Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 19 & 20 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 19 & 20 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Wednesday, January 18, 2017 | 5:15:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
 Eddy akajikuta akitetemeka kwa hasira na uchungu mwingi. Machozi yakazifi kumwagika, huku akiwa ameyang’ata meno yake kwa hasira kali. Taratibu damu za pua zikaanza kumwagika, kizunguzungu kikali kikamkata, akayumba mara ya kwanza ya pili walinzi wake wakamdaka asianguka chini.
 
Tukio hilo likamuogopesha sana Shamsa, aliye simama nyuma yake, kwa mara nyingine nguvu zikamuishia Shamsa na kujikuta akikaa chini mwenyewe bila hata kupenda. Roho ya Rahab, ikazidi kumuuma kwani uwezo wa kutenda msaada kwa familia ya Eddy, anao ila akifanya msaada wa kuwafufua, watu wote watamkimbia, na kuamini kwamba yeye si mwanadamu na itakuwa ni miongoni mwa kasfa chafu kwa raisi Praygod, kwamba ameoa jinni.
   
ENDELEA
Madaktari waliopo katika eneo hilo wakaanza kumpatia Eddy huduma ya kwanza pamoja na Shamsa, ikawalazimu kuweza kusimamisha hudmua za mazishi kwa muda, kusubiria wahusika wakuu kkukaa katika hali nzuri. Baada ya lisaa, Eddy na Shamsa wakarejea katika viwanja vya hapo kwenye jumba lake kuendelea na mazishi ya familia yake. Rahab hakuwa na jinsi zaidi ya kuacha mazishi hayo kuweza kufanyika, huku moyoni mwake akizidi kuumia, akimuhurumia kijana mdogo Junio, kwani umri unampasa sana kuweza kuendelea kuishi katika dunia hii. 
 
Viongozi wakubwa wakaanza kuondoka katika jumba la Eddy, kila mmoja akiamini kwamba kazi ya Mungu haina makosa na wengine wakiingiwa na hofu pamoja na mashaka makubwa ya kutaka kujua ni lini Mzee Godwin anaweza kukamatwa mikononi mwao.
 
“Eddy jikaze kaka yangu, tutazidi kuwa pamoja”
Rahab alizungumza maneno ya kumfariji Eddy huku akiwa amemkumbatia
“Sawa dada Rahab”
“Ina bidi upae mapumziko ya kwenda mbali na hapa, ili akili yako ikatulie”
“Hapana Rahab, hapa ni nyumbani kwamngu na ndipo walipo lala wapenzi wangu, siwezi kwenda popote nitakaa hapa hapa”
“Hapana Eddy, inabidi ukatafute sehemu ya kwenda kutuliza akili wewe pamoja na Shamsa, tambua ya kwamba unavyo endelea kukaa na kutazama hayo makaburi huo weza kusahau kamwe”
 
“Ni kweli siwezi kusahau, ila……”
Eddy akastukia akipigwa busu zito la mdomo na Rahab, jambo lililo mstua sana.
“Madam samahani unafanya nini?”
Eddy alizungumza huku akijitoa mikononi mwa Rahab
“Unaogopa nini Eddy, tambua hapa tupo chumbani peke yetu”
“Namuheshimu muheshimiwa”
“Hayupo”
Rahab alizungumza huku akianza kuvua kitenge alicho jifunga kiunoni mwake na kubakiwa na skintait, pamoja na tisheti nyeusi alivyo vaa, iliyo bandikwa picha ya Junio, Phidaya pamoja na mama Eddy.
                                                                                                ***
Mapigo ya moyo ya Mzee Godwin yakaanza kumuenda mbio, akajaribu kumtingisha Manka aweze kuamka, ila Manka hakuweza kujibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kukaa kimya. Mzee Godwin gafla akasikia minong’ono ya watu nyuma yake, akageuka na kukuta vijana wawili wakiwa wamesimama huku wakichukua tukio la kuwaka moto la gari hiyo ndogo.
Walipo muona mzee Godwin wakastuka, kwani nao ni miongoni mwa watu walio weza kuiona picha yam zee Godwin kwenye mitandano ya kijamii akitafutwa kama Rubin na jeshi la polisi la Tanzania.
“Huyu si ndio yule gaidi”
 
Mmoja aliropoka huku akiigeuzia simu yake upande aliopo mzee Godwin ili kumchukua video. Kama mbogo aliye uliwa mwanaye, mzee Godwin akanyanyuka kwa kasi ya ajabu na kuwarukia vijana hao masharo baro. Akaanza kuwatandika ngumi za kutosha huku akiwatukana matusi ya uchungu sana. Vijana hao walilia kama watoto wadogo, wakajutia ni kwanini walisimamisha gari na kuja kushuhudia ajali hiyo. Mzee Godwin akachomoa mkanda wa suruali yake na kuandelea kuwachapa vijana hao kwa hasira kali, hadi wakapoteza fahamu.
Mzee Godwin akamgeukia Manka, kwa bahati nzuri akamkuta akitingisha tingisha mkono mmoja, kwa haraka akamuweka begani na kuanza kukimbia naye kuelekea alipo simamisha gari la polisi, akamuingiza Manka ndani na kuondoka naye katika eneo hilo,
 
Kila alipo mtazama binti yake huyo, waliye potezana naye miaka mingi ya nyuma roho yake ikaingiwa na furaa kubwa sana, moyoni mwake akaanza kumuomba Mungu ampe binti yake nafasi nyingine ya kuweza kuishi.
Majira ya saa mbili usiku akafika katika     handaki alilo muacha Tom, kwa haraka akafungua mfuniko wa kuingilia kwenye handaki hilo kisha akamshusha Manka ambaye bado fahamu hazijamrejea.
 
“Tom fungua mlango wa chumba cha kwanza”
Mzee Godwin alimuamrisha Tom huku akiwa anahema sana kutokana na kuchoka sana pmoja na wasiwasi mwingi unao mtawala. Akamlaza Manka juu ya kitanda.
“Babu huyu naye ni nani?”
“Utamjua hembu tumpe nafasi ya kuweza kupumzika?”
“Amefanyaje?”
“Heiii Tom sihitaji maswali Mengi”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira na kutoka nje ya chuma hicho, Toma akamtazama kidogogo Manka usoni kisha na yeye akatoka.
                                                                                                 ***
Wasamaria wema walo kuwa wakikatika katika barabara kuu, yakutokea mikoa ya Tanga na Arusha, wakasimama kwenye sehemu walipo ona moshi mwingi ukiendelea kuonekana katika upande wa pili wa barabara. Abiria waliomo katika basi la Ngorika, wakashuka kwenda kujaribu kuangalia gari hilo linalo teketea kwa moto. 

Wakakuta vijana wawili wakiwa wamelala pembeni huku wakionekana kupoteza fahamu na miili yao ikiwa imajaa makovu ambayo, hakuna ambaye aliweza kuyatilia mashaka kwani waliamini kwamba ajali hiyo ya gari ndogo ndio imeweza kusababisha majeraha hayo.
“Niwazima hawa?”
Jamaa mmoja alizungumza huku akiwatazama. Kijana mwengine mrefu na mweusi kiasi, akawatazama vijana hao jinsi walivyo lala chini, baadhi ya watu wakataka kuwanyanyua.
 
“Hembu musiwanyanyue mara moja, sogeeni pembeni”
Alizungumza na kuwafanya watu wengine kumshangaa, kwani majeruhi hao wanahitaji msaada wao na si kuwaacha katika eneo hilo.
“Wewe kijana mjinga kweli, hao wangekuwa ni wadogo zako ungewaacha waendelee kulala hapo chini?”
Mzee mmoja wa kichaga alimjia juu kijana huyo anaye onekena ni mstaarabu na mtulivu sana, mwenye sura ya kipole.
“Mzee wangu nimewaomba na sijataka kutimia nguvu, hivi munavyo ona hawa wamepata ajali kweli?”
 
“Wewe unaonaje?”
Mzee huyo aliendelea kumropokea kijana huyo, aliye achia tabasamua pana kisha akaendelea kutazama sehemu walipo lala vijana hao. Kila alipo zidi kuchunguza kwa umakini eneo hilo, ndipo alipo gundua kwamba kuna mtu ambaye aliweza kuwadhuru vijana hao kwa kuweza kuwapiga sana.
 
Kitu kilicho zidi kumshangaza kwa vijana hao, shawakuweza kuporwa kitu cha aina yoyote, simu zao zipo katika eneo la tukio. Akachukua simu za vijana hao wawili, kwa bhati nzuri moja ya simu bado ilikuwa inaendelea kurekodi tukio katika eneo hilo. Akaisave video hiyo kisha akaanza kuitazama, sauti za vijana hao zikasikika kwenye video hiyo huku picha ya gari hilo linalo malizikia kuteketea kwa moto. 
 
Video hiyo ikamuonyesha mzee Godwin, akiwa amemshikila binti mmoja, ila gafla mshika kamera ya simu hiyo, akastukia akiangushwa chini na kuanza kulia kwa uchungu mkali ikiashiria kwamba mzee huyo aliweza kuwapiga vikali.
“Haya munaweza kuwachukua vijana hao”
Kijana huyo alizungumza huku akizichukua simu hizo, kisha akaituma video hiyo kwenye simu yake kisha akaituma makao makuu alipo kuwa ameitwa kwa ajili ya kazi maalumu
                                                                                                            ***
     Agnes na Jaquline baada ya kufanya tukio la kuituma video ya vitisho kwa bwana Rusev, wakaagana na mzee ambaye aliweza kuwafundisha mbinu nyingi za kupambana kutumia miili yao pasipo kutumia silaha za moto. 

Agnes aliweza kufuzu kwa asilimia mia, katika kujua mbinu hizo za kupambana. Moja kwa moja wakafunga safari hadi mjini Mosscow, huku wakiwa wameziweka nywele zao katika mfumo ambao si rahisi sana kwa watu kuweza kumstukia Agnes kwamba ni muuaji aliye weza kuhusika na kifo cha waziri wa mambo ya nje wa Marekani bwana Paul Henry Jr, mwaka mmoja ulio pita.
 
Kwa kutumia hati feki zilizo tengenezwa na Jaquline mwenye utaalamu mkubwa wa kuweza kufanya hiyo kazi, wakapanda ndege na moja kwa moja wakafunga safari hadi nchini Marekani pasipo mtu wa aina yoyote kuwastukia.
 
Wakafika salama na moja kwa moja wakaelekea katika jiji la Chikago, ambapo wakakodi chumba kwenye moja ya magorofa ambayo hutumiwa na watu kukodi vyumba pale ambapo mtu anapo hitaji kufanya kitu na kila kitu kinacho stahili kuwemo ndani ya chumba kimo ndani ya chumba.
Wakaweka mabegi yao makubwa kwenye moja ya kabati kisha, Jaquline akafungua laptop yake na kuanza kufanya moja ya kazi ambayo ni miongoni mwa mpango ambao wameupanga kuufanya
 
“Bingoo”
Jaquline alizungumza huku akiwa na furaha sana
“Nini?”
“Nimesha ipata ramani nzima ya whaite house”
Jaquline alizungumza huku akimgeuzia Agnes ramani hiyo, inayo onekana kwenye laptop.
“Hivi kweli Jack tutafanikiwa kweli kwenye huo mpango tulio upanga?”
“Agy kwa uwezo tulio nao ni lazima tuiteke whaite house, tukisha fanikiwa tu, lazima kina Fetty waweze kuachiwa”
 
“Ila mimi mwenzio naogopa, kwani hiyo kazi ni ngumu sana unajua?”
“Agnes usijali kila kitu niachine mimi, lazima tuishushe whaite house”
Jaquline alizungumza huku akiwa amejiamini sana, jambo lililo mpa faraja Agnes kupata mpiganaji ambaye anaweza kumsaidia katika mpango wa kuwatorosha Fetty, Halima na Anna, ambao wapo chini ya uangalizi wa serikali ya Marekani katika gereza la Gwantemana lililopo katikati ya bahari kwenye moja ya kisiwa kinacho lindwa sana kupita maelezo.
                                                                                                            ***
Rahab akamsukumia Eddy kwenye sofa lililopo ndani ya chumba hicho cha kupumzikia alipo kuwa ameingia Eddy kwa ajili ya mazungumzo maalumu na Rahab. Rahab akamkalia mapajani Eddy, na kuendelea kumnyonya midomo yake, kwa haraka Rahab akashusha ulimi wake kwenye sikio la upende wa kushoto la Eddy na kuanza kulinyonya, na kuufanya mwili wa Eddy kuanza kusisimka, kwa hisia kali za kimapenzi.
 
“Madam Rahab unafanyaje lakini?”
“Tulia, hii ni zawadi yangu kwako”
Rahab, hakutaka kumpa nafasi Eddy ya kuweza kufanya kitu chochote, kwani tayari alisha gundua ni wapi akimgusa Eddy hisia zinamsisimka sana. Rahab akauchukua mkono wa Eddy na kuuzamisha kwenye skintaite yake. Gafla mlanngo ukagongwa kwa nje.
“Nani?”   
Eddy aliuliza kwa sauti nzito, iliyo mlegea kiasi
“Mimi”
Sauti ya raisi Praygod ilisikika nje ya mlango na kumfanya Eddy na Rahab kukurupuka, wote wakiwa na wasiwasi mkubwa wa kufumaniwa.
                                                                                 
SORRY MADAM (20) (Destination of my enemies)

Kila mmoja akajiweka sawa mavazi yake kisa Eddy akakaa kwenye sofa, na kuanza kumwagikwa na machozi mengi. Rahab akapiga hatua taratibu hadi mlangoni na kuufungua. Akakutana na mumewe akiwa katika sura ya kujiuliza maswali ambayo asinge penda kuyazungumza kwa mdomo wake. Raisi Praygod akaingia ndani, moja kwa moja akaelekea kwenye sofa alilo kaa Eddy, kwa jinsi alivyo mkuta Eddy, wasiwasi wake taratibu ukapungua, kwani tayari wivu wa mapenzi ulisha anza kumvaa Raisi Praygod.
 
“Eddy kwenye maisha ni lazima kuna vitu ambavyo binadamu wote tutavipitia, iwe ni mchungaji, shehe, raisi au waziri, sote njia yetu ni moja. Nilazima tutaondoka duniani”
Raisi Praygod alizungumza kwa sauti ya upole iliyo  jaa hekima ndani yake, mkono wake mmoja akiwa ameuweka begani mwa Eddy.
 
“Natambua kwamba, kifo siku zote huwa kina umiza, ila hatuna budi kujikaza. Kuwa mkakamavu Eddy wananchi bado wanahitaji msaada wako katika kuwatumikia. Ukiwa kama kiongozi ukiyumba basi nao watakosa ukakamau”
Eddy akamtazama raisi Praygod kidogo kisha, akaendelea kutazama chini, akilini mwake akajutia ni kwanini ameweza kumpa nafasi Rahab ya kuushika mwili wake, tena katika siku muhimu sana kama hii.
“Nitakuandalia ndege uende,nchi yoyote utakayo ihitaji ukapumzike kwa muda ili mawazo na unyonge ukuepukie”
“Asante muheshimiwa”
 
Wakati mazungumzo yanaendelea Rahab, amekaa pembeni akiwasikiliza kwa umakini, macho ya Rahab hayakucheza mbali sana na sura ya Eddy.
“Nikutakie mapumziko mema, baby tuondoke sasa”
Raisi Praygod akanyanyuka kwenye sofa, pamoja na Rahab.
“Eddy jikaze kama nilivyo kuambia wewe ni mwanaume haya ni mapito tu hutakiwi kuyachukulia kama ni kitu kisicho isha, hakikisha unaziongoza hisia zako katika hili”
 
Rahab alizungumza maneno ya kujiamini, sana. Wakatoka ndani ya chumba hicho na kumuacha Eddy akiwa ametawaliwa na mawazo mengi. Muda haukupita sana Shamsa akaingia akiwa katika hali ya unyonge, taratibu akafika kwenye sofa alilo keti Eddy, akajilaza na kichwa chake kukiweka kwenye mapaja ya Eddy. Uso mzima wa Shamsa umetawaliwa na machozi mengi, kila alipo jaribu kuyafumba macho yake kuutafuta usingizi ila akashindwa kwani sura ya Junio mara nyingi iliweza kusumbua katika hisia zake.
“Muheshimiwa una mgeni”
Mlimzi mmoja wa Eddy alizungumza akiwa amesimama mbele ya Eddy. Eddy akatingisha kichwa kuruhusu mgeni huyo kuweza kuingia ndani ya chumba. Macho ya Eddy yakagondana na macho ya Madam Merry aliye simama katikati ya mlango, akijishauri kuingia ndani ya chumba hicho.
                                                                                                      ***
“Babu tutaendelea kukaa humu humu ndani ya hili pango?”
“Kwa nini unauliza hivyo?”
“Kwa maana naona hatuzungumzii swala lolote la kuweza kutoka ndani ya hili pango”
“Tutato………”
 
Mzee Godwin akanyamaza na kumtazama Manka aliye simama kwenye mlango wa chumba walicho muingiza muda mrefu tangu amuokoe kutoka kwenye ajali. Manka hakuamini kitu anacho kiona mbele yake, kwani kukutana na baba yake mzazi ni swala ambalo hakulitegemea kabisa na jinsi baba yake anavyo tafutwa basi hakuamini kama atakuja kumuona akiwa hai.
“Babaaa…!!”
Manka aliita huku akipiga hatua za taratibu kuelekea sehemu alipo kaa mzee Godwin. Mzee Godwin akanyanyuka taratibu na kumfwata Manka sehemu alipo simama, wakakumbatia huku wote wakimwagikwa na machozi ya furaha
“Baba upo hai?”
“Ndio mwananangu”
“Ehee kumbe ni baba na mwana!!!?”
 
Baada ya kukumbatiana kwa muda mrefu, kila mmoja akaketi kwenye kiti ili kuweza kuhojiana mambo mawili matatu.
“Baba kwa nini unaendelea kutafutwa tena na nchi nzima”
“Ni story ndefu mwanangu ila yatakwisha pale nitakapo yatimiza malengo yangu”
“Malengo gani baba”
“Utayafahamu tukiendelea kuwa pamoja. Ila Manka wangu haujabadilika sana”
“Kwa nini baba?”
“Kila nikikutazama bado ninaiona roho yangu ipo ndani mwako, natumaini utaungana name katika hili tunalo kwenda kulifanya”
 
“Baba, sihitaji kuwa adui tena na familia yako, hapa nilipo fikia panatosha baba nahitaji kufa”
“Nini? Unacho kizungumza umekifikiria kweli?”
“Ndio baba, sihitaji kuendelea kuishi, niliyo yafanya ni mengi sana, juzi juzi nimemgpnga mtoto mdogo amefariki, bado askari wanaendelea kufanya uchunguzi katika hilo”
“Je wamegundua kwamba ni wewe?”
“Lazima watakuwa wamefwatilia kila rekodi za usajili wa gari langu. Baba najisikia vibaya, niliahidi kwa Mungu wangu kwamba sinto ua tena ila imeshindika baba”
 
Mankla alizungumza huku machozi yakimwagika, mzee Godwin akamsogelea Manka hadi kwenye kiti alicho kaa, akamshikilia mikono yake miwili na kuinyanyua sura ya Manka kidogo, wakatazamana.
“Manka unatakiwa kuwa mkakamavu, bado unamiaka mingi yakuishi mwanangu, nahitaji kuweza kutimiza ndoto zako”
“Ndoto, ndoto gani baba, siwezi kutimiza ndoto zangu nikiwa ninaandamwa na polisi kwa kosa la mauaji”
“Huyo kijana uliye mgonga ana umri gani?”
“Kama miaka nane au saba hivi”
 
Mzee Godwin akajikuta akikuna kichwa chake, kwa haraka akaka kwenye kiti kinacho tazamana na moja ya computer, kwa bahati nzuri computer hizo zimeunganishwa na internet, kwa haraka akaanza kutafuta kitu alicho hitaji kukitafua kupitia kwenye mtandao wa jeshi la polisi, kutokana yeye alikuwa ni kiongozi wa jeshi, ni mambo mengi na siri nyingi za nchi ya Tanzania anazifahamu.
Akaingiza namba za siri ambazo hutumika kufungulia mtandao huo wa polisi unao  husika katika maswala ya upelelezi. Akakutana na namba taarifa nyingi kati ya taarifa hizo ni moja ya video, aliyo onekana akiwapiga vijana alio taka kumpiga picha
 
“Fuc***”
Mzee Godwin alizungumza kwa hasira hadi Tom na Manka wakastuka
“Nini tena babu?”
“Hakuna kitu”
Mzee Godwin akaachana na taarifa hiyo, akatafuta taarifa ambayo inahusiana na ajali ya Junio Eddy. Akafanikiwa kuipata pamoja na maelezo yake.
“Manka”
“Bee”
“Njoo uone”
Manka akasimama pembeni ya mzee Godwin. Manka hakuamini macho yake kwani, picha ya kijana aliye mgonga chini ya picha hiyo kuna jina la kijana huyo ambaye ni Junio Eddy Godwin
 
’Ina maana ni mtoto wa Eddy!!?”
“Ndio”
“Mungu wangu!!!”
Manka akahisi kuchanganyikiwa, kila alipo fikiria matukio ambayo alimfanyia Eddy kipindi akiwa anasoma mkoani Arusha, ajahisi kichwa kinaweza kumpasuka kwa mawazo mabaya
“Piga picha Eddy akifahamu wewe ndio msababishaji wa kifo cha mwanae atakuacha kweli?”
Swali la Mzee Godwin likawa kama msumari wa mato ulio tua kwenye moyo wa Manka na kusabisha maumivu makali kupita maelezo.
 
 ***
 “Unaendeleaje?”
Eddy alimuuliza madam Merry mara baada ya kuingia ndani ya chumba hicho
“Nina unafuu kidogo, japo nina maumivu kwa mbali”
“Utapona usijali”
“Asante. Pole sana kwa yale yaliyo tokea”
Eddy akashusha pumzi nyingi na kumtazama Madam Merry aliye nyongea sura yake kutokana na kuumwa, kisha akamjibu kiunyonge.
“Asante”
“Tunaweza kuzungumza sisi wawili tu?”
Madam Merry alizungumza huku akimtupia  macho Shamsa aliye lala kwenye mapaja ya Eddy. Eddy akamuamsha Shamsa, akamuomba aelekee sebleni, Shamsa akatii.
 
“Natambua kwamba upo katika hali ngumu sana, ila nimeona wewe ndio mtu sahihi ambaye ninaweza kukupa taarifa hii, kabla hayajatokea yakutokea”
“Una maana gani kusema hivyo?”
Madam Merry akaka kimya kwa muda kidogo huku akiwa ametazama pembeni akionekana kuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana kisha akamtazama Eddy usoni.
“Mimi na baba…… baba yako tu tulikuwa tunashirikiana?”
“WHAT ARE YOU SAY………!!!??”(UNASEMA NINI………!!!??)
 
Eddy alizungumza huku akiwa amemkazia macho Madam Merry aliye anza kutetemeka kiasi.
“Ndio, leo nimekuja kukiri kilakitu kwako, sihitaji kufa pasipo kuweza kuikiri dhambi hii. Miaka kadhaa ya nyuma niliweza kuungana na baba yako. Alitokea sana kunipenda Godwin, nikajikuta nikizama kwenye dimbwi la mapenzi yake……”
Madam Merry alizungumza kwa uchungu huku machozi yakianza kumwagika usoni mwake
“Lengo kubwa lilikuwa niweze kupata nguvu ya kulipiza kisasi cha mume wangu Derick, uliye muua kwa kumkata kata vipande kama mnyama pori.”
 
“Iliniuma sana Eddy lile tukio, halikufutika moyoni mwangu kiurahisi kama ulivyo dhani. Hii ni kutokana na Derick kuwa ndio mwanaume wangu wa kwanza kunivua usichana wangu”
“Eddy roho yangu ilijaa unyama kama unyama ambao ulinitendea kwa mume wangu, hata kama naye aliweza kukuulia mwanao. Nilimuingiza John rafiki yako kipenzi kwenye kikosi cha Mzee Godwin, kutokana pia nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Johm.”
 
Machozi yakaanza kumlenga lenga Eddy usoni mwake
“Nilimtumia John kuweza kukupata wewe, akutese akunyanyase ili adhima ya moyo wangu iweze kukamilika. John alikupenda sana, tena sana. Ila kutokana na ushetani wangu na nguvu ya mapenzi kati yetu, iliweza kumbadilisha na kuwa adui yako namba moja”
“Madam Stop, I don’t want hear anymore”(Madam acha, sihitaji kusikia zaidi)
Eddy alizungumza huku machozi yakimwagika, matukio ya kikatili aliyo weza kufanyiwa na rafiki yake John yakaanza kumjia kichwani mwake, akakumbuka jinsi alivyo weza kumuua John na Sheila uchungu ndivyo ukazidi kuongezeka moyoni mwake
 
“Eddy yoyote katika yote mimi ndio msababishaji wa maisha yako kuingia uhasama na wote, hii nikutokana na wivu wa mapenzi nilio kuwa nao juu yako”
“Wivu, eheheeee, wivu kivipi?”
Madam Mery akaka kimya kidodogo huku akimtazama Eddy aliye simama akizunguka zunguka ndani ya chumba hicho akionekana kuchanganyikiwa kiasi.
 
“Kipindi tukiwa kwenye mahusiano, niligundua kwamba upo katika mahusiano na Salome, iliniuma sana, kwani nilipo gundua Salome ametembea na wewe, kisha akatembea na mkuu wa shule ambaye alikuwa ni muadhirika, iliniuma sana. Nikajiapiza kuhakikisha ninafanya kitu utakacho jutia maisha yako yote.”
Madam Mery alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi, taratibu akapiga magoti chini huku akiendelea kulia kwa uchungu mwingi.
“Ila mimi nilitembea na Salome kabla hajaadhirika, na hata hapa ukinipima sina HVI”
“Nalitambua hilo Eddy”
 
Shamsa akiwa sebleni amejilaza kwenye sofa, kwa haraka akurupuka na kusimama hadi walinzi walipo sebleni wakamshangaa. Akili yake kwa haraka ikamkumbuka Madam Mery ni mke wa waziri wa fedha nchini Somali, na ndio huyo huyo ambaye siku walipo kuwa Somalia na Eddy, alikuja kwenye hoteli yao na kulala na Eddy, jambo ambalo lilianza kumpa mashaka Shamsa. Akaanza kutembea kwa haraka hadi kwenye mlango wa chumba alipo Eddy, akataka kuingia ila akasita, akisikia miguno ya mtu kulia, ikambidi atege siko lake vizuri kwenye mlango.
“Muheshimiwa yupo ndani?”
Shamsa akastushwa na sauti ya askari mmoja aliye simama nyuma yake
“Ndio yupo ndani, ila anamazungumza”
“Basi kuna ili faili ningependa mpatie pale atakapo maliza mazungumzo”
“Linausiana na nini?”
 
“Na kesi ya mtu aliye sababisha kifo cha junio”
Kwa haraka Shamsa akalichukua faili na kulifungua mbele ya askari huyo hata kabla hajaondoka. Shamsa akastuka kukuta picha ya msichana ambaye alisha wahi kumuona sehemu ila kumbukumbu zake hazikumbuki ni sehemu gani ambayo aliweza kumuona. Shamsa akajikuta akiusukuma mlango na kuingia dani ya chumba hicho. Akamkuta Madam Mery akiwa amepiga magoti, wote wakamtazama Shamsa ambaye ameingia gafla,
“Dady huyu ndio aliye muua Junio”
Eddy kusikia taarifa hiyo, akastuka, kwa haraka akalichukua faili hilo na kulifunua, kitu alicho kiona picha ya Manka pamoja na jina lake pembeni.
“MANKA……..!!!! MANKA SI ALIKUFA…….??.”

    ==> ITAENDELEA
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  

                            

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts