Get the latest updates from us for free

Home » » Trump akataa kulipwa mshahara wa urais Marekani

Trump akataa kulipwa mshahara wa urais Marekani

Written By Bigie on Monday, November 14, 2016 | 1:58:00 PM

Rais mteule wa Marekani, bilionea Donald Trump amesema hatakubali kupokea mshahara wa urais pindi atakapokuwa madarakani.

Trump ameweka msimamo huo weekend katika mahojiano maalum na mtangazaji maarufu, Lesley Stahl katika kipindi cha 60 Minutes, aliyetaka kufahamu kuhusu uamuzi wake juu ya mshahara wake akiwa ni mfanyabiashara mkubwa.
 
“Sijawahi kuzungumzia hili, lakini jibu langu ni hapana,” alisema. “Nafikiri inanibidi kupokea kwa mujibu wa sheria $1, kwahiyo ntachukua $1 (Sawa na shilingi 2,200 za Tanzania) kwa mwaka. Lakini hata sijui ni nini,” aliongeza.
 
Ingawa mtangazaji huyo alimkumbusha Trump kuwa anaiacha $400,000 kwa mwaka, rais huyo mteule alisisitiza, “sitachukua mshahara. Sitapokea.”
 
Wakati wa kampeni, Trump aliahidi kuwa atajiweka kando na biashara zake endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani, na kwamba atajikita zaidi katika kutimiza ahadi zake kwa Wamarekani. Alisema kuwa biashara zake ataziacha mikononi mwa watoto wake.

Mbali na hivyo, Donald Trump, amemteua Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama Mkuu wa Wafanyakazi.
 
Bwana Priebus ana uhusiano wa karibu na Spika wa Baraza la Wawakilishi Paul Ryan. Wandishi  wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na Baraza la Congress kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts