Home » » Sherehe za Maulid: Waziri Nchemba awataka Watanzania kuwafichua watu wanaotumia dini kufanya vurugu

Sherehe za Maulid: Waziri Nchemba awataka Watanzania kuwafichua watu wanaotumia dini kufanya vurugu

Written By Bigie on Monday, December 12, 2016 | 1:32:00 PM

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania wote nchini kuungana kwa pamoja na kuwataja watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya vurugu kwa kuhusisha vitendo hivyo na dini kwani watu hao wanaweza kusababisha nchi kupoteza amani.

Waziri Nchemba ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida ambapo alisema mtu ambaye anamcha Mungu hawezi kuwa akijihusisha na vitendo hivyo na Serikali ya awamu ya tano itakuwa ikimchukulia hatua mhusika bila kuhusisha dini.

“Wizara yangu inahusika na taasisi zote zinazohusika na ibada, niwambie jambo moja tutofautishe udini na kumcha Mungu, mtu anaposhika sana dini ni mshika dini na mtu unanayemcha Mungu ni mchaMungu sio mdini, makosa yote katika nchi yanafanywa na makundi mawili ya watu wenye dini na wasio na dini,

“Kosa lolote ambalo likifanywa liwe kosa la ambae alifanya kosa, sio kosa la dini, akifanya Mkristo kosa la mtu sio la dini, akifanya Mwislamu kosa ni lake si la dini, na hata kama hana dini kosa ni lake yeye, na tusaidiane kuwa tunawafichua wanaosababisha vurugu,” amesema Nchemba.

Pia Nchemba ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa amekabidhi msaada wa mabati 1,000 kwa ajili ya kutumika kujenga misikiti na kuahidi kuwa baada ya wiki moja atawapatia gari aina ya Noah.

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts