Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 9 & 10 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 9 & 10 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Thursday, December 29, 2016 | 1:03:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
“Muheshimiwa tumemkosa”
Askari walio agizwa kwenda kumfwatilia Mzee Godwin walikuja huku wakihema kana kwamba ni kweli waliweza kumfwatilia ila ukweli ni kwamba walipo toka ndani ya chumba cha walicho kuwepo na kwenda nje ya geti, wakatazama kila upande na kushauriana wakimbie kimbie, kama nusu saa ili kuitoa miili yao jasho, ili wakirudi watoe ripoti ya kwamba hawakufanikiwa kumuona mzee Godwin. Eddy akawatazama kwa muda jinsi wanavyo hema
“Hamuna kazi, kuanzia sasa rudishni magwanda kwenye vituo vyenu vya kazi”
Askari hao wakabaki wamemtumbulia mimacho Eddy na mmoja akaanza kuangua kilio kikubwa cha kujutia
   
ENDELEA
“Muheshimiwa mimi kwetu ninategemewa, na mimi itetezi change ni hii kazi”
Askari huyo alizungumza huku akiendelea kulia kwa machozi, Eddy hakuhitaji kusikiliza kitu cha aina yoyote zaidi ya kuwasisitiza wakalilie mbele ya safari kwani hawana sifa ya kuwa maaskari.
Hali ya Phidaya ikaendelea kuwa tata huku daktari na manesi wakindelea kuyastua mapigo ya moyo yaweze kufanya kazi, ila haikuwa rahisi kama wanavyo zoea kufanya kwa wagonjwa wengine
 
“Dokta vipi?”
Nesi Maria aliuliza huku akiwamgikwa na jasho jingi kwani nimara nyingi wamejaribu kumstua Phidaya ila juhudi zao hazikuzaa matunda
“Atakuwa amekufa nini?”
Doktar Khan alimuuliza nesi Maria kwa sauti ya chini ili waziri Eddy aliyopo nje asiweze kusikia kinacho endelea ndani ya chumba hicho
“Hata mimi pia nahisi hivyo kwani si kawaida”
“Sasa utamuambiaje huyo waziri hapo nje?”
“Nani niwaziri?”
Nesi Maria alizungumza kwani kwa kipindi chote alicho kuwa anazungumza na Eddy hakujua kwamba ni waziri
 
“Mungu wangu, mimi sijajua……!!!”
“Ohooo hapo sasa na wewe unaharibu, mimi nimesikia watu hapo nje wakiangua vilio baada ya kuambiwa hawana kazi”
“Mmmmm ehee Mungu sijui itakuwaje”
Wakiwa wakiendelea kujadilia, taratibu mashine ikaanza kuonyesha vimishale viwili vya kijani ikiashiria mapigo ya moyo ya Phidaya ayamesha anza kudunda japo kwa utaratibu bali anaashiria kwamba yu hai na si mfu kama wanavyo hisi
“Ohhh asante Mungu wewe baba wa majeshi, hakuna lishindikanalo kwako”
Nesi Maria alisali kwani kupona kwa Phidaya ndio kupona kwa kazi zao wanazo zitegemea maishani mwao.
                                                                                             ***
    Upasuaji wa kutoa risasi zilizo kuwa kwenye kifua cha Madam Mery, ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa na madaktari wakafanikiwa kuweza kuzitoa risasi hizo kwa usalama kisha wakamshona vizuri Madam Mery na kumpeleka kwenye chumba maalumu cha wagonjwa mahututi. Kwa msaada wa mashine akaendelea kupumua huku dripu la maji na damu yakiendelea kufanya kazi ya kuongeza maji na damu vilivyo pungua mwilini mwa Madam Mery.
 
Usiku wa manane Madam Mery akaweza kufumbua macho yake kwa mara ya pili, kwani mara ya kwanza alikua wakiomba kuzungumza na Eddy, pale alipo pata hofu kwamba anaweza kupotea maisha yake muda wowote kuanzia pale
 
Akayazungusha macho yake kwenye kila kono ya chumba, kwaufahanu wake unao fanya kazi vizuri akagundua kwamba pale ni hospitali. Pameni ya kitanda akaona kuna kifaa maalumu ambacho ukikiminya nesi au daktari aliye karibu mtambo huo wa kisasa unao weza kuwataarifu manesi na madaktari kwamba mgonjwa wa chumba Fulani ana hitaji msaada.
Hazikupita dakika tano mlango wa chumbani kwakr ukafunguliwa na kuingia nesi mrefu kiasi aliye jazia maungo yake ya nyuma
“Nikusaidie nini?”   
Nesi huyo alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Madam Mery.
“Eddy, Eddy waziri namuhitaji”
 
Madam Mery alizungumza, kutokana na uwepo wa Eddy kwenye hospitali hii uliwafanya watu wengi kuutambua uwepo wake. Hakuwa na kipingamizi nesi huyo, aliye vaa kagauni kalisho ishia kenye maagoti na kuyafanay makalio yake makubwa kutingishika vibaya mno kila anapo tembea
Nesi akaongoza hadi sehemu alipo Eddy, nje ya chumba, kwaheshima zote akasimama mbele ya Eddy
“Muheshimiwa kuna mwana mama anakuhitaji kwenye chumba cha wagonjwa mahuti”
Kabla Eddy hajamjibu neno lolote nesi huyo mlango wa chumba alicho lazwa mke wake, ukafunguliwa akatoka doktar Khan, akiwa na tabasamu usoni mwake
“Dokta vipi mke wangu?”
Doktar Khan akashusha pumzi nyingi kisha akaanza kuzungumza
 
“Tumejitahidi kadri ya uwezo na..”
“Mke wangu amekufa doktar?”
Eddy aliuliza kwa wasiwasi mwingi
“Hapana hajafa, tumeweza kuyaokoa masha yake, ila kwa sasa atakuwa chini ya uangalizi wa manesi watau, mutamuona kesho asubuhi kwa sasa nitaomba mumuache apumzike”
“Sawa”
Eddy alijubu kwa unyonge huku akitamni kuzungumza kitu kwa daktari huyo, ila akajikuta akisahau ni kitu gani alihitaji kukizungumza. Hapakuwa na jinsi yoyote ikambidi Eddy amuombe Mzee Mboho kukaa nje ya chumba hicho hadi yeye pale atakapo rejea, yeye akaongozana nesi aliye kuja kumuita na kufikishwa kwenye chumba alichopo Madam Mery
                                                                                                ***
      Mzee Godwin baada ya kutoka kwenye geti la hospitali akakodi taksi iliyo mfikisha kwenye hoteli aliyo kuwa amefikizia na Madam Mery, akaingia bafuni na kunyoo ndevu zake zote alizo kuwa nazo na kumfanya arudi kwenye sura ya ukijana japo ni mzee, akakushanya nguo zake na kuziingiza ndani ya begi alilo kuja nalo, akiamini anaweza kuifanya kazi yake na kuimaliza ila hali tayari ilisha kuwa mbaya kwani mwanae Eddy anamamlaka makubwa serikalini na endapo atamtia nguvuni nilazima atahukumiwa. 

Mzee Godwin akatoa kwenye chumba cha hoteli na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu, hakuhitaji kutumi lifti kuhofia kukamatwa kizembe pale lifti itakapo funguka na kukumbana na kundi la askari. Akaanza kushuka kwenye ngazi akitokea gorofa ya saba kushuka chini, na kila mara akawa na kazi ya kuchungulia chini kuona kama atakutana na mtu yoyote.
 
Mzee Godwin akafanikiwa kufika nje ya hoteli pasipo kustukiwa akakodi taksi nyingine na kumuomba dereva kumpeleka kwenye uwanja wa ndege wa mwalimu Julias K.Nyerere ili aweze kuondoka nchini Tanzania haraka iwezekanavyo na kuelekea brazil alipo weka makazi yake ya maficho.
Mzee Godwin akastushwa kukuta gari zipatazo sita za polisi zikiwa zimefunga barabara ambayo walihitaji kupita kuelekea uwanja wa ndege. Na kundi hilo la askari wote walionekana kuwa na silaha mikononi mwao na wawili wakiwa namatochi makubwa yakiimulika taksi hiyo
                                                                                                   ***
     Eddy akafungua mlango na kuingia ndani ya chumba alicho lazwa Madam Mery na kumkuta akiwa yupo macho. Taratibu Eddy akaka kwenye kiti cha pembeni ya kiti cha Madam Mery, huku akiwa na maswali mengi ni kwanini amemkuta Madam Mery akiwa amepigwa risasi nyumbani kwake na kama alikuja na mzee Godwin imekuwaje wameanza kushirikiana na mzee huyo. Ila kutokana Madam Mery ni mngonjwa hakuhitaji kuuliza swali lolote zaidi ya kusubiria kitu kilicho mfanya yeye kuitwa hapo
 
Madam Mery alipo mtazama Eddy, akajikuta akimwagikwa na machozi, kila alivyo lia maumivu kwa mbali akaanza kuyasikia kwani dawa ya maumivu aliyo chomwa ndio ilikuwa ina kwenda kuishia kupoma.
“Eddy kwanza nahitaji kukuambia kitu kitu kitakacho tokea muda wowote, Godwin amepanga kutegesha bumu kwenye uwanja wa ndege wataifa na kuteka ndege ambayo, atataka kuitumia kwa shuhuli zake binafsi”
 
Maneno ya Madam Mery yakamfanya Eddy kustuka kwani hajafanikiwa kumtia mikononi mzee Godwin, Eddy kwa haraka akaitoa simu yake mfukoni, akajaribu kuiwasha akakuta imezima
“Mungu wangu”
Eddy alionekana kuchanganyikiwa, akajaribu mara kadhaa kuiwasha simu yake ila haikukubali kuwaka, kwa haraka akatoka nje ya chumba pasipo kumuaga madama Mery kwa bahati nzuri akakutana na nesi aliye kuwa amemuita 
 
“Lete lete simu yako”
Eddy alizungumza na kumfanya nesi huyo kuanza kujipapasa papasa ila akajikuta akishangaa
“Ahaa nimeicha kule mapokezi ninaichaji”
Alizungumza na kuanza kukimbi kuelekea mapokezi, huku Eddy akifwata kwa nyuma. Kila walio pishana naye alihisi kuna jambo linalo endelea, wakafika kwenye chumba cha mapokezi, nesi huyo akaingia ndani naichomo simu yake kwenye chaji na kumkabidhi Eddy aliye onekean kuchanganyikiwa.
 
“Unafunguaje hiii”
Eddy alizungumza baada ya kushindwa kufungua mfuniko wa simu ili kuweza kubadilisha line za simu na aweke yakwake. Nesi akamsaidia kufungu simu hiyo, kisha akatoa line yake na kumpa Eddy, akaweka line yake na kuchua batrii na kuiweka na kuiwasha simu hiyo pasipo pasipo kuurudishia mfuniko wa nyuma. Eddy kwa haraka akatafuta namba ya mkuu wa polisi, kisha akaipiga. Ikaita kwa muda  na kupokelewa na sauti iliyo jaa usingizi
“Haloo”
“Kuna tukio la ugaidi lanataka kutendeka muda wowote kuanzia sasa, huku uwanja wa ndege wa JK unatakla kulipuliwa”
 
Eddy alizungumza kwa haraka haraka huku akihema
“Wewe nani kwani?”
Mkuu wa askari aliuliza
“Unataka kunijua mimi ni nani?”
“Ndio kwa maana wewe ugaidi Tanzania utokee wapi, hembu acha upuuzi wako. Acha tulale sisi”
“Kabla hujakata simu, kuanzia sasa huna kazi pumbavu wewe. Unazungumza na waziri wa Ulinzi Eddy, Eddy Godwin”
“Muhe……”
Eddy akaakata simu na kutafuta simu ya makamu msaidizi wa kamanda huyo wa kanda maalumu, akaipiga namba hiyo hata sekunde tano hazikupita, simu ikaokelewa
 
“Ndio muheshimiwa”
Kamanda huyo alizungumza kwa wasiwasi mwingi, na kumuomba dereva wa gari anaye muendesha kusimamisha pembeni
“Kuna tiukio la uwanja wa ndege kulipuliwa hakikisheni munafunga barabara ya kwenda uwanja wa taifa na gari zote munazisimamisha na kuzikagua na mumkamate Godwin aliye kuwa mkuu wa jeshi la ulinzi”
“Sawa mkuu nimekuelewa, kwanza nipo doria muda huu na vijana”
“Fanya hivyo kuanzia sasa hivi unachukua nafasi ya mkuu wako, nimefukuza kazi muda huu”
“Ohh asante sana muheshimiwa”
 
Eddy akakata simu, akakata simu na kumpigia simu mkuu wa ulizi katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere, simu yake nayo ikapokelewa ndani ya muda mchache
“Haloo”
“Panga vijana wako, waimarishe ulizi kunahatihati ya uwanja wa ndege kulipuliwa kwa bomu”
“Haaaa…..!!!”
“Unashangaa nini?”
“Hapana nimekuelewa muheshimiwa”
Kilicho muokoa mkuu huyu kuto fukuzwa kazi ni kuweza kuikumbuka sauti ya Eddy aliyo toka kuisikia kwenye bunge mida ya saubuhi na wala hakufahamu namba yeka waziri huyo ameitolea wapi. Hakutaka makuu zaidi ya kupiga simu kwenye sekta nzima za ulinzi uwanja wa ndege kuwaamuru askari kudumisha ulinzi kwa anaye ingia na kutoka na kila waliye mtilia mashaka akamatwe kwa mahojiano
                                                                                             ***
    Dereva taksi akasimamisha taksi yake baada ya kuona gari nyingi za polisi zikiwa mbele yake.
 
“Wanataka nini hawa”
Dereva taksi alijisemea mwenye akisubiria kuungwa mkono na mteja wake Mzee Godwin aliye kaa siti ya pembeni mwake. Mzee Godwin alitambua kwamba anaye tafutwa ni yeye kwani tayari mwanae amesha kuwa na mkono mrefu serikalini wakuweza kufanya chochote ndani ya dakika kikafanyika. Kila askari aliye kuwa doria aliweza kusambaziwa picha ya mzee Godwin, kwenye namba yake ya whatsapp na hata aliye kuwa hayupo doria aliweza kutumia ujumbe wa kumuamrisha kuweza kuingia kazini, usiku huo wa saa tisa.
“Haya ndo matatizo ya hii kazi”
Askari mmoja  alizungumza akiwa anajiandaa kupata chakula cha kitandani kutoka kwa mke wake
“Kuna nini?”
“Tumepigiwa simu ya upepo, inanibidi kuwasili kituoni muda huu”
 
“Jamani mbona wanawatesa hivyo”
“Ahaa wee acha tu mke wangu, ngoja nijiandae niende”
Askari wote waliopo ndani ya jiji la Dar esaalam wakawa wapo macho kwa muda wausiku, wakiendelea kufanya masako mkali kwa kila gari waliyo kutana nayo kwenye barabara ikitembea kwa muda huo, si wenye magari waliweza kukumbana na kasheshe ya kukaguliwa, bali hata pikipiki na watembea kwa miguu walio kuwa wakiamka majira hayo kuwahi kwenye kazi zoa, nao wakumbana na doria hiyo kali
“Shuka kwenye gari”
Mzee Godwin alizungumza kwa sauti nzito ya kukoroma tofauti na suati aliyo kuwa ameizungumza nayo kwa mara ya kwanza alipo mkodi dereva huyo
“Mzee wangu vipi, gari si yangu hii bwana kama vipi shuka wewe”
 
Mzee Godwin hakutaka mazungumzo mengi, akachomo bastola yake kwenye soksi, mguu wa kulia na kiumtandika risasi moja ya kichwa, dereva taksi na kumuua hapo hapo. Alafungua mlango wa dereva na kimsukumia nje, akakaa kwenye siti ya gari nakuanza kulirudisha nyuma jambo lililo wafanya askari kuanza kuishambulia taksi hiyo kwa risasi. Mzee Godwin akafanikiwa kuigeuza taksi hiyo kwa utaalamu mkubwa, na kugeukia inapo toka, ubaya zaidi wapo kwenye daraja ambalo kwa chini linapitisha maji ya mto
 
Risasi za polisi zikapiga kwenye matairi ya nyuma na kuzifanya rimu za gari hilo kuanza kuserereka kwenye lami na kuifanya gari hiyo kushindwa kwenda kwa kasi na kuzidi kuyumba yumba. Mzee Godwin akashududia gari nyingine za polisi zikija mbele yake sehemu anapo elekea. Hakua na uchaguzi wowote zaidi ya kugonga bomba za daraja, zikavunjika na kuifanya gari kuanza kushuka kwenye mto huyo wenye maji mengi chini pamoja na mawe makubwa.

SORRY MADAM (10) (Destination of my enemies)

Mzee Godwin akawahi kuufungua mlango wa gari kabla halija fika chini, kisha akajirusha peke yake na kuingia ndani ya maji. Askari wakafika sehemu ambayo taksi hiyo imedumbukia na kuanza kushambulia kwa risasi wakiamini mtu aliyopo kwenye gari hilo ni lazima atakuwa hai.
 
Risasi zinazo ingia ndani ya maji ya mto huu, hazikuweza kumpata mzee Godwin, ambaye alizama ndani ya maji ambayo yanakwenda kwa mwendo wa kasi, hii ni kutokana na maji hayo kuwa mengi. Mazoezi ya kijeshi yakaweza kumsaidia mzee Godwin kuwatoroka polisi ambao waliendelea kumulika mulika katika sehemu ambayo gari hilo limedumbukia.
 
Hadi yanajiri majira ya saa kumi na mbili asubuhi hawakufanikiwa kumuona mzee Godwin, ila taksi iliyo tumiwa na mzee huyo kutorokea ilibaki sehemu ya tukio, huku mwili wa dereva taksi ukichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha kuhifadia maiti hospitali ya taifa Muhimbili.
“Muhehimiwa  tumemkosa”
“Endeleni kudumisha ulinzi kila sehemu, na muhakikishe munamkamata, ninawapa masaa ishirini na nne kuweza kulikamilisha hilo”
Eddy alizungumza na mkuu wa jeshi la polisi, kwa njia ya simu huku akiwa amekaa pembeni ya kitanda cha mke wake ambaye bado anaendelea kupumulia mashine.
 
“Sawa muheshimiwa”
Eddy akakata simu, nakushusha pumzi nzito huku akimfikiria mzee Godwin, ambaye ni amekoswa koswa kuuawa na baba yake huyo ambaye hadi sasa hivi hatambui ni nini chanzo cha mzee huyo kugeuka na kuwa katili sana kwake wakati kipindi cha nyuma alimpenda sana na kumfundisha mambo mengi sana
Mama Eddy akaingia kwenye chumba, alichopo Eddy na mkewe, akiwa ameongozana na Junio. Eddy akamsalimia mama yake huyo ambaye hakuonekana kuwa na furaha moyoni mwake.
 
“Mama mbona kama haupo sawa?”
Mama Eddy akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Eddy aliye nyanyuka na kumpisha sehemu ambayo alikuwa amekaa.
“Jana kulitokea nini?”
Eddy akamtazama mwanaye kisha akamuomba mama yake waweze kutoka nje, wazungumze kwani asinge penda mazungumzo hayo Junio aweze kuyasikia. Wakakaa kwenye viti vilivyopo nje ya chumba alicho lazwa Phidaya.
“Jana hapa, Mzee Godwin alikuja, mimi nikiwa nipo nje. Basi nikamkuta akimchezea chezea mke wangu akitaka kumuingilia kimwili”
 
“Wewe hayo yanatokea ulikuwa wapi?”
“Mimi nilikwenda kununu maji”
“Ila Eddy, kama ni hili swala usinge lipeleka kwenye vyombo vya sheria japo wewe kwa sasa unahusika na sheria ila si vizuri”
“Sasa mama hapo unahisi mimi ningefanya nini?”
“Ungefanya hata kwa njia nyingine, yaa ni hvi niniavyo zungumza, kila stesheni ya televishion ukifungua ni Godwin Godwin, na waandishi wengine wasivyo na aibu wanaongezea maneno kwamba ni mume wa waziri mkuu mstafu. Kusema kweli mimi sijisikii vizuri kwa hilo”
Bibi Junio alizungumza kwa sauti ya upole huku akiwa ametizama chini, Eddy akabaki kimya kwani hakujua ni kitu gani anaweza kukizungumza ili mama yake aweze kumuelewa.
 
“Eddy ni bora hili swala ungelipeleka kama ulivyo kuwa unalipeleka pale awali, hembu tazama sasa hivi jinsi familia sasa hivi inavyo zalilika kwenye vyombo vya habari”
Mama alizungumza na kutoa gazeti kwenye pochi yake, gazeti hilo zimepambwa na maandishi meusi yaliyo andikwa kwa herufi kubwa yakisomeka (BABA JAMBAZI, MAMA WAZIRI MSTAAFU, MTOTO STERING, NI BONGE LA MOVIE), chini ya maandishi hayo kuna picha tatu, moja ikiwa ya mzee Godwin akiwa amevalia mavazi yake ya jeshi, nyingine ikiwa ya mama huku yakwangu ikiwa chini ya hizo picha mbili.
“Hilo ni gazeti la leo, na kama waandishi wa habari wakijua upo hapo watakuja kuleta fujo hapa wewe fanya uende nyumbani kwako ukabadilishe hizo nguo kisha ukafanye mambo mengine”
 
“Mama siwezi kuondoka na kumuacha mke wangu hapa. Kwani lolote linaweza kujitokeza”
“Hata kama mama, ila tambua kwamba mkwe wangu huko ndani hali yake ni mbaya, hivi makelele ya hao waandishi yakihamia hapa hospitalini, utamjua ni nani ni mbaya kwako aliye tumwa kuja kumuua mke wako hapa”
Maneno ya bibi Junio yakamfanya Eddy kukaa kimya huku akishusha pumzi nyingi.
 
“Nitakaa hapa na mke wangu hadi hali yake iwe nzuri, omba ulinzi wa askari wa jeshi la polisi wawili waje kulinda hapa la sivyo siwezi kukubaliana wewe kuendelea kukaa hapa”
“Ila ma….”
“Hakuna cha mama, mimi nahitaji amani. Nahitaji amani ya moyo wangu, nakupenda sana mwanangu, nampenda mjukuu wangu, nampenda mkwe wangu. Pia ninampenda sana Godwin wangu”
Bibi Junio alizungumza huku machozi yakimwagika, kwa uchungu mkubwa
“Mom what, are you seriously?”(Je upo makini?)
Eddy alishangaa kumsikia mama yake kwamba bado anampenda mzee Godwin
                                                                                         ***
Kwa bahati nzuri maji ya mto huo, yanaelekea baharini, ikawa ni nafasi nyingine kwa mzee Godwin kuweza kuingia kwenye bahari ya hidi, akatazama kila sehemu, ila hapakuwa na uwepo wowote wa mtu kwenye eneo hilo. Mzee Godwin akatafuta sehemu iliyo tulia na kujitupa chini na kulala, usingizi wa magamu gamu ulio andamanana na njaa kali pamoja na hofu kubwa ya kuweza kukamatwa na jeshi la polisi kwani tayari amaanza kusakwa kila kona ya Tanzania.
 
Kijua cha machana kikaanza kupenya kwenye macho ya Mzee Godwin ambaye aliye amejilaza pembeni ya mti wa mkoko, akafumbua macho yake na yaliyo jaa uchovu mwingi, taratibu akanyanyuka huku akijikung’uta machanga ulio mjaa sehemu za mgongoni na kichwani, hii ni kutokana na kujilaza chali.
Kila sehemu aliyo tazama hakuona uwepo wa mtu kufika katika eneo hilo. Taratibu akaanza kuelekea upende wa kaskazini mwake, huku kila muda akiwa makini sana kwa kutazama kama kuna mtu anamfwatilia au laa.
 
Akafanikiwa kukuta kidao kidogo kwa mahesabu ya haraka haraka wanaingia watu wapatao wawili, huku ndani ya kidao hicho kilichopo pembezoni mwa fukwe ya bahari kukiwa na makasia mawili, Mzee Godwin hakuitaji kupoteza muda kabisa, alicho kifanya ni kufungua kamba ya manila iliyo kuwa imefungwa kwenye mti wa mkoko, kuelekea kwenye kidau hicho, ili kisiweze kuchukuliwa na maji kipindi yanapo ongezeka pembezoni mwa fukwe hiyo. 

Akakisukuma hadi kwenye maji kisha akavua, shati lake na kulifunga kichwani ili kuzuia makali ya juu, linalo piga sama kwenye utosi wake. Taratibu akaanza kupiga makasia huku akiwa anaimani anapo elekea atapata msaada na kikubwa zaidi, anahitaji kuondoka nchini Tanzania kabla hajaingia kwenye mikono ya mwanaye Eddy. 

Haikuwa kazi rahisi kwa mzee Godwin kuweza kuendesha kidau hicho, hii ni kutokana na kuto kuwa na uzoefu katika kuendesha chombo hicho ambacho mara nyingi hutumiwa na wavuvi wadogo wadogo.
 
Kila alivyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyozidi kwenda katikati ya bahari, pande zote amezungukwa na maji ambayo yametulia sana, nguvu nyingi anazo zitumia, zikazidi kulitesa tumbo lake ambalo lilianza kukoroma kwa njaa kali iliyo anza kumpiga kisawasawa, kila alipo jaribu kujipa moyo ndivyo hali ilivyo muwia ugumu kwani, nguvu zilidi kumuishia, njaa nayo haikucheza mbali, akaikuta akijinyoosha ndani ya kimtumbwi hicho, huku akijaribu kuvuta pumnzi nyingi, ili aweze kupata nguvu za kumuwezesha kuendesha kimtumbwi hichi. 

Gafla kufumba na kufumbua, mzee Godwin akajikuta akitupwa ndani ya maji na kimtumbi kumfunika kwa juu, jambo lililo anza kumchanganya, na kujikuta akianza kupiga mafumba kadhaa ya maji kwenye kinywa chake
                                                                                                          ***
 “Mama huwezi kumpenda mtu jambazi, katili, gaidi kama yu…..”
“Eddy Stop talking”(Eddy acha kuzungumza)
Bibi Junio alizungumza huku machozi yakimtoka, akamtazama Eddy kwa muda, huku akionekana kumvumilia mwanaye, na laiti angekuwa si waziri angemtandika kibao cha shavu, ila akamstiri kutokana na wauguzi wanao pita pita kwenye kordo walipo kaa.
“Godwin is your blood dady”(Godwin ni baba yako wa damu)
“It’s impossible”(Haiwezekani)
Eddy alijibu huku machozi yakimlenga lenga kwani mtu aliye mpa mareso makali kipindi cha nyuma leo hii amuambie kwamba ni baba yake wa damu
 
“Mama mbona siwaelewi”
“Huo ndio ukweli halisi mwanangu, wewe si mtoto wa Godfrey, baba yako wewe ni Godwin. Am your mother na natambua ni nani aliyenipa ujauzito wako”
Eddy akajikuta akishusha pumzi huku macho yakiwa yamemtoka kiasi kwamba akawa anajihisi kuchanganyikiwa kwani si jambo rahisi kwani anavyo tambua kwamba baba yake halisi ni Godfrey
“Unataka kujua ukweli eheee?”
Mama Eddy alizungumza kwa uchungu mkubwa huku wakitazama na mwanye, hadi baadhi ya wauguzi wakaanza kuyatega masikio yao kuweza kusikia ni kitu gani mama huyo anahitaji kukizungumza kwa mwanaye huyo

==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts