Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 17 & 18 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 17 & 18 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Saturday, January 14, 2017 | 2:36:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
. Akiwa gorofa ya kwanza kwenda gorofa ya pili, akakutana na askari wawili wakishiuka chini, akaishusha kofia yake chini kidogo, akapisha na askari hao wakimtazama.
“Ngoja kwanza”
Askari mmoja alizungumza baada ya kushuka ngazi sita kwenda chini, akatoa picha iliyopo mfukoni mwake.
“Ndio huyu tunaye mtafuta”
Askari mmoja alizungumza na kuanza kupandisha kwenda ngazi za juu huku akikimbia, kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona mzee Godwin akitembea kwenye moja ya kordo.
“Simama polisii”   
Askari huyo alizungumza huku bunduki yake akiwa amemnyooshea mzee Godwin kwa nyuma.

ENDELEA
“Nyoosha mikono yako juu”
Watu walio karibu na eneo alipo simama Mzee Godwin pamoja na askari hao walipo nyuma yake mita chache kutoka sehemu alipo, wakabaki wakishangaa tukio hilo kwani hawakujua ni kwanini askari hao wamemshikia mtutu mtu huyo. Taratibu Mzee Godwin akanyoosha mikono yake juu, huku akiwa bado hajageuka kuwatazama askari hao. Askari mmoja akamkonyeza mwenzake amfwate mzee Godwin, kwenda kumfunga piungu.
 
Kwa umakini mkubwa askari huyo akaanza kutembea kwa kunyata huku bunduki yake aina ya SMG akiwa ameishika vizuri mikononi mwake. Kitendo cha kumfikia Mzee Godwin, ikawa ni moja ya kosa kubwa sana, mzee Godwin akageuka na teke la mguu wa kustoto, lililo mchota askari huyo miguu yake na kujikuta akianguka kama mzingo na bunduki yake akiitupia pembeni, kwa uharaka wa hali ya juu, mzee Godwin, akaichomoa bastola yake iliyo ichomeka kiunoni mwake kwa nyuma. 

Hakuhitaji hata kuwa na huruma na askari aliye mshikia bunduki, akibabaika. Akapimga risasi moja ya paja askari huyo, akaanguka huku akilia kwa uchungu na maumivu makali sana.
 
Mlio wa bastola yake ukawafanya watu kutawanyika, si madaktari wala wagonjwa walio jiweza, kila mmoja akaikoa roho yake, hata kushangaa kwao kukaingia doa. Askari wengine walio kuwa kwenye maeneo tofauti ya hospitali, baada ya kusikia mlio huo wakakimbilia katika jengo hilo la maabara.
 
Askari aliye anguka chini, baada ya kuona mwenzie ametandikwa risasi ya paja na anaendelea kuhangaika hangaika chini, huku akilia, akajaribu kurusha teke la chini, ambalo lilimuangusha mzee Godwin. Askari huyo akanyenyuka, huku akikunja ngumi, mzee Godwin akasimama huku akitabasamu, kwani akimuangalia askari huyo, umri wake wapata miaka ishirini na tatu hadi tano.
 
Askari akaanza kurusha ngumi zake, zilizo mkosa Mzee Godwin, kwani aliweza kuzikwepa zote huku akiendelea kumuonea huruma kijana huyo. Mzee Godwin akakimbia kwa kasi, askari huyo akanzanza kumfukuza, mzee Godwin akafika hadi karibu ya ukuta, kwa uwezo mkubwa alio kuwa nao akakanyaga ukutani, na kujigeuza kwa kasi, askari huyo akakutana na teke zito la kichwa lililo muangusha chini, na kupoteza fahamu hapo hapo.
 
“Nice job, kijana”
Mzee Godwin alizungumza huku akijiweka sawa koti lake. Akiwa katika kordo hiyo, askari mmoja akajitokeza akiwa na bunduki. Askari akaanza kufyatua risasi kwa mawenge yaliyo muingia baada ya kumuona wezake wakiwa wamelala chini, mmoja akiwa ametulia kimya na mwengine akiendelea kulia huku damu nyingi zikiwa zimesambaa kwenye sakafu.
 
Mzee Godwin, akauvamila mlango ulipo mbele yake, na kuingia ndani ya chumba hicho, alicho wakuta madaktari wawili wakiwa wamelala chini ya meza kwa woga. Mzee Godwin akaufunga mlango kwa ndani kisha akaichomoa bastola yake.
“Simameni”
Aliwaamrisha askari hao, wakatoka chini ya meza huku kila mmoja akionekana kuwa ni muoga kupindukia, kwani haja ndogo ilianza kuitotesha suruali yake.
 
“Vueni nguo haraka”
Kila walicho ambiwa ndicho ambacho madaktari hao waliweza kukifanya, Mzee Godwin naye akaanza kuvua nguo zake na kubakiwa na nguo za ndani.
“Wewe kikojozi vaa hizi”
Akamrushia daktari nguo zake, kisha yeye akachukua nguo za daktari mwengine. Alipo maliza kuvaa mavazi hayo ya kidaktari pamoja na miwani, akamuamrisha daktari huyo kuvaa, kofia yake aliyo kuwa ameivaa.
 
       Gari za polisi wa vikosi vya kutuliza ghasia F.F.U, zikazidi kuongezeka katika hospitali ya muhimbili, hii ni baada ya kupata habari kwamba, gaidi Mzee Godwin ameweza kuonekana katika hospitali hiyo na kuwashambulia askari wawili. Wananchi walipo katika eneo la hospitali wakawekwa chini ya ulinzi mkali, hapakuwa na aliye ruhusiwa kuingia ndani ya hospitali, wala aliye ndani ya hospitali hakuruhusiwa kuweza kutoka nje. Hii yote ni kuhakikisha gaidi wao hajichanganyi na wananchi na kuweza kutoweka katika eneo la hospitali.
                                                                                                   ***
       Nguvu na umahiri wa kikosi cha bwana Rusev kikazidi kuongezeka siku hadi siku, akazidi kuchukua vijana mbali mbali katika mataifa ya kiafrika, akawaingiza katika kikosi chake ili kuhakikisha mipango yake anayo ipanga inakwenda vizuri sana.
“Muheshimiwa mipango yako ni nini?”
Mshauri wake wa karibu alimuuliza bwana Rusev mara baada ya vijana zaidi ya ishirini kutoka nchi ya Afrika kuweza kuingizwa kwenye kambi yake, iliyopo chini ya bahari.
“Nahitaji kuifanya dunia nzima kuwa na kiongozi mmoja tu, ambaye ni mimi”
 
“Ila muheshimiwa itawezekana kweli, kutokana mataifa mengi yana nguvu sana”
“Kwa ukimya ambao tumeufanya tangu kifo cha Pual Hennry Jr, sasa ninakwenda kuitingisha dunia. Nahitaji ndoto za Adolf Hitler niweze kuzitimiza mimi”
Bwana Rusev alizungumza huku akitabasamu. Akiendelea kuwaangalia vijana hao, wakinza kupatiwa mafunzo maalumu katika ngome yake, ambayo ni ngumu sana kwa mtu kuweza kuifahamu.
Simu ya mshauri wake, ikaingia ujumbe wa video ulio mstua sana, ikabidi amuonyeshe bosi wake bwana Rusev.
 
“RUSEV, RUSEV RUSEV, Umenimiss eheee”
Sauti na sura ya Jaquline, vinaoenekana kwenye simu hiyo. Bwana Rusev akajikuta akiitumbulia macho video hiyo aliyo tumwa na muda mchache ulio pita.
“Huyu Malaya yupo hai?”
Bwana Rusev alizungumza kwa hasira huku akiendelea kuitazama video hiyo.
“Najua utashangaa, kuniona nipo hai. Hahahaaaaaa, ngoja niende kwenye point muhimu. Niliapa kwamba nilazima nitakuua, na hii ni moja ya ahadi nitakayo ifanya siku na muda wowote.”
 
“Ila kabla ya kufanya hivyo kutana na mgeni rafiki yako mpendwa”
Video hiyo ikasogezwa pembeni, ambapo bwana Rusev akaiona sura ya Agnes akitabasamu.
“Umewaacha wezangu wamekwenda jela kwa ajili yako, sasa tambua kazi ni moja tu. Tutakupeleka kuzimu mw………”
Bwana Rusev kwa hasira akaizima video hiyo ya vitisho kutoka kwa mabinti ambao anawatambua vizuri sana.
“Muheshimiwa ut…..”
Bwana Rusev akamtandika ngumi nzito mshauri wake huyo, kisha akaondoka kwa hasira na kuwafanya baadhiya askari wake kushangaa tukio hilo.
                                                                                                     ***
       Mzee Godwin kuchungulia dirishani, akaona askari wengi wakiwa wamemiminika katika eneo la hospitalini, wakiwa na silaha nzito pamoja na mbwa wakali.
“Shitii”
Mzee Godwin alizungumza huku akijikuna kichwa chake
“Shika meza huko”
Aliwaamuru madkatari hao kuisukumia meza hiyo kubwa kwenye mlango, kwani alihisi muda wowote mlango unaweza kuvunjwa na askari walipo nje.
 
“Laleni chini”
Mzee Godwin aliendelea kuwaamrisha madaktari hao walio tii, kwani pasipo kuweza kufanya hivyo wanaweza kupoteza maisha yao. Katika kukichunguza chumba, kwa bahati nzuri akaona sehemu ya juu kuna sehemu inaweza kufunguka.
“Mukinyanya kichwa tu, ninawapasua ubongo”
Mzee Godwin alizungumza huku akipanda juu ya meza hiyo, akiendelea kutafuta ni jinsi gani anaweza kuifungua sehemu hiyo yenye mfuniko mgumu kiasi. Kwa bahati nzuri akafanikiwa kufungua mfuniko huo, akachungulia juu ya dari, akakuta uwazi mkubwa ambao unaweza kumruhusu yeye kuweza kupita pasipo wasiwasi.
 
“Hivi ni kwanini tusivunje mlango?”
Askari mmoja alishauri, wezake kwani ni muda umekatika wamekaa nje ya mlango huo wakishikilizia kitu kinacho endela ndani.
“Humo ndani kuna madaktari tukifanya hivyo tunaweza kuwapelekea wakauliwa
“Ila mkuu tutaendela kukaa hapa hadi saa ngapi?”
Hapakuwa na jibu lolote alilo litoa mkuu wao huyo, anaye hofia maisha ya madaktari hao.
 
Mzee Godwin akaendelea kufwata njia hiyo iliyopo juu ya dari, akafanikiwa kufika kwenye moja ya sehemu yenye upenyo mdogo, akatizama chini na kugundua ni chumba cha kuhifadhia vitu vya maabara, akapatizama hapakwa na mtu wa aina yoyote, Kwa kutumia vidole yake akavingiiza kwenye matundu madogo ya mfuniko huo kisha akaufungua, na kuusogeza pembeni. Akashusha kichwa taratibu na kuchungulia chini, alipo hakikisha kwamba hakuna mtu yoyote, taratibu akashuka chini, kimya kimya pasipo kutoa kishindo cha aina yoyote.
“Shitiii pesa zangu?”
Mzee Godwin akajilaumu sana, kwani kiasi kikubwa cha pesa amekiacha kwenye koti alilo mvalisha daktari aliye kuwa akijikojolea kwa woga. Hakuwa na jinsi tena ya kuweza kurudi katika enoeo hilo, akachungulia dirishani akakuta eneo hilo lipo kinya, ila kuna umbali wa gorofa moja chini.
 
“Hapa nashuka”
Mzee Godwin alijisemea kimoyo moyo, taratibu akaanza kushuka, kwenye ukuta huo, wenye vishikizo vidogo vidogo. Akafanikiwa kufika chini. Sehemu aliyo simama imezungukwa na maua maua mengi. Akanyata taratibu hadi kwenye sehemu ya lango la gorofa hilo, akakuta askari wengi wakiwa wanaendeleza ulinzi.
      Akaachana na askari hao, na kuanza kutembele kuelekea kwenye upande wa jengo la kuhifadhia damu, akafanikiwa kufika nyuma ya jengo hilo pasipo kuweza kustukiwa. Akiwa katika kuchungulai chungulia, akastukia akishikwa bega kwa nyuma
 
“Dokta unafany……..”
Baada ya kutazamana na mtu anaye msemesha, askari huyo akanyamaza gafla, baada ya kugundua huyo anaye muita daktrai ni gaidi. Mzee Godwin kwa haraka sana, akaizungusha kwa nguvu shingo ya askari huyo aliye mtumbulia macho na kuivunja. Kwa haraka akamvua mavazi askari huyo na kuchukua nguo zake. Alipo maliza kuvaa nguo za askari huyo, pamoja na kofia lake aina ya helment. Akaanza kutembea kuelekea getini kwa kujiamini sana.
“Vipi unaelekea wapi?’
Askari mmoja alimuuliza baada ya kumuona akihitaji kufungua mlango wa gari hilo.
 
“Nahitaji kwenda kuchukua askari wengine”
Mzee Godwin alizungumza huku akibadilisha sauti yake, kutokana huyo aliye muuliza anacheo kikubwa zaidi ya mavazi aliyo yavaa, ikambidi awe mpole kidogo kusikilizia jibu la mkubwa wake huyo, anaye onekena kuchanganykiwa kidogo.
“Nipeleke kwa waziri wa ulinzi”
“Wapi nyumbani kwake?”
“Ndio muheshimiwa ameniiita”
Mzee Godwin akatii, wakaingia kwenye gari hilo aina ya ‘Landrove defender’ na kuondoka katika eneo hilo la hospitalini pasipo hata kustukiwa na askari yoyote, hata aliiye mpakiza hakuweza kumtambua.
 
Kutokana na king’ora alicho kiwasha, magari mengi barabarani yaliwapisha. Haikuwachukua muda mwingi sana wakafanikiwa kufika katika jumba la waziri Eddy, mkuu huyo wa polisi akashuka na kuelekea katika moja ya hema walilo kaa viongozi wakubwa. Eddy taratibu akiwa anatoka sebleni kwake pamoja na Rahab. 

Macho yake akaitazama gari ya polisi iliyo fika muda si mrefu. Askari huyo ambaye ni mzee Godwin aliyomo ndani ya gari hiyo, alipo yageuza macho yake kutazama nje yakakutana na Eddy stuka na kuanza kumtilia mashaka.
                                                                                 
SORRY MADAM (18)  (Destination of my enemies)

Wakiwa katika mtazamano huo, ambao mzee Godwin hakuhitaji kuweza kuyakwepesha macho yake, kumtazama Eddy ili asistukiwe. Ving’ora vya gari za polisi vikaingia ndani ya jumba hilo huku nyuma kukifwatiwa na msafara mkubwa wa magari yapatayo nane, ikiashiria raisi anaingia katika eneohilo.
“Sogeza gari yako pembeni?”
Askari mmoja alimuamuru Mzee Godwin pasipo kujua ni gaidi wanaye mtafuta. Mzee Godwin akawasha gari na kuisogeza pembeni na kuzipa nafasi gari zinazo ingia kukaa ktika eneo ambalo alikuwa amelisimamisha gari la polisi.
 
Eddy hakuwa na haja ya kuendelea kumtazama askari huyo, akiamini kwamba atakuwa amemfananisha kutokana na mawenge ya kumfikiria sana mzee Godwin. Akajumuika pamoja na Rahab kumpokea muheshimiwa Raisi bwan Praygod Makuya. Moja kwa moja wakaelekea kwenye mahema ambayo, wapo viongozi wengine walio weza kufika katika maombolezo hayo.
 
“Ina maana hata Eddy mwenyewe hajanitambua?”
Mzee Godwin alijiuliza huku, akiiweka sawa gari hiyo ya polisi kutoka katika geti la jumba la waziri Eddy. Moja kwa moja akaanza safari ya kuelekea nje ya jiji la Dar es Salaam ambapo, amemuacha Tom. Moyoni mwake akajikuta akianza kuingiwa na uchungu mzito, juu ya kifo cha mke wake. Baadhi ya matukio yanayo husiana na mke wake kipindi wakiwa katika mahusiano, zikaanza kumjia kichwani mwake. Na ukakamavu wake wote machozi yakaanza kumwagika sana.
Kila jinsi alivyo zidi kukumbuka matukio mema ya mke wake hadi anamzalia mtoto wa kiume ambaye ni Eddy, hasira na uchungu ndivyo vilivyo zidi kuongezeka, akajikuta akizidisha mwendo kasi wa gari hiyo ya polisi.
 
Kumbukumbu zake, zikahamia kwenye siku ambayo dokta wa familia alipo weza kumpa taarifa kwamba Eddy si mwanae wa kumzaa, ila ni mtoto wa pacha wake. Uchungu, ukaizidisha hasira yake, akiamini kwamba kwa makosa aliyo weza kuyafanya mke wake ndiyo yalipelekea familia yake iliyo kuwa na faraha na amani kuweza kupangaranyika, na uhasama mkubwa ukatawala kati ya baba na mke pamoja na mtoto.
Gafla mzee Godwin akajikuta akifunga breki za gafla, kwa kadri ya uwezo wake, akajikuta akiikwepa gari ndogo, iliyo hama na kumfwata upande wake huku nayo ikiwa katika mwendo kasi.
 
   ***
“Nastahili kufaa mimi”
Maneno ya binti mmoja, aliye lewa, alizungumza huku akizidi kugugumia mafumba ya pombe kali, hadi watu baadhi walipo ndani ya mgahawa huo wakaanza kumshangaa.
“Oya cheki yule manzi anavyo kata ulabu”
Kijana mmoja limuambia mwenzake aliye kaa naye karibu mara baada ya kuweza kumuona msichana huyo akiwa amesha angusha mizinga miwili ya whyne, huku akiwa na mzinga wa tatu ukimalizikia malizikia kuisha.
“Alafu ni bonge la manzi aiseee”
“Yaaa masister duu wengine wanashida kweli kweli”
“Pale utakuta anakunywa kutokana na mapenzi yamemuharibu”
“Nikamtokee nini?”
“Hembu kalmia mpododo wako hapa, dada humjui unataka ukamtokee, kwanza anaonekana ana mkwaja mrefu”
 
“Etii ehee”
“Hakuna cha etiii”
Wakaendelea kumshangaa dada huyo aliye umbika kwa maumbile mazuri pamoja na sura nzuri ya kuvutia, hadi dada huyo akawastukia kwamba vijana hao wawili wanamtazama. Akaachia msunyo wa nguvu, hadi watu wengine ambao hawakuwa na muda naye ikabidi wamtazame kwa muda.
“Shenzi nyinyi”
Dada huyo alizungumza, kwa dharau kubwa, taratibu akasimama, huku akiyumba yumba sana. Akachomoa noti mbili ya dola mia mbili kisha akamzibandika kwa nguvu mezani, taratibu akaanza kutembea huku akiyumba sana.
 
‘Nimeuaaa’
Alijisemea kimoyo moyo huku akizidi kutembea kwa hatua zakuyumba, akafika kwenye gari yake aina ya ‘Crown’, akafungua mlango wa upande wa dereva na kujitupia ndani ya gari. Kila alipo tizama mbele, akilini mwake, alikumbuka jinsi alivyo weza kumgonga mtoto mdogo, akiwa na gari yake aina ya Verosa. Kisha akkimbia kuepuka kukamatwa na polisi,
“Weee mtoto weweeeeee, poleeeeeeeee”
Alijisemea kwa sauti iliyo legea, akawasha gari yake, kabla hajaondoka, kioo cha mlango wake ukagongwa na muhudumu wa mgahawa huo ulipo maeneo ya bagamoyo.
“Samahani dada, kutokana na kiasi ulicho kunywa cha pombe, tungependa kukupa dereva akakupeleka hadi huko unapo elekea”
 
“Wewe kijana ni kum***** nini, unadhania hii gari ni ya baba yakooooooo”
Kwa tusi alilo litoa dada huyo, likamfanya muhudumu huyo kupata kigugumizi hata cha kuzungumza, dada huyo akafunga koo cha gari lake, akafunga mkanda, akakanyaga breki pamoja na mafuta na kuzifanya tairi za nyuma kuanza kuserereka kwa nguvuu, hadi watu walipo karibu na eneo hilo wakabakiw ameduwaa. Kisha akaachia breki na kuifanya gari hiyo kuchomoka kwa kasi katika eneo la maegesho, kwa bahati nzuri geti la eneo la kutokea lipo wazi. Kwa mwendo huo huo wa kasi, akafanikiwa kufika eneo la kuingia barabara kubwa itokayo mkoani na kuelekea Dar es Salaam.
 
“Waoooooooo fast and furious hahahaaaaaaaaaaaa”
Dada huyo alishangilia sana, akijifananisha na wacheza filamu ya kimarekani ijulikanayo kwa Fast and Furious. Akazidi kukanyaga mafuta, huku akihakikisha kila gari lililopo mbele yake analipita kwa mwendo mkali, huku kwa mara kadhaa akiwa anawaonyeshea kidole cha katikati madereva anao wapiti, akiashiria kuwatukana na wao si lolote wa sichochote mbele ya gari lake hiyo ndogo.
Kwa mbali katika eneo la barabara iliyo nyooka, akaiona gari ya polisi ikija kwa kasi huku ikiliza king’ora.
 
“Ahaaa mumenifwata hadi huku eneeee”
Alizungumza kwa dharau, huku akibenua midomo yake kwa dharau kubwa, akazdisha mwendo kasi hadi ikafika spidi mita mia na sabini, akiamini spidi mita kumi zilizo baki kufika mia na themanini, atazimalizia pale atakapo weza kulifikia gari hiyo ya polisi. Mita chache kutoka linapo kuja gari la polisi, gafla akahama upande wake na kuifwata gari ya polisi, nakulengana nayo uso kwa uso. 
 
Binti huyo akayafumba macho yake akiamini huo ndio mwisho wa maisha yake, kwani gari hizo zitagongana uso kwa uso, ila gafla akastukia gari yake ikipitiliza, mbele na gari ya polisi ikiwa imemkwepa, kitendo cha kulishangaa tukio hilo, akajikuta gari ikimshinda na kuanza kuserereka kuelekea pembezoni mwa barabara, akajitahidi kufunga breki, ila tayari alisha chelewa, gari hiyo ikaenda kugonga mti mkubwa wa mkuyu, na hapo hapo ikatulia, huku moshi mwingi ukiwa unatoka maeneo ya mbele, kwenye bonet.
 
“Pumbavuu”
Mzee Godwin alizungumza huku akisuka kwenye gari kwa hasira, akachomoa bastola yake, kwa mwenzo wa haraka akaelekea sehemu gari ndogo hiyo ilipo elekea, Nia na dhumuni lake ni kwenda kumshikisha adabu dereva huyo mpumbavu aliye damiria kuitoa roho yake wakati bado ana kazi ngumu mbeleni mwake.
Akaifikia gari ndogo hiyo, na kukuta dereva wake akiwa amezibwa na ftuza kubwa lililo jaa upepo mwingi. Akiwa katika kumfikiria ampige risasi afe, moto mdogo ukaanza kuwaka kwenye boneti ya gari hilo.
 
‘Wewe natakiwa nikuulie nje’
Mzee Godwin alizungumza huku akianza kumpa masaada dada huyo, mwenye mwenye nyingi zilizo mfunika usoni mwake. Akafanikiwa kumtoa ndani ya gari hilo, ili kuyaokoa maisha yake na dada huyo, akambeba na kukimbilia naye, kabla hawajafika mbali, gari hiyo ikalipuka, na kuchanguka, mzee Godwin akajikuta akianguka chini huku akiwa amemkumbatia binti huyo.
Mzee Godwin akaanza kuhema sana, huku akilitazama gari hilo likiteketea kwa moto, ulio toa moshi mwingi mweusi na unao palia sana, pale unapo uvuta. Akaanza kumffunua nywele binti huyo zilizo tanda usoni mwake, Mzee Godwin akastuka huku akiwa amemtumbulia macho binti huyo.
“MANKAAA……..!!!!”
                                                                                               ***
Zoezi la kumkamata Mzee Godwin, likawa gumu zaidi baada ya askari kugundua muhusia wanaye muhitaji amesha watoroka muda mwingi, katika ya hispitali ya muhimbili.
Taarifa zikazidi kusambazwa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kwamba endapo watamuona gaidi Mzee Godwin, basi watoe taarifa kituo cha polisi, kwani mtu huyo ni hatari sana na tayari amesha weza kuua askari walikuwa wakifanya msako huo.
Kila mtandao wa kijamii, wananchi wakaendelea kupashana taarifa na kusambaza picha za Mzee Godwin akiwa katika mikao tofauto tofauti, kuanzia alivyo kuwa kijana hadi sasa alivyo kuwa mzee.
 
Ulinzi ukazidi kuimarisha katika mipaka yote ya kutoka nchini Tanzania, idadi ya polisi ikazidi kupelekwa mipakani, ili kuhakikisha kwamba Mzee Godwin anatiwa nguvuni.
Kwa jinsi jeshi lilivyo mpenda, waziri Eddy, alivyo wafanyia mabadiliko muda mchache tangu kuingia kwake madarakani, basi wakajikuta wakifanya kazi kwa juhudi kuhakikisha wanamfurahisha kiongozi wao huyo.
 
    ***
Makaburi matatu yaliyo chimba katika eneo la jumba la waziri Eddy, yakaandaliwa kwa kuweza kuhifadhia miili mitatu ya wapendwa wa Eddy pamoja na Shamsa. Jinsi Eddy kila alilivyo yatizama majeneza matatu yaliyopo mbele yake, machozi ya uchungu yakazidi kumwagika. Hakuamini mke wa mtoto wake alio pambana kadri ya uwezo wake leo wamesha poteza pumzi.
 
Eddy taratibu akapiga magoti kwenye jeneza la Junio, lililo funguliwa ili aweze kutoa heshima zake za mwisho kwa mwanaye huyo. Jinsi anavyo mtazama haamini kama mwanaye leo amekuwa mfu.
“Junio, Junio, Dady….ni… nipo hapa nimekuletea zawad…..i mwanangu wake up my boy. Kwa kwaa nini uondoke wakati hata shule ba….baadoo hujakwenda”
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika sana, hakuwa ambaye aliweza kuyazuia machozi yake pale Eddy alipokuwa akiyazungumza maneno hayo.
 
“Junio I love you my son”
Eddy alizungumza kwa uchungu zaidi, huku akikumbua jinsi alivyo kuwa akicheza na mwanaye, mpira nchini brazil kwenye fukwe zilizo tulia. Akakumbuka jinsi Junio alivyo mfunga goli zuri walipo kuwa wakicheza mpira huo na jinsi alivyo kuwa akishangilia na wezake.Eddy akaangua kilio kikubwa zaidi, kilicho wafanya walinzi wake kumnyanyua na kumuhamishia kwenye jeneza la Phidaya.
 
Eddy akakaa kimya huku akimtazama Phidaya mke wake, mrembo kupita wanawake wote alio wahi kuwaona dunia, akajikuta akiachia tabasamu lililo ambatana na machozi mengi ya uchungu. Alicho kifanya ni kupitisha kiganja chake cha mkono wa kulia katika shavu la Phidaya, aliye wa baridi sana. Eddy akajikuta akishindwa kuzungumza chochote zaidi ya kufuta machozi yake, na kupiga hatua moja mbele kwenye jeneza la mama yake.
 
“Mom…….”
Eddy aliita kisha akakaa kimya, akamtizama mama yake huyo aliye weza kumfundisha mambo mengi. Kumbukumbu za mama yeke alivyo weza kutekwa na mee Godwin, Afrika kusini na kupelekwa kwenye mapango ya utumwa, na jinsi alivyo weza kumuokoa, Eddy akajikuta akitetemeka kwa hasira na uchungu mwingi. Machozi yakazifi kumwagika, huku akiwa ameyang’ata meno yake kwa hasira kali. Taratibu damu za pua zikaanza kumwagika, kizunguzungu kikali kikamkata, akayumba mara ya kwanza ya pili walinzi wake wakamdaka asianguka chini.
 
Tukio hilo likamuogopesha sana Shamsa, aliye simama nyuma yake, kwa mara nyingine nguvu zikamuishia Shamsa na kujikuta akikaa chini mwenyewe bila hata kupenda. Roho ya Rahab, ikazidi kumuuma kwani uwezo wa kutenda msaada kwa familia ya Eddy, anao ila akifanya msaada wa kuwafufua, watu wote watamkimbia, na kuamini kwamba yeye si mwanadamu na itakuwa ni miongoni mwa kasfa chafu kwa raisi Praygod, kwamba ameoa jinni.
  
    ==> ITAENDELEA
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts