Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 21 & 22 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 21 & 22 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Monday, January 23, 2017 | 6:24:00 PM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA   
Kwa haraka Shamsa akalichukua faili na kulifungua mbele ya askari huyo hata kabla hajaondoka. Shamsa akastuka kukuta picha ya msichana ambaye alisha wahi kumuona sehemu ila kumbukumbu zake hazikumbuki ni sehemu gani ambayo aliweza kumuona. Shamsa akajikuta akiusukuma mlango na kuingia dani ya chumba hicho. Akamkuta Madam Mery akiwa amepiga magoti, wote wakamtazama Shamsa ambaye ameingia gafla,
“Dady huyu ndio aliye muua Junio”
Eddy kusikia taarifa hiyo, akastuka, kwa haraka akalichukua faili hilo na kulifunua, kitu alicho kiona picha ya Manka pamoja na jina lake pembeni.
“MANKA……..!!!! MANKA SI ALIKUFA…….??.”
   
ENDELEA
“Manka………!!!”
Madam Mery alizungumza huku akinyanyanyuka, Eddy na Shamsa wote wakamgeukia na kumshangaa.
 
“Hembu nione”
Madam Mery akachukua faili alilo lishika Eddy, macho yakamzidi kumtoka huku akimtazama Manka kwenye picha,
“Unamfahamu huyo?”
Eddy aliuliza huku akimtazama Madam Mery ambaye anaonekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana. Madam Merya akajibu kwa kutingissha kichwa akionekana kumfahamu Manka.
“Hakufa”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama Eddy usuoni kwa macho ya wasiwasi mwingi.
“Una maana gani?”
                                                                                              ***
“Ila Eddy ni chanzo cha mume mume wangu kufa”
Manka alizungumza huku akimtazama Mzee Godwin.
“Kwani, kwani uliolewa?”
“Hapana baba, ila nilikuwa na mwanaume ambaye nilimpenda sana, na alikuwa anafanana sana na Eddy”
“Nilimpenda sana yule mwanume, nakumbuka Eddy aliamua kumpa mume wangu kazi ya kwenda kumuoa Sheila aliye kuwa ni mpenzi wake, ila haikuwa hivyo kwani siku ya harusi yao ndipo walipo vamiwa na mume wangu kutekwa na kuuawa”
 
Maneno ya Manka yakamkumbusha Mzee Godwin, tukio ambalo yeye ndio alikuwa ni muhusika mkuu katika kupanga mpango mzima wa kuweza kumteka Eddy kwenye harusi yake yeye pamoja na mke wake. Huku akimtumia John kuweza kukamilisha mipango yote hiyo. Ila kitu ambacho kilimchanganya Mzee Godwin ni siku alipo gundua kwamba mtu waliye weza kumuu si Eddy, ila swali lililo muumiza sana kichwani mwake kijana huyo ni nani, na ametoka wapi. Leo ndio anapata jibu kamili kwamba yeye ndio muhusika mkuu wa kifo cha mpenzi wa mwanae kipenzi Manka.
 
Mzee Godwin taratibu akamvuta Manka hadi kifuani mwake na kumkumbatia taratibu, akaanza kumbembeleza ili asimwagikwe na machozi.
“Hatuna jinsi ya kufanya mwangu, tambua ninatafutwa ina bidi niweze kurudi makao makuu haraka iwezekanavyo”
“Makao makuu?”
 
“Ndio makao makuu ya kikosi changu cha DFE(Destination of my enemies)”
“Sawa, ila kuna Madam Mery yupo wapi?”
Mzee Godwin akamtazama Tom, kisha akamgeukia Manka. Kwa jinsi macho yam zee Godwin yanavyo oenekana Manka tayari akagundua kuna kitu cha tofauti kinacho endelea baina ya Mzee Godwin na Madam Mery, ambaye alisha tambulishwa na baba yake kama mama yake mdogo.
“Kuna kazi nahitaji nikupe kabla hatujaondoka”
 
“Sawa baba”
“Tom, huyu ni Manka ni dada yako, kuanzia hivi sasa. Jiandaeni kwa kuondoka”
Tom na Mzee Godwin wakaingia kwenye chumba amacho kimehifadhiwa pesa nyingi, wakaanza kuvikusanya vibunda vya pesa  na kuviweka kwenye mabegi yaliyo kuwa na nguo. Manka akaanza kupitia pitai vitu ambayo vipo kwenye computer ambayo baba yake alikuwa anafwatilia baadhi ya kesi ikiwemo ya kwake, hapo ndipo akakutana na sura ya binti ambaye, anakumbuka alisha wahi kuwa rafiki yake enzi za utoto.
 
“Huyu si Fetty?”
Manka alijiuliza huku akiendelea kuiangali picha ya Fetty, akasoma maelezo ya msichana huyo na kukuta habari ambayo ilimshangaza sana.
“Fetty ni gaidi?”
Mzee Godwin na Tom wakamaliza kukusanya pesa hizo, kisha wakaanza kuchukua baadhi ya silaha ambazo Tom hakujua kazi yake ni nini.
 
“Babu hizi za kazi gani?”
“Ni kwaajili ya kujilinda unaweza kutumia?”
“Hapana, nimezoea kuona kwenye video, wakina Van dame, kina Rambo wakizitumia”
“Je unahitaji kujua kuzitumia?”
“Ndio”
Tom alijibu kwa shahuku kubwa akionekana anahitaji kufahamu kutumia bunduki, jambo lililo mfanya mzee Godwin kuachia tabasam pana. Wakatoka na kumkuta Manka akiendelea kuwa bize akisoma historia ya wasichana waliopo kundi moja na Fetty wanao sadikika kuwa chini ya mikono ya serikali ya kimarekani.
 
  **
       Ni usiku ulio tawala shamra shamra nyingi katika ikulu ya Marekani ijulikana Whaite house, ulinzi mkali umeimarishwa kwenye kila kona ya eneo zima la ikulu. Wageni rasmi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi ya Marekani na hata nje ya nchi ya Marekani wameudhuria, katika sherehe ya kuzaliwa kwa raisi Markn Tosh. 
 
“Nimefika”
Sauti ya Jaquline ilisikika kwenye sikio la Agnes kupitia kifaa, maalumu alicho kifaa kwenye sikio lake, Agnes kwa kutumia mitambo maalumu ya Satelaite, anaweza kumuona Jaquline kila sehemu anapo pita, akitumia gari ndogo ya kifahari anai ya Ferrari Spider. Kwa kutumia kadi maalumu ya mualiko waliyo ipata kwa binti mmoja anaye fanya kazi ndani ya ikulu hiyo, aliweza kuionyesha kwa walinzi wanao kagua kadi ya kila mmoja anaye katika katika eneo hilo.
Wakamtazama Jaquline kwenye computer kama ni miongoni mwa waalikwa, kwa bahati nzuri wakamkuta ni mualikwa mmoja wapo.
 
“Welcome miss”
“Thank you”
Baada ya kumkagua, taratibu Jaquline akanza kupiga hatua kuelekea ndani ya ukumbi, wa ikulu. Macho ya Jaquline yakakutana na macho ya Lidya, binti aliye weza kuwasaidia katika kuingia katika sherehe hiyo, huku wakiwa wamemshirikisha katika mpango wao mzima wa kumteka raisi. 

Lidya ni binti wa kikorea aliye kulia Marekani tangu akiwa na umri wa miaka sita, baba yake Mr Jang Woo, aliweza kuhamishiwa kikazi nchini Marekani, kama mpelelezi kwenye kitengo cha CIA. Jambo lililo mlazimu kuweza kuhamia na binti yake Lidya, aliye mbadili jina kutoka katika Jang Woo hadi Lidya, hii ni kutokana na sababu za kimsingi alizo weza kuziona ni muhimu kwa yeye kufanya hivyo ili binti yake kuweza kuwa salama.
 
Lidya akiwa katika umri wa miaka kumi na mbili, baba yake aliweza kupoteza maisha kwenye shambulizi la kigaidi la kulipuliwa kwa magorofa ya kiuchumi ya Marekani yaitwayo Twin Tower, na gaidi la kimataifa Osama bin Laden. Kuanzia hapo, Lidya akaanza kulelewa chini ya uangalizi wa serikali ya kimarekani katika kikosi cha CIA(Central Intrligrnce Agency). 
 
Katika kukua kwake, wakiwa katika mafunzo ya ujasusi nchini Russia ndipo, alipo weza kukutana na Jaquline aliye muokoa kwenye ajali ya bomu lililo tegwa kwenye gari lao na magaidi walio tumwa na bwana Rusev, Jaquline akiwa ni miongoni mwa magaidi hao, ila aliweza kufanya hivyo kutokana na kutokea kumuoenea hurua binti huyo mdogo kuangamia katika kifo hicho. 

Kuanzia hapo Lidya akatokea kumpenda sana Jaquline na kumuheshimu kama dada yake.
Jaquline akajichanganya na wageni wengine, huku akifwata maelekezo kutoka kwa Agnes, aliye muacha hotelini akitumia laptop yake kuweza kuona kamera zote za ikulu hiyo zinavyo fanya kazi, hii ni baada ya kupewa namba maalumu(Code) na Lidya zinazo tumia na askari walipo chumba maalimu cha ulinzi.
 
“Jiweke karibu na raisi”
Agnes alimpa maelekezo Jaquline naye akafanya hivyo, muda wote watu wakiwa wanaendelea kupiga stori za hapa na pale, ndivyo jinsi Jaquline alivyo zidi kuendelea kuwasoma walinzi wote walipo kwenye ukumbi huo.
 
 Wakati huo huo, askari mmoja akaanza kumtilia mashaka Jaquline, kwani muda wote Jaquline yupo peke yake, hana mtu wa kuzungumza naye. Askari huyo ambaye ni miongoni mwa askari wanao mlinda raisi moja kwa moja akaelekea chumba cha ulinzi, ili kufwatilia taafa muhimu za binti huyo kwani kila mgeni aliye ingia ndani ya ukumbi huo ana taarifa muhimu zinazo julikana na ikulu, na endapo kutajitokeza tatizo lolote basi, kukamatwa kwake ni rahisi.
 
“Mvute karibu huyo binti”
Askari huyo alimuamuru mmoja wa mafundi mitambo waliomo kwenye chumba hicho cha ulinzi kilicho jaa computer nyingi, za kisasa na zenye uwezo wa hali ya juu katika matumizi yake.
“Tafuta taarifa muhimu za huyu binti”
Kijana huyo mwenye utaalamu wa mkubwa katika maswala ya coputer, akaanza kufanya kazi aliyo agizwa. Kila kilicho anza kufanyika, Agnes aliweza kukiona, kwenye laptop yake, jinsi askari huyo wanavyo jaribu kutafuta taarifa za Jaquline.
“Jina lake ni Livna Livba, uraia ni Senegal, ni mfanya biashara mkubwa”
 
Kija huyo alimjibu askari huyo, kwani Lidya yeye ndiye aliye weza kuandika taarifa hizo za uaongo na kuzituma kwenye mtandao, na endapo kutatokea kitu chochote kuhusiana na Jaquline basi iwe ni rahisi kwa yeye kuto weza kujulikana uhalisia wake halisi zaidi ya sura yake tu.
“Kuna mgeni yoyote kutoka Afrika?”
“Ngoja nicheki orodha ya wageni”
Kijana huyo anaendelea kufanya alicho agizwa. Kwa bahati nzuri akakuta jina la Livba Livna katika orodha ya wageni walio weza kuhuzuria katika sherehe hiyo”
Agnes akajikuta akishusha pumzi nyingi, baada ya kuona tukio hilo, limeweza kutatulika.
 
“Muheshimiwa kuna tatizo”
Kijana mwengine alimwambia askari huyo, aliye kimbilia moja kwa moja kwenye sehemu alipo kaa kijana huyo na computer yake, hapo ndipo alipo weza kuiona sura ya Agnes na akionekana yupo kwenye moja ya hoteli kubwa iliyopo karibu na ikulu hiyo.
“Securty code zimeibwa, narudia tena Securty code zimeibwa, number 99902, kuna tatizo narudia tena kuna tatizo”
Askari huyo alitoa taarifwa kwa walinzi wote waliopo katika eneo la ikulu, huku akitoka kwenye chumba hicho, kwa haraka sana.
 
“Kuwa makini naona kama kuna jambo linalo endelea”
Agnes alimuambia Jaquline aliye endelea kuwatazama askari waliopo katika ukumbi, akagundua baadhi ya askri wanaondoka katika ukumbi huo wakieelekea nje. Agnes akawashuhudia askari baadhi wakiingia kwenye magari na kuondoka ikulu.
“Wanakwenda wapi hawa”
Agnes alijiuliza mwenyewe pasipo kugundua kwamba tayari amesha stukiwa kwamba yupo kwenye hoteli moja iliyopo karibu na ikulu, na amejulikana kwamba yeye ndio aliye husika na mauaji ya kiongozi wao bwana Paul Henry Jr.
                                                                                                  ***
“Maana yangu huyu binti yupo hai”
Eddy akamtizama Madam Mery huku akiwa amemkazia macho makali, Eddy akakumbuka siku ambayo alirudi katika kazi ya kuwaokoa Phidaya, alipo rudia nyumbani kwa Amina, rafiki wa Manka aliye kwenda kufanya naye kazi ya kuikomba familia yake, alikuta nyumbani kwa Amina kumetulia sana, akakumbuka jinsi alivyo weza kushuka na masanduku ya pesa na kuingia nayo ndani, ndipo alipo weza kukuta michirizi mingi ya damu kwenye sakafu pamoja na ukutani, ila kabla hajagundua lolote ndipo alipo weza kuvamiwa na kikundi cha kigaidia huku, Shamsa akiwa ni miongoni mwa magaidi hao.
 
Eddy akamgeukia Shamsa na kumtazama kwa macho makali, akihisi hili jambo anaweza kuligundua, ila Shamsa hakuonyesha dalili yoyote ya kufahamu kitu kinacho zungumzwa hapo.
“Mimi ndio niliye weza kumchukua Manka”
Madam Mery alizungumza na kumfanya Eddy kumtazama vizuri Madam Mery
 
“Tuligundua uwepo wako nchini Somalia, tulifwatilia hadi sehemu ambayo ulifikizia, hadi siku unatoa na yule binti….”
“Binti, binti gani?”
“Uliye ongozana naye kwenye kazi ya kwenda kuvamia kundi lilolo mteka mke wako”
Eddy akakumbuka vizuri kwamba binti huyo alikuwa ni Amina.
“Ndipo nilipo weza kuvamia huku nyuma na kumchukua Manka na kuondoka naye, ila niliacha vijana wawili wawasubiri hadi murudi, wawaangamize”
Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbiao Eddy, kwani anayo  yazungumza Madam Mery ni mambo ambayo yanazidi kuumiza moyo wake.
 
“Vijana wangu waliweza kumuona binti huyo akirejea peke yake ndipo walipo weza kumvamia, na kumuua, ila waliondoka naye. Asubuhi yake wakamtupa barabarani”
Shamsa akastuka na kufumba mdomo wake kwa mshangao mkubwa, kwani tukio la wao kuelekea kwenye kambi ya wakimbizi majira ya asubuhi, waliweza kuuona mwili wa dada mmoja ukiwa umelazwa katikati ya barabara huku macho yake yakiwa yametobolewa,
Eddy kwa hasira akamsukuma Madam Mery kwenye sofa na kuiwahi shingo yake na kuanza kuiokaba, huku machozi yakimwagika, mwili mzima ukimtetemeka.
 
“Eddy usimuuee”
Shamsa alizungumza huku akiushikilia mkono wa Eddy ulio ishika shingo ya madam Mery, aliye anza kutepa tapa huku akijaribu kuzungumza kitu
“Ed…dy un…iniu…a hu…toj..ua siri za DFE”
“DEF, NDIO NINI WEWE MALAYAAAAAAAAAAAAAA”
Eddy alizungumza kwa hasira kali hadi Shamsa akasogea pembeni, kwani hakuwahi kumuona Eddy akiwa amekasirika kwa kiasi kikubwa kama hicho.
 
SORRY MADAM (22)  (Destination of my enemies)

Eddy akaendelea kuliminya koo la madam Mery. Kiasi cha kumfanya aanze kufurukuta kama mtu anaye kata roho.
“Babab unamuuaaaaaa”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya juu na yenye uklali sana, Eddy akaigeuza sura yake na kumtazama Shamsa, akamkuta akimwagikwa na machozi mengi usoni mwake. Eddy akamuachia Madam Mery, akakamata moja ya kiti kilichomo ndani ya chumba hicho na kukitupa chini kwa nguvu hadi kikakatika. 
 
“Fu***”
Eddy alizungumza huku akijishika kichwa cheke akijaribu kuituliza hasira yake iliyo pitiliza, walinzi wake  wapatao wanne wakaingia ndani ya chumba baada ya kusikia kishindo kizito cha kiti hicho. huku wakiwa na bastola zao mikononi.
 
“Bosi vipi?”
Mkuu wao alimuuliza ila Eddy hakujibu chochote zaidi ya kuyang’ata meno yake kwa hasira, Shamsa akatingisha kichwa akiwaashiria kwamba wamuche na watoke nje, wasi[o ubishi wowote wakatii na kutoka nje. Sauti ya meno ya Eddy jinsi anavvyo  yatafuna kwa nguvu na kwa hasira, ikatawala ndani ya chumba, kila mmoja akawa kimya kabisa hususani madam Mery ambaye hakudhubutu hata kuutingisha mguu wake akiogopa kitendo kilicho jitokeza muda mchache ulio pita kinaweza kujirudia. Isitoshe anamfahamu vizuri Eddy akiwa kwenye hasira kali anaweza hata kuua.
 
“Am sorry”
Eddy alizungumza huku akikaa kwenye sofa, akiendelea kuhema kwa hasira kama simba dume lililo kosa mawindo yake aliyo kuwa akiyasubiria kwa muda mrefu. Samahani ya Eddy hapakuwa na aliye ijibu si Shamsa wala madam Mery kila mmoja akawa kimya kama vile hayupo ndani ya chumba hicho.
 
“Shamsa kalete vinywaji”
Shamsa akamtazama Madam Mery aliye kaa kiunyonge kwenye sofa, akamtazama Eddy ila akakutana na macho makali yaliyo mfanya atoke ndani ya chumba pasipo kumuaga yoyote. Ukimya ukaendelea kutawala hadi alipo rejea shamsa akiwa na glasi tatu za juisi. Akampa kila moja glasi yake na yeye akabakiwa na glasi yake.
“Ed…….”
Eddy akamkatihs Shamsa kwa kunyanyua mkono wake wa kulia, ili Shamsa asiendelee na anacho hitaji kukizungumza kwa wakati huo. 
 
“Kalaleni tutazungumza asubuhi”
Kwa sauti nzito aliyo itumia Eddy. Madam Mery akawa wa kwanza kunyanyuka kwenye sofa, Shamsa akafwatia wote wakatoka ndani ya chumba hicho na kumuacha Eddy peke yake wakiwa hatua kadhaa kutoka kwenye mlango wa chumba hicho wakasikia mlio waglasi ukipasukua. Shamsa akataka kurudi ila madam Mery akamshika mkono akimuomba asifanye hivyo.
 
“Muache atakuwa salama”
Madam Mery alizungumza kiunyonge huku akiwa amemshika mkono Shamsa, taratibu wakaondoka. Wakapandisha gorofani kwenye vyumbavya kuiala. Machozi mengi yakaanza kumwagika Eddy, kila alipo ikumbuka sura ya mwanae, machozi yakaendelkea kumwagika, akijiona ni baba ambaye hana thamani tena kwenye haya maisha kwani ameshindwa kumlinda mwanae kuepuka ajali ambayo ilitokea. Akalishika faili lenye picha ya Manka, kwa hasira akaitoa kwenye faili hilo na kuiminya minya, kwa nguvu.
“Wewe na baba yako ni lazima niwaue”
                                                                                                            ***
“Ni m,uda wa kuonndoka sasa”
Mzee Godwin alimuambia Manka anaye onekana kuwa bize sana na kufwatilia taarifa za Fetty pamoja na wezake kwenye mtandao.
“Ni muda wa kuondoka sasa”
Mzee Godwin alizuingumza baada ya kila kitu kukiweka sawa, akishirikiana na Tom ambaye hadi sasa havi aelewi kitu cha aina yoyote
 
“Babu kwahiyo tunarudi kijijini?”
“Hapana Tom, tunakwenda nje ya nchi ya Tanzania. Tuna pesa ya kutosha ni muda sasa wa sisi kuondoka”
Tom ikamlazimu kukubali hivyo hivyo kwani anayaelewa maisha ya kijijini mwao kwamba ni magumu sana kupindukia. Wakasaidiana kubeba mabegi yenye fedha ya kutosha pamoja na silaha baadhi, wakatoka kwenye handaki hili lililopo chini ya ardhi. Wakaingiza mizigo yot e kwenye gari.
“Ila kabla hatujaondoka, Manka nahitaji uifanye kazi moja”
“Kazi gani baba?”
 
Mzee Godwina akamvuta pembeni Manka kumuambia hiyo kazi, ambayo Tom hakupaswa kuweza kuisikia, wakarudi na kuingia ndani ya gari na safari ikaanza. Ukimya mwingi ukatawala ndani ya gari, kila kinacho endelea kwernye maisha yake Tom alihisi ni kama muujiza kwani hakutarajia ipo siku atakuja kukutana na pesa nyingi kama waliyo iweka kwenye babegi yao. Usiku mzima wakautumia katika kusafiri barabarani hadi wakafika mkoani Arusha, pasipo kukamatwa na askarti, hii ni kutokana na gari waliyo itumia ni gari ya polisi. 

Majira ya saa kumi alfajiri wakawa wamewasilia mkoani Arusha, wakamshusha Manka na kumkabidhi kiasi cha kutosha cha pesa, pamoja na silaha ambazo Manka alihitaji kuweza kuzitumia katika kazi yake iliyop[o mbeleni mwake. Mzee Godwin na Tom wao wakaendelea na safari yao kuelekea nchini Kenye.
 
“Arusha nimerudi tena”
Manka alizungumza mara baada ya kuingia kwenye moja ya mgahawa ulio funguliwa, alfajiri na mapema, akapata supu nzito kwa ni tangu jana hakuweza kupata chochote mdomoni mwake, alipo jiweka sawa akaelekea kwenye moja ya nyumba ambayo anaimiliki, ili kujipanga vizuri kwa kazi ambayo anakwenda kuiendea
                                                                                                                 ***
Agnes machale yakanza kumcheza akasimam kwa haraka na kuelekea dirishani, akafungua pazia, na kutazama nje, akaona gari kadhaa nyeusi zikisimama chini ya hoteli hiyo, wakashuka watui wapatao nane walio valia suti nyeusi na kuingia kwenye hoteli yao.
“Shit”
Agenes akarudi kwa haraka kwenye laptop yake, akaizima kwa haraka na kuiweka kwenye begi lake, jambo lililo poteza mawasiliano na chumba cha mawasiliano Ikulu.
 
“Jaquline mambo yameharibika fanya utoke huko, wamenifwata huku”
Taarifa aliyo itoa Agnes ikampa waswasi mwingi Jaquline aliyomo kwenye ukumbi wa sherehe ndani ya ikula ya Marekani. Agnes kila kitu muihimu ndani ya begi lake la mgongoni, akaitoa bastola yake, akachomoa magazine, akakuta risasi za kutosha. 

Akaifunga kiwambo cha kuzuia sauti, kisha akatoka ndani ya chumba alichopo. Akaangalia kordo ndefu yenye milango mingi kwenye kila upande, akashusha pumzi nyingi, akaziweka vizuri nyele zake ndefu na kuanza kutembea kwenye kordo hiyo akiwa tayari kwa lolote litakalo jitokeza kwemye kordo hiyo kwani anatambua ni lazima askari hawa watatumia lifti kuweza kufika kwenye gorofa aliyo kuwepo yeye. Akafika kwenye milango miine ya lifti iliyopo kwenye kordo hiyo, Kila lifti ikawa inamuonyesha inakuja juu, huku namba za jinsi lifti inavyo soma, pale zinapo pita kila gorofa, ikionekana pembeni.
 
“Wapop gorofa ya sita eheee”
Agnes alijisemea huku akiendelea kuzihesabu namba hizo kwani yeye yupo gorofa ya tisa. Akataka kuondoka ila akasita, akachomoa bastola yake na kusimama kwenye moja ya lifti ya upande wa kushoto kwake. Lifti hiyo ilipo fika gorofa ya tisa mlango wake ukafunguka, macho ya askari wawili waliomo kwenye lifti hiyo yakakutana na macho ya Agnes aliye shika basatola a;iyo waelekezea. Agnes akatingisha kichwa akiwaashiria wasifanye chochote na bastola zao walizo zishika, kwa haraka akaingia ndani ya lifti hiyo na kuifunga.
 
“Wekeni chini silaha zenu”
Askari hao wakafanya kama walivyo agizwa kufanya, askari walio kuwa kwenye lifti nyingine wakaelekea kwenye chumba walicho elekezwa na wahudumu kwamba ndipo alipo binti wanaye mtafuta, pasipo kugundua kwamba wezao wamewekwa chini ya ulizni mkali wa bnti huyo huyo wanaye mtafuta..
“Upo salama Agy”
“Yap”
“Upo wapi sasa hivi?”
“Kwqenye lifti na maboya wawili nimewaweka chini ya ulinzi”
“Ok hakikisha kwamba huwaui kwani itakuwa ni hali nyingi mbaya kwetu sote”
 
“Poa dada Jaqie
Agnes alizungumza kiswahili akiamini kwamba askari hao kutoka ikilu hawaelewi chochote kinacho endelea katika mazungumza hayo, lifti hiyo ikaelekea hadi gorofa ya mwisho ya ishirini. Agnes akawaamuru askari hao kutoka ndani ya lifti, wakapandisha ngazi hadi juu kabisa ya gorofa hilo.
Askari wengine, wakafika kwenye chumba ambacho walielekezwa, hawakukuta mtu yoyote zaidi ya vitu vilivyo changuliwa changuliao ikionekana muhusika alitoroka muda mchache ulio pita. 
 
“Where is team C”(Ipo wapi timu C)
Mkuu wao aliuliza baada ya kuona vijana wake wawili hawapo, ikawabidi kuanza kufanya mawasiliano na vijana hao kupitia vifaa maalumu vya vinasa sauti walivyo vivaa kwenye masikio yao.
Kwa tukio la kuwashutkiza, Agnes akawapiga askari hao nyuma ya shingo zao, na wote wakapoteza fahamu na kuanguka chini. Vishindo hivyo vikawastua wezao ambao wahawakujua ni wapi walipo. Agnes akatazama eneo lote la juu ya gorofa hiyo, akagundua kuna moja ya gorofa ipo karibu sana na gorofa hiyo, ambayo hiyo kidogo ipo chini kidogo.
 
“Hapa naruka”
Askari wakaanza kupata mashaka na kurudi kwa haraka kwenye lifti zao, na kupandisha juu kabisa ya gorofa hiyo wakiamini ndipo walipo wezao. Wakafika gorofa ya ishirini wakapandisha kwenye gazi ambazo zinaelekea moja kwa moja juu kabisa ya gorofa hiyo, kitendo cha wao kufika tu wakashuhudia binti wanaye mtafuta akiruka kwenye gorofa nyingioni ya jirani.
“Mfwateni huyo”
 
Mkuu wao alitoa agizo ambalo vijana wake wawili wakaanza kutimua kasi, kujaribu kwenda kuruka kama alivyo fanya binti huyo anaye onekena kuwa na utaalamu wa kipekee wa kuruka sana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Agnes akasimama huku akiliweka vizuri begi lake la mgongoni, akachomo bastola yake na kuwatazama vijana wawili wanao jiandaa kuruka kumfwata, wa kwanza akajitahidi kuruka, akiwa hewani katikati ya gofa hilo kwenda jengine, akakutana na risasi mbili za miguu zilizo mfanya kupoteza muelekeo badala ya kwenda mbele akajikuta akianza kwenda chini kwa kasi, jambo lililo mstua mwenzake akasita kufanya alicho fanya mwenzake huyo aliye mshuhudia akiangukia kwenye gari lililo egeshwa chini pembeni ya gorofa hizo.
 
“LUKASSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS…………………………………………..!!!!”
Askari huyo alipiga ukelele wa maumivu na uchungu baada ya kumshudia mwenzake huyo akikata roho, yeye akiwa gorofani, kelele hizo zikawafanya askari wangine walio kuwa wakiwa huduma ya kwanza wezo kukimbilia alipo mwenzao. Agnes akatabasamu kwa dharau kisha akamnyooshea kidole cha kati askari huyo anaye lia kwa uchungu kisha akaondoka zake kwa kujiamini sana.
                                  
    ==> ITAENDELEA
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  
   

Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts