Serikali imewaomba wakazi wa mkoa wa Kagera walioathirika na tetemeko
la ardhi kuendelea kujijengea wenyewe kwakuwa michango yote yenye
thamani ya shilingi bilioni 5.4 iliyochangwa na wadau kwaajili ya
kusaidia na walioathirika imeelekezwa kwa taasisi za serikali, na si
wananchi binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja
Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu, alisema hadi sasa zimechangwa
shilingi bilioni 5 na milioni 427.
Alisema kamati ya maafa ya mkoa huo
imeshatumia kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni 130 kukarabati
miundombinu ya serikali iliyoathirika na kwamba fedha zilizobaki bilioni
4 na milioni 296 nazo zimeelekezwa huko.
Aidha aliwatoa wasiwasi wananchi waathirika wanaosubiri kupata msaada
binafsi watalazimika kuchukua michango iliyotolewa na wadau wengine
walioahidi kusaidia waathirika moja kwa moja na kwamba hata misaada hiyo
ikipatikana watasaidiwa waathirika walio katika makundi maalumu kama
wazee na walemavu.
“Fedha hizo ni kusaidia ujenzi wa wananchi waliobomolewa nyumba
hususan kwa makundi maalumu ambayo ni
wazee,walemavu,wagonjwa,wajane,wagane,wasiojiweza na yatima na wameomba
kupatiwa orodha ya makundi hayo kwa awamu na awamu ya kwanza ni awamu ya
watu 370 imeshawasilishwa ikiambatanishwa na picha za majengo
yaliyobomoka,” alisema Kijuu.
Hata hivyo uamuzi huo wa serikali umepingwa vikali. Tetemeko hilo la ardhi lilitokea September 10 mwaka huu na kusababisha madhara makubwa mkoani Kagera.
Post your Comment