Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 13 & 14 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 13 & 14 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Thursday, January 5, 2017 | 10:45:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA           
    Junio akaanza kuangaza macho yake huku na huku akiwa nje ya geti la hospitali, akimtafuta baba yake ni sehemu gani ambapo yupo. Kwa hahati nzuri akamuona akiwe amesimama kwenye moja ya sehemu iliyopo upande wapili wa barabara
Eddy akiwa katika msongamano wa mawazo akifikiria ni nini afanye, breki kali za gari zikamstua na kumfanya ageuke kwa haraka na macho yake kutazama barabarani, ambapo alimshuhudia mwane Junio akiwa katikati ya barabara, huku gari aina ya Verosa, ikiwa imemlanga Junio, aliye shikwa na bumbuazi asijue ni nini afanye.

ENDELEA
“Junioooooooooo”
Eddy alipaza sauti kama mwenda wazimu kumstua mwanae huyo wa kiume, ila haikuwa hivyo kwani gari hiyo tayari ilishamfikia Junio karibu na kumbamiza kwa nguvu, akarushwa juu futi kadhaa kisha akaanguka chini kwenye lami, na kichwa chake kikaanza kuvuja damu sehemu ya usogoni.
 
Mlio wa risasi, ukawastua watu wote walio ndani ya hospitali hadi wale waliopo nje, na kuwafanya kila mmoja kuweza kutafuta ustarabu wake kwa kukimbia sehemu anayo ifahamu yeye kwani kila mmoja alihisi sehemu hiyo si salama, kutokana na fununu za kwamba Mzee Godwin alipanga kuweza kufanya mashambulizi katika sehemu muhimu, ikiwemo hospitalini.
 
Miguu ya Eddy ikachanganya kasi ya ajabu, hadi katika sehemu alipo lala mwanaye aliye anza kuzingirwa na wananchi walio fika kuweza kutoa msaada kwa mwanae.
“Juniooo”
Eddy alizungumza huku akiwa katika mshangao mkubwa, akimtazama mwanaye mwenye sura nzuri akivujwa na damu puani pamoja na sehemu ya nyuma ya kichwa ikiashiria kwamba mwanaye ameweza kupasuka kichwa kwa nyuma,
Wanaume walio majasiri waliweza kunyanyua Junio na haraka haraka, wakamuingiza ndani ya hospitali kwani kwa mbali mapigo yake ya moyo bado yanakwenda taratibu. 

Baadhi ya askari walio weza kufika katika eneo la tukio wakamchukua waziri Eddy na kumungiza ndani ya hospitali, kwani kwa kipindi chote alikuwa amesimama kwenye kundi lawatu akizitazama damu nyingi za mwanaye zilizo kuwa zimetapakaa kwenye lami.
 
“Muheshimiwa yupo wapi?”
Mzee Selemani Mbogo alimuuliza daktari huku akiwa anahema sana, na jasho jingi likiendelea kumwagika kwani alicho kishuhudia katika chumba alicho lazwa mke wake kinaogopesha sana.
“Aaa..a amepelekwa chumba cha mapumziko?”
“Nipeleke”
Mzee Selemani Mbogo akamshika mkono muhudumu huyo hadi kwenye chumba alicho pumzisha Eddy, akamkuta akiwa ametulia kimya huku amejikunyata asijue ni kitu gani kilicho tokea kwa wakati ule.
 
“Muheshimiwa muheshimiwa”
Mzee Mbogo alimuuita Eddy na kumfanya amgeukie na kumtazama kwa muda huku macho yake yakiwa mekundu huku machozi yakimwagika kwa wingi. Mzee Mbogo akasimama kwa muda huku akiwa na bumbuazi akiwa na maswali mengi kwani yeye ndio mtu wa kwangu kuingia katika chumba alicho lazwa mkewe baada ya mlio wa risasi kusikika.
“Muheshimiwa kuna tatizo”
Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa unyenyekevu wa hali ya juu, Eddy akaachia tabasamu dogo huku machozi yakimwagika
 
“Nimeona, Junio ame…….”
Eddy hakuweza kumalizia sentensi yake, machozi yakamtiririka kwa wingi mno. Mzee Mbogo akaki akiwa ameduwaa, akashusha pumzi nyingi na kumfwata Eddy kitandani alipo kaa na kumshika bega la kushoto.
“Twende ukaone”
Mzee Mbogo akamshika mkono Eddy na kumvuta mkono Eddy, ila Eddy akajikaza misuli yake akiashiria kwamba hato weza kwenda mahala popote. Mlango ukafunguliwa kwa pupa na kuingia nesi mmoja akiwa anahema kwa nguvu akioenekana ametoka kukimbia kwani jasho jingi pia liliweza kimwagika.
 
“Muheshimiwa unaitwa chumba alicho la…laa lazwa mkeo kuna tatizo”
Nesi huyo alizungumza huku akihema sana, Eddy akamtumbulia macho nesi huyo, kichwani mwake kukamjia picha ya mke wake kipenzi PHIDAYA.
 
Eddy bila hata kusukumwa na mzee Mbogo, akakurupuka kitandani na kutoka nje ya chumba huku akiwa katika kasi ya ajabu sana, akafanikiwa kufika hadi sehemu ya nje ya chumba alicho lazwa Phidaya, akakuta baadhi ya askari wa jeshi la polisi wakiwa wamesimama kuimarisha ulinzi huku manesi, wagonjwa na wanandugu walio kuja kutembelea wagonjwa wao, wakiwa wamekusanyika nje ya chumba cha mke wake, huku maaskari wakijaribu kuwazuia kuwez kuona nini kinaendeleka ndani ya chumba hicho. 

Kasi ya Eddy ikapungua baada ya kukuta hali kama hiyo, akajikuta taratibu akiaanza kutembea kwa mwendo wa kawaidia, ila akiwa na hamu ya kuweza kufika mlangoni mwa chumba hicho, ila tatizo kubwa likawa kwenye miguu yake kwani ilijawa na uzito wa gafla,

       Kwa kujikongoja taratibu akaweza kufika kwenye mlango ambapo ulifungwa, askari mmojaa akagonnga mlango huo akiashiria kwamba walipo ndani waweze kuufungua mlango huo, nafasi ya mlango ulipo weza kufunguliwa, kwa msaada wa askari huyo Eddy aliweza kuingizwa ndani kujishuhudia kilicho tokea. Macho yakamtoka Eddy, kizunguzungu kikali kikamkamata na kujikuta akianguka chini, kabla hajafika sakafuni baadhi ya watu wakamdaka na kumlaza chini taratibu.   
                                                                         
(Nusu saa kabla)
     Baada ya mjukuu wake kutoka, mama Eddy akaitazama bastola aliyo kuwa ameishika Eddy nakujikuta akishusha pumzi nyingi zilizo mfanya kukigeuza kichwa chake kwa mkwe wake aliye lala kitandani huku ajitambui, akaachia tabasamu pana kisha taratibu akamsogelea Phidaya aliye lala pasipo kijitambua, akaushusha uso wake taratibu na kulibusu paji la uso la Phidaya, huku machozi yakimwagika kwa wingi.
 
“Najua mwanangu anakupenda sana, si wewe tu hata mwanaye anampenda”
Mama Eddy alizungumza huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake, akajipangusa machozi yake kisha akarudia tena kumbusu Phidaya kwenye paji la uso wake.
“Eddy nisamehe mwanangu, sihitaji mtoto wa watu aweze kupata tabu kwa ajili yangu, kwani mimi ndio mkosefu mkuu katika haya yote”
 
Mama Eddy akaiweka bastola yake pembeni na kukitoa kifaa maalumu cha kumsaidia Phidaya kupumua kisha kwa kutumia nguvu zake zote akaanza kumkaba Phidaya shingoni, Phidaya akaanza kurusha rusha miguu yake kuweza, kuipigania roho yake isitoke kwa wakati huo ila hakuwa na jinsi kwani yupo katika wakati wa kuto kujitambua. Mama Eddy alipo jiridhisha kazi yake imefanikiwa na Phidaya ametulia kimya, akausokomeza mdomo wa bastola mdomoni mwake na kumtazama Phidaya tena usoni na kuachia tabasamu pana.
 
Mzee Mbogo akiwa halitambui hili wala lile akiwa hatua chache kutoka ulipo mlango wa chumba alicho lazwa mke wa Eddy, mlio mkubwa wa bastola ukamshua, na kujikuta akiwa amesiama, watu waliokuwa eneo la karibu wakaanza kuchanguka pasipo yeye, ujasiri mkubwa ukamvaa na kujikuta akikimbilia katika chumba hicho, akausukuma mlango na kuingia ndani. Hakuamini macho yake, akamkuta Mama Eddy akiwa amejifumua kichwa chake kwa risasi na kumuangukia Phidaya aliye kimya kitandani na damu nyingi zikasambaa kwenye shuka lililo mfunika Phidaya.
“Mungu wangu!!!”
Mzee Mbogo alizungumza huku akiwa ameuziba mdomo wake kwa kiganja, akataka kupiga hatua chache kuingia ndani ya chumba hicho ila miguu ikashindwa kumsogeza ndani, ikabidi kugeuka na kutazama nje.
 
      Kwa kiwewe alicho kipata hakuweza hata kujua ni wapi aendee, ni  nini azungumze, hata manesi walio kuwa wamejibanza kwenye kona mbalimbali kika mmoja akijitahidi kuyaokoa maisha yake, wakaanza kuchungulia na kumuona mzee huyo akiwa anatetemeka nje ya mlango. Wakaendelea kusikilizia kwa dakika kadhaa, kuona kama mtu aliye fyatua hiyo risasi atatoka nje au laa. 

Hadi walipo fika askari wawili wenye bunduki, ndipo mzee Mbogo akarudiwa na kumbukumbu zake kuweza kujitambua ni wapi alipi. Kila askari aliye chungulia ndani ya chumba hicho, aliweza kutoka nje kupata mwangaza wa mwanga wa nje, kwani chumba hicho kimetapakaa damu nyingi sana.
“Eddy, EDDY”
Mzee Mbogo alizungumza na kuanza kukimbia huku na huku kumtafuta Eddy ni wapi alipo, haikuwa kazi rahisi kuweza kumpata Eddy, hadi alipo weza kumsimamisha nesi mmoja na kumuulizia bosi wake huyo ni wapi alipo.
 
  ***
    Mstuko mkubwa ukampata Shamsa na kujikuta furaha yote ikitoweka usoni mwake, haikuwa ni mstuko kwa Ajay kuanguka chini na kuonekana kama ameumiua sana, ila mstuko, ambao ulianza kujenga hisia mbaya kichwani mwake. Picha ya mdogo wake Junio ikamjia kichwani mwake, na kujikuta moyo wake ukikumbwa na maumivu makubwa sana kiasi kwamba akaanza kujihisi mnyonge sana. Taratibu akaanza kuondoka kwenye kundi kubwa la mashabiki walio fika uwanjani, huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga lenga.
 
“Shamsa unakwenda wapi?”
Kajol alimuita Shamsa, aliye kuwa akitembea pasipo kujua ni wapi anakwenda kwani kichwani mwake alkijisikia vibaya sana.
Kajol akawahi kumshika mkono Shamsa na kumsimamisha akilini mwake, Kajol akahisi ni labada Ajay alivyo anguka vibaya uwanjani na kutolewa na machela.
“Njoo ukae hapa”
Kajol kwa upendo mkubwa akamsogeza rafiki hadi kwenye moja ya kiti na kumkalisha kisha na yeye akavuta kiti kingeni cha plastik kilicho kuwa pembeni na kumshika begani.
 
“Usijali Ajay atapona tu sawa wangu?”
Shamsa hakujibu kitu chochote, mapigo ya moyo yakazidi kumuenda kasi kiasi kwamba akajikuta jasho likianza kumwagika. Kitendo cha jasho kumwagika Shamsa, kikamstua sana Kajol na kuhisi kwamba rafiki yake ameshikwa na homa ya gafla. Kajol akamuwekea mkono shamsa kwenye shavu kutazama kama kuna kitu chochote kilicho mpata, mwili mzima wa Shamsa ukawa unachemka kwa joto kali sana.
 
“Mungu wangu, Shamsa unaumwa wewe!!”
Shamsa akatingisha kichwa kukataa kwamba anaumwa, Kajol hakutaka kukubaliana na rafiki yake huyo ikambidi amuage ukaombe msaada wa madaktari waliopo ndani ya uwanja. Shamsa akaitoa simu yake mfukoni na kuiwasha, ujumbe wa njia ya whatsapp ukaingia huku kikiwa na namba ngeni.
 
“Ni nani?”
Shamsa alijiuliza kabla ya kufungua ujumbe huo wenye meseji kumi, huku meseji inayo onekana kati ya kumi inamuuliza kwa herufi kubwa ‘WEWE NDIO SHAMSA EDDY?’
Ikamlazimu Shamsa kuweza kuufungua ujumbe huo na kukutana na mlolongo mkubwa wa picha ambazo hazionekani vizuri hadi azifungue, akafanya hivyo. Picha ya kwanza ikamstua na kumfanya mapigo ya moyo kuzidi kumuenda kasi, akajaribu kusimama ila nguvu za miguu zikamuishia na kuanguka chini, akapoteza fahamu.
 

  SORRY MADAM (14) (Destination of my enemies)

      Kajol anafika sehemu alipo muacha Shamsa akiwa na madaktari wawili, wanamkuta Shamsa akiwa chini huku mkononi mwake akiwa ameishika simu yake. Kwa haraka madaktaari wanamuwahi na kuanza kumpa huduma ya kwanza. Kajol anaichukua simu ya Shamsa, anashindwa kuifungua kutokana na namba za siri zilizopo kwenye simu hiyo.
“Tunahitaji msaada wa gari lawagonjwa”
Daktari mmoja alizungumza na simu, ndani ya dakika tano gari moja ya wagonjwa ikafika katiika sehemu walipo. Wakamuingiza Shamsa ndani ya gari na kumuwahisha hospitalini.
                                                                                             ***   
      Mafumba ya maji aliyo kunywa mzee Godwin yakazidi kuufanya mwili wake kuishiwa na nguvu na kujikuta akiishiwa na pumzi na kupoteza fahamu. Mwili wa mzee Godwin ukaanza kuelea juu ya maji. Giza likazidi kuenea juu ya anga huku kukiwa na hali kubwa ya mawingu ya mvua, ikiashiria kwamba ni ni muda wowote mvua inaweza kunyesha.  

Akiwa anaendelea kuelea juu ya maji ya bahari, radi na upepo mkali vikaanza kupiga baharini, vitone vidogo vidogo vya mvua vikaanza kunyesha. Hali iliyo wafanya baadhi ya wavuvi wadogo wadogo kuanza kuzitoa boti zao kwenye bahari kwani hali ya hewa tayari imesha anza kuchafuka na kuwa mbaya. Bwana Tukuyu, akiwa na wasaidizi wake wanne, wakapita na boti yao inayo tumia mashine mbili, karibu na ulipo mwili wa mzee Godwin
“Jamani yule si mtu?”
Mzee huyo aliwauliza vijana wake, huku akipunguza mwendo kasi wa boti yake hiyo ambayo kwa siku ya leo amefanikiwa kuvua samaki kiasi.
 
“Ndio mzee, alafu anaoenekana kama amezimia”
“Tukampe msaada”
Taratibu akaisogeza boti yake hadi sehemu alipo lala mzee Godwin, vijana wake wawili ambao ni mahiri sana katilka kuogelea wakajitosa ndani ya maji kisha wakasaidiana na wezao walio ndani ya boti, wakamuingiza mzee Godwin ndani ya boti hiyo, jambo lililo mfanya mzee Tukuyu kustuka kidogo, ila akajikaza vijana wake hao wasiweze kustukia kitu chochote. Wakaanza kumminya mzee Godwin tumboni ili kuweza kumtapisha maji aliyo kunywa. Zoezi halikuwa gumu la kumtapisha mzee Godwin, baada ya muda mzee Godwin fahamu zake zikamrudia, na kukurupuka kwa haraka.
 
“Nipo wapi hapa?”
Mzee Godwin aliuliza huku alkiyafumbua huku akitazama kila mtu aliye mzunguka
“Upo mikono salama”
Mzee Tukuyu alizunumza huku akimtazama Mzee Godwin jinsi anavyo babaika, kijana mmoja akamletea mzee Godwin kikombe cha kahawa ya moto ili kuweza kumuweka sawa.
“Kunywa upate nguvu kidogo”
Mzee Tukuyu alizungumza huku akimtazama Mzee Godwin aliye baki ameshika kikombe cha kahawa huku akisita sita kuweza kukinywa.
 
Mzee Godwin akaanza kunywa taratibu kahawa hiyo huku akiendelea kuvuta kumbukumbu ni kitu gani kilicho weza kumtokea, kitu cha mwisho alicho weza kukumbuka ni pale kidau chake kilivyo weza kupinduliwa na mawimbo mazito. Hapakuwa na mazungumzo yoyote hadi wakafika ufukweni mwa bahari, Mzee Tukuyu akaondoka na Mzee Godwin na kuelekea nyumbani kwake ambao ni kwenye moja ya kijiji kijulikanacho Pande kilichopo mkoani Tanga. 
 
“Jisikie huru mzee mwenzangu, hapa ndio nyumbani kwangu”
“Asante sana”
“Sijui unanikumbuka?”
Mzee Gowin akamtazama kwa muda mzee Tukuyu, kisha kwa mbali akaanza kuhisi kwamba huyu mtu anamfahamu.
“Ndugu yako Tukuyu hapa, unakumbuka kipindi unaingia jeshini mimi ndio niliekupokea kipindi kile ulikuwa bado kijana mdogo sana”
 
“Ahaaaaa, za masiku ndugu yangu?”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa na furaha kubwa kwani anamkumbuka vizuri mzee Tukuyu, ni moja ya mwanajeshi aliye mtangulia mwaka mmoja katika kazi. Kipindi ambacho mzee Godwin anajiunga na jeshi, Mzee Tukuyu alikuwa ni miongoni mwa watu wake wakaribu sana, ila walikuja kupotezana kipindi Mzee Godwin alipo kwenda masoni nchini Cuba, baada ya kurudi Mzee Godwin akapandishwa cheo na kuhamishwa katika kambi waliyo kuwepo. Usiku mzima ukawa ni usiku wa wao kukumbushana mambo mbalimbali yaliyo weza kutokea kwenye ujana wao huku mzee Godwin akimsimulia rafiki yake huyo mkasa mzima wa maisha yake tangu walipo achana.
 
     ***
      Shamsa baada ya kupaata nafuu, akakuta pembeni yake kukiwa na mzee mefu mweusi pamoja na rafiki yake Kajol.
“Vipi Shamsa?”
“Junio”
Ikawa ni sentesi ya kwanza ya Shamsa kuzungumza, mzee huyo akamtuliza kwanza ili aweze kuzungumza kilicho mleta hapo hospitalini
“Mimi ninaitawa Paul Lukanyangwa, ni balozi wa Tanzania hapa nchini Tanzania, nimeagizwa nije kukupa uangalizi kwa ajili ya kwenda nchini Tanzania”
“Twenda hata sasa hivi?”
“Kwa sasa hivi ni ngumu hadi upate ruhusa ya daktari”
“Kajol kamuuite dokta mwambie kwamba mimi nipo salama tu”
 
Kajol akafanya kama rafiki yake alivyo mtaka, baada ya muda akarejea akiwa na daktari ambaye alianza kumchunguza na kugundua kwamba yupo salama. Baada ya kurithika kwa vipimo daktari akampa ruhusa Shamsa ya kuweza kutoka hospitalini, wakaondoka na moja kwa moja wakaeleka makao makuu ya ubalozi wa Tanzania.
“Nahitaji kwenda na rafiki yangu?”
“Ila tiketi ni moja iliyo andaliwa kwa ajili yako”
“Nahitaji kwenda na Kajol”
Shamsa alizungumza huku machozi yakimwagika, Kajol akawa na kazi ya kumbembeleza rafiki yake huyo aliye fiwa na mdogo wake. Utaraibu wa kumkatia tiketi Kajol ukafanikiwa kufanyika, majira ya saa nne usiku wakaondoka na ndege ya shirika la India. Njia nzima Shamsa akwa anaomba kuweza kufika salama ili kuweza kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa Junio .
 
 ***
Siku mbili zikakatika pasipo Eddy kuweza kuzinduka baada ya kupoteza fahamu, madaktari na manesi wakawa na kazi ya kuweza kuyaokoa maisha ya waziri Eddy aliye pata mstuko baada ya kushuhudia mwili wa mama pamoja na mke wake wakiwa wamefariki. Kilio kikazidi kuongezeka kwa Shamsa ambaye muda wote hakuhitaji kukaa mbali na Eddy, aliye mkuta hospitalini mara baada ya kushuka kwenye ndege.
Shamsa akiwa amejilaza pembeni ya kitanda huku akiwa amekaa kwenye kiti, akastushwa na kitu kilicho mshika kwenye mkono wake alio uweka kwenye kifua cha Eddy. Akafumbua macho yake taratibu na kumkuta Eddy akiwa anachezesha chezesha mkono wake ulio mshika.
 
“Eddy Eddy”
Shamsa aliita huku akimtazama Eddy usoni aliye yafumba macho yake. Eddy akazidi kuutingisha mkono wake, kama mtu anaye zidi kujitahidi kutoka sehemu fulani, iliyo yahatari sana. Shamsa akautoa mkono wake kwa nguvu kwenye kiganja cha Eddy, akasimama haraka na katoka ndani ya chumba na kwenda kumita daktari.
Madaktari wakaingia ndani ya chumba walipo mlaza Eddy, wakamkuta hali yake ikiwa ni ileile ya kurusha mkono wake mmoja.
 
“Baba anakufaa…….?”
Shamsa aliuliza huku machozi yakimwagika usoni mwake
“Hapana, nesi mtoe binti nje”
Nesi mmoja akamshika mkono Shamsa na kutmoa nje ya chumba hicho na kumkabidhi kwa askari wanao endelea kulilinda eneo hilo. Madaktari wakendelea kufanya juhudi zao zote za kuhakikisha wanayaokoa maisha ya waziri Eddy, ambaye mwili wake wote ulianza kutetemeka kwa nguvu hadi kupelekea smashine ya kupumulia waliyo muwekea puani kuweza kuanguka chini.
 
“Itabadi tumchome sindano ya usingizi”
Daktari mmoja alishauri
“Naona si nzuri kwani mishipa yake imekakamaa, hii inaweza kupelekea umauti wake”
Ikawa ni kazi ya madaktari kuweza kuendelea kuminyana na waziri Eddy, ili asiendelee kuruka ruka katika kitanda hicho. Kilicho zidi kuwastua zaidi ni jinsi ulimi wake alivyo utoa kwa nje huku ukiambatana na mapovu mengi. Kila daktari alijikuta akiwa amechanganyikiwa kwa hali ya waziri Eddy, kila walicho jaribu kukifanya hakikuweza kuleta matumaini yoyote kwa mgonjwa wao.
                                                                                                ***
Habari ya hali kuwa mbaya ya waziri Eddy, ikamfikia Raisi Praygod Makuya, pamoja na mke wake Rahab
“Inabidi twende hospitali mume wangu”
“Sawa, ila nina kikao kimoja hapa, au fanya hivi wewe tangulia kisha mimi nitakuja”
“Sawa”
Raisi Praygod akatoka katika chumbani kwake na kuelekea moja kwa moja kwenye ofisi yake, ambapo amejiandaa kuweza kukutana na balozi wa Ujerumani kuweza kujadiliana na mambo ya kiuchumi. Rahaba hakuona haja ya kuendelea kulala kitandani, akajiandaa haraka haraka, alipo hakikisha kwamba yupo salama. Akatoka ndani ya chumba
 
“Madam leo hupati kifungua kinywa?”
Mlinzi wake wa kike alimuuliza mara baada ya kuona wanaelekea nje na si kwenye chumba cha yeye kupata kifungua kinywa
“Hapana tunaelekea ocean road hospital”
“Sawa madam, gari zipo tayari”
“Samson yupo wapi?”
“Yupo na muheshimiwa anajukumu la kumlinda”
“Mmmmm sawa”
Rahab akaingia ndani ya gari lake, ambalo hulitumia kama mke wa raisi. Taratibu wakatoka ndani ya ikulu, safari ya kuelekea hospitalini alipo lazwa waziri wa ulinzi ikaanza. Mawazo taratibu yakaanza kutawala kichwani mwa Rahab, kila alivyo jaribu kuvuta hisia zake juu ya Eddy, akaona jinsi anavyo teseka. 
 
“Mungu wangu”
Alijikuta akizungumza kwa sauti kubwa hadi mlinzi wake akamgeukia na kumshangaa
“Kuna tatizo lolote Madam?”
“Hapana”
Wakafika hospitalini, moja kwa moja wakaelekea katika ya wagonjwa mahututi alipo lazwa waziri Eddy
“Madam heshima kwako”
Askari waliopo katika eneo hilo walimpa heshima Rahab, naye akawasalimia, macho ya Rahab yakamtazama sana Shamsa aliye kaa pembeni ya chumba hicho, huku akimwagikwa na machozi mengi. Taratibu akamsogelea Shamsa na kuchuchumaa taratibu
 
“Binti nyamaza ehee”
Rahaba alizungumza kwa sauti ya upole, kwa kutumia kitambaa chake alicho kishika akamfuta Shamsa machozi yanayo mwagika. Shamsa kwa uchungu na maumivu makali ndani ya moyo wake akamkumbia Rahab kwa nguvu na kuendelea kulia sana. Kila aliye weza kumuona Shamsa aliweza kulengwa lengwa na machozi, kwani kulia kwake kunaashiria kwamba ana hali ngumu sana ya maumivu anayo kutana nayo kwenye maisha yake.
 
“Shiiii….. dady atapona sawa”
Rahab aliendelea kumbembeleza Shamsa, huku na yeye machozi yakimwagika. Wakiwa wamekumbatiana mlango ukafunguliwa, akatoka daktari akiwa katika sura iliyo jaa majonzi mengi, Rahaba baada ya kuligundua hilo kwa haraka akasimama na kumtazama daktari huyo usoni.
 
“Madam…..”
Daktari huyo alijikuta akimuita Rahab, na kuishia katikati mara baada ya kumtazama Shamsa aliye simama pembeni yake. Daktari akabaki kimya akiwa katika hali ya kunto kufahamu asememe nini mbele ya mke wa raisi. Akaingiza mkono wake kwenye mfuko wa koti, akatoa simu yake na kuiwasha. Alipo hakikisha imewaka, akaingia upande wa meseji na kuandika maneno mafupi kisha akamkabidhi Rahab. Rahab kabla hata hayaisoma akastukia akipokonywa simu na Shamsa, hakuamini alicho kiona kimeandikwa kwenye simu hiyo kwa herufi kubwa
(MUHESHIMIWA AMETUTOKA)
Taratibu Shamsa akaiachia simu hiyo, huku miguu ikimlegea na kujikuta akianza kwenda chini, kabla hajafika sakafuni Rahab, akamdaka.
 
==> ITAENDELEA

Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts