Home » » TANZIA: Mbunge Hafidh Ali Tahir Afariki Dunia Alfajiri ya Leo Akiwa Mjini Dodoma

TANZIA: Mbunge Hafidh Ali Tahir Afariki Dunia Alfajiri ya Leo Akiwa Mjini Dodoma

Written By Bigie on Friday, November 11, 2016 | 9:24:00 AM

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, Job Ndugai (Mb) anasikitika kuwatangazia kuwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Hafidh Ali Tahir amefariki dunia leo saa 9 alfajiri katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.

Taarifa zaidi kuhusu msiba huu zitatolewa hapo baadae. Spika anaungana na Wabunge wote katika kuomboleza msiba huu.

Awali Marehemu pia alikuwa mwalimu wa soka kwenye timu ya Bunge Sports Club na mpaka usiku wa Novemba 10 alikuwa pamoja na Wabunge katika vikao  mpaka saa 2.45 usiku.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts