Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 5 & 6 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 5 & 6 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Saturday, December 24, 2016 | 5:44:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”   
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya kwa uwoga akaichukua simi yake aliyo kua ameiweka pembeni ya glasi iliyo jaa juisi ya embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya kioo iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa kutetemeka Phidaya akaitafuta namba ya simu ya mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye taratibu akainadika kwenye simu yake na kuipiga namba hiyo.                                                                      

ENDELEA
“Mwanangu Phidaya”
Mzee Godwin alijibu kwa kujiamni, jambo lililo zidi kumchanganya Eddy ambaye mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, kwani uhasama wake na Mzee Godwin ni mkubwa kupita kiasi.
“Nakuomba usifanye chochote kwa mke wangu, nakuomba baba yangu”
“Mmmm leo ndio unajua kwamba mimi ni baba yako?”
 
Mzee Godwin aliendelea kuzungumza kwa dharau jambo lililo zidi kumpagawisha Eddy, kwani umbali kutoka Dododma hadi Dar es Salaam, unachukua muda mwingi sana kuweza kufika mbaya zaidi bado anakipengele cha kumalizia bungeni kuweza kujibu maswali atakayo ulizwa kama waziri wa ulinzi, ambaye amechukua majukumu ya kusimamia sekta zote za jeshi kuanzia polisi hadi jeshhi la kujenga taifa, na wizara ya mambo ya ndani ikatolewa katika usimamizi wa jeshi la polisi na kubaki ikiendelea kusimamia mabo mengi na si jeshi la polisi, ambalo lilihamishiwa kwenye wizara ya ulinzi moja kwa moja
 
“Leo, mke wangu atanipikia chakula kizuriii, kwahiyo usiwe na wasiwasi wowote, wewe endelea kupiga kazi”
Baada ya kuzungumza hivyo mzee Godwin akakata simu, na kuizima kabiasa kisha akamtazama Phidaya ambaye bado anaendelea kutetemeka mwili wake wote kwa woga mwingi ulio mtawala. Madam Mery akatoa kitambaa cheupe kilicho kunywa vizuri ambacho walikipulizia madawa ya kulevya kisha akamkabidhi mzee Godwin.
 
Mzee Godwin akamsogelea Phidaya sehemu alipo na kumziba na kitambaa hicho puani mwake, Phidaya akajitahidi kushindana nguvu na mkono wa mzee Godwin ulio mziba puani ila akajikuta akishindwa, huku nguvu zikianza kumuishia taratibu taratibu hadi akalala fofofo.
 
Mzee Godwin akambeba Phidaya begani na kuingia naye ndani, ambapo wakamlaza kwenye moja ya sofa kubwa walilo likuta hapo sebleni, kisha akaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine kuweza kutafuta funguo ya gari walizo  zikuta zimewekwa sehemu maalu za maegesho. Madam Mery yeye akawa na kazi ya kuchungulia madirishani ili kuweza kuona nje kama kuna mtu anaingia aweze kumstua mzee Godwin ambaye anaendelea kuwajibika na utafutaji wa funguo hizo.
 
Mngurumo wa gari, ukisimama nje, ukamstua Madama Mery aliye kuwa ameketi kwenye sofa, kila mara akitazama tazama saa yake ya mkononi, akihesabu muda jinsi unavyo kwenda. Akasimama kwa haraka na kwenda kuchungulia dirishani, akamuona mtoto mdogo wa kiume akishuka kwenye gari hilo aina ya BMW Z8, huku akiwa ameongozana na mtu anaye onekana kama ni dereva. 

Kwa jinsi mototo huyo anavyo fanana na Eddy moja kwa moja Madam Mery akagundua kwamba huyo ni mtoto wa Eddy. Kwa haraka Madam Mery akapandisha ngazi za kuelekea gorofani, ambapo ndipo alipo Mzee Godwin. Kwa bahati nzuri akakutana na Mzee Godwin akitoka kwenye moja ya chumba akitaka kuelekea kwenye chumba kingine.
 
“Vipi?”
“Kuna watu wanakuja” 
Madam Mery alizungumza huku akihema kwani, alizipandisha ngazi hizo zipatzo thelathini kwa kukimbia
“Kina nani?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitembea kuelekea sehemu ambapo ataweza kuiona seble vizuri. Mzee Godwin akamshuhudia mjukuu wake Junio  akiingia huku nyuma akiwa ameongozana na dereva wa gari aliye mleta. Junio akamkimbilia mama yake aliye lala kwenye sofa na kumrukia kwa lengo la kumstua, ila hakufanikiwa kumstua mama yeka kwani hakuweza kustuka wala kutikisika, jambo lililo mpa wasiwasi mwingi Junio na kumfanya anze kulengwa lengwa namachozi.
 
  ***
    Eddy akajaribu kuipiga tena namba ya Mzee Godwin iliyo toka kumpigia muda mchache ulio pita ila haikupatiokana, wasiwasi mwingi ukazidi kumsumbua Eddy, akajaribu kupiga kwa mara ya pili ila hali ikawa ni ile ile ya kuto kupatikana kwa namba hiyo. Akajaribu kuipiga namba ya mke wake, ikaita pasipo kupokelewa.
“Mungu wangu?”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka ndani ya chumba huku jasho jingi likimwagika mwilini mwake, na kujikuta akifungua vifungo vyote vya shati lake. Eddy akafungua mlango na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu, ya hoteli aliyo fikizia akielekea sehemu  ya mapokezi, kabla hajafika akakutana na askari wake anaye mlinda
“Vipi muheshimiwa”
“Nahitaji kwenda, Dar sasa hivi”
Eddy alizungumza kwa haraka huku akizidi kupiga hatua kuelekea nje ya hotel hiyo kwenda kwenye maegesho ya magari.
 
“Unakwenda kufanya nini muheshimiwa?”
“Mke wangu ametekwa, fanya hivi mpigie simu naibu waziri, mkabidhi mafaili yangu yote na kipindi cha pili yeye ndio atajibu maswali sawa”
“Sawa mkuu”
Eddy akafika kwenye gari lake, na kumkuta dereva akiwa amejilaza.
“Shuka nipishe niendeshe”
Eddy alizungumza na kumfanya dereva wake kustuka kutoka usingizini
“Mmmmm”
“Hujanisikia au, nimekuambia kwamba zunguka upende wapili wa gari, tunahitaji kwenda Dar es Salaam sasa hivi”
“Muheshimiwa ni jukumu langu mimi kukuendesha”
“Wewe mzee, mimi ni nani yako? Nimekuambia nipishe”
Eddy alizungumza kwa hasira na kumfanya mzee Selemani Mbogo, kutii amri ya bosi wake, akashuka kwa haraka na kuzunguka upende wapili wa gari, askari akataka kuingia kwenye gari ila Eddy akamzuia
“Wewe baki, hakikisha document zangu zote unampa naibu waziri sawa?”
“Sawa mkuu”
“Naomba bastola yako”
 
Hapo askari akasita kidogo kuichomoa bastola yake aliyo ichomeka kiunoni mwake, kwa ishara Waziri Eddy akamuomba amkabidhi bastola hiyo, taratibu askari huyo akaichomoa na kumpa bosi wake. Eddy akaipokea na kuifunga mlango wa gari, akaliwasha, akakanyaga mafuta pamoja na breki na kuzifanya tairi za gari hilo kuserereka, na kutoa moshi mwingi, kisha akaachia breki na kulifanya gari hilo kuchoka kwa kasi, na kuwafanya watu wlaiopo katika eneo la hoteli kushangaa.
 
Kwa bahati nzuri, waziri Eddy akafanikiwa kuliingiza gari hilo barabarani, pasipo kuligonga sehemu yoyote. Akawasha taa zote za gari, akishiria kwamba anaomba nafasi kwa kila gari lililopo mbele yake, Safari ikaanza ya kuelekea Dar es Salaam, huku kila muda waziri Eddy akizidi kuongeza mwendo wa gari hilo la serikali aina ya Landcruser VX X8. Maombi ya Mzee Selemani Mbogo, yakwa ni kumuomba Mungu wasiweze kupata ajali kwani, mwendo anao tembelea bosi wake ni mkali sana na endapo itatokea tatizo kidogo inaweza kuwa ni ajlali kubwa, itakayo waponda ponda hadi mifupa yao.
 
Macho ya Mzee Selemani Mbogo aliye kaa siti ya pembeni, mwa Eddy, alishuhudia mlolongo wa gari zipatazo sita zikiwa zimeongozana huku kati ya hizo magari matatu yakiwa ni malori yenye trela, mawili, mawili. Eddy hakujali kwamba wapo kwenye kilima, alicho kifanya yeye ni kuanza kupita gari moja baada ya jengine,huku mshale wa spidi mita ukielekea kwenye spidi miambili na ishiri.
 
Kitendo cha kumaliza kilima hicho mabasi mawili yanayo tokea Dar es Salaam, kwenda Dodoma, yakawa yanakuja kwa kasi upande ambao wamuiba ili kuweza kuyapita magari haya ambayo Eddy alihisi kwamba yanakwenda kwa mwendo mdogo, japo nayo pia yapo kwenye mwendo kasi.
Mzee Selemani Mbogo, akajikuta akiyafumba macho yake, kwani ni mida chache zimebakia kutoka pale walipo na kukutana na mabasi hayo ambayo nayo yapo kwenye mwendo kasi. 

Alicho kifanya Eddy ni kuzidi kuipeleka gari  yake, upande wa kulia, na kutoka kabisa nje ya barabara na kuingia kwenye barabara ya vumbi,na kuyafanya mabasi hayo yapite kwa kasi huku  madereva wake wakipiga honi zao. Yalipo pita magari hayo, akairudisha gari yake ndani ya barabara ya lami, na kuendelea kutembea kwa kasi ile ile, iliyo wafanya maderava wa magari walio pitwa kuishangaa gari hiyo ya serikali ambayo namba zake zionaonyesha ni gari ya waziri wa ulinzi.
“Mmmmmm”
Dereva mmoja wa roli aliguna, huku akiishuhudia gari hiyo, ikipandisha kilima kingine hadi wanashusha ikawa imepotea kwenye uwepo wa macho yao. 
 
“Mzee wewe ni muoga sana eheee?”
Eddy alimuuliza mzee Selemani Mbogo, baada ya kumtazama na kumkuta amefumba macho yake pasipo kuyafungua.
“Eheee….!!”
Mzee Mbogo akakosa jibu zaidi ya kuendelea kushangaa wala hakujua ni jinsi gari, Eddy aliweza kuyakwepa mabasi hayo ambayo walikuwa wagongane nayo uso kwa uso. Kwa mwendo kasi wa gari,alio utumia Eddy, hadi wanafika Morogoro mjini, walitumia masaa mawili na nusu, kuingia kwenye ardhi ya mkoa huo.
Eddy akapunguza mwendo wa gari, kuepuka kugonga baadhi ya wandesha pikipiki waliopo Morogoro mjini, alipo pata nafasi ya kukikiacha kiplefti cha Morogoro mjini, kasi ya gari lake ikaongezeka, tena ikwa ni rahisi sana kwake kutokana barabara hiyo imenyooka sana, na magari yanayokwenda kwenye barabara hiyo mengi yanakwenda kwa kasi
“Nipe lisaa, nitakua nimesha ikanyaga mbezi, na kama hakuna foleni huu mchana hdi lisaa na nusu nitakua nyumbani”
Eddy alimuambia Mzee Mbogo na kumfanya abaki ameduwaa, pasipo kujibu kitu chochote kile.
                                                                                            ***
“Mama, mama mamaaaa”
Junio alimuita mama yake huku anamtingisha, ila mama yake hakustuka kabisa na kumfanya Junio kuanza kulengwa lengwa na machozi.
“Ka Devi mama amekufaaa”
Junio alimuambia dereva wa bibi yake, kwa haraka Devi akamsogelea Phidaya na kumuwekea kiganja cha mkono kwenye kifua chake, mapigo ya moyo akayasikia yakifanya kazi kwa mbali sana, jambo lililo anza kumstua Devi mwenye. Devi akachukua simu yake na kumpigia bosi wake mama Eddy.
“Tunafanyaje sasa?”
Madam Mery aliuliza huku mwili ukimtetemeka,
“Tuwaue wote wawli”
Mzee Godwin alizungumza huku akiikoki bastola yeka.

SORRY MADAM(6) (Destination of my enemies)

“Godwin……!!!”
“Nini?”
“Usiwaue, kwani hawana hatia yoyote”
Madam Mery alizungumza kwa sauti iliyo jaa upole kwani hakuamini kama Godwina atachukua uamuzi huo haswa kwa Junio ambaye fika amefanana naye sana, ikiashiria kwamba hiyo ni damu yao, japo ni Eddy ni mtoto wa mdogo pacha wake.
“Ndio mama, tumefika nyumbani hapa tumekuta mama anamatatizo”
 
Devi alizungumza kupitia simu, huku akizunguka zunguka zunguka sebleni
‘Mpeleke hospitalini’
Sauti ya bibi Junio, ilisikika kwenye simu ya Devi, akizungumza huku akiwa na wasiwasi mwingi
“Sawa muheshimiwa”
Devi akakata simu na kuiweka mfukoni, kisha akarudi kwenye sofa alilo lala Phidaya, akaikunya mikono ya shati lake refu jeupe, kisha akamnyanyua Phidaya aliye mzito kiasi,
 
“Junio fungua mlango”
Devi alizungumza na kumfanya Junio akimbilie mlanoni na kuufungua mlango wa sebleni, wakatoka nje,  Junio akakimbia kwenye gari na kufungua  mlango wa gari, siti za nyumba. Devi akamuingiza Phidaya ndnai ya gari kisha wao wakaingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi pasipo kugundua kwamba ndani ya jumba hilo kulikuwa na watu ambao wamesababisha Phidaya kuwa katika hali kama hiyo.
“Umeona sasa”
 
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti ya ulali akimfokea Madam Mery, aliye mshukuru Mungu kwa upande mmoja, kwani hakuhitaji kuona damu ya mtoto mdogo kama Junio ikimwagika mbele ya macho yake.
“Lakini hilo sio lengo letu lililo sababisha sisi kufika hapa”
“Wewe mwanamke utaniyumbisha kwenye mipango yangu”
Mzee Godwin akafyatua risasi mbili, zilizlo tua kifuani mwa Madam Mery na kumuangusha chini huku akitoa ukelele wa maumivu huku akiwa haamini kwa kile alicho kifanya mpenzi wake huyo
 
“G..ood..win kweli unaniu…a”   
“Kufa pumbavu wewe”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira huku akifungua kiwambo cha kuzuia sauti cha bastola yake, amabyo kulisaidi kuzuia sauti ya risasi mbili alizo mtandika madam Mery zisisikike nje. Mzee Godwin akashuka kwenye ngazi haraka na kutoka nje, akapiga hatua za kasi hadi nje ya geti ambalo lipo wazi. Akatizama pande zote za barabara iliyo tulia hakuona gari lolote, jambo lililo zidi kumchukiza.
“Shiiiitii”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa amechukia sana, akapita mtu wa bodaboda ya pikipiki, akamsimamisha na kumuomba aelekee barabara aliyo hisi, gari alilo pakizwa Phidaya ndipo lilipo kwenda
                                                                                  ***
    Kweli ndani ya masaa mawili, Eddy akaingiza gari lake kwenye geti lake alilo likuta wazi, Wasiwasi mwingi ukamuingia, akashuka ndnai ya gari huku akiwa na bastola aliyo pewa asakri wake. Mzee Selemani Mbogo naye akashuka kwenye gari huku akimfwata Eddy kwa nyuma, wakafika kwenye mlango wakuingilia ndani, tararibu Eddy akausukuma mlango, huku kidole chake kimoja kikiwa kwenye traiga tayari kwa kufyatu risasi kwa yoyote atakaye jaribu kumfanyia shambulizi lolote. Akachungulia ndani, ambapo kidogo kagiza kametawala,
“Muheshimiwa”
 
Mzee Mbogo aliita kwa sauti cha chini, huku akimuonyesha Eddy damu zinazo churuzika kwenye ngazi zikitokea juu gorofani. Eddy kwa hatua za haraka akaanza kutembea kuelekea kwenye ngazi hizo, wasiwasi mwingi, ukamjaa mwili mwake huku akiamini damu hiyo ni yamke wake Phidaya. Akapandishia ngazi kwa haraka hadi juu kabisa. Hakuamini macho yake baada ya kumkuta Madam Mery akiwa amalala kwenye sakafu, huku damu zikiendelea kumwagika kifuani mwake taratibu,
“Huyu bado yupo hai”
Mzee Selemani Mbogo alizungumza baada ya kuishika damu ya madam Mery inayotoka kwenye kifua chake na kukuta bado niyamoto. Eddy akatembea kwa haraka kuelekea kwenye chumba cha Junio lilicho kua wazi, akaingia na kukuta pakiwa pamachanguliwa vibaya.
Akatoka na kuiongia chumba cha Shamsa na kukuta nacho kikiwa kimevurugwa mno, pia hapakuwa na dalili yoyote ya kuwa na mtu
 
“Phidaya, Phidaya”
Eddy aliita kwa sauti ya juu huku akieeleka kwenye chumba chao, akafungua na kukuta kikiwa kimepangwa vizuri na hapakuwa na mtu aliye pakanyaga humo ndani. Akarudi sehemu alipo Madam Merya na kukuta mzee selemani Mbogo, akimpa huduma ya kwanza Madam Mery
Eddy akaitoa simu yake mfukoni na kukuta ikiwa imezima, akaiwasha na kukuta ikiwa imepungukiwa na chaji, Mfululizo wa meseji zikaingia kwenye simya yeka, huku nyingi zikiwa ni zamama yake.
(MKEO YUPO OCEA ROAD HOSPITAL, FANYA UFIKE HARAKA)
Eddy kuisoma meseji hiyo, kidogo ikampa nguvu hata ya kusaidia na mzee Selemani Mbogo kumbeba Madam Mery ambaye hadi sasa hivi maisha yake, yapo hatarini kupotea kwani ni damu nyingi zimemtoka mwilini mwake.
“Endesha”
 
Eddy alimuambia Mzee Selemani, huku yeye akipanda siti ya nyuma walipo mlaza Madam Mery, huku kicha cha Madam Mery akikiweka mapajani mwake, na kiganya cha mkono wake wakulia akikiweka kwenye kifua cha madam Mery ili damu isiendelee kumwagika. Wakaondoka na kwenda hadi Hospitali ya Ocean Road, ambapo, wakaomba masaada kwa manesi, ambao wakampakiza Madam Mery kwenye kitanda cha kusukuma na matairi. Moja kwa moja wakamkimbizi Madam Mery kwenye chumba cha upasuaji, ili kuweza kutoa risasi
“Eddy Eddy”
Eddy akageuka nyuma na kukutana na mama yake akiwa amejifunga kitenge kiunoni mwake, huku akijifuta kwa jasho
“Mama vipi, mke wangu yupo wapi?”
“Yupo chumba cha wagonjwa mahututi, hali yake sio nzuri kabisa”
Eddy akaondoka na mama yake huku wakiwa wameongoza, wakitembea kwa kasi kwenye kordo ya hospitali hiyo kutazama hali ya mke wake.
“Chumba hichi”
 
Mama yake alizungumza huku akiusukuma mlango wa chumba hicho, na kuingia ndani. Akamkuta Junio akiwa pembeni ya kitanda, huku akiwa analia sana. Phidaya kwa wakati huo aliwekewa mashine za kumsaidia kupumu, huku pembei kukiwa na mashine za kuhesabu mapigi ya moyo wake unavyo dunda kwa kila dakika. Junio akamkimbila baba yake na kumkumbatia huku akimwagika na machozi mengi.
“Dady, mama anakufaaaa”
Junio alizungumza huku machozi yakimwagika, jambo lililo zidi kumtia uchungu Eddy
“Noo, tumuombee mama, hawezi kufariki”
Eddy alizungumza kwa kujikaza tu, ili kumfariji mwane na asiyaruhusu machozi yake kutoka mbele ya mwanae huyo
“Dokta yupo wapi?”
“Nilikuwa naye ofisini kwake, pale nilikuwa ninatoka ofisini kwake, ndio nikakuona”
“Anasemaje?”
“Hajanipa jibu la kuelekewa”
“Baki na mtoto”
Eddy akafungua mlango na kutoka ndani ya chumba hichi alicho lazwa mke wake. Moja kwa moja akaongoza hadi kwenye ofisi ya dokta, aliye elekezwa na mama yake ndio aliye muhudumia mke wake baada ya kufikishwa hapo hospitalini.
 
“Karibu muheshimiwa”
Daktari huyo mwenye asili ya kihindi alishtuka mara baada ya kumuona Eddy ameingia ndani ya ofisi yake huku sura yake ikiwa imepoteza furaha.
“Mke wangu amepatwa na nini?”
“Kaa basi chini muheshimiwa Waziri”
Eddy akamtazama daktari huyo kwa mamcho makali yaliyo jaa uchungu, kisha akaka kwenye kiti alicho omba kukaa na dokta huyo.
“Mke wangu anatatizo gani?”
“Tumemfanyia uchunguzi mke wangu na kugundua kwamba, amevuta sumu kali sana ambayo laiti kama angechelewa kuletwa hospitalini basi, angefarki. Tumemuwekea tripu za maji, ili kuweza kuisafisha sumu hiyo ambayo inakimbilia kuua kiumbe kilichopo tumboni”
“Do…do…do…kta ii…iiinamaana mke wangu…. Ni mjamzito”
“Ndio, na kiumbe endapo kitavuta sumu hiyo basi kitaweza kutoka kabla ya siku zake”
                                                                                          ***
    Katika pita pita zake, huku akijilaumu moyoni mwake ni kwanini hajafanikisha adhima ya kumuua mke wa mwanae, kwasababu ya Madam Mery aliye mzubaisha hadi mwanamke huyo akachukuliwa. Pikipiki iliyo mpakiza ya bodaboda aliye mkodisha tangu asubuhi, ikaisha mafuta mbele ya hospitali ya Ocean Road
“Ohhh samahani mzee wangu pikipiki kidogo imekata mafuta”
 
“Wewe kijana mbona mzembe sana, utaendeshaje pikipiki hadi inakuzimikia kwa mafuta”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti ya kufoka sana
“Samahani sana mzee wangu”
“Pumbuvu sana wewe kijana”
Mzee Godwin alizunumza huku akizunguka zunguka, kwa bahati nzuri macho yake yakamshuhudia mke wake Mama Eddy akitoka nje ya hospitali hiyo, huku simu yake ikiwa sikioni akionekana anazungumza natu
“Unanidai shilling ngap?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitoa pochi yake mfukoni, huku macho yake yote yakiwa kwa mama Eddy.
“Elfu hamsini”
Akachomoa noti tano za elfu kumi kumi, nakumkabidhi dereva bodaboda pasipo kumtazama, kisha akaanza kupiga hatua kuelekea alipo Mama Eddy, huku taratibu hasira kali dhidi ya mke wake huyu ikiongezeka na kujikuta akiichomoa bastola yake tayari kwa kumpiga risasi.

==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com      
 
  

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts