Get the latest updates from us for free

Home » , » SORRY MADAM -Sehemu ya 23 & 24 (Destination of my enemies)

SORRY MADAM -Sehemu ya 23 & 24 (Destination of my enemies)

Written By Bigie on Sunday, January 29, 2017 | 9:29:00 AM

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
“LUKASSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS…………………………………………..!!!!”
Askari huyo alipiga ukelele wa maumivu na uchungu baada ya kumshudia mwenzake huyo akikata roho, yeye akiwa gorofani, kelele hizo zikawafanya askari wangine walio kuwa wakiwa huduma ya kwanza wezo kukimbilia alipo mwenzao. Agnes akatabasamu kwa dharau kisha akamnyooshea kidole cha kati askari huyo anaye lia kwa uchungu kisha akaondoka zake kwa kujiamini sana.

ENDELEA
Agnes akaanza kushuka chini kwa kutumia ngazi katioka gorofa aliyo ingia huku mara kwa mara akifanya mawasiliano na Jaquline ambaye aliamua kusitisha zoaezi la kumteka raisi, akatoka nje, gari aliyo kuja nayo ikamchukua na moja kwa moja akaelekea sehemu ambayo Agnes alimuelekeza
                                                                                                      ***
     Hadi kuna pambazuka Eddy, hakuweza kupata hata lepe la usingizi, akanyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekaa usiku kucha, akatoka nje na moja kwa moja akaelekea kwenye makaburi ya familia yeka. Akasimama kwa dakika kadhaa akiyatazama makaburi hayo, hakuamini kwamba ni kweli familia yake imeweza kupotea gafla na kubaki akiwa peke yake, kila alipo mfikiria mzee Godwin machozi ya hasira na uchungu ndivyo yalivyo zidi kumwagika. Akastukia akishikwa mkono wake wa kushoto taratibu akaigeuza shingo yake na kumkuta Shamsa akiwa amesimama pembeni yake huku naye akionekana kuwa na huzuni nyingi sana usoni mwake.
 
“Madam Mery ameondoka”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku macho yake akiwa ameyaelekezea kwenye makaburi hayo matatu
“Amekwenda wapi?”
“Hakuniambia ni wapi alipo kwenda”
“Achana naye”
“Ila baba, kuna mambo mengi muhimu amaniambia nikuambia”
“Mambo gani?”
Eddy alizungumza huku akimtazama Shamsa usoni aliye onekena kusita kwa kile ambacho anahitaji kwenda kukizungumza mbele ya Eddy anaye mchukulia kama baba yake mlezi.
“Mbona umekaa kimya huwezi kuzungumza?”
“Ni ni kuhusiana na baba yako?”
“Baba yangu……!!”
“Ndio mzee Godwin”
 
Eddy akatazama kila kona, akamshika mkono Shamsa, wakatafuta sehemu iliyo tulia kwenye moja ya bustani zilizopo ndani ya njumba lake la kifahari.
“Alikuambia kuhusiana na nini?”
“Jana usikua alinieleza kila kitu kuhusiana na kikundi cha D.F.E. Hicho ni kikundi ambacho kimeanzishwa na mzee Godwin mwenyewe, kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba wanalipiza visasi kwa wale wote ambao waliweza kuwatemndea ubaya katika maisha yao.”
 
“Aliniambia kwamba hicho ni kikundi kikubwa sana na kina wafuasi wengi ambao wengine wamo ndani ya serikali yetu ya Tanzania, na anashirikiana nao”
“Amekutajia majina?”
“Hapana hajanitajia majina. Ila anadai wafuasi hao ni watu wakubwa sana serikalini, si Tanzania pekee bali nchi nyingi za Afrika pamoja na nchi za Amerika, ikiwemo Marekani”
Shamsa akanyamaza kimya kidogo kisha akaendelea kuzungumza kwa umakini kile alicho ambiwa kukizungumza kutoka kwa madam Mery ambaye alihofia kufanya hilo.
 
“Watu hao wana chata ndogo kwenye sehemu za miili yao, yenye maandishia meusi D.F.E. Ameneniambia kwamba msaidizi wa mambo yote ya kikundi hicho ni mtu ambaye anakujua vizuri kuanzia A hadi Z, ukimuachilia kiongozoi wao mzee Godwin”
“Ni nani huyo?”
“Alinitajia kwa jina moja tu……..JONH”
Eddy akatumbua macho yake huku akimtzama Shamsa, akiwa haamini kitui alicho kizungumza kwani kumbukumbu ya mwisho anakumbuka jinsi alivyo vikata viungo vya John kwa kulipiza kisasi cha mambo yote aliyo mfanyia.
 
“JOHN…..JOHN…….!!!”
“Ndio huyo huyo John, pia ameniambia mtu wa kwanza kuweza kulengwa katika mikakati yao ni wewe, wanataka kukuangusha chini, ten echini kabisa ya aridhi”
Eddy akajikuta akishusha pumzi nyingi, woga wa gafla ukamuingia moyoni mwake, kajasho kembamba kakaanza kumwagika kwani hakujua ni jinsi gani ambavyo wanaweza kumuangusha.
 
“Ahaa….aaaa aahaame ame kwenda wapi Madam Mery?”
“Hakuaniambia ni wapi anapo elekea kwa sasa, ila kitu kingine cha mwisho alicho niambia nikuambia ni kwamba, ujiudhuru nafasi yako hiyo ya uongozi kwani ni rahisi kwa wao kuweza kukupata, pili kati ya watu ambao unafanya nao kazi serikalini wana kisasi na wewe, ikiwemo wale ambao uliwaharibia biashara zao kipindi ambapo iliingia madarakani, wana uchungu na kisasi kikubwa juu yako”
 
Eddy akahisi kichwa chake kinapasuka kwa maumivu makali ambayo anayapata kwa taarifa hiyo ambayo si nzuri kwa upande wake. Taratibu akanyanyuka kwenye kiti alicho kaa na moja kwa moja akaelekea ndani kwake. Akafungua kabati lake lenye baadhi ya vitu muhimu, akatoa kikopo kidogo chenye dawa za kutuliza mawazo, akatoa vidogo kadhaa na kuvimeza, pasipo kutumia maji, kisha akajitupa kitandani.
 
“Kwa nini kila kitu kinanitokea mimi tuuuuuuuuuuuuu”
Eddy alizungumza kwa sauti ya ukali iliyo jaaa jasira na uchungu ndani yake, akiwa katika kuhangaika hangaika kitandani kujaribu kuutafuta japo usingizi, mlango wake ukagongwa mara mbili.
“Nani?”
Mlango ukafunguliwa pasipo mtu huyo kujibu, Eddy akamkuta Rahab akiwa amesimama mlangoni peke yake, Rahab akapiga hatua moja mbela na kuufunga mlango kwa ndani.
“Umefwata nini huku ndani?”
Eddy alizungumza huku akishuka kitandani
 
“Nimekuja nahitaji kuzungumza na wewe?”
Rahab alizungumza huku akipiga hatua kadhaa kumfwata Eddy kitandani
“Twende tukazungumzie nje ila si ndani ya chumba ninacho lala na mke wangu”
Eddy alizungumza kwa ukali kidogo, hakujali Rahab ni mke wa raisi au laa, kabla Eddy hajafika mlangoni Rahab akamuita na kumfanya Eddy kugeuka na kutazama ni kitu gani ambacho Rahab anamuitia.
“Eddy ninakupenda?”
“Upo sawa wewe?”
“Ndio nipo sawa, na ninacho kizungumza ni kitu kitokacho moyoni mwangu”
 
Rahaba akapiga hatua kadhaa hadi alipo simama, wakatazama kwa muda, kitendo ambacho kikaanza kumfan ya Rahab kumwagikwa na machozi.
“Eddy nipo tayari kuacha kila kitu kwenye maisha yangu, ili niwe na wewe. Wewe ni mwanaume wa kwanza katika haya maisha yangu kukupenda, ni mwauaume abaye umeweza kuziteka hisia zangu tangu siku ya kwanza nilipo kuona picha yake nyumbani kwa mama yako”
“Eddy nimekuwa mtumwa kuanzia siku hiyo nimekuwa ni mtu wa kuishi na majuto ya kwanini niliamua kuolewa na Praygod, ambaye si chagua la moyo wangu”
                                                                                                      ***
Wasiwasi mwingi ukaanza kumtawala Raisi Praygod, kila alipo jaribu kuipiga simu ya mke wake, inaita hadi kukata, akamuita mlinzi wake mmoja anaye muamini sana.
“Mama yupo wapi?”
“Ametoka kama dakika kumi zilizo pita hivi”
“Ameenda wapi?”
“Hakuniambia, ila ngoja kwanza nimpigie dereva wake”
Kijana huyo akatoa simu yake mfukoni na kumpigia dereva wa madam Rahab, simu ikaita baada ya muda ikapokelewa
“Upo wapi?”
“Nipo nyumbani kwa muheshimiwa Eddy”
“Upo na madam?”
“Ndio, ameingia ndani?”
“Mlinzi wake yupo wapi?”
“Yupo nje ya gari, kwani vipi?”
“Ahahaa hakuna kitu”
 
Kijana huyo akakata simu, na kumtazama raisi Praygod anaye onekena kujawa na wasiwasi kwani si kawaidia ya mke wake kuto kupoke simu kwa kipindi kirefu.
“Yupo kwa waziri wa ulinzi bwana Eddy Godwin”
‘Eddy Eddy’
Wivu wa mapenzi ukaanza kuusumbua moyo wa raisi Praygod, kila alipo jaribu kuvuta baadhi ya kumbukumbu, siku jinsi alivyo wakuta Eddy na mke wake kwenye chumba cha waziri huyo kijana mdogo, alihisi kitu kilicho kuwa kikiendelea ila hakuweza kukiweka kichwani mwake akiamini kwamba ni jambo la kawaida.
 
‘Kwanini leo tena aende kama walisha maliza kuzungumza jana?’
Raisi Pryagod alijiuliza tena kichwani mwake swali ambali jibu lake likajaa wasiwasi mwingi, akakumbuka kitu kimoja kilicho mstua, wakati Rahab anamueleza anakwenda kuonana na Eddy kwenye chumba chake, rangi ya mdomoni mwake, ilikuwa imekolea vizuri tu. Ila alipo ingia na kuwakuta rangi hiyo ya mdomoni haikuwa kama vile alivyo ingia nayo.
‘Au alimkiss mke wangu kilazima?’
Hapo ndipo raisi Praygod akahisi kuna kitu ambacho kinaendelea kwa watu wawili hao, asira na uchungu mkali ukampanda moyoni mwake.
 
“Andaa ndege nahitaji Eddy na mwanae aliye baki wapelekwe mbali na Tanzania”
“Sawa muheshima na tuwapeleke wapi?”
“Popote ila mbali na Tanzania, na hii taarifa umpelekee baada ya kila kitu kuwa sawa”
“Sawa muheshimiwa”
“Ila Lube, hakikisha kwamba hili jambo umuelezi mke wangu,  iwe siri yako mimi na wewe”
“Sawa muheshimiwa”
“Pia hakikisha unawafwatilia hatua moja hadi nyingine, na kila kinacho endelea hakikisha kwamba unaniambia”
Raisi Praygod akajikuta akiachia tusi zito, lililo jaa hasira, akihisi hali ya mahusiano kati ya Eddy na Rahab
“Nitakuuaa wewe mshezi Eddy”
                                                                                                           ***
Madam Mery akiwa ndani ya basi la Ngorika liendalo mkoani Arusha, mawazo mengi yakamtawala moyoni mwake, kila alipo jaribu kufikiria mambo aliyo mfanyia Eddy, roho yake ilizidi kumuuma sana hadi wakati wingine akatamani kufa kwani hastahili kabisa kuwa binadamu anaye paswa kusamehewa.
 
Akaanza kukumbuka jinsi mahusiano mazuri yaliyo kuwepo kati yake na Mzee Godwin, kipindi alipo mleta Eddy shuleni kwake kumuanzisha kidato cha tano. Ni siku ambayo mzee Godwin aliweza kumkabidhi Eddy kwake awe anamtzama kwa kila kitu na hata baadhi ya pesa ya matumizi ya Eddy aliweza kumuachia endapo Eddy ataishiwa na pesa iwe rahisi kumsaidia. 

Uchshi, ukaribu na uzuri wa Eddy, ndivyo vitu ambavyo vilimkosesha ujasiri na ustahimilivu wa kuzuia hisia zake za mapenzi juu ya Eddy. Kitu kilicho muumiza akili ni jinsi gani ambavyo angeweza kumuanza Eddy katika swala zima la mahusiano isitoshe yeye alikuwa ni mwalimu wake.
 
Siku ambayo aliweza kumkuta Eddy chumbani kwake akiwa ameshika mdoli wake ulio kaa kama jinsia ya mwaume, alio kuwa akiutumia katika kujichua pale hamu, zinapo mzidi, ndipo ikawa nafasi yake ya kuweza kufanya kila kitu kwa ajili ya kumpata kijana huyo aliye tokea kuutesa moyo wake.
 
‘Mapenzi yalinifanya niwe mjinga’
Madam Mery alijisemea kimoyo moyo huku akiachia tabasamu dogo, kila alipo kumbuka mambo ambayo walifanya kitandani na Eddy, akajikuta akizidi kuumia sana moyoni mwake
‘Eddy am sorry again’
Hapo machozi yakamwagika madam Mery hata kijana aliye kaa naye pembeni ya siti akashnagaa ni kwanini mama huyu anamwagikwa na machozi.
                                                                                                     ***
Rahab akaikamata shingo ya Eddy, kwa haraka akaupeleka mdomo wake, kwenye lipsi za Eddy, safari hiii akatuma kila aina ya mbinu kuhakikisha anapata penzi la Eddy, ambaye mwanzoni alikuwa ni mgumu sana kuweza kumruhusu Rahab kuweza kufanya hivyo. Ila Rahab akafanikiwa kupeleka mikono yake sehemu ambayo, hisia za kimapenzi za Eddy ndipo zilipo. 

Wakiwa kama watu wanao kimbizwa wakajikuta wote wakivua nguo zao na kubaki kama walivyo zaliwa, Eddy akambeba Rahab hadi kwenye kitanda na kuanza kuonyesha ujuzi wake kwenye kitengo hicho cha kitandani ambacho hakina cheo maalumu kwa mtu yoyote. Kwa raha ambazo Rahab alianza kuzisikia akajikuta akipiga makelele kama mtoto mdogo, kwa mara kadhaa akajikuta akilitaja jina la Eddy.
“Madam yupo wapi?”
Lube alimuuliza mlinzi wa kike wa Rahab, mara baada ya kufika nyumbani kwa waziri Eddy.
 
“Yupo ndani, anamazungumza muhimu anazungumza na muheshimiwa”
“Nina ujumbe wake nahitaji kwenda kumuona”
“Sawa”
Latifa hakuwa na wasiwasi wowote kwani Lube ni miongoni mwa walinzi wanao walinda raisi Praygod pamoja mke wake. Lube akaingia hadi sebleni hakumkuta mtu yoyote, baada ya kutaza maeneo yote ya vyumba vya chini, pasipo kuwaona Eddy na Rahab. 

Ikambidi kupandisha gorofani kutazama seble nyingine ambayo alihisi kwamba wanaweza kuwemo humo, ila cha kushangaza hakuweza kuwaona. Akiwa amesimama sebleni akautazama mmoja wa mlango, ambao akahisi kitakuwa ni chumba cha kulala cha waziri Eddy, akatembea kwa hatua za kunyata hadi kwenye mlango huo.
Lube hakuamini kusikia miguno ya kimahaba, huku sauti ya mke wa raisi, ikiwa imeizidi sauti ya waziri Eddy.
“Eddy nipo tayari kumuacha mume wangu, niende popote na wewe”
 
Maneno hayo ya Rahaba yakamstua sana Lube. Lube akakumbuka maneno ya raisi Praygod aliyo toka kumumbia muda mchache ulio pita kwamba awafwatilie watu hao hatu kwa hatua na chochote ambacho kitaendelea ajulishwe. Kwa haraka Lube akatoa simu yake mfukoni, akaingia upande wa kurekodi sauti, na kuanza kurekodi sauti hizo za mahaba zilizo jaa ahadi nyingi za kimapenzi, ikiwemo  sifa kedekede ambazo Rahab anamwagia Eddy.

 Lube akiwa anaendelea kurekodi tukio hilo kwa sauti, Shamsa akasimama nyuma yake na kushuhudia kila kitu ambacho Lube anakifanya nje ya mlango wa baba yake, kitu kilicho mchukiza sana Shamsa, na kujikuta akimshika bega Lube, kwa ajili ya kujmshambulia kuzuia sirihiyo kuweza kuvuja
                                                                                
SORRY MADAM (24) (Destination of my enemies)

Kitendo cha Lube, kugeuka akakutana na kofi zito la uso lililo mfanya kufumba na kumfumbua macho yake mara kadhaa na kigiza kikali kikapita kwenye usawa wa macho yake asitambue kofi hilo amepigwa na nani, kabla hajajiweka sawa, ngumi nzito, ikatua tumboni mwake na kujikuta akijikunja, huku akigugumia mguno mkali wa maumivu, kigoti kikatua kwenye kidevu chake na kumfanya anyanyuke juu pasipo kupenda, huku baadhi ya meno yake yakigongana gongana kinywani mwake. 

Shamsa kwa haraka akamdaka shingo Lube na kumpokonya simu ailiyo ishika na kuidumbukiza mfukoni mwa suruali aliyo vaa, kisha kwa haraka akaupitisha mkono wake mmoja kwenye kiuno cha Lube na kuikuta bastola ikiwa imechomekwa nyuma ya kiuono chake, akaichomoa na kuishika mkononi mwake na kuendelea kumgandamiza Lube ukutani.
 
“Nani amekutuma?”
Shamsa alimuuliza Lube kwa sauti ndogo ambayo si rahisi kwa watu waliomo ndani kuweza kumsikia,  Lube akabaki akiwa katika kushangaa shanga, kwani hakuamini mtu anaye mshushia shambulio hilo ni binti ambaye mara nyingi anamuona ni mpole na mnyonge sana. Gafla akastukia kichwa kizito kikitua kwenye pua yake na kumfanya atoe ukelele mkali hadi Eddy na Rahab wakastuka, wakiwa katikati ya mchezo wao.
“Kuna nini huko nje?”
Eddy alizungumza huku akiutazama mlango wa kuingilia chumbani kwake, kwani sauti hiyo inaonekana kutokea nje ya mlango wake.
 
“Mmmm hata sijui”
“Ngoja nitazame”
“Bwana acha, tumalizie raha yetu”
Rahab akamshinda Eddy kwenye maamuzi na kuamua  waendelee na kitendo chao, kinacho wafurahisha sana. Shamsa, alipo muona Lube amelegea kwa pigo hilo akamvu na kumuingiza ndani ya chumba chake na kumsukumia kwenye sofa.
“Wewe ni nani?”
“Ehehehheee……………..!!!”
“Nakuuliza wewe ni nani?”
Shamsa alizunngumza kwa sauti ya ukali hadi Lube akaanza kutetemeka kwa owga, Lube akatoa kitambulisho chake na kumuonyesha Shamsa kwamba yeye ni miongoni mwa wafanyakazi wa ikulu na nimlinzi wa kiongozi wa nchi raisi Praygod Makuya. 
 
“Nani amekutuma?”
Likawa ni swali jengine lililo mfanya Lube kuwaza meneno ambayo raisi alimuambia masaa machache nyumba kwamba iwe siri kati yao na asimuambie mtu wa aina yoyote.
“Hakuna aliye nituma”
Luba akajibu kwa dharau huku akiikunja midomo yake, akijiona amekuwaje kupigwa na kabinti kadogo ambacho alikachukulia kama kimdoli
 
“Ahaa hakuna eneee……….!!”
Bila ya hata huruma, Shamsa akamtandika Lube teke lililo tua kwenye sehemu zake za siri na kumfanya Lube kujikunja na kugugumia kwa maumivu makali ambayo hakuwahi kuyapata tangu kuzaliwa kwake. Shamsa akaikoki bastola ya Lube na kumuelekezea, akionekana hana masihara hata kidogo na endepo Lube ataleta ujinga basi risasi zilizomo kwenye bastola hiyo zitaishilia mwilini mwake. 

Shamsa akarudi nyuma nyuma hadi kabati. akafungua kabati lake la nguo, akatoa moja ya mkanda wa suaruali, akamvuta Lube kutoka kwenye sofa aliyo kaa na kumuangusha chini. Luba akajigeuka kwa kasi ya ajabu na kuichota miguu ya Shamsa na kumuangusha chini na kuifanya bastola aliyo ishika kuangukia pembeni. 

Wote wakajikuta wakinyanyuka kwa pamoja na kukunja ngumi za mikono yao. Lube akatema kwanza fumba la mate lililo jaa damu. zilizo tokana na kichwa alicho tandikwa nje, Shamsa akauzungusha mkanda mara mbili mkononi mwake kuhakikisha kwamba mkando huo hauwezi kumponyoka.
 
Lube akarusha la hewani, Shamsa aliweza kuliona mapema, kwa kasi ya ajabu akabonye chini, akanyanyuka kwa ngumi nzito iliyo tua sikioni mwa Lube na kumfanya ahisi ukelele mkali, kwenye sikio hilo. Akatingisha kichwa chake mara kadhaa akijitahidi kuyaondoa maumivu hayo makali.
 
“Umeniotea eheeeee”
Lube alizungumza huku akifungua vifungo vya shati lake, akakunja mikono ya shati hilo iliyo mirefu, akajinyoosha viungo vyake kiasi na kujiweka sawa. Shamsa akamtazama jinsi Lube alivyo jiweka kwa haraka akakimbia kwenye pembe ya kitanda, akakanyaga na mguu wa kushoto, ukaupa fursa mguu wa kulia kugeuka na teke zito lililo yua shingoni mwa Lube aliye kuwa akimfwata kwa nyuma pasipo kujua lengo la Shamsa ni nini kwake. Teke hilo zito likamfanya Lube, kuanguka mzima mzima pasipo hata kujitingisha, akiashiria amepoteza fahamu. Kwa haraka Shamsa akamlaza Lube kifudifudi na kuifunga mikono yake kwa nyuma kwa kutumia mkanda alio ushika.
 
Shamsa akamtazama kwa muda Lube aliye lala chini, akatoka chumbani kwake, akelekea jikoni akachukua jagi na kuweka maji ya baridi yenye vibarafu vidogo vidogo, akarudi chumbani kwake, kwa kutumia maji hayo akamwagia Lube ya kichwani na kumfanya akurupuke kwa haraka huku akihema kwa nguvu
“Naona umerudi kutoka kuzimu si ndio”
Shamsa alizungumza huku akiwa amekaa kwenye sofa na bastola akiwa ameielekezea kwa Lube aliye lala chini.
 
“Swali langu ni lile lile, ni nani aliye kutuma?”
Luba hakujibu chochote zaidi ya kukaa kimya na kumtazama Shamsa kwa hasira kali
“Nahesaba hadi tatu baada ya hapo tutaonana ahera madukani sawa bwana kaka?”
“No nakuomba usiniue nipo tayari kukueleza kila kitu ambacho utaniambia nikueleze”
“Unauhakika?”
“Ndio nipo tayari”
Lube alizungumza kwa woga hadi akahisi haja ndogo ikiwa inataka kumwagika
                                                                                                    ***
Mzee Godwin na Tom wakafika kwenye moja ya mji, wakatekeza gari ya polisi wanayo itumia, kwa pesa walizo nazo wakanunua mavazi ambayo si rahisi kwa mzee Godwin kujulikana kwamba yeye ni muhalifu, anaye tafutwa kila kona ya Tanzania.
 
“Babu hapa ni wapi?”
“Hapa kunaitwa Namanga ni mpakani kati ya Tanzania na Kenya”
“Ahahaaa ila kuna baridi?”
“Ndio mana tukanunua makoti ili kuweza kujikinga na baridi hii, huku sio kama kule pwani ni upepo tu wabahari ndio unawanya muoene baridi”
Kutokana ni majira ya mchana, ikawabidi wakae kwenye moja ya kimgahawa kidogo kujipatia chakula, wakivu vuta muda wakisubiria Manka kutekeleza kazi ambayo amempatia, ili waondoke naye.
 
“Babu napenda sana siku moja niwe kama wewe”
“Kama mimi kivipi?”
“Nahitaji kuwa mmoja wa watu wako, nahitaji kulipiza kisasi na mimi?”
“Ahahaaa, Tom unajua nini maana ya kisasi?”
“Kisasi kwa uwelewa wangu, ni kulipiza baya kwa aliye weza kukufanyia mabaya.”
“Sasa unahitaji kulipiza kisasi cha nani?”
“Kwa mtu aliye weza kuniulia kaka yangu na kusababisha pia mama na baba kufariki kwa mstuko babaada ya kusikia kifo chake”
 
“Kaka yako, alikuwa ni nani?”
Tom akamatazama Mzee Godwin usoni kisha akaachia tabasamu pana kidogo, akachukua glasi iliyo jaa juisi na kuinywa taratibu kulisuuuza koo lake.
“Anaitwa DERICK”
“Derick……..!!! Ahaa sawa usijali kila kitu kitakuwa sawa”
Jina la Derick halikuwa geni kichwani mwa mzee Godwin, akamtazama Tom kwa macho ya kumchunguza, akagundua ukweli na uchungu ulio mtawala Tom.
                                                                                                  ***
Majira ya saa kumi na moja jioni madam Mery akafika mkoani Arusha moja kwa moja akaelekea nyumbani kwake alipo paacha miaka mitano iliyo pita pasipo kupakanyaga. Ukimya wa nyumbani kwake halikuwa jambo la kumuogopesha sana kwani hakuacha mtu yoyote aliye weza kuitunza hiyo nymba yake aliyo inunua miaka sita iliyo pita, nyasi ndevu zilizo izunguka nyumba yake, ziliashiria kwamba hapakuwa na mtu ambaye Alisha wahi kufika hapo kabla yake kwani geti lake hakulifunga kabisa zaidi ya kulitegesha na kuonekana kama limefungwa. 

Akazunguka nyuma ya nyumba kwenye vyungu vikubwa ambavyo ameoteshea maua, akasimama kwenye moja ya chungu na kuchukua funguo ya mlango wa kuingia katika mlango wa mbele wa nyumba yake. Sehemu alipo icha funguo hiyo ndipo sehemu aliiweka kipindi anaondoka kuelekea nchini Somali kwa kazi maalumu aliyo pewa na Mzee Godwin kuwa kama mfanyakazi wa bamnk ya Bacrayce nchini humo.
 
Akarudi upande wa pili wa nyumba na kufungua mlango wake, akakutana na vumbi jingi lililo tanda ndani ya sebule yake likiambatana na mitando mingi ya buibui.
“Ahaaaaa”
Akashusha pumzi nyingi akitazama uchafu mwingi uliomo ndani ya nyumba yake hiyo, akaaza kufungua mlango mmoja baada ya mwingine iliyo kuwemo kwenye nyumba ytake kuchunguza kama kuna usalama wowote.
 
‘Kwa leo siwezi kulala humu’
Madan Mery akafunga nyumba yake na kutoka getini, akatazama kila kona ya mtaa wake ano ishi, hapakuwa na mabadiliko makubwa sana ya eneo hilo, akaita usafiri wa pikipiki, akamuomba dereva ampeleke kwenye moja ya hoteli ambayo mara nyingi huitumia katikia kupumzika. Wakati, akiwa njiani kuelekea katika hoteli hiyo, Manka hakuwa mbali naye, kuanzia anaingia nyumbani kwake, Manka aliweza kumuona na kuhakikisha ana mfwatilia kwa ukaribu wa hali ya juu, kama alivyo pewa maagizo na baba yake mzee Godwin. 

Taarifa za madam Mery kuelekea mkoani Arusha zilitolewa na miongoni mwa walinzi wa Eddy, walio wekwa na serikali kumlinda kiongozi huyo mara baada ya mauaji ya familia yake kutokea, huku mlinzi huyo Brian anashirikiana fika na mzee Godwin na nimiongoni mwa wanachama wa kundi la D.F.E
 
Pasipo Madam Mery kutambua anafwatiliwa, kipindi alipo kuwa akitoka nyumbani kwa Eddy, mlinzi huyo aliweza kumfwatilia hadi alipo fika stendi ya mabasi ubungo, na kupanda basi la kuelekea mkoani Arusha, ndipo akampa taarifa bosi wake mzee Godwin, na kwabahati nzuri tayari Mzee Godwin alisha fika mkoani Arusha akiwa katika harakati za kuondoka ndani ya nchi ya Tanzania. Kikubwa ambacho ni cha hatari zaidi ni kwamba Madam Mery alisha toa siri zao zote kwa binti mdogo Shamsa, hadi makao makuu yao yanapo patikana.
 
Jukumu alilopewa Brian ni kuweza kumfwatilia Shamsa na kuhakikisha kwamba anamuondoa dunia, na akipata nafasi aweze kumteka Eddy na kuwa mikononi mwake.
Madam Mery kufika Hotelini, Manka naye akawa amesha wasili, kwa kutumia usafiri wa taksi, akamlipa dereva wa taski na kushuka kuelekea ndani alipo elekea madam Mery.

 Akamshuhudia Madam Mery akielekea kwenye lifti iliyo mpeleka gorofa ya tano kwenye hoteli hiyo. Naye akaingia kwenye lifti ya pembeni iliyo mpeleka kwenye gorofa aliyo eleke madam Mery, ndani ya dakika moja akawa amesha fika kwenye gorofa hiyo akamshuhudia madam Mery akiingia kwenye moja ya chumba namba 1220. 

Baada ya Madama Mery kuingia ndani ya chumba hicho akachomoa bastola yake na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuanza kutembea kwa mwendo wa kasi katika kordo hiyo akielekea kwenye chumba alicho ingia Madam Mery
                                                                                                  ***
“Raisi Pray ndio ameniagiza……………..”
Lube alizungumza huku akihema sana, akisikilizia maumivu ya viungo aliyo weza kupewa na Shamsa, ikiwemo shingo yake aliyo shindwa kuigeuza kwa muda sasa
“Amekutuma nini?”
“Ameniambia kwamba niweze kumfwatilia muheshimiwa na madam Rahab”
“Baada ya kuwafwatilia?”
“Ameniambia wewe na muheshimiwa niweze kuwatafutia sehemu ya mbali na Tanzania muondoke mukaishi huko hapa haitaji kuwaona”
 
“Una uhakika kwa uliyo yazungumza?”
“Ndio ninauhakika dada yangu, ila ninakuomba usimwambiea muheshimiwa tafadhali”
Shamsa akamtazama Lube jinsi anavyo zungumza kwa woga mwingi ulio mtawala huku machozi yakimwagika usoni mwake, akamnyanyua na kumkalisha kitandani huku akiwa emendeleea kumuelekezea bastola yake.
“Sina haja ya kuweza kukuua ila ninauwezo huo wa kukua endapo utafungua hilo bakuli lako kuweza kumueleza huyo raisi wako kwa kitu ulicho weza kukisikia”
 
“Sawa”
“Poteee na nisikuone ukirudi tena hapa”
Shamsa alizungumza huku akimfungua Lube mkanda alio mfunga kwenye mikono, taratibu Lube akatoka ndani ya chumba cha Shamsa huku macho yake yakiitzama bastola yake asiamini kwamba binti huyo ameweza kumzibiti vya kutosha.
“Ohhhhhhhh Eddy wewe ni noma”
Rahaba alizungumza huku akilala pembeni ya Eddy mara baada ya kumaliza mechi iliyokuwa na ushindani wa hali ya juu.
 
“Kwa nini?”
“Mmmmm sijapata ona, mwanaume mwenye kasi kama wewe aiseee ahahaa hapana yaani mmmmm…..”
“Hakuna kitu”
“Mmmmm natamani niendelee kufanya siku nzima ila yule bwege ananisubiri huko ikulu kwake”
“Hivi ni kwanini umeweza kumsaliti mume wako?”
“Kuna sababu nyingi sana, ila moja wapo simpendi”
 
“Ilikuwaje ukakuoa?”
“Ilikuwa ni kama bahati mbaya kuokota embe dodo chini ya mpapai, ila pia nipo kwa ajili ya kuhakikisha wezangu ninaweza kuwakomboa”
Rahab alizungumza huku akikaa kitako, taratibu akamgeukia Eddy na kuanza kumchezea kifua chake kipana, kilicho weza kujazia vizuri kwa mazoezi.
“Eddy nina historia ndefu sana kwenye maisha yangu, hadi leo nimefanikiwa kufika hapa kusema kweli ni kazi kubwa sana, ila kuna siri nitakueleza tukiendelea kuwa pamoja”
 
“Siri, siri gani………..!!?”
“Kuhusiana na maisha yangu ila kwa leo tuishie hapa”
Rahaba akanyanyuka kitandani na kuelekea bafuni na kumucha Eddy akiwa katika alama ya mshangao kwani hakujua ni siri gani ambayo Rahab anahitaji kumueleza, Rahab akatoka bafuni, akajifuta maji mwili mzima kwa kutumia taulo, akavaa nguo zake na kujiweka sawa kama alivyo ingia, muda wote Eddy akiwa kitandani akimtazama jinsi anavyo jiremba, hapo ndipo Eddy akautambua uzuri wa Rahab kuanzia chini hadi juu.
 
“Eddy nahitaji unioe”
“Niku…….”
Rahab akamziba kwa kidole kimoja mdomoni, taratibu akaushusha mdomo wake na kumpiga busu zito la mdomo Eddy na kuzidi kumpagawisha
 
“Tutaonana siku nyingine”
Rahab akanyanyuka kitandani na kuondoka, akamuachia maswali mengi Eddy, dakika hata mbili hazikupita Shamsa akaingia chumbani kwa Eddy bila hata ya kubisha hodi, mkononi akiwa ameshika bastola huku mkono mwingine akiwa ameishika simu ya Lube, huku akiwa ameiweka sauti iliyo rekodiwa, sura yake akiwa ameikunja kwa hasira akichefuliwa na tukio alilo lifanya Eddy pamoja na mke wa raisia, kwa bahati mbaya akamkuta Eddy ndio ananyanyuka kitandani akiwa kama alivyo zaliwa na wote wakabakiwa wakiwa wametazamana.

==> ITAENDELEA
 
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia ubuyublog.com  


Advertisement
hapa

Post your Comment

Habari Mpya

Popular Posts