Home » » Wakopaji Twiga Bancorp Waanza Kusakwa

Wakopaji Twiga Bancorp Waanza Kusakwa

Written By Bigie on Sunday, November 6, 2016 | 11:15:00 AM

Kama ulikopa Twiga Bancorp, bado hujasalimika inabidi tu uwasilishe fedha hizo, kwani Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema inaendelea na uchunguzi wa watu waliokopa ili iwabane.

Benki hiyo imefilisika na kuwekwa chini ya usimamizi wa BoT baada ya kubainika kuwa mtaji uko katika hali mbaya kiasi cha kuweka hatarini fedha za wateja.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndullu alisema wiki iliyopita kuwa benki hiyo ilikuwa na mtaji hasi wa Sh21 bilioni baada ya kuanza na mtaji wa Sh7.5 bilioni unaokubalika kisheria.

Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu orodha ya wakopaji wa benki hiyo, msimamizi wa benki wa BoT, Kennedy Nyoni amesema kwa sasa bado wanachunguza  waliokopa na ripoti itatolewa wiki ijayo.

“Tulichofanya ni kuchukua usimamizi wa hiyo benki na kumweka mtu wetu pale. Sheria ya Benki inatoa siku 90 za uchunguzi, lakini hadi wiki ijayo tutakuwa tumepata taarifa. Hata leo (jana) tuko ofisini tunaendelea na uchunguzi,” amesema Nyoni.

Akizungumza na waandishi wakati wa kutangaza kufilisika kwa benki hiyo, Gavana Ndulu alisema bado benki hiyo inazo mali zinazofikia Sh90 bilioni na Sh9 bilioni kati ya hizo haziko vizuri.

Alisema wametumia kifungu namba 56(1) (g)(I) na 56(2) (a-d) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, kuiweka Twiga chini ya usimamizi wa BoT.

Twiga Bancorp ilianzishwa mwaka 1992 ikiwa chini ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), na mwaka 1998 ikabadilishwa na kuruhusiwa kufanya kazi zote za kibenki isipokuwa za kupokea au kuchukua fedha za akaunti za kawaida.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts