Home » , » RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 103 & 104 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 103 & 104 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Written By Bigie on Thursday, December 15, 2016 | 10:44:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Nikamvuta na kumuingiza chooni, mikamuonyesha bomu lilipo, Sote tukajikuta tunashangaa kutokana bomu hilo limebakisha sekunde hamsini na tisa, kabla halijalipuka na sote hapa hatujui jinsi ya kulitegua, na muhudumu akaanza kulia, akijaribu kunikumbatia kwani mwisho wetu umefika.
 
ENDELEA
"Una chochote cha kukatia"
Nilizungumza huku nikimtoa muhudumu huyu, mwilini mwangu, kwani kukumbatiana kwetu sio suhulisho la bomu hili kuacha kuacha kulipuka. Hakunijibu zaidi ya kubabaika, kwa mawenge yaliyo mchanganya kupita maelezo. Akaanza kujipapasa huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, akatoa, kikatia kucha(Nail cutter), akaitupa chini huku akiendelea kuikagua mifuko ya nguo zake alizo zivaa. Kwa haraka nikaokota kikatia kucha, nikapiga magoti chini, huku nikiwa ninajiamini kwa lile ninalo kwenda kulifanya. 
 
   Sekunde za bomu hili, zikazidi kurudi nyuma, huku zikiwa zimebakia sekunde thelathini na mbili kabla halijalipuka. Nikaanza kuzichambua nyaya nyingi ndogondogo zipatazo ushirini, zikiwa na rangi tofauti tofauti.
 
"Ishirini na tano"
Muhudumu aliniambia, huku macho yake akiwa ameyatumbulia kwenye bomu, linalo zionyesha sekunde hizo, zinavyo rudi nyuma.
"Mungu wangu"
Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka.
"Kumi na tano"
Nikashika nyaya moja nyekundu na kuikata, chakushangaza, bomu likaendelea kurudisha sekunde zake nyuma.
"Nane"
Nikazidi kuchanganyikiwa, na kukata wanya mweusi, hali ikawa ni ile ile.
"Tano"
Mikono yote, ikazidi kutetemeka hadi nikaangusha kikatia kucha, nikakiokota kwa haraka, hata kukaa mkononi vizuri, nkawa ninashindwa kukishika.
"Tatu"
 
Nikamuona muhudumu, akipiga ishara ya msalaba akiashiria mwisho wetu ndio unakaribia, nikashika waya wa rangi ya kijani, sekunde ikawa imebaki moja, nami nikawa nimeukata. Sekunde hiyo ikasimama hapo hapo na bomu kuzima. Nikashusha pumzi nyingi, huku mwili wangu wote ukiwa umesha vuja jasho lakutosha hadi shati nililo livaa, likawa limelowana kabisa. Kumtazama muhudumu nikamkuta akiwa ameyafumba macho yake huku jasho likimwagika shingoni nwake.
 
"Tumefanikiwa"
Nilizungumza kwa sauti ya unyonge huku nikimtazama usoni muhudumu, akayafumbua macho yake taratibu, huku akihema. Akalitazama bomu nililo lichomoa na kulishika, akabaki akiwa ameduwaa. Akanishika mkono taratibu na kuninyanyua, akanikumbatia huku akilia kwa furaha.
"Asante Mungu, kweli wewe ni mwema. Hakuna kama wewe"
Alizungumza huku akiendelea kulia, nakunifanya na mimi machozi kunimwagika kwani sikutarajia kama nitaweza kufanikiwa kulitegua bomu hili, taratibu akaniachia, huku akijifuta machozi usoni
 
"Unaitwa nani?"
"Eddy, Eddy Godwin"
"Am Tasiana, from Arusha Tanzania"(Mimi ni Tasiana natokea Arusha Tanzania)
"Mimi pia natokea Tanzania, ila A leve nilisoma Arusha"
"Waooo, nashukuru kukufahamu"
Tasiana akanikumbatia kwa mara ya pili, akawasiliana na marubani wa ndege hii, kupitia kijisimu kidogo wanacho kitumia kuwasiliana, wakamuomba tuelekee kwenye chumba walipo, tukiwa na bomu hilo, ila tuhakikishe hakuna abiria atakaye liona, ili kuto hatarisha amani ya walio wengi.
Tasiana akachukua mfuko mtupu, mweusi. Akaliweka bomu, nikaongozana naye hadi chumba cha marubani. Tukawaelezea hali halisi juu ya tukio zima na jinsi mchungaji Frank, alivyo nipa vitisho nikiwa ninapishana naye kwenye mlango wa chooni.
 
"Hakuna aliye toka ndani ya ndege, ngoja tukifika Afrika kusini, tutafanya upelelezi kabla watu hawaja ruhusiwa kushuka kwenye ndege"
Rubani mmoja alizungumza huku akilitazama tazama bomu hilo nililo mpatia.
"Ukimuona si utamkumbuka?"
"Ndio, nilikuwa nimekaa naye ila simuoni kwenye siti yetu"
"Ulikaa siti gani?"
Nikamtajia rubani, huyo herufi ya siti niliyo kuwa nimekaa, akatazama mkanda mzima, kwenye kiji tv chao kidogo unao rekodiwa na kamera zilizo tegwa kila kona ya ndege. Tukamuona mzee huyo akiingia kwenye moja ya chumba walicho dai ni stoo, chenye gazi za kushukia chini, kunapo hifadhiwa mizigo mikubwa mikubwa.
 
"Ngoja nimfwate"
Nilizungunza kwa kujiamini, huku nikiwatazama marubani hawa wapatao wanne, huku wawili wakiwa niwasaidizi.
"Itaweza kumkamata?"
"Nitahakiksha nalifanikisha hilo"
Wakanitazama machoni, mkuu wao akanipa ruhusa.
"Tuongozane"
Tasiana aliomba tuongozane pamoja.
"Wewe baki, ngoja nikajaribu kulifanya na hili kama nitafanikiwa"
"Tafadhali twende pamoja"
Tasiana aling'ang'ania kwenda, ikanibidi nimkubalie tu. Tukaongozana hadi kwenye chumba hicho, pasipo wasafiri wezangu kuelewa kitu gani kinacho endelea, hakikuwa chumba kikubwa sana, kwani kina ngazi zakushuka chini kulipo na mizigo mikubwa. Tukafanikiwa kushuka chini, kwa wingi wa mizigo iliyo fungwa kwenye mifurushi mikubwa, ilitufanya tubaki tukiwa tumesimana na kuduwaa.
 
"Atakuwa wapi?"
Tasiana aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendea kupepesa pepesa macho yetu kila kona ya eneo hili lilolo kubwa.
"Nifwate nyuma na kuwa mkimya"
Tukaanza kupita kwenye vinjia, vilivyo tenganishwa kwa maburungutu makubwa ya mizigo. Nikaanza kupata wasiwasi, baada ya kukuta shati alilo kua amelivaa mzee yule, likiwa chini. Tasiana akataka kuliokota ila nikamzuia asifanye hivyo.
"Kwa nini nisiliokote?"
Nikatingisha kichwa nikimuashiria Tasiana asifanye chochote dhidi ya shati hilo.Tukalipita, hatua kumi mbele, tukakuta suruali aliyo kuwa ameivaa.
Kwa kutumia mguu nikaisogeza kuitazama kama kuna kitu kimefunikwa, ila hatukuona kitu.

Arufu ya moshi wa sigara, ukaanza kuingia kwenye pua zetu, ulitokea upande wa pili wa sehemu ilipo mizigo hiyo. Tukapiga hatua za tahadhari hadi sehemu inapo tokea harufu ya moshi huo wa sigara, tukakuta kipande cha sigara kikiwa chini, kikiendelea kuteketea taratibu.
 
"Yumo humu humu"
Tasiana aliniambia huku akitazama tazama kila kona ya hili eneo. Nkakikanyaga kipande cha sigara hadi kikazimika. Nikapiga hatua mbili mbele, nikastukia kitu lizito kikinipiga kifuani mwangu na kuniangusha chini, nikaamka kwa haraka kutazama ni nini kilicho nipiga.
Mtu aliye valia nguo nyeusi tupu akawa amesimama mbele yangu, huku amevalia kinyago kilicho ificha sura yake, mkono wake wa kulia, ameshika chuma kifupi alicho toka kunipiga nacho muda mchache ulio pita.
 
"Buuuuuuuupuuuuuuuuuu"
Alizungumza maneno kama aliyo niambia mzee yule nilipo kuwa nikipishana naye mlangoni mwa chooni.
"Rudi nyuma"
Nilimuambia Tasiana, naye akafamya hivyo. Taratibu nikavikunja vidole vya mikono yangu, na kugeuka kuwa ngumi.
"Hahaaaaaa"
Mtu huyo alicheka, kwa dharau kubwa huku akiendelea kunitazama machoni mwangu. Nikarusha ngumi kadhaa, ila akazikwepa zote na kunitandika chuma cha mgongo kilocho nifanya nitoe ukelele mkali wa maumivu.
 
Nikajipanga tena kufanya mashambulizi kwa mtu huyu, kila nilivyo zidi kupambana naye, ndivyo jinsi alivyo nizidi kwa mbinu za kupigana.
  Akakitupa chini chuma chake alicho kishika na kukunja ngumi, akiashiria tunapigana kwa mkono, sikukata tamaa ya kupamba naye, baadhi ya ngumi na mateke niloyo mpiga, kidogo yakanipa matumaini ya kuamini nitamudu. Ila naye hakuwa nyuma katika kurusha makonde mazito tena yaliyo shiba kwa ujazo mzuri tu wa ngumi, kwani akinipiga konde moja nilazima nilisikilizie kwa sekunde kadhaa.
"Eddy utakufaa"
Tasiana aliniambia huku akinitazama jinsi ninavyo vuja damu, zikitokea chini kidogo ya jicho la kushoto baada ya kupigwa ngumi nzito, niliyo jitahidi kuizuia kwa mikono yangu, ila ilipita hovyo hiyo na kunipasua sehemu hiyo.
"Kama humuwezi tuondoke"
 
Nikamtazama Tasiana jinsi anavyo zungumza kwa wasiwasi, nikatingisha kichwa kuashiria kwamba bado sijashindwa. Nikaitazama miguu ya mtu huyo jinsi inavyo irusha rusha kwa haraka akinifwata, nikatambua anatumia upiganaji wa kichina unao itwa 'kung fu' na mimi sikuwa na mfumo maalumu wa kupigana ndio maana nikajikuta nikipigwa kizembe, kiasi hichi.
'Mtu anaye pigana kung fu, wewe tazama miguu yake na mikomo yake kabla hujafanya shambulizi lolote kwake'
 
Niliyakumbuka maneno ya mzee Godwin, kipindi akinifundisha utotoni, hadi mtu huyu ananikaribia nikawa nimemtazama kwa umakini, anavyo kuja kwa kasi. Akarusha mateke kazaa, nikaweza kuyakwepa na kumpiga ngumi ya tumbo iliyo mrudisha nyuma na kumfanya ajipinde kiasi.
   Tukaanza kuyumbishwa, hii ni baada ya ndege kuanza kutua, kwa bahati mbaya Tasiana akateleza na kuangukia sehemu aliyopo mtu huyo. Akamkamata Tasiana na kukichomoa kisu chake  na kumuwekea Tasiana shingoni.
 
Katika kurupushanani za ndege kutua kwenye ardhi, Tasiana akafanikiwa kumtoa mtu huyo kinyago cha usoni mwake, sikuamini kumuona Mzee Godwin, kwani muda wote nilivyo kua nikipambana naye nilihisi kuwa ni yeye, hii nikutokana na mapigo aliyo kuwa akiyatumia kushambuliana na mimi, ila sikuwa na uhakika kama ni yeye. Nikiwa nimeduwaa kumtazama Mzee Godwin, aliye endelea kujitazama kwa macho makali, nikastukia kumuona Tasiana akianguka chini, huku amechomwa kisu cha tumboni.
 
Mzee Godwin, akanifanyia ishara ya kunichinja kwenye shingo kisha akaondoka,  na kumuacha Tasiana akiendele kuugulia kwa maumivu makli. Nikataka kumfwata mzee Godwin, ila Tasiana akaniita kwa kuhitaji msaada wangu, ili kuyaokoa maisha yake yaliyopo hatarini kupotea.
"Eddy nisaidie ninakufaa, mimi"


  SORRY MADAM (104)

Nikakimbia hadi sehyemu alipo angukia Tasiana, kwa haraka nikamuweka vizuri huku kichwa chake akiwa amekilaza katika mkono wangu wa kulia, huku mkono wangu mwengine ukiwa na kazi ya kuzizuia damu zilizo kuwa zikimwagika kuto kuendelea kutoka katika jeraha lake alilo chomwa na kisu.
 
“Eddy ninakufa mimi”
“No huwezi kufa Tasiana”
Niliendelea kumfariji Tasiasa, huku nikiwa ninaendelea kusubiria ndege kuweza kutua kwenye ardhi, kwani sehemu tuliyopo ilinilazimu kuweza kuegamia moja ya mzigo ili tusianguke. Kwa kutumia kijiisimu kidogo alicho kuwa anakitumia Tasiana, nikaweza kuomba msaada kutoka kwa wahudumu wengine. Hadi ndege inasimama kabisa ardhini, hali ya Tasiana kusema kweli haikuwa nzuri kiasi cha kumfany ayafuyafumbe macho yake, huku mapigo ya moyo yakimuenda taratibu sana. 

Tukasaidiana na wezake kumpa huduma ya kwanza. Nikiwa ninaendelea kutafakari ni nini cha kufanya huku nikizunguka zunguka sehemu tuliyopo. Nikauona mwili wa mtu, ukiwa umelala chini na umesukumizwa chini ya moja ya mzigo mkubwa huku miguu yake ikiwa imetokezea kwa nje.
 
Nikamuita mmoja wa polisi kati ya polisi wanne walio ingia sehemu tulipo, kwa kusaidiana naye tukamvuta na kumtoa nje, sikuamini kumuona yule mchungaji akiwa ameuawa kikatili huku macho yake yakiwa yamepasuliwa na inavyo onekana ameminywa kwa vidole vigumu hadi yakapofuka.
 
“Unamjua huyu?”
Aliniuliza kwa lugha ya kingereza, nikamtazama machoni askari kisha nikatingisha kichwa kwa kumuashiria kwamba ninamfahamu mtu huyo. Akawaita wezake kuja kulishuhudia tukio hili la kinyama.
“Inabidi twende kituoni kwa mahojiano zaidi”
Askari mmoja alizungumza huku akinitazama machoni.
“Sawa, ila kwa sharti moja tu”
“Lipi?”
“Nahitaji kubadilisha hizi nguo zimejazana damu kama ninyi munavyo niona”
“Kwa hilo hakuna tatizo”
 
Kilicho niokoa dhidi ya hawa askari kuto kunichukualia mimi kama muhalifu, ni kwa jinsi marubani walivyo waeleza juu ya tukio zima la kutegua bomu lililo kuwa limetegwa ndani ya ndege hii. Nikatafutiwa nguo nyingine, nikazibadilisha  na kutoka sehemu ya juu ambapo nikakuta baadhi ya abiria wakiwa wameketi kwenye siti wakisubiri safari iiendele, huku wengine wakiwa katika mlolongo wakishuka na kukaguliwa. 
 
Nikamuona Tasiana akiingiazwa kwenye gari la wagonjwa na kuondoka katika eneo la uwanja wa ndege, sikufahamu wanakwenda katika eneo gani. Nikashuka kwenye gazi za ndege huku nyuma yangu nikiwa nimeongozana na askari wawili. Baadhi ya waandishi wa habari walikatazwa kunipiga picha yoyote, huku mmoja wa askari akisikika akiyazungumza maneno haya mara kwa mara pale alipokuwa akisogezewa maiki za waandishi wa habari.
 
“HUYU JINA LAKE NI EDDY NA WALA SI GAIDI”
Maneno yake yakazidi kunipa matumaini ya kuamini kwamba kile kilichopo mbele ya maisha yangu hakita kuwa kigumu sana kwani sina hatia yoyote katika hilo. Tukaingia kwenye moja ya gari la polisi lenye rangi nyeusi, huku tukiwa na askari wawili wenye pikipiki kubwa nyeupe zenye kupiga king’ora, mmoja akiwa mbele na mwengine akiwa nyuma.
“Mbona munanipeleka kwenye mahojiano huku kukiwa na askari wengie?”
“Hii ni kwaajili ya usalama wako kwanza, ndani ya nchi hii, ugaidi umekidhiri sana, hususani kwa mtu ambaye anahitajika kutoa msaada wa kukamatisha mtu au kundi kubwa la watu wakiwemo matajiri na viongozi serikalini, bila ya kumfanyia ulinzi wa kutosha basi anaweza kuuawa”
 
Askari alizungumza huku nikiendelea kutazama pikipiki ya askari inayo kuja nyuma yetu. Tukafanikiwa kufika kituo cha polisi salama salmin, nikapelekwa kwenye moja ya ofisi kwa ajili ya kukutana na mkuu wa kitengo hicho cha mahojiano
“Hembu nielezee tukio zima jinsi lilivyo tokea kwenye ndege”
Mzee wa makamo alimiuliza swali hilo, huku tukiwa tunatazama machoni. Nikamuelezea kila kitu kilivyo kuwa ndani ya ndege hadi maafa ya Tasiana kuchomwa kisu nikiwa pamoja naye.
 
“Muuaji ulifanikiwa kuiona sura yake?”
Nikafikiria kwa sekunde kadhaa, ikanilazimu kuktaaa kwamba sikumuona sura yake. Kutokana na kinyago alicho kuwa amekivaa usoni. Ila ukweli ni kwamba ninatambua kila kitu kuhusiana na Mzee Godwin na endapo nitawaeleza ninamtambua, nitalazimika kujibu maswali mengi ambayo yangenipotezea muda wangu mwingi. Baada ya kuridhika na mahojiano yangu, wakanipeleka, hospitali kupatiwa matibabu ya majeraha yangu kisha wakanipeleka hotelini kwa ajili ya kulala, hadi kesho nitakapo endelea na safari yangu ya kuelekea nchini Tanzania.
 
Usiku kucha nikiwa ndani ya Hoteli sikuweza kupata usingizi hata kidogo, swali lililo niumiza akili yangu ni kwanini hadi leo mzee Godwin anachuki juu yangu.  Sababu ya mimi kuwa ni mtoto wa pacha mwenzake haikuwa kubwa sana yakunifanya niwe adui yake aliye tumia muda wake mwingi katika kunisaka kila kona ya dunia ila kuiangamiza nafsi yangu.
 
“Kuna kitu kinacho endelea hapa, ambacho mimi sikifahamu, itabidi nifwatilie kwenye kumbukumbu za mama.”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kulala kwenye kitanda, huku macho yangu yakitazama feni linalo zunguka taratibu juu ya chumba hichi.
Asaubuhi na mapema nikawahi kuamka ili kuiwahi ndege niliyo kuwa nikisafiria kwenda nayo Tanzania, kwani ililazimika ndege hiyo kuzuiwa kwa muda ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika kabla haijaendelea na safari yake kuelekea mashariki mwa Afrika. Nikafika uwanja wa ndege nikiwa nimevalia kofia kuepuka watu wengi kunitazma tazama mimi, nikaingia kwenye kitengo cha usafirishaji ambapo nikakabidhiwa hati yangu ya kusafiria pamoja na mizigo yangu iliyo kuwa imehifadhiwa hapo.
 
“Ndege itaondoka muda gani?”
Nilimuuliza muhudumu wa ndege yetu, baada ya kukabidhiwa kila kilicho changu na mamlaka husika walio kuwa wamevishikilia vitu vyangu.
“Saa tisa jioni, tunasubiria kupata ruhusa ya kuondoka hapa uwanja wa ndege, kutoka katika ofisi za Interpol”
“Ahaa basi ngoja nikazunguke zunguke mjini mida ya saa saba nirudi”
“Sawa”
“Hivi yule mwenzenu, amepelekwa hospitali gani?”
“St Hellen Hospital”
“Sawa, nitamuomba dereva taksi anipeleke hapo”
“Sawa”
 
Nikaiacha mizigo yangu kwa muhudumu huyu wa ndege ambaye nilikuwa nikizungumza naye, nikatoka nje na kumuomba dereva  taksi kunifikisha katika hospitali hiyo niliyo mtajia jina. Nikafika hospitalini nikaelekea moja kwa moja sehemu ya mapokezi ambapo nikamuomba muhudumu kunipeleka kwenye chumba alicho lazwa Tasiana. Wakanipeleka na kunionyesha chumba chake, nikaingia na kumkuta akiwa amelala. 

Huku akiwa amezungukwa na mashine nyingi zinazo msaidia kupumua. Nikamtazama dada wa watu jinsi alivyo mzuri, nikajikuta mchozi yakinimwagika kwani pasipo mzee Godwin sidhani kama angelala kwenye kitanda hichi kwa wakati kama huu, tana akiwa hajitambui kabisa. Nikaivua saa ya dhahabu, niliyo pewa na Pretty na kuiweka pembeni mwa kichwa chake, kama zawaidia itakayo msaidia baada ya kupata nafuu kwani saa hii ni ya gharama sana.
 
“Ninakuomba hii saa, akiamka muambie umepewa na Eddy”
Nilimuambia nesi huyu ambaye amevalia mavazi ya watakatifu wa kike(masista), akaniahidi kuitunza hadi Tasiana atakapo pona na ataufikisha ujumbe wangu kama nilivyo muambia. Nikaondoka na kurudi uwanja wa ndege, nikaichukua mizigo yangu na kukaguliwa vizuri, kisha nikaruhusiwa kwenda ndani ya ndege. Baada ya masaa kadhaa, safari ikaanza kuelekea Kenya kisha inamalizikia Tanzania. Muda wote ndani ya ndege nikawa ninamuomba Mungu katika kunisiaidia ili kuweza kufika nchini Tanzania salama salimi. 
 
Hadi tunafika Kenya, hapakuwa na Tatizo lolote ndani ya ndege, tukakaa Kenya kwa masaa kadhaa, kisha safari ya Tanzania ikaanza, ambayo ikatuchukua masaa machache kuingia katika anga la Tanzania. Ndege ikatua kwenye uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere, nikasali sala ya kumshukuru Mungu kwa kuweza kunifikish salama Tanzania. Hadi ninatoka nje ya uwanja moyo wangu ukawa umetawaliwa na furaha kubwa sana kwani ni muda wa mimi kuiona familia yangu japo Pretty aliniambia niipeleke mbali na Tanzania, familia yangu ila siwezi kuufanya ujinga kama huo.
 
“Hapa ndipo ninapo nilipo zaliwa, siwezi kwenda sehemu yoyote”
Nilizungumza huku nikitazama mandhari tofauti tofauti yaliyopo nje ya uwanja huu, nikamuita muhudumu kati ya wahudumu wanao zunguka zunguka ndani ya uwanja huu
“Samahani ni wapi wanapo uza lini za simu?”
”Nyoosha kulia, utaona maduka ya simu ukifika hapo utajua ni mtandao gani unahitaji kuutumia”
“Asante”
Nikaenda nilipo elekezwa, nikawakuta wadada kadhaa wakiwa wanawahudumia watu wengine, na mimi nikajichochochomeka kati ya wateja, nikaelezea shida yangu, nikatenmgenezewa lini mpya ya simu kwa bahati nzuri wakaniambia nikiweka tu salio laini hiyo itaanza kufanya kazi.
“Niwekee”
Nikatoa noti ya dola mia na kumpa dada huyo, aliye nisajilia laini yangu.
“Hapo utajua unaniwekea vocha ya kiasi gani”
Akabaki amenitumbulia mimacho akinitazama machoni kwa mshangao, akaanza kuminya minya simu yake huku akinitazama usoni mwangu kana kwamba ananifananisha na mtu fulani ila anashindwa kuniambia ni mtu gani. Akaniingizia salio la laki moja, kabla sijaondoka akaniita
 
“Samahani kaka”
“Bila samahani”
“Sijui nimekufananisha au laa”
“Umenifananisha na nani?”
“Mtoto wa waziri mkuu aliye zikwa miezi iliyo pita”
“Sasa dada yangu kama mtu amezikwa atatembeaje?”
“Hapana unaweza kuwa ni pacha wake”
“Hapana, kwani huyo mtoto aliye zikwa, walisema ana pacha wake?”
“Hapana”
“Basi si mimi”
“Ila naye anaitwa Eddy”
“Majina tu yamefanana”
Nikamuaga dada huyu na kuondoka zangu, nikatafuta sehemu iliyo tulia na kumpigia simu blanka
“Dogo upo wapi?”
“Home nani?”
“Acha ujinga hujui sauti yangu”
“Ohoooo kaka Eddy”
Nilimsiki Blanka akizungumza kwa furaha kubwa.
“Nisikikilize, njoo unichukue uwanja wa ndege ila usimuambia mtu kama nipo hapa”
“Nakuja sasa hivi nipe dakika kumi nitakuwa hapo”
“Powa”
 
Nikakata simu, kutokana nimefika mida hii ya saa sita mchana, nina amini barabarani hakuna foleni nyingi zinazo weza kumfanya akachelewa sana. Nikatafuta sehemu na kukaa. Ndani ya robo saa nikamuona Blanka akishuka kwenye gari aina ya Haria, akaanza kutazama pande zote za sehemu wanapo tokea wageni, nikamfwata hadi sehemu nilipo. Akanikimbilia na kunikumbatia kwa furaha sana.
“Eheee mbona usoni una plasta?”
“Ahaaa nilipata kajitatizo kadogo”
“Mmmmm pole”
Blanka akizungumza huku akilichukua begi langu na kulibebe, tukaingia kwenye gari na kuianza safari.
“Tunaelekea kwa mama au kwa kina Junio?”
“Kwa kina Junio kwanza. Ila mama anaendeleaje?”
“Mama kidogo ana kiunafuu”
“Mungu ni mwema atapona”
“Ni kweli”
 
Tukafika katika jumba ambalo ndipo ilipo familia yangu, mlinzi akatufungulia geti, nikamuona Shamsa akicheza na Junio kwenye moja ya bustani yanye majani yaliyo katwa vizuri. Walipo liona gari la Blanka, Junio akakatisha mchezo na kuja kasi kwenye gari kumpokea shangazi yake. Junio alipo niona akageuza kumfwata Blanka na kuzunguka upande wa pili wa gari ambapo, akanirukia kwa furaha. Nikamkumbatia huku machozi yakinilenga lenga kwa furaha. Shamsa naye hakuhitaji kubaki nyuma, akanikumbatia kwa furaha kubwa.
“Hamujambo?”
“Hatujambo dady”
“Mama yupo wapi?”
“Anapika jikoni”
Nikambebea Junio na kumshika mkono Shamsa, sote tukaingia ndani, Junio akaanza kumuita mama yake.
“Nini bwana, umesha anza makelele yako Junio”
Niliisikia sauti ya Phidaya ikitokea jikoni akionekana kumkemea Junio aliye kuwa akimuita muda wote.
 
“Shiiiiiii”
Niliwanyamazisha, nikaelekea jikoni ambapo nikamkuta Phidaya akiwa bize akikata kata nyama. Nikamnyatia kwa nyuma taratibu na kumziba macho yake. Akatulia kwa sekunde kadhaa huku akishika shika mikono yangu.
“Eddy”
Phidaya aliita kwa sauti ya upole, iliyo jaa furaha kwa mbali. Nikavitoa viganja vyangu machoni mwake, akanigeukia na kunitazama. Kwa furaha kubwa Phidaya akanikumbatia huku akiruka ruka kama mtoto. Bila hata salamu, akaniwahi mdomo wangu na kuanza kuninyonya mdomo wangu, alipo ridhika akaniachia, huku machozi ya furaha yakimwagika.
 
“Baby”
“Ndio mke wangu”
“Nimekumicjeee”
“Hata mimi mke wangu”
Furaha ikarudi upya kwenye maisha yangu, nikamshukuru MUNGU kwa kuweza kunikutanisha tena na familia yangu, wakiwa katika hali nzuri ya furaha na afya nzuri. Tukapata chakula cha mchana, baada ya kumaliza sikuhitaji kupoteza muda, sote tukaelekea nyumbani kwa mama. Wahudumu wa mama wakaanza kunishangaa sana, ila sikuwalaumu kutokana wanatambua kwamba mimi nimefariki. Blanka akanitambulisha kwa daktari anaye muhudumia mama.
 
“Hali ya mama inaendeleaje?”
“Tumuombe Mungu atamponya, huku nami nikiendelea kuhakikisha ninayaokoa maisha yake kadri ya uwezo wangu”
Dokta Angelina alizungumza huku akinitazama. Nikamuomba dokta Angelina kuingia chumbani kwa mama, akaniruhusu bili kipingamizi. Taratibu nikaufungua mlango wa chumba cha mama na kuingia ndani, nikamkuta mama akiwa amelala kitandani huku amekondeana sana. Sikuamini kama nitamkuta kwenye halii hii mbaya. Nikapiga hatua hadi kwenye kitanda chake, taratibu nikapiga magoti chini huku machozi yakinilenga lenga. Nikamshika mkono wake wa kulia, ulio chomekwa sindano ya dripu la maji, sura ya mama imebadilika sana huku imekunjamana kwa kukonda, mashavu yake yameingia ndani huku nywele zake zikiwa na rangi ya kahawia.
 
“Mama”
Niliita huku machozi yakianza kunimwagika taratibu, nikarudia tena kumuita ila hakuniitikia kabisa.
“Mama, mwanao Eddy nipo hapa. Nakuomba ufumbue macho yako japo unione mama yangu. Sikufa mama nipo hai, nimerudi tena nyumbani……”
Kidogo mwili wa mama ukatingishika, nikajikuta nikiwa nimemkazia macho nikimtazama machoni mwake, taratibu akayafumbua, akakigeuza kichwa chake upande wangu, akanitazama kwa muda huku akiwa amenishangaa
 
“Mama ni mimi Eddy, mwanao wa pekee”
Mama akaendelea kunitazama, baada ya muda akatabasamu akishiria kufurahi uwepo wangu. Nikamuunga mkono na mimi nikatabasamu huku nikitokwa na machozi ya furaha kidogo. Gafla mama akayafumba macho yake, mwili wake ukaanza kutetemeka, hali ikazidi kuwa mbaya baada ya kuanza kuirusha rusha miguu yake kwa nguvu hadi kitanda kikaanza kutingishika tingishika. Nikazidi kuchanganyikiwa zaidi  baadaya ya mapovu kuanza kumtoka mdomoni, na mwili wake ukizidi kukakamaa.
“Doktaaaaa Doktaaaaa……………..!!!!”
Niliita kwa sauti ya juu, ya kuchanganganyikiwa kwani hali ya mama, ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba nikaanza kuhisi kumpoteza duniani mama yangu kipenzi.

==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts