Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 11 & 12 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 11 & 12 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Saturday, December 31, 2016 | 12:58:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Mama mbona siwaelewi”
“Huo ndio ukweli halisi mwanangu, wewe si mtoto wa Godfrey, baba yako wewe ni Godwin. Am your mother na natambua ni nani aliyenipa ujauzito wako”
Eddy akajikuta akishusha pumzi huku macho yakiwa yamemtoka kiasi kwamba akawa anajihisi kuchanganyikiwa kwani si jambo rahisi kwani anavyo tambua kwamba baba yake halisi ni Godfrey
“Unataka kujua ukweli eheee?”
Mama Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa huku wakitazama na mwanye, hadi baadhi ya wauguzi wakaanza kuyatega masikio yao kuweza kusikia ni kitu gani mama huyo anahitaji kukizungumza kwa mwanaye huyo


ENDELEA
“Mama”
Eddy alimuita mama yake kwa sauti ya chini, akaupitisha mkono wake mmoja kwenye bega la mama yake na kumkumbatia huku akiendelea kusononeka
 
“Eddy natambua kwamba Godfrey alikuambia mambo mengi kuhusiana na sisi, ila yote aliyo zungumza kwako ni uongo mwanangu”
Mama Eddy aliendelea kuzungumza huku  machozi yakiendelea kumwagika, macho ya Eddy yakazunguka kwenye eneo walilopo na kuwastua wauguzi wa kike ambao mara kwa mara waliweza kuwatazama. Eddy akamnyanyua mama yake na kuongozana naye hadi lilipo gari lake na kuingia ndani. Akafunga vioo vyote vya gari ili sauti isitoke nje
 
“Mama nimesha kua sasa, nahitaji kujua ukweli wa kila kitu kuhusiana na yupi ni baba yangu kati ya Godwin na Godfrey?”
Mama Eddy akashusha pumzi nyingi, huku taratibu akiipa nafasi akili yake kuweza kuvuta kumbukumbu zake za nyuma.
 
        ******
 Miaka arobaini na tano iliyo pita, nilikuwa ni binti mzuri sana mwenye kuvutia machoni mwa wengi, nilikuwa ninapendezeshwa na mama yangu, kila asubuhi nilipo kuwa ninaamka. 

Kipindi hicho nilikuwa ninami mitatu, jambo ambalo liliwafanya wazazi wangu kwa kipindi kile kuweza kunianzisha masomo ya chekechea. Ilikuwa ni furaha kubwa kwangu mimi, kuweza kuanza shule mapema kiasi hichi, ila nilijikuta ninakuwa kivutio kwa wanafunzi wengine wakiwemo Godwin na Godfrey, ambao nao pia walikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wa chekechea niliyo kuwa ninasoma, Godwin na Godfery walitokea kuwa marafiki zangu sana, hii nikutokana na kufanana kwao. Kila mmoja alikuwa na sifa zake za kipekee
 
Godwin yeye alikuwa ni mcheshi, mpenda michezo, mteteaji. Alikuwa ananitetea kila pale nilipokuwa ninaonelewa na baadhi ya wanafunzi wezetu ambao walikuwa wakizivuta nywele zangu nilizokuwa nimesukwa mabutu mabutu.
 
Ila Godfrey alikuwa ni mvivu darasani, alikuwa hapendi michezo na mara nyingi alikuwa anapenda kukaa na wasichana wengine, jambo lililo kuwa likitukera mimi na Godwin. Tulibahatika kusoma shule ya msingi pamoja, hadi tunafika sekondari sote tukawa katika shule mmoja. Ila Godfrey alikuwa bize na visichana wengine. Nilimpenda sana Godfrey nikawa ninawivu naye japo sikumueleza ukweli kwamba ninampenda sana na kumuhitaji. Godwin alinipenda sana kiasi kwamba sikuwa na jinsi zaidi ya kujikuta nikimpenda Godwin.
 
Tulipo maliza kidato cha nne mimi nilibahatika kwenda kusoma Uingereza, kutokana baba yangu alikuwa na uwezo na pia alikuwa ni mwanasheria mkuu wa kipindi hicho. Nilikaa Uingereza kwa miaka nane. Kwakipindi chote sikuwa na mawasiliano kati ya Godwin na Godfrey, ila nilikuja kusikia kwamba baba yao alifariki kwa ugonjwa wa sartani ya damu. Na sikuweza kujua ni wapi walipo. Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwatafuta ila sikuweza kupata mafanikio.
 
Nilipo anza kazi ya udaktari kwenye kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Muhimbili, ndipo kuna siku kulitokea ajali ya basi, hapo ndipo nilipo weza kumpata Godwin, akiwa ni miongoni mwa majeruhi wa ajali hiyo. 

Godwin alikuwa mahututi, ilinilazimu kumfanyia upasuji mimi na madaktari wezangu, Alipo pata nafuu, mapenzi yetu yakafufuka upya. Ndipo nilipo amua kuanza kuishi naye nikiwa katika mapenzi mazito, ndipo alipo mleta Godfrey kuja kuishi nasi pale nyumbani. Godwin kwa kipindi hicho alikuwa nimwanajeshi, na alikuwa anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo mbalimbali. Ninakumbuka alipangiwa safari ya kwenda Pakistani, huko walipangiwa kwenda kukaa kwa kipindi kisicho julikana. 
 
Ulikuwa ni usiku wa fauraha na majonzi mimi na Godwin, pale tulipo kuwa kitandani, kwani ilikuwa ni muda mchache tangu tufunge ndoa yetu. Siku hiyo ndio siku ambayo nilikuwa kwenye  siku za hatari kama mwanamke, aliye kamilika, niliweza kuzipokea mbegu za Godwin, na kujua kabisa zimekwenda kuingia kwenye mfuko wangu wa uzazi. Asubuhi ya siku iliyo fwata tulimsindikiza Godwin hadi kwenye uwanja wa ndege
“Gody, mlinde shemeji yako, najua ninapo kwenda nipagumu sana, ila ningependa nirudi nimkute mke wangu akiwa salama”
 
“Sawa ndugu, nitamlinda hakuna kitakacho mpata”
“Baby usilie, kila kitu kitakuwa sawa, pia moyo kondo mbona ni siku chake tu nitarejea”
“Godwin si kweli, najua unapo kwenda si sehemu salama”
“Noo baby nitarudi siku za si nyingi”
Godwin alinibusu mdomoni mwangu, kisha akanyanyua begi lake kubwa alilokuwa amehifadhia vitu vingi kisha taratibu akanikumbatia vya mwisho mwisho kisha akaondoka na kwenda kuungana na wanajeshi wengine, kwa macho yangu nilimshuhudia akiingi kwenye ndege na kuondoka, jambo lililo nipa uchungu mkubwa sana kwenye maisha yangu
 
“Shem twende nyumbani”
Godfrey alinibembeleza kwa uchungu pale nilipo ninalia nikimshuhudia mume wangu akiondoka nchini na kuniacha mimi peke yangu. Kusema kweli Godfrey alikuwa ni mzuri sana, na wakuvutia kupita Godwin ambaye mafunzo ya jeshi yaliweza kumkomaza kwa kipindi alicho kuwa akifanya hayo mazoezi magumu
 
Tulirudi nyumbani, huku tukiwa katika hali ya huzuni, hususani mimi ndio upweke ulinijaa sana moyoni mwangu, moja kwa moja niliingia chumbani kwangu kwa ajili ya kulala, ili nijitahidi kuzoea mazingira ya upweke. Sikujua ni kwanini nilikuwa na huzuni kubwa sana kwa kipindi hicho tofauti sana na ilivyo kuwa akisafiri nchi za afrika. Nilivua nguo zangu zote na kujitupa kitandani, usingizi fofofo ulinipitia.

 Ila nilivyo kuwa katikati ya usingizi, nilistukia kitu kikinipapasa kwenye makalio yangu, nikastuka na kufumbua macho yangu, hapo ndipo nilipo mkuta Godfrey akiwa nyuma kitandani, akinipapasa na mikono yake. Nilijitahidi kumuomba asifanye kitu chochote, ila kwa ushawishi namaneno yake matamu aliweza kunishawishi na kujikuta nikifanya naye mapenzi, huku akiahidi kwamba itakuwa ni siri kubwa kati yangu mimi na yeye.
 
Ila mapenzi yalizidi kukua siku hadi siku, hapo ndipo nilipo kuja kuhisi kwamba ninaujauzito, ambao ulianza kuniumiza kichwa changu. Ila nikiwa katika kipindi hicho kwabahati nzuri nilibahatika kupata mawasiliano na Godwin, niliweza kumuelelea juu ya hali yangu kwamba mimi ni mjamzito. Kusema ukweli Godwin alishangilia na kuwa ni mtu mwenye furaha kusikia kwamba mimi ni mjamzito. Na kwakipindi chote alikuwa akiniambia kwamba anafanya mpango aweze kupata japo likizo ya wiki moja ili aje kuniona nikiwa katika hali yangu ya ujauzito
 
“Hiyo ni mimba yangu na si ya Godwin”
Godfrey alinitishi, kwamba ujauzito ni wakwangu, na nikikataa kwamba si wakwake, atakuja kusema ukweli kwa kaka yake, ambaye siku zote walipendana sana na sikupenda siku hata moja kuja kuwachonganisha Godwin na Godfrey. Nilimueleza ukweli baba yangu, ambaye alisha nifanyia mpango wa mimi kuingia serikalini na kuwa kiongozi mkubwa. 

Baba yangu alichukizwa na Godfrey kunifanyia hivyo, ndipo alipo anza kusuka mpango wa kumuangamiza Godfrey, ili siri isivuje nje kwamba nilikuwa na mahusiano naye. Siku ninapata uchungu wa mimba yako Eddy, Ndipo siku Godwin alipo fika nyumbani na kunikuta katika hali hiyo, huku Gofrey alikuwa hayupo nyumbani amekwenda kwenye mishe mishe zake. Godwin hakubadili hata nguo zake za jeshi, alinipeleka hospitalini ambapo ninashukuru Mungu niliweza kubahatika kujifungua salama na kukupata wewe.
 
Godwin alifurahi sana kwani wewe na yeye mulifanana sana, hapakuwa na mtu ambaye aliweza kutofautisha kufanana kwenu, Moyoni nikapata amani kwamba mtoto amefanana na baba yake.
 
Vitisho vya Godfrey vilizidi kupamba moto, hai ikafikia hatua kwamba ikanilazimu kuanza kuufanya mpango wa kuweza kumuu, ili siri ibaki kuwa pale pale. Niliingia serikalini na kuwa mbunge wa viti maalimu, Mwaka mmoja nikiwa kama mbunge wa viti maalumu  babu yako Mzee Eddy alifariki kwa ajali ya gari akitokea kazini. Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwangu, kipindi hicho Godwin alikuwa amerudi  Pakistani kuendelea na kazi waliyo itiwa kule.
 
   Godfrey alinipa kitisho kwamba ataweka kila kitu wazi kwenye mazishi ya kumuaga baba yangu, hapo ndipo nilipo tumia nguvu ya ziada ya kuwatuma watu ambao walimteka Godfrey na kumtesa sana, Nilimpa nafasi ya moja, aweze kuondoka nchini, la sivyo nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe, ili siri yangu ibaki pale pale. 
 
Ulizidi kukua na kuwa ni mtoto mzuri, uliye weza kupata marafiki wengi wakubwa, kwawatoto ulikuwa ni kivutio kizuri machoni mwa wengi, ulipo fikisha miaka mitatu uliweza kupata mkataba katika kampuni moja ya waingereza inayo tengeneza nguo za watoto, na walikutumia wewe kama njia ya matangazo kwa kuzitangaza nguo zao. Baba yako alipo rudi, hakuhitaji kusikia kwamba unaendelea kufanya hivyo. Alijaribu kumtafuta pacha wake ili kuweza kujua kwamba yupo wapi, ila hakufanikiwa, kwani nilimuambia aliondoka kwa kipindi kirefu na sikuweza kumpata.
 
Miaka mingi ilipita, hapo ndipo Godwin alipo kuja kugundua kwamba mimi nilihusika katika mauji ya mdogo wake, Na pia akahisi kwamba wewe si mwanae ni damu ya mdogo wake, hapo ndipo alipo anza kufanya visasi vya kutaka kukua wewe na mimi kwani alijiapiza kwamba asinge hitaji kuona mimi ninaendelea kuishi, wala wewe kuishi kwani alihitaji akuue ili amsahau mdohgo wake
 
          **
    Mama Eddy alimaliza kuzungumza historia fupi iliyo mfanya Eddy kumwagikwa na machozi, kwani kosa hakuwa nalo Mzee Godwin, kuso kubwa lipo kwa mama yake
“Eddy am sorry”(Eddy samahani)
Mama Eddy alizungumza huku akijaribu kumshika mkono Eddy, ambaye aliusogeza pembeni kwani hakuhitaji
“Mama you’re a killer”(Mama wewe ni muaji)
Eddy alizungumza kwa hasira huku akishuka kwenye gari, kwa hasira na kumuacha mama yake akiendelea kulia kwa uchungu.
                                 

     SORRY MADAM (12)  (Destination of my enemies)

Eddy akatoka na kutembea kwa hasira hadi nje ya geti na kuvuka barabara na kutafuta sehemu iliyo tulia na kukaa hapo, ili hasira iweze kumshuka, hakuamini kwamba makosa ya mama yake yamesababisaha matatizo makubwa makubwa kwenye maisha yao.
Baadhi ya watu walio kuwa kwenye eneo hilo, hawakusita kumtazama Eddy ambaye wanamfahamu kama waziri wa ulinzi, hawakujuwa ni kwani yupo pale kwa wakati huu.
 
          ***
Junio akiwa pembezoni mwa kitanda cha mama yake, akijitahidi kumfanyia maombi kwa Mungu, ili aweze kupona. Akahisi kukanyaga kitu kigumu chini ya uvungu wa kitanda, akainama taratibu na kuchungulia kuona ni kitu gani kilichopo chini ya uvungu wa kitanda hicho. 

Akakuta bastola ikiwa ipo chini ya kitanda alicho lalia mama yake. Akaichukua na kuitazama vizuri, hakuwa mgeni sana kuona silaha hiyo, kwani kwa mikiki mikiki aliyo pitia kwenye maisha yake, milio ya risasi kwake ilikuwa ni jambo la kawaida japo anaumri mdogo sana. 

Akaitazama vizuri na kunyanyuka, akiwa ameishika mlango wa chumba ukafunguliwa, akaingia bibi yake akiwa na macho mekundu akionekana kama ametoka kulia muda si mrefu
“Juniooo”
Mama Eddy aliita kwa sauti ya juu, huku aliyo mfanya Junio kushangaa kwanini bibi yake anamuita kwa sauti hiyo. Bibi yake akapiga hatua hadi sehemu alipo simama na kumpokonya bastola hiyo
 
“Umeitoa wapi hii?”
Mama Eddy alimuuliza kwa sauti ya ukali
“Hapo chini ya kitanda”
Junio alijibu kwa sauti ya uoga kwani hakuwahi kumuona bibi yake akiwa katika hali ya kukasirika kama hiyo, Mama Eddy alipo gundua, kuna hali ya hofu kwa mjukuu yake kipenzi anaye mpenda kuliko kitu chochote, taratibu  akapiga magoti na kumkumbatia mjuu kuu wake
“Nisamehe kwa kukufokea”
Mama Eddy alizungumza huku akiendelea kulia, Junio hadi muda huu hakuelewa ni kitu gani kinacho endelea kwa bibi yake
 
“Baba yupo wapi?”
Junio aluuliza kwa wasiwasi mwingi huku akimtazama bibi yake
“Yupo nje ya geti”
“Anafanyaje?”
Mama Eddy hakujibu chochote zaidi ya kuangua kilio kilicho changanyikana na uchungu mwingi. Mama Eddy akaiokota bastola yake na kujiwekea kichwani huku akimuachia mjukuu wake
“Bibi…..!!!”
Junio aliita huku machozi yakimwagika, kwani anatambua kwamba bibi yake kuna kuti kinamsumbua hadi anafikia hatua ya kutka kujiua
“Nenda kamuite baba”
Junio kwa kuchanganyikiwa akachomoka kwa haraka na kuanza kukimbilia nje ya geti
 
     ***   
    Sifa za uzuri wa Shamsa, zikaanza kuenea katika chuo kizima, huku vijana wakiume wanao jihisi wao niwazuri hawakucheza mbali na Shamsa, ambaye tangu afike chuoni hapo, alibahatika kupata rafiki mmoja wa kike ambaye anaishi naye chumba kimoja, uzuri wa rafiki yake huyo ni kwamba wapo darasa moja, na rafiki yake anaifahamu vizuri lugha ya kiswahili. 
 
“Habari”
Suuti ya kiume ya kijana mmoja wa kihindi ilimsalimia Shamsa, mara baada ya kukaa kwenye kiti chake darasani, akageuka na kumtazama kijana huyo ambaye anaonekana kuwa ni mgeni machoni mwake na ndani ya darasa hilo. Uzuri zaidi kijana huyo amemsehemsha kwa lugha ya kiswahili.
 
“Salama tu vipi?”
“Safi, naitwa Ajay Khan, wewe ni Shamsa?”
“Umelijuaje jina langu?”
“Chuo kizima umakuwa maarufu kwa uzuri wako?”
Ajay Khan alizungumza na kumfanya Sahmsa kutabasamu, na ukitazama ni kweli, japo vijana wengi kwenye chuo hicho cha udaktari wao ni wahindi halisi, ila yeye kwa bahati nzuri aliweza kuchanganyia na muafrika na kumfanya uzuri wake uwe maradufu, huku vijana wengi wakimtamani kimapenzi
 
“Asante”
“Sijui ninaweza kupata nafasi ya kuzungumza na wewe?”
“Kwanza umejua vipi kiswahili?”
“Ahaaa mimi ninandugu, Tanzania, maeneo ya Kariakoo pale kuna maduka ya baba zangu wadogo na nimeishi Tanzania kwa miaka kama mitano hivi”
“Ahaa kumbe unapajua Tanzania?”
Shamsa, alizidi kujisikia furaha kwa kumpata rafiki mwengine anaye itambua lugha ya kiswahili, kabla hajamjibu Ajay Khan, profesa akingia darasani kwa ajili ya kuwafunidisha kushusiana na somo la mifupa
 
“Tutazungumza baadae”
Ajay Khan alizungumza kwa sauti ya chini, huku akifungua vitabu vyake na kumfanya Shamsa aachie tabasamu pana lililo mfanya azidi kuonekana kuwa yeye ni msichana nzuri na wakuvutia sana. Baada ya kipindi hicho, kwisha, Shamsa akaingiza vitabu vyake kwenye begi lake la mgongoni na kutoka nje ya darasa, huku kila mwanafunzi akiondoka zake, kwani ni muda wa mapumziko
“Shamsa Shamsa”
Ajay Khan aliita kwa sauti ya juu, huku akimkimbilia Shamsa. Shamsa akageuka na kumtazama Ajay Khan
 
“Vipi?”
“Nahisi ulisahau kwamba tutazungumza baadae”
“Ohoo samahani, unajua masomo yanabana ukitegemea kwamba wiki ijayo ni mtihani”
“Hakuna kitakacho haribika”
“Ehee niambie?”
“Napenda kukualika leo uje kwenye mechi yetu ya Rugby”
“Wewe ni mchezaji pia?”
“Ndio si unaona misuli hii”
Ajay Khan, akatunisha misuli yake na kuifanya ionekane vizuri, Shamsa akatabasamu
“Ni saa ngapi?”
“Saa kumi jioni”
“Basi nitajitahidi kuja, kwa maana mimi sio mpenzi sana wa michezo hiyo”
“Mmm itabidi uipende tu”
“Sawa nitakuja”
 
Wakaachana kila mmoja akaelekea kwenye mabweni yao, huku Ajay Khna, akianza kuamini kwamba mpango wake wa kumpata mtoto mzuri kama huyo unaanza kufanikiwa katika siku chache zijazo. Muda wa mechi, Shamsa na rafiki yake, Kajol Khapoor, wakeelekea kwenye uwaja ulipo kwenye eneo la chuo, ambao unayumika kwa mchezo wa rugby. Uwanja mzima umejaa wanachuo na watu toka nje ya chuo, kwani ni mechi inayo husisha timu ya chuo chao, pamoja na timu moja ya club, iliyo kuja kuomba kuweza kucheza timu hiyo ya chuo. Shamsa na Kajol wakatafuta sehemu ambayo wanaweza kukaa na kuona vizuri kiwanja hicho kwa juu, wakapata viti viwili, na kukaa huku pembeni yao kukiwa na wanachuo wengine walio valia sare za timu ya chuo chao.
 
“Unajua ni sisi tu hatujavaa sare, na tumekaa sehemu walipo vaa sare wezetu”
Shamsa alizungumza akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa
“Hakuna tatizo kwani wao si wanafunzi kama sisi”
“Mmm haya”
Wachezaji wakaanza kuingia uwanjani, huku makofia yao wakiwa wameyashika mikononi, macho ya Shamsa yakatua kwa Ajay Khan, aliye miongoni mwa wachezaji hao. Akaitazama jezi ya Ajay Khan, kwa nyuma imeandikwa jila AJAY, kwa maandishi makubwa huku namba themanini, ikiwa imeandikwa kwa maanshi makubwa.
 
Ajay Khan, kwa haraka akaanza kupitisha macho yake kwenye majukwaa yaliyopo katika uwanja, akijitahidi kutafuta Shamsa kama amweza kufika kwenye kiwanja hichi. Kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona kwenye mashabiki wa timu yao, huku Shamsa na mwenzake wa pembeni wao wakio ndio hawajavalia jezi za timu yao. Ajay Khnan kwa ishara akambusu Shamsa kisha akavaa kofia lake ambalo mchezo huo unawahitaji kuvaa hivyo ili wasiweze kuumia vicha vyao, kwani ni mchazo unao tumia nguvu sana.
 
“Amekubusu wewe yule kaka?”
“Hapana Kajol hajanibusu mimi”
“Mmmm haya mwaya”
Mchezo ukaanza, kwa kasi kubwa, huku Ajay Khan akionekana kushambulia wapinzani wake, kwa kasi alizo kuwa nazo ziliweza kuwafanya wezake kumpatia mpira, kila mara walipo upata na Ajay Khan, aliweza kuwapita kwa spidi wachezaji wa timu pinzani na mpira kwenda kuuweka mwisho wa mstari ambapo kwa mchezo huo hilo linahesabika ni goli.
 
 Uwanja mzima, ukawa unalitaja jina la Ajay, Ajay. Kila mmoja alimshangilia na kila alipo ushika mpira kila mmoja alitarajia kumuona Ajay akifika kwenye mstari wa mwisho wa wapinzani wao na kuuweka mpira chini na kuhesabu goli. Hali ya Ajay kupanda kiumaarufu, ikapenya moyoni mwa Shamsa na kujikuta akitamani Ajay awe ni mtu wake wa karibu, isitoshe ni mtu ambaye anaifahamu nchi aliyo tokea kwa sasa. 

Ajay akajirusha juu kuunyaka mpira alio rushiwa na mwenzake, Kwa bahati mbaya beki wa timu pinzani kwa nguvu akamrukia na kwakutumia bega lake akampiga tumboni na kuanguka naye chini, na kumfanya Ajay Khan atulie kimya, jambo lililo wafanya mashabiki wote pamoja na Shamsa kukaa kimya na kukodoa macho yao kila mmoja akiamini muanguko wa Ajay Khan umeleta matatizo makubwa kwa Ajay
                                                                                                 ***
    Junio akaanza kuangaza macho yake huku na huku akiwa nje ya geti la hospitali, akimtafuta baba yake ni sehemu gani ambapo yupo. Kwa hahati nzuri akamuona akiwe amesimama kwenye moja ya sehemu iliyopo upande wapili wa barabara
 
Eddy akiwa katika msongamano wa mawazo akifikiria ni nini afanye, breki kali za gari zikamstua na kumfanya ageuke kwa haraka na macho yake kutazama barabarani, ambapo alimshuhudia mwane Junio akiwa katikati ya barabara, huku gari aina ya Verosa, ikiwa imemlanga Junio, aliye shikwa na bumbuazi asijue ni nini afanye.

==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts