuma. Yakaingia barabara ya lami, na kuondoka kwa mwendo wa taratibu. Amina akawasha gari, taratibu tukaanxa kuyafwata.
"Tunaelekea wapi?"
"Tunayafwatilia hayo magari moja wapo ndipo alipo mke wako?"
"Umejuaje?"
"Hawa jamaa huwa wanafanya biashara ya kuuza wañawake wanao wateka katika nchi za ulaya, ambapo huku wanakwenda kuuzwa kwenye makasino na mabaa makubwa kwa ajili ya ngono"
"Sasa hapa wanawapeleka wapi?"
"Hii moja kwa moja wanakwenda baharinia àmbàpo wanawasafirisha kutumia meli"
 
"Mmmmmmmm"
"Usigune hii ndio dunia bwana"
Amina alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari"
Nikaanza kuzitoa bastola moja moja, na kuanza kuzikagua kama zina ubora kwa maana nimatambua chochote kitatolea muda wowote tuliwa kwenye hio safari ambayo hadi sada hivi sitambui kama kuma udhibitisho wowote wa Phidaya kuwa ñdani ya magari haya yenye makontena makubwa.
Kadri tulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mahari hayo yalivyo zidi kuyoyoma, Amina hakukata tamaa, kila magari yalipo kunja naye akakunja pasipo kuhofia kama wahusika wameugundua, uwepo wetu wa kuwafwatilia kwa nyuma.
"Usiyafwate kwa ukaribu zaidi watatustulia"
 
"Usiogope"
"Kivipi"
"Hakuna kitakacho jitokeza"
"Mmmm"
Kitu ninaçho kiamini maishani mwangu, ni kuto kumuamini mtu yoyote, mbaya zaidi wale nilio waamini wote walinifamyia unyama wa hali ya juu, nikajikuta nilihangaika na kuteseka vibaya mno. Akili yangu ikaanza kumfikiria Amina, sikuhitaji kumpa uaminifu wa aina yoyote. Magari tuliyo yafwata, tukayashuhudia yakikunja kushoto mwa barabara na kuiacha barabata ya la lami na kuingia barabara ya vumbi. Amina akasimamisha gari
"Mbona umesimamisha gari?"
"Huku walipo ingia ni hatari sana"
"Kwahiyo itakuaje?"
"Itatulazimu kwenda kwa miguu, kutokana sio mbali saña na hapa"
 
Tukashuka kwenye gari, tukachukua silaha zetu, kila mmoja akachukua silaha yake, tukaanza kuchanja mbuga kwa kutumia miguu. Kigiza kwa mbali kilisha anza kujitokeza, huku saa yangu ya mkononi ikinionyesha ni saa kumi na mbilo na robo. Tukatembea zaidi ya dakika kumi. Tukafika kwenye moja ya fensi , iliyo zunguka majengo machakavu, ambayo yapo pembezoni mwa bahari. Tukapenya kwenye fensi hii, iloyo na uwazi mkubwa kidogo.
 
Kwa mwendo wa haràka, wenye umakini, tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyumba. Tukashuhudia jinsi watoto wengi wa kike wakishushwa kwenye magari hayo. Amina akachukua kamera yake, na kuanza kurekodi matukio yote yanayo endelea, huku akizivuta karibu sura za wasichana hao, weñgine walipaswa kuwa mashuleni, ila ndio hivyo wametekwa.
 
Nikamuona Phidaya akisukumwa, kitoka kwenye gari alilo kuwepo, kuanguka kwake chini, kukanifanya nitake kujitoa muhanga, ila Amiña akaniwahi
"Umataka kufanya nini?"
"Mke wangu yule"
"Kwahiyo? Hembu tumia akili, wewe huoni walivyo wengi. Unadhani utapona?"
Amina alizumgumza huku akiwa amenikandamiza ukutani kwa nguvu zake zote.
Nikamshuhudia askari mmoja akimpiga Phidaya mgongoni kwa kutumia kitako cha bunduki mgongoni, baada ya Phidaya kukataa kunyanyuka, chini.
 
"Amina tunasubiria nini?"
"Ngoja kua mvumilivu"
Amima akiwa anaendela kurekodi, nikalichunguza eneo zima, nilawaonà askari wote katika maeneo walio kaa. Nikachukua kiwambo cha kuzuia sauti na kukifumga kwenye bastola yangu. Nilipo hakilisha kila kitu kipo sawa, sikuhitaji kusubiri, nikaanza kufyatua risasi kwa askari mmoja baada ya mwengine, nilianza kuwamaliza pasipo wao kujijua wanakwisha, kutoka na bastola yangu kuto kutoa mlio wa aina yoyote. Ñikaanza kusonga mbele pasipo kuhofia kitu cha anai yoyote, huku nikowa nahasira kali dhidi ya askari walio mtesa mke wangu
 
   Askari hao wakastuka, baada ya Amina kumlenga mmoja, kwa bahati mbaya akamkosa na risasi ikapiga katika tairi la gari moja na kulifanya litoe mlio. Yakaanza majibizani ya rusasi kati yetu na watekaji hawa, haikuwa kazi rahisi kwani, wengine waliongezeka wakitokea kwenye meli waliyo kua wakiisubiria kuja kuwabena Phidaya na wezake.
 
"Nimezaliwa siku moja, nitakufa siku moja"
Nilizungumza baada ya kuona mashambulizi yakianza kutuelemea upande wetu, isitoshe risasi zilitupungukia. Ikatulazimu kuokota baadhi ya bunduki za askari walio fariki, Kusema kweli, Amina anajua kujituma, jinsi anavyo piga risasi unaweza kuhisi ni mwanaume, kumbe ni mwanamke. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi tulivyo zidi kuanza kuwamiliki maadui zetu, wengi tuliweza kuwaua, hadi tukafanikiaa kufika katika eneo wipo lala chini Phidaya na wenzake. Maadui zetu wakaanza kukimbia ovyo, baada ya mashambulizi kuwa makali sana. Ikawa ninafasi kwetu kuhakikisha wanaondoka kabisa, wengine wakaingia kwenye meli yao.
 
"Unakwenda wapi?"
Amina aliniuliza baada ya kuniona nikikimbili kwenye meli hiyo, ambayo hadi kuwashwa kwake na kuondoka ni shuhuli kubwa sana.
"Walinde hawa"
Nikadi kukimbia, huku mkononi mwangu nikiwa nimebeba bumduki aina ya AK 47, walizo kua wakitumia hawa maadui. Nikafanikiwa kuingia ndani ya meli, Kazi yangu ikawa  ni moja tu, kuhakikisha haondoki adui hata mmoja katika eneo hili. Nikafanikiwa kuwateketeza karibia wote.Taratibu nikaanza kunyata kuelekeà chumba cha manahoza, kitendo cha kufungu mlango, nikastukia nikirudishwa nyuma kwa kupigwa teke la uso. Kwa bahati mbaya nikajikuta nikiiachia bunduki na ikaangukia mbali nami.
 
Nikanyanyuka na kukutana na jitu refu kwenda juu. Nikamtazama vizuri jinsi alivyo jazia misuli yake, kwa haraka haraka nikamfananisha na mwana mereka mmoja nchini Mareni, anayevitwa 'BIG SHOW'. Likanza kurusha makonde ambayo nilianza kuyakwepa, kutokana na urefu wake, ninamfikia kiunoni, kwa kimo changu. Katika kukwepa kwangu, akanibahatisha kunitandika teke moja, la miguu. Nikajikuta nikianguka kifudi fudi. Akaninyanyua na kuñirusha kwenye mapipa yaliyopo karibu nasi, nakunisababishia maumivu karibi mwili mzima.
 
Likanifwata na kujaribu kuniinua, ila nikalikwepa. Kwa haraka nikanyanyuka, nikaanza kumpiga mateke ya miguu. Likanza kuyumba. Nikazidisha juhudi ya kulipiga miguuni hadi likaànnguka chini. Ñikaiokota bunduki yangu, nikataka kufyatua risasi ila hapakuwa na risasi iliyo toka.
 
Likaanza kucheka kwa dharau. Huku taratibu likinyanyukà. Nikaitoa magazine na kuikuta haina risasi hata moja. Nikaanza kurudi nyuma kwenda kilipo chumba cha manahoza. Nikaingia ndani, nalo likazidi kumifwata. Ndani ya chumba hichi nikakuta, masanduku mawili yaliyo wazi, huki yana pesa nyingi dola za kimarekani. Ninaamini mtu huyu ndio alikua mnunuzi wa wasichana hawa. Likaanza kunirushia mskonde mazito. Sikutaka kurudi nyuma zaidi ya kukabiliana nalo, kufa na kupona. 

Baadhi ya ngumi zake zikawa zinanipata kisawa sawa mwilini mwangu. Sikulaza damu, na mimi nikazidi kujituma kupigana, huku ngumi zangu nikijitahidi kupiga kwenye sehemu za viungio vya mwili wake. Taratibu likaanza kulainika, hata ngumu kurusa likaanza kushindwa kwani, nilimpiga sana kwenye viungio vya mabega, tena kwa kujaribu kupanda kwenye baadhi ya meza, ili kumfikia kwenye mabega yake.
 
Nikafanikiwa kuona sime mbili zikiwa zimechomekwa kwenye moja ya kabati la vioo. Nikazichukua zote mbili na kusimama, nikilisubiria jitu hili kunyanyuka, baada ya kuanguka chini.
Likafungua moja ya droo, likkatoa bomu la kutega kwa sekunde
 
"We are going to die, kid”(Tunakwenda kufa mtoto)
Lilizungumza huku likiminya minya batani za bomu hilo, kwa haraka nikakimbia, mguh mmoja nikakanyaga kwenye meza, nikajinyanyua juu, sime moja nikàishusha kwenye mkono wake ulio shika bomu na kukatika, bomu likaangukia pembeni, jamaa akaanza kulia kwa maumivu makali huku damu ikiwa inàmtoka kwa wingi, mkononi mwake.
Nikaliokota bomu, nikakuta zimebaki dakika mbili, kabla halijalipuka. Nikamkata mkobo wake wa pili, na kumzidishia maumivu. Nikatupa sime pembeni, nikachua masanduku ya pesa na kuyafunga, bomu likawa limebakisha dakila moja na sekunde kumi.
 
"Your going to die grand paaa"(Unakwenda kufa babuu)
Nilizungumza huku nikilichukua bomu na kulidumbukiza kwenye mshati wake. Nikayabeba masanduku haya yenye kilo kilo moja zsidi ya ishirini. Yakanifanya nishindwe kutembea kwa kasi. Nikazidi kujotahidi kukimbia huku nikiwa nimeyabeba. Mlipuko mzito ukaanza kusikika nyuma yangu, ukitokea kwenye chumba cha manahoza. Pembeni nikaona dirisha la kioo, nikalivunja kwa kutumia masanduku haya ya chuma, nikajirusha kwenda chini, kwenye maji huku nikiiacha meli ikizidi kulipuka kwa moto mkali
 
                   ****SORRY MADAM(88)****

ENDELEA
   Kitendo cha mimi kuzama, ndani yà maji ikawa ndio pona pona yangu, kwani moto mkubwa ulizidi, kurindima juu ya maji, Masanduku yenye pesa yakaanza kunishiñda nguvu, ikanilazimu kuyaachini, yakazidi kwenda chinni. Taratibu nikaanza kujilegeza mwili wangu na kuanza kw, hadi nikatolea usawa wa bahari.
   Nikailuta meli ikiendelea kuteketea kwa moto mkali, nikatazama sehemu nilipo waacha Amina na wezake ila sikuzioa gari mbili zilizo kua zimewabeba.
Wasiwasi wangu, ukawa juu ya Phidaya, ikanilazimu kuogelea kuelekea ukingoni mwa bahari. Kitendo cha kufika ukingoni mwa bahari, kundi la watu si chini ya saba, wamesimama mbele yangu huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Nikajikuta nikiishiwa ujanja nisijue nini nifanye
 
"Toka nje ya maji"
Jamaa aliye valia kilemba kichwani mwake aliniamrisha niweze kufamya alicho agiza. Nikawatazama vizuri, nikagundua hawa ni miongoni mwa wale wali mteka mke wangu Phidaya. Nikatoka huku mwili wangu wote ukiwa umelowa kwa maji.
"Piga magoti kabla hatujakumwaga ubongo"
Nikapiga magoti taratibu, sikuwa na ubishi kwani tayari nipo chini ya ulinzi wao. Wakaanza kunong'onezana, walizungumza kisomali. Macho yangu yakatazama kila pande ila sikuona magari yote mawili. 
 
"Umeharibu biashara yetu mshenzi wee"
Jamaa alizungumza, huku akinipiga teke la kifua lililo niangusha chini. Sauti ya simu ya upepo ya mmoja wao ikasikika ikizungumza
"Mkuu wasichana wametukimbia tayari wamefika kwenye mikono ya wanejeshi wa UN. Over"
Nikuona mkuu wao akianza kuzunguka zunguka mithili ya mwenda wazimu aliye changanyikiwa. Akaanza kujipiga piga kichwani kwa mkono hadi kilemba kikaanguka chini, akanigeukia, huku akiwa amenikodolea mimacho mikali iliyo jaa hasira kama chui.
 
Akaanza kunisogelea sehemu, niliyo piga magoti chini, huku mkono wake mmoja ukichomoa bastola aliyo ichomeka kwenye mkanda wa suruali yake. Nikamtazama kila hatua anayo ipiga kumifwata nilipo, hatua moja kabla hajanifikia. Nikauvuta mguu wake kwa nguvu, akaanguka chini, kwa kasi ya akabu nikamuwahi, kumpiga kabali, iliyo wafanya watu wake kuzikoki bunduki zao wakiwa tayari kwa kufyatua risasi
"Waambie watu wako waweke silaha chini, lasivyo nakuvunja koromeo lako"
Nilizungumza huku, nikizidi kuliminya koo la jamaa huyu, mwenye mwili mwembamba kiasi ila ulio komaa. Watu wake wakashusha silaha zao chini, hapakuwa na sehemu nyimgine ya kukimbilia zaidi ya kurudi nyuma, kuelekea kwenye maji. 
 
"Musitufwate"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali, iliyo wafaya watu wake kusimama wakinikodolea mimacho. Nikafika ukingoni kabisa wa bahari. Nikawatazama jinsi walivyo duwaa, pasipo kusubiri kitu chochote, nikaizungusha shingo ya mkubwa wao, na kuivunja kabisa, nami nikajirusha kwenye maji. Nikawacha wakimkimbilia bosi wao, niliye muacha akiwa eanguka katika sehemu tuliyo simama.
 
Mwanga wa moto, wa meli inayo endelea kuteketea, ukanisaidia kuona vitu vilivyomo ndani ya maji. Nikayaona masanduku ya pesa. Nikaanza kuyafwata sehemu yalipo angukia. Kabla sijayafikia, mikawaona jamaa wakijirusha ndani ya maji mmoja baada ya mwengine, lengo lao kubwa ni kunifwata mimi sehemu nilipo. Ikanilazimu kubadili muelekeo na kuachana na masanduku ya pesa.
 
Kasi yao ya kunifwata ikazidi kuongezeka. Nikapanda juu kwa kasi ili kupata pumzi itakayo nisaidia kupambana na jama hawa
  Nilastukia mmoja wao akinivuta ndani ya maji huku akiwa amenishika miguu. Nikaanza kupambana nao, huku wezangu wakiwa na visu vikali. Japo katika maisha yangu nimekutana na mambo mengi sana kuhusiana na kupambana na maadui, ila hawa wasomali ni mziki mwingine. Sikutaka kukubaliana na kushindwa japo, visu vyao mara kadhaa vimejikata kata maeneo ya mikononi, kila nilipo kua nikijaribu kuvizuia visinifikie mwilini mwangu.
 
Nikafanikiwa kupata kisu cha jaa, mmoja niliye mtoboa macho, kwa vidole vyangu, ikamlazimu kukiachia kisu hicho. Nikazidi kupambana nao pasipo kukata tamaa, Nikazidi kuwapunguza hadi nikawamaliza kabisa. Nikaogelea taratibu hadi eneo nilipo zama mara ya kwanza na masanduku ya pesa. 

Nikavuta pumzi yakutosha kisha nikazama tena ndani ya maji. Nikayachukua yote, hivyo hivyo nikajikaza kupanda tena juu, na nikafanikiwa kutokeza juu kabisa. Nikatoka nayo hadi nchi kavu, nikatazama usalama wa kila eneo, nilajiridhisha hakuna mtu atakaye nidhuru. Taratibu nikaanza kujikongoja, huku mwanga wa mbala mwezi ukinisaidia kuona niendapo. Japo mwendo wangu ni wakuchoka sana, ila nikajika kutembea hivyo hivyo.
 
"Baba mwema ni yule anaye ipigania familiavyake"
Nilijifariji hulku nikisonga mbele, nikafanikiwa kufika sehemu tulipo liacha gari la Amina. Kwa bahata nzuri nikalikuta. Nikayaingiza masanduku yote ndani ya gari. Sikuikuta funguo ya gari, ikanilazimu kukata nyaya mbili za hasi na chanya, zilizopo pembeni ya mskani. Nikazikutanisha kwa pamoja gari ikawaka.
"Hahaaahaaaaa"
Nilianza kucheka mimi mwemyewe baada ya gari kuwaka, nikaligeuza kwa haraka na kurudi katika sehemu tulipo toka na Amina
Gari ikaanza kutoa mlio wa kuishiwa na mafuta, kwa kumbulumbu zangu, kuna sehemu niliona sheli, na sehemu niliyopo hadi sheli ilipo si mbali sana. Nikafanikiwa kufika ilipo sheli, saa ya kwenye gari inaonyesha ni saa kumi na mbilo asubuhi. Nikafungua sanduku moja nilachomoa noti kadhaa za dola mia, japo zimetota kwa maji, ila hazijaharibika.
 
Nikazungumza na muhudumu, akanijazia tanki la gari. Nikampa noti tatu za dola mia, kisha nikaondoka na kumuacha akishangaa kwani nikiasi kikubwa sana cha pesa ukilinganisha na mafuta aliyo niwekea kwenye gari.
Safari ya kurudi, kwa Amina ikaanza, njia nzima nikawa makini kwa kila gari lililo karibu yangu.
Nikafanikiwa kufika nyumbani kwa Amina, nikalisimamisha gari sehemu anapo lisimamisha, nikashuka ndani ya gari, nilitizama kila kona ya yumba, nikaridhika na usalama. Nikashusha masanduku ya pesa ndani ya gari. Nikaingia nayo ndani.
 
Niajikuta nikiyaweka chini, kwa haraka, hii nibaada ya kukuta damu nyingi zikiwa zimetapakaa kwenye sakafu, pamoja na sehemu ya ukutani. Mapigo ya moyo yakaanza kuniendaa mbio. Nikaanza kufwata michuruziko ya damu iliyo elekea chumbani mwa amina kabla sijufikia mlango wa chumbani kwake, kitu kizito kikangia kupitia dirishani. Kikaanza kutoa moshi mkali ulioa anza kunipalia, nikagundua ni bomu la machozi, lililo ambanata nailio ya risasi iliyoanza kusikika ikitokea nje.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts