Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 7 & 8 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 7 & 8 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Monday, December 26, 2016 | 8:46:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA   
“Unanidai shilling ngap?”   
Mzee Godwin alizungumza huku akitoa pochi yake mfukoni, huku macho yake yote yakiwa kwa mama Eddy.
“Elfu hamsini”
Akachomoa noti tano za elfu kumi kumi, nakumkabidhi dereva bodaboda pasipo kumtazama, kisha akaanza kupiga hatua kuelekea alipo Mama Eddy, huku taratibu hasira kali dhidi ya mke wake huyu ikiongezeka na kujikuta akiichomoa bastola yake tayari kwa kumpiga risasi.

ENDELEA
    Mama Eddy baada ya kuzungumza na simu, akaingia ndani ya hospitali na kumfanya Mzee Godwin kusimama kwenye moja ta gari lililo egeshwa kwenye maeneo haya huku macho yake akimsindikiza mke wake huyo, ambaye alimshuhudia akizungumza na Eddy kisha wakaondoka
“Eddy Eddy Eddy”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa amekasirika, tukio kubwa linalo muuliza kichani mwake ni pale anapovuta picha jinsi pacha mwenzake alivyo kuwa akifanya mapenzi na mke wake huyo, jambo linalomfanya kuzidi kumchukia Eddy
 
“Nitakuua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwashuhudia Eddy na mama yake wakitoka tena nje ya hospitali huku wakiwa na Junio, aliye bebwa mikononi mwa Eddy akionekana kupitiwa na usingizi. Gari la mama Eddy likafika sehemu walipo simama huku kukiwa na dereva ndani yake.
 
“Nitakuja basi asubuhi, kumuona mgonjwa. Ngoja nikamlaze huyu chekbud wako”
“Sawa mama, usisahau kuja na chakula”
“Sawa nitakiandaa mimi mwenyewe”
Mama Eddy akaingia siti ya nyuma alipo lazwa Junio aliye jichokea kwa usingizi.
“Mama kumbuka hajala huyo akifika ale”
Eddy alizungumza huku gari la mama yake likiondoka taratibu, Eddy akalisindikiza kwa macho gari hilo hadi linatoka kwenye geti, Macho ya Eddy yakashuhudia mtu akiwa amejibanza kwenye moja ya gari huku akionekana kama anachunguza kitu fulani, kutokana na mwanga hafifu ya eneo la maegesho hakuweza kumuona sura yake.
Eddy akataka kwenda ndani ila roho yake ikasita kabisa na kujikuta akianza kupiga hatua za taratibu kwenda sehemu lilipo gari hilo. Mzee Godwin akatabasamu, alipo kua anamuona Eddy akija katika eneo alipo jificha yeye. Akaishika bastola yake huku akimsubiria kwa hamu kubwa, Eddy afike ili amuulie mbali
Gafla simu ya Eddy ikaita na kumfanya asimame na kuitoa mfukoni mwake, na kukuta ni namba ya spika wa bunge, akaitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akaipokea
 
“Ndio kiongozi habari”
Eddy akuzungumza huku akitazama pembeni upande ambapo hayupo mtu aliye hitaji kumuona ni nani na kwanini anajificha
“Salama vipi, mbona umekimbia bila taarifa?”
“Kuna matatizo yakifamilia ilinibidi niwahi kuyatatua”
“Kwema lakini?”
“Hapana si kwema kiongozi, kwani mke wangu alivamiwa na majambazi na kumuwekea sumu, pia nikakuta mwili mwengine wa rafiki wa karibu ukiwa ndani ya nyumba yangu, naye akiwa amepigwa risasi”
“Aisee, basi mimi nilijua kwamba umekimbia maswali”
“Hapana kiongozi”
 
“Pole sana, vipi polisi umewataarifu?”
“Bado, ila hili swala nitalimaliza kimya kimya”
“Basi kama ni hivyo, ila nikusifie kwa vidonge vyako vya leo, Umeniburudisha japo nilikuwa ninajikaza”
“Ni moja ya kazi yangu”
“Basi endelea na majukumu ukiwa saswa utaniambia”
“Sawa kiongozi”
Eddy akakata simu na kuzunguka sehemu alipo hisi kuna mtu, ila hakukuta mtu yoyote aliyepo kwenye eneo hilo. Kumbe kitendo cha Eddy kuzungumza na simu, ikawa ni nafasi kubwa sana kwa Mzee Godwin kutembea kwa hatua za haraka na kuingia kwenye jembo moja la kuhifadhia nguo, ikiwemo mashuka, neti, na mavazi ya kidaktari
 
“Kumbe huyu mwanamke hajafaa, nilazima nimuue”
Mzee Godwin alizungumza baada ya kumsikia Eddy akidai kwamba Madam Mery hajafa. Mzee Godwin akavaa moja ya koti la kidaktari akachukua na kipimo cha kupimia mapigo ya moyo, kisha kwa haraka akaanza kupita wodi moja baada ya nyingine ya wagonjwa mahututi
 
    Halikuwa ni jambo la kustukiwa mara moja kwamba yeye sio dokta, hii nikutokana na wingi wa wafanya kazi katika hospitali hii, huku wengine wakiwa wameingia zamu ya usiku wakiwapokeza wezao walio fanya kazi kutwa nzima. Eddy akapiga namba za Mzee Seleman aliye kuwa akisimamia ufanyiwaji wa oparesheni wa Madam Mery kutolewa risasi
“Ndio bosi”
“Hali ya mgonjwa inaendeleaje?”
Eddy alizungumza huku akiingia ndani, kuelekea kwenye chumba alicho lazwa mke wake
“Bado madaktari wanaendelea kuzitoa risasi, nipo kwa nje hapa ninachungulia kwenye kioo cha mlangi
“Sawa hakikisha haumruhusu mtu kuwa karibu ya mgonjwa zaidi ya madaktari, au nikuongezee nguvu ya ziada?”
 
“Hapana”
“Sawa fanya hivyo”
Eddy baada ya kumaliza kuzungumza na mzee Selemani Mbogo, simu yake ikazima chaji kabisa na kujikuta akiidumbukiza mfukoni mwake. Eddy akafika kwenye chumba alicholazwa Phidaya, akaingia na kukaa pembeni ya kitanda cha mke wake na kuanza kumtazama usoni mwake, na kuanza kufikiria ni kitu gani ambacho anaweza kumfanya Mzee Godwin pale atakapo mtia mikononi
“Sasa huyu mzee amevuka mipaka kwa sasa, nitamuua kimya kimya”
Eddy alizungumza kwa sauti ya chini kabisa huku akiendelea kumtaza mke wake kwa macho ya masikitiko. Taratibu akamshika mkono mke wake ambao haujachomwa sindano ya dripu, taratibu akaubusu kisha akakanyanyuka na kuanza kupiga hatua taratibu za kuelelea kwenye mlango
 
Mzee Godwin akajaribu kupitia kila wodi ya wagonjwa mahututi ila hakufanikiwa kumuona Madam Mery, ambaye kwa wakatii huu yupo katika chumba cha upasuliwaji. Akajikuta akiwa amesimama nje ya moja ya chumba huku macho yake yakitazama sehemu anapo tokea upande wa kushoto kwenye kordo ndefu sana, huku akiendelea kujiuliza ni wapi alipo Madam Mery ambaye anaweza kufichua mipango yake ambayo ameipanga. Simu yake ikaita kutazama akakauta ni namba ambayo anawasiliana nayo sana.
 
“Bosi kuna watu nimewapata”
Sauti hiyo ya kiume inayo kwaruza kwaruza kwenye simu, ilisikika vizuri masikioni mwa mzee Godwim
“Wapo wangapi?”
“Wanne, na inavyo onekanani ni watu wenye uchungu sana na kazi, ila ni wanawake”
“Wanawake, hivi mwanamke kweli tunaweza kufanya naye kazi?”
Mzee Godwin alizungumza huku akipiga hatua kusogea pembeni kidogo mwa chumba hicho kilicho
“Bosi niamini hakuna litakalo haribika, kila kitu nimekiweka kwenye mpango sawia”
“Basi fanya hivyo nahitaji kuonana na hao watu”
“Inabidi uje huku nilipo, si unajua afya yangu ilivyo”
“Sawa, nitawasiliana nawe”
 
Eddy akafungua mlango na kutoa nje chumba chake, hakumtazama daktari aliye mpa mgongo huku akioenekana akiminya minya simu yake. Eddy akaelekea upande wa kulia ambapo kuna duka la hospitali, nia yake kubwa ni kwenda kununu maji. Mzee Godwin alipo geuka na kumtazama mtu aliye toka kwenye chumba hicho, akamshuhudia Eddy akizidi kutokomea kwenye kordo hiyo ndefu akielekea upande wa kulia.
 
Mzee Godwin akageuka na kukitazama chumbu hichi, akagundua ni chumba nacho cha wagonjwa mahututi, akatazama pande zote mbili za kordo, hakuona mtu anaye mfwatilia, akashika kitasa cha mlango na kuingia ndani ya chumba hicho. Mzee Godwin hakutegemea kumkuta mkwe wake akiwa kwenye kitanda kilicho zungukwa na mitambo ya kumsaidia kuhema, huku akionekana kuwa ni mfu mtarajiwa.
 
“Waooooooo”
Mzee Godwin alizungumza huku akipiga hatua akielekea kwenye kitanda alicho lala Phidaya, kama kawaida yake akaanza kumchezea nywele zake ambazo ni ndefu. Taratibu akaichomoa bastola yeke na kukikaza vizuri kiwambo cha kuzuia sauti na kuisogeza taratibu kwenye paji la uso wa Phidaya, aliye lala fofofo bila hata kujitambua, Kabla hajafanya chochote, macho ya Mzee Godwin yakatua kwenye kifua cha Phidaya, akazishuhudia chuchu za Phidaya zilizo tengeneza bonde zuri katikati, taratibu akajikuta akiupeleka mkono wake wa kushoto kifua cha Phidaya na kuuingiza kwenye nguo aliyo ivaa, na kuanza kushika chuchu zake taratibu huku akiziminya minya kwa hisia kali sana.
 
Mwili wa Mzee Godwin ukaanza kusisimka, na kujikuta bastola yake akiiweka pembeni ya kitanda, kisha kwa mkono yake miwili akaanza kufungua vifungo vya shati la Phidaya na kuziacha chuchu zake waze wazi, taratibu akapiga magoti chini, na kuanza kunyonyoa moja baada ya nyingine, huku kichwa chake kikiwa kimesahau ni kitu gani anacho kifanya na kitamletea madhara gani
 
    Eddy akafika kwenye duka la hospitali ambapo, akatoa pesa na kununua maji makubwa ya baridi pamoja na biskuti. Akamuomba muhudumu wa duka kukaa na chenchi hiyo, kwani asubuhi atarudi kununua baadhi ya mahitaji kama dawa ya mswali na mswaki wenyewe. Akaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida akirudi kwenye chumba alichopo mke wake kwani hakuhitaji kukaa mbali sana na mke wake, laiti angejuwa wala asinge dhubutu kuendelea kutembea kwa mwendo huo
 
Mzee Godwin akazidi kunogewa na kujikuta akiuingiza mkono wake mmoja kwenye suruali yake na kuanza kuchezea uume wake, huku akitoa miguno ya raha. Eddy akazidi kuukaribia mlango wa chumba alicho lazwa mke wake, huku akiwa hajui hili wale lile. Mzee Godwin naye akazidi kuzinyonyo chuchu za Phidaya, kiasi kwamba hadi zikaanza kubadilika rangi na kuweka uwekundu fulani
Eddy akafika mlangoni kabla hajashika kitasa akamuona Mzee Seleman akija kwa kasi, huku anakimbia akimfwata yeye ikamlazimu kusimama na kumsubiria amsikilize ni kitu gani anahitaji kuambiwa.
 
“Muheshimiwa, muheshimiwa”
Mzee Selemani aliita huku akiwa anahema kama amekimbizwa na mbwa wakali sana walio simama na kumuacha aende zake
“Vipi?”   
“Mgonjwa mgonjwa anakuita anataka kuzungumza na wewe”
Mzee Selemani Mbogo alizungumza huku akihema sana, hadi akawa anarudia baadhi ya maneno anayo yazungumza.
“Basi ngoja niweke vitu ndani, twende pamoja”
“Muheshimiwa wewe twende kwani hali yake ni mbaya, anasema kuna siri anahitaji kukuambia wewe”
 
SORRY MADAM (8)   (Destination of my enemies)
  
“Mmmmm”
Eddy akaguna na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye alipo lazwa Madam Mery. Mzee Godwin akamtoa Phidaya mashine ya kumsaidia kupumua, na kuanza kumnyonya mdomo wake, kwa papara na hamu ya kumuingilia kimwili mkwewe kwa bahati mbaya akatingisha meza iliyo jirani na kitanda, na kulifanya jagi la kioo lililo kuwa mezani hapo kuanguka chini na kupasuka.
 
Gafla Eddy akasimama, baada ya kusikia mlio wa kitu cha kioo kikipasuka kikitokea kwnye chumba alicholazwa Phidaya. Eddy akageuka na kutazama nyuma kuangalia mlango wa chumba hicho ulipo mbali kidogo kutoka katika sehemu walipo simama.
‘Nenda kamuone Madam Mery’
‘Nenda katazame kuna nini kwenye chumba cha mke wako’
Ni sauti mbili zilizo kua zikiendelea kubishana kwenye akili ya Eddy.
 
“Muheshimiwa twende”
Mzee Selemani Mbogo alimsisitizia waziri Eddy waendelea na safari hiyo ambayo ni muhimu sana kwao kuweza kwenda. Taratibu Eddy akataka kupiga hatua kuelekea anapo seme Mzee Mbogo, ila akajikuta mzito sana kuendelea na safari hiyo, kwa hatua za haraka haraka zilizo changanyika kila alipo zipiga, zikamfanya Eddy aweze kukimbia kuelekea kilipo chumba alicho lazwa mke wake Phidaya.
 
Mzee Godwin alilitazama jagi lililo pasuka, na kulipotezea, akaushusha mdomo wake kwa mara nyingine kwenye chuchu za Phidaya. Zilizo kaa vizuri kana kwamba binti mdogo anaye anza kuvunja ungo na huwezi kuamni kwamba anamtoto wa miaka mitano. 

Pumzi nzito za kimahaba zikazidi kumtoka mzee Godwin na kujikuta akiushusha mkono wake mmoja hadi sehemu za siri za Phidaya. Ugumu alio ukuta ni skintait aliyo ivaa Phidaya pamoja na chupi, vilivyo mfanya mzee Godwin, kujikuta akiulazimisha mkono wake kuingia kwenye nguo hizo za ndani. 
 
Gafla mlango ukafunguliwa na kujibamiza, macho ya Mzee Godwin yakatua kwenye sura ya Eddy aliye yatumbua macho yake, huku akionekena kutetemeka kwa hasira kali, aliyo nayo. Kufumba na kufumbua mzee Godwin akajikuta akiona nyota nyota kwenye macho yake, hii ni baada ya Eddy kukimbia kwa kasi hadi sehemu alipo piga magoti na kumtandika ngumi nzito ya uso, iliyo muangusha chini, kabla hata Mzee Godwin hajafanya chochote, kutafuta ni wapi alipo iweka bastola yake akastukia akinyanyuliwa na kutandikwa kichwa kikali cha pua kilicho zidi kuifanya pua yake kumwagika na damu nyini na kuzidi kumchanganya Mzee Godwin. 

Eddy hakujua nguvu alizo nazo zilitokea wapi kwani, alimshika mzee Godwin na kumuweka begani mwake na kunyanyua kuu kisha akambwaga chini mithili watu wanao pigana myereka.
 
Mzee Selemani  Mbogo akaingia ndani ya chumba alicho ingia bosi wake na kumkuta akiwa anamshindilia ngumi mwanaume ambaye alisha wahi kipindi cha nyuma, akiwa ni mkuu wa jeshi la ulinzi JWTZ.
 
“Muheshimiwa muheshimiwa”
Mzee Mbogo aliita huku akijitahidi kumshika Eddy mabegani na kumnyanyua ili asiendelee kumkandamiza ngumi mzee huyo. Haikuwa kazi rahisi kwa mzee Selemani Mbogo, kwani misuli iliyo kaza ya Eddy ilimpa ugumu wa kuweza kuendelea kumuamua asiendelee kumshambulia mzee huyo.
 
“Hhaaahahaaa”
Mzee Godwin alicheka kila konde alilo pigwa na mwanaye, Eddy akazidi kuendelea kufanya mashambulizi kwa mzee Godwin, ila gafla mambo yakabadilika kwani Mzee Godwin aliweza kuidaka ngumi ya Eddy iliyo kuwa ikielekea kumpiga kwenye uso wake. Mzee Mbogo ikabidi atoke kasi kwenda kuomba msaada kwa askari wanao linda kwenye hospitali hii. 

Mzee Godwin, akamzungusha Eddy aliye kuwa amemkalia kwenye tumbo lake, akambwaga chini na yeye akawa juu, akashusha makonde mawili ya nguvu yaliyo tua kwenye mikono ya Eddy aliye kinga kichwa chake kisiweze kupigwa na makonde hayo mazito. 

Eddy akajitutumua na kujaribu kumrudisha chini Mzee Godwin ila hakuweza kwani aliweza kuzidiwa nguvu na baba yake huyo, aliye jazia kwa misuli na nimkakamavu kutokana na kazi yake ya jeshi aliyo kuwa akiifanya kwa takribani miaka thelethini na tano, kabla hajapotea kwa kuhofia kukamatwa baada ya kusadikika yeye ndiye aliye mteka mke wake ambaye alikuwa ndio waziri mkuu.
 
Mzee Godwin akamnyanyua Eddy na kumrushia kwenye kitanda alicho lala Phidaya asiye jielewa, Eddy akajitahidi kwa uwezo wake wote asitue kwenye mwili wa mke wake na kujikuta akiangukia upande wapili wakitanda na kuangukia bega. Mzee Godwin akaichukua bastola yeka kabla hajamfyatulia risasi Eddy askari wawili wakaingia ndani ya chumba hichi, askari wakaonekana kustushwa na kukutana na mdomo mdogo wa bastola ukiwa umewaelekea wao.
 
Eddy akajaribu kunyanyuka ili kuitoa bastola yake aliyo ichomeka nyuma kwenye mkanda wake, ila maumivu ya bega la mkono wakulia yakamfanya ashindwe kufanya hivyo, akajaribu kuupeleka mkono wakulia ukakubali kufika sehemu alipo ichomeka bastola yake, ila kwabahati mbaya hakuikutwa na hakujua ni wapi ilipo angukia. Kwa aishara Mzee Godwin, akawaamrisha askari hao kusogea mlangoni nao wakatii kutokana hawakuwa na silaha yoyote, wao walihisi ni ugomvi mdogo wakuwatenganisha watu walio ambiwa wanagombana.
 
Kitanda kikaanza kutingishika, Eddy alipo mtazama mke wake akamkuta akiwa anarusha rusha miguu kama mtu anaye elekea kukata roho, Eddy akataka kunyanyuka ila kwa ishara mzee Godwin akamuamrisha akae chini la sivyo atamfumua ubongo, Mzee Godwin akaufikia mlango huku akiendelea kujifuta damu zinazo mtoka puani mwake na mkono mmoja akiwa amewaelekezea bastola yake Eddy na askari walio jipendekeza kuingilia ugomvi usio wahusu.
 
Mlango ukafunguliwa na Mzee Selemani Mbogo akaingia huku akiwa anahema akiamimini kwamba ugomvi umetatuliwa na askari hao. Mzee Mbogo akastukia akivutwa ndani nakusukumizwa kwenye sakafu na kuangukia uso wake alipo geukuka kuangalia ni nani aliye fanya hivyo akakutana akitazamana na bastola.
 
“Eddy  nikihitaji kuua nitakuua kwa mkono wangu ila si kwakutumia risasi, weka hilo akilini”
Mzee Godwin alizungumza kwa dharau huku akiachia tabasamu pana, kisha akafungua mlango na kutoka nje
“Kamkamateni yuleee”
Eddy alizungumza huku akijinyanyua na kumzuia mke wake kwa mkono mmoja ili asianguke kitandani kwani tayari alisha anza kusoge pembezoni mwa kitanda.
“Muheshimiwa anabastola yule”
Askari mmoja alizungumza sentensi iliyo mchukiza Eddy akajaribu kurusha kofi kwa mkono wake wa kulia ila akashindwa kwa maumivu makali
 
“Kuanzia leo huna kazi”
Asakri huyo baada ya kusikia hivyo wakatoka kasi kumfwatilia Mzee Godwin sehemu alipo kwenda.
“Na wewe unashangaa nini nenda kawaite madaktari”
Eddy alimfokea mzee Mbogo na kumfanya naye atoke kasi ndani ya chumba nakuelekea kwenye mapokezi kuomba msaada kwa manesi walio kaa kwenye sehemu hiyo.
“Mke wangu usife”
Eddy alizungumza huku akiendelea kujitahidi kumtuliza Phidaya ambaye kwa sasa alianza kumwagikwa na povu mdomoni mwake. Manesi watatu wakingia ndani ya chumba wakiwa wameongozana na mzee Mbogo ambaye jasho linamwagika na kuhema juu.
 
“Mungu wangu…..!!”
Nesi mmoja alizungumza baada ya kuona kifaa kiliicho kuwa kikimsaidia Phidaya kupumulia kikiwa kinaning’inia kwenye mtungi wa gesi. Kwa haraka akakichukua na kumfuta povu linalo toka mdomoni mwake na kumvalisha, hewa ilivyo anza kuingia mapafuni mwake taratibu ikaanza kumtuliza Phidaya kurusha rusha miguu yake na baada ya muda akaanza kurudi katika hali yakawaida japo fahamu zake bado hazijamrudia
“Kaka kwani imekuaje hadi mgonjwa akawa katika hali hii?”
Nesi aliye muwekea Phidaya kifaa cha kupumulia kwenye pua yake alizungumza huku akimshika bega la kushoto Eddy aliye ikunja sura yake kwa maumivu makali
“Hembu nione”
Nesi huyo alizungumza kwa kujiamini huku akihitaji kuliona bega la Eddy.
 
“Linauma”
Kwa uzoefu alio kua nao nesi Maria akagundua kwamba bega la Eddy halijavunjika zaidi ya kutenguka. Akamshika shika Eddy ambaye kila alipo shikwa alijihisi maumivu makali kwenye bega lake hilo, gafla nesi Maria akaliminya kwa nguvu bega la Eddy na kumfanya atoae ukelele mkubwa kwani nitukio ambalo hakulitegemea kulipa kutoka kwa nesi Maria aliye onekani kuwa na umri kati ya miaka arobaini hadi arobaini na tano. Ukelele wa Eddy ukapenya kwa haraka kwenye masikio ya Phidaya na kujikuta akiyafumbua macho yake, akiwa kama mtu aliye toka kwenye njozi nzito yakutisha.
“Pole ehee”
Nesi Maria alizungumza huku akiendelea kumgusa gusa Eddy begani
 
“Muheshimiwa”
Mzee Selemani Mbogo aliita na kumfanya Eddy kugeuka na kumtazama kwa ishara yakidole mzee Mbogo akamuonyesha Eddy jinsi mke wake anavyo endele kushangaa shangaa kwenye chumba alicho kuwepo.
“Baby umeamka…..”
Eddy alizungumza kwa furaha huku akimtazama mke wake akataka kujaribu kumtoa mashine ya kupumulia ila Nesi Maria akamzuia asifanye hivyo
“Huyo bado hajarudi katika hali yake ya kawaida, hapo bado akili yake inavuta kumbukumbu ni wapi alipo na ukimtoa hiyo mashine anaweza kufariki”
 
Nesi Maria alizungumza na kumfanya Eddy asimamishe zoezi lake la kutaka kukitoa kifaa hicho kilicho funika mdomo pamoja na pua ya Phidaya. Phidaya akaigeuza shingo yake na kumtazama Eddy, akaachia tabasamu dogo kisha akafumba macho yake na kuifanya mashine iliyopo pembeni ya kitanda inayo hesabu mapigo ya moyo kutoa mlio wa kupiga kelele, ndogo huku mistari miwili myekundu ikikatiza kwa kasi, ikiashiria mapigo ya moyo ya Phidaya yameacha kufanya kazi
“Jamani nawaombeni mutupishe, nesi Lily nenda kamuite dokta Khan”
 
Nesi Maria alizungumza huku akiheme, akiianza kumkandamiza kandamiza kwa nguvu Phidaya kifuani mwake, Wasiwasi mwingi ukazidi kumtawala Eddy ambaye macho yake tote amayetoa kwa mke wake ambaye ametulia tuli, kwenye swala la kutoka nje hakuwa mmbishi zaidi ya kutoka nje kuwaacha manesi waendelea kufanya kazi yao. 

Hawakwenda mbali na chumba alichopo Phidaya, wakawashuhudia daktari wa kuhindi akija kwasi huku nyuma yake kukiwa na nesi aliye pewa jukumu lakwenda kumuita. Wakaingia ndani ya chumba na kuanza kumfanyia litakalo wezekana Phidaya ili kuweza kuyaokoa maisha yake, kwakutumia mashine za umeme zinazo stulia mapigo ya moyo, wakaanza kufanya hivyo kwa haraka,
 
“Again”(Tena)
Dokta Khan alimuamuru nesi Maria kuweza kurudia kuyastua mapigo ya moyo ya Phidaya anaye onekana kulala kuzidi kuwa katika hali mbaya sana,
Wakiwa nje ya chumba alicho lazwa Phidaya, Eddy hakuweza kutulia kila mara akawa na kazi ya kuzunguka zunguka kwenye kordo ya hospitali huku kila mara akijaribu kumuomba Mungu kuweza kufanikisha mkewe kuweza kupona.
 
“Muheshimiwa tumemkosa”
Askari walio agizwa kwenda kumfwatilia Mzee Godwin walikuja huku wakihema kana kwamba ni kweli waliweza kumfwatilia ila ukweli ni kwamba walipo toka ndani ya chumba cha walicho kuwepo na kwenda nje ya geti, wakatazama kila upande na kushauriana wakimbie kimbie, kama nusu saa ili kuitoa miili yao jasho, ili wakirudi watoe ripoti ya kwamba hawakufanikiwa kumuona mzee Godwin. Eddy akawatazama kwa muda jinsi wanavyo hema
“Hamuna kazi, kuanzia sasa rudishni magwanda kwenye vituo vyenu vya kazi”
Askari hao wakabaki wamemtumbulia mimacho Eddy na mmoja akaanza kuangua kilio kikubwa cha kujutia

==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts