Home » » Serikali yafunguka kuhusu fao la kujitoa

Serikali yafunguka kuhusu fao la kujitoa

Written By Bigie on Thursday, November 24, 2016 | 7:16:00 AM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi Ajira na Vijana) Bibi Jenista Mhagama amesema serikali itakaa na wadau ili kuangalia namna ya kulimaliza sakata la fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo jana  katika mkutano wa sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) mjini Dodoma uliofunguliwa leo na Waziri Mkuu Mjini Dodoma, ambapo katika risala yake, TUCTA ilihoji kuhusu  marekebisho ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na ucheleweshwaji wa malipo ya pensheni.

Mhagama alisema kuwa baada ya uongozi wa TUCTA kukamilika, itabidi wakutane na kukaa pamoja kuainisha sera inataka nini na hali ya uchumi ya sasa ikoje huku wakiangalia dhana nzima ya hifadhi ya jamii nayo inataka nini.

“Kuna haja ya kuangalia sera inataka nini, tunapaswa tuangalie mabadiliko ya kiuchumi katika nchi yetu na kutazama dhana nzima ya hifadhi ya jamii kwenye maisha yetu ya uzeeni. Tukikaa pamoja, yaani, mwajiri, mfanyakazi na Serikali, tutapata njia ya kisheria ya kuweza kulifunga jambo hili ili lisiendelee kuwa kero kwa wafanyakazi wetu,” alisema.

Msikilize hapa waziri Mhagama akifunguka.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts